Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Ludovick baada ya kukutana na Rwakatale tarehe 28Dec saa 5 muda mfupi baadae yaani saa 5:59 alimpigia simu Mwigulu Nchemba kwa kutumia namba ya simu ya Mwigulu ambayo ameiandikisha kwenye kumbukumbu na vitabu vya Bunge Lissu anadai wana rekodi ya mazungumzo yao.

Kama ni kweli mazungumzo yakupanga mission yalifanyika basi ViJANA wa CHADEMA hata hapa JF kelele ni nyingi kumbe zinachagizwa na kusumbuliwa na njaa. Kiboko chao, weka pesa mezani. Kelele zote zinaisha.
 
Leo katika press conference ya mawakili wanaomtetea Lwakatare wamedai Michuzi alikuwa akipongezana na Usalama wa taifa kuwa ile video ni nzuri.Waungwana naomba CV yake nijue aliingiaje pale Ikulu mpaka kuwa mpiga picha wa rais, je, elimu ilizingatiwa?

Mkuu hii ni serikali ya kishikaji, elimu siyo kigezo cha kupata kazi ikulu, kigezo kinachozingatiwa ni uwezo wako wa kujikomba, kujipendekeza, kumsifia na kulamba viatu vya muishiwa dhaifu na familia yake.
 
ninahamu ya kusikia Ludovick na Mwigulu waliongea nini kwenye simu.....muda utaongea.

kwa hili ninaimiss sana MWANAHALISI ndugu yangu......WANGEANIKA KILA KITU!
naamini kufungia Mwanahalisi, ni mpango mkakati wa CCM na serikali yake ili mipango yao ya kihalifu isipate watu wa kuianika hadharani.
HIVI HALIWEZI KUINUKA GAZETI LINGINE KUIFANYA HII KAZI ILIYOACHWA NA MWANAHALISI?
KUBENEA NA TIMU YAKO TUNAKUMISS.
 
na kwa taarifa zaidi ni kuwa polisi wana video yenye dakika 27.06 na maneno yanatofautiana sana na yaliyoko kwenye You tube iliyowekwa kwenye mitandao .

Vedio ya You tube ni dakika 19.6,

Swari:

Je hii ya police wameitoa wapi?

Je Mwigulu kawapelekea police?
 
Wahalifu kama huyu DPP nao wanastahili mafao ya kustaafu, au wastahili kupelekwa jela baada ya ukombozi!

Zitazuka hoja za kutengeza truth and reconsiliation commission kuwezesha haya yasahaulike ili mustakabali wa amani na utulivu umee mizizi. Utakuja kuniambia hili.... Haya tumeyaona Kenya, Rwanda, South Afrika, au hata Zanzibar for that matter. Sijui Cosovo kulizuka nini lakini wanasiasa ni wepesi sana kujifanya wanatetea umoja na mshikamano ili aliyeumia asikumbushie matezo yake. Hawa CCM wanatakiwa kubamizwa tu sasa ili kila mtu awe anauguza makovu huko mbele wakati wa truth and reconsiliation. Amani haitufikishi popote...
 
Hivi sasa wanasheria wa CHADEMA wanafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la Lwakatare na makosa ambayo alishitakiwa nayo.

Anaeleza kuwa kama ameshitakiwa kwa ugaidi lazima makosa hayo yawe ni ya kigaidi, ila makosa ya Kidnapping na abduction ni makosa ya kawaida ya jinai , na kama ili yawe ya kigaidi ni lazima hayo makosa yawe yamefanyika kwa malengo ya kigaidi , na hata hati ya mashitaka haina maelezo ya makosa ya ugaidi .

Nyongeza: kuhusu video amesema tayari kuna ushahidi wa kimawasiliano baina ya Mwigulu Nchemba ya tarehe 28.12.2012 wakiwasiliana na Ludovick saa 5:55 asubuhi , na Lwakatare amesema kuwa yeye alikutana na Ludovick kuanzia saa tano asubuhi tarehe 28.

Aidha , ameongeza kuwa tarehe 27.12.2012 Denis Msacky alimpigia simu Lwakatare wakati akiwa njiani kurejea akitokea Kagera , akiwa Morogoro na kumuuliza kama yupo DSM , akamjibu yuko njiani.

Tatu, tarehe 29.12.2012 Mwigulu Nchemba , akiwa na Zitto na Mtatiro Star Tv , kipindi cha tuongee asubuhi ndipo alisema kuwa ana mkanda wa viongoz i wa chadema wakipanga mauaji ......sasa haya yote yatajulikana mahakamani.

Ziada .

Maelezo aliyotoa Lwakatare polisi kuhusu maneno yaliyoko kwenye video alisema kuwa yeye anakumbuka siku ya tarehe 28, alikuwa nyumbani kwake na Ludovick ndio alienda kwake , ila picha ya video ni ya kwake , sura ni ya kwake ila baadhi ya maneno yaliyoko sio ya kwake na ameandika hivyo , kwa hiyo kuhusu ukweli wa mkanda majibu ya kina yanatakiwa kutoka polisi , Mwigulu na Denis ndio wanajua nini kipo kwenye mkanda . Hivyo picha limeanza kuonekana , na kwa taarifa zaidi ni kuwa polisi wana video yenye dakika 27.06 na maneno yanatofautiana sana na yaliyoko kwenye You tube iliyowekwa kwenye mitandao .

Sasa polisi nao waliulizwa ni kwanini hawajamkamata aliyeweka hiyo you tube kwenye mitandao walitoa majibu yao na mawakili wanaendelea na uchunguzi wao.

Panaponitatiza ni hapo penye blue ,inamaana kuwa hata yule ambaye polisi wanayedai alikuwa chambo(Yaani Denis Msaky) pia yumo kwenye huu mchezo wa kuigiza?Inaelekea alikuwa anajua kinachoendelea.Maana Episode hii imeleta maswali mengi zaidi kuliko majibu.Huu siyo ugaidi ni ujinga wa kuchafuana tu.
 
Katika pre emptying ya Mawakili wa Lwakatare,

Watu hawawezi kupanga mauaji katika sehemu ya wazi wanayopitapita watu?Mmmmh----Aiseee!Nani kasema!--Hebu jiulize na wewe,Hii ni strong argument kweli ya kumtetea mtu?

Ni Kweli Lwakatare alirekodiwa,Sura yake,ILA baadhi ya maneno sio yake....LAKINI HAKUREKODIWA KWA RIDHAA YAKE,NA HIYO NI MAKOSA?Mmmmmh---Jamani...Mtu anasikika kurekodiwa KUTEKA NA KUMDHURU MWINGINE<HALAFU UNATEGEMEA ATATOA RIDHAA AREKODIWE?--Mmmmh---What an argument jamani.....Dah!(Utadhani Video iliyopelekwa inawaonyesha Wanakunywa pombe na kupiga Soga za Kulima Viazi------Eti "Kuna sheria ya kuzuia mkosaji asirekodiwe"?)

Usalama wa Taifa hauna ruhusa ya kurekodi mawasiliano ya Vyama vya Siasa kwa ajili ya faida ya Chama Tawala---Mmmmh,Jamani jamani---OK OK,Ikithibitika Chama Tawala kimewafanyia Uhuni ili Usalama wa taifa wamrekodi Lwakatare,basi hii haitaondoa "dhana" ya kwamba Lwakatare alifanya Kosa,bali tu itabidi "Chama Tawala" wafunguliwe mashtaka na atakayeona wamefanya Kosa.

Saa 5.55 tarehe 28/12/2012 Mwigulu awasiliana na Ludovick----Eeeeeh?SWALI LETU WENGI LIMEKUWA NI NANI ALIMREKODI LWAKATARE?Kila Mtu anaendelea kuwa na jibu lake Kichwani....Siku ya kurekodiwa mkanda,Mwigulu anawasiliana na Ludovick(ambaye inasemekanika ni mtu mwaminifu ndani ya Wakuu wa Chadema),Kesho yake Mwigulu anasema tunao ushahidi wa CHADEMA kupanga mambo ya Uuaji....Mmmmmh,What a coincidence,...kweli Mwigulu ni Kijukuu cha mtume kama hakuwa ameshaupata huu Mkanda..

Kesi irudi mahakama ya Kwanza ilipofunguliwa?---Kwa sababu hapo ndio lazima Kesi kama hiyo LAZIMA isikilizwe?---Wameshasema kwamba "walikuwa wamekosea" Kuipeleka pale,kwani inaonyesha mahakama ile haina uwezo wa kuendesha Kesi hiyo------Suala litofautishwe hapa---Kati ya sehemu ambayo Kesi itafutwa kwa sbabu Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza,na lile la kwamba Kesi itafutwa kutokana na kwamba itaonekana "watu hawajafanya makosa wanayotuhumiwa"..

Ok OK.....Tusubiri mambo yanaendaje
JF---Kila mtu mwandishi,mchambuzi,mropokaji,Mwana Intelijensia----raha ndani ya Karaha yani
Tunaendelea kusikiza wengine wanachambueje mambo.

Hebu nisaidie kufahamu, if you don't mind, katika hayo makundi hapo juu kwenye red nikuweke kundi lipi?
 
my thoughts exactly ..

Hivi sasa wanasheria wa CHADEMA wanafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la Lwakatare na makosa ambayo alishitakiwa nayo.

Anaeleza kuwa kama ameshitakiwa kwa ugaidi lazima makosa hayo yawe ni ya kigaidi, ila makosa ya Kidnapping na abduction ni makosa ya kawaida ya jinai , na kama ili yawe ya kigaidi ni lazima hayo makosa yawe yamefanyika kwa malengo ya kigaidi , na hata hati ya mashitaka haina maelezo ya makosa ya ugaidi .

Nyongeza: kuhusu video amesema tayari kuna ushahidi wa kimawasiliano baina ya Mwigulu Nchemba ya tarehe 28.12.2012 wakiwasiliana na Ludovick saa 5:55 asubuhi , na Lwakatare amesema kuwa yeye alikutana na Ludovick kuanzia saa tano asubuhi tarehe 28.

Aidha , ameongeza kuwa tarehe 27.12.2012 Denis Msacky alimpigia simu Lwakatare wakati akiwa njiani kurejea akitokea Kagera , akiwa Morogoro na kumuuliza kama yupo DSM , akamjibu yuko njiani.

Tatu, tarehe 29.12.2012 Mwigulu Nchemba , akiwa na Zitto na Mtatiro Star Tv , kipindi cha tuongee asubuhi ndipo alisema kuwa ana mkanda wa viongoz i wa chadema wakipanga mauaji ......sasa haya yote yatajulikana mahakamani.

Ziada .

Maelezo aliyotoa Lwakatare polisi kuhusu maneno yaliyoko kwenye video alisema kuwa yeye anakumbuka siku ya tarehe 28, alikuwa nyumbani kwake na Ludovick ndio alienda kwake , ila picha ya video ni ya kwake , sura ni ya kwake ila baadhi ya maneno yaliyoko sio ya kwake na ameandika hivyo , kwa hiyo kuhusu ukweli wa mkanda majibu ya kina yanatakiwa kutoka polisi , Mwigulu na Denis ndio wanajua nini kipo kwenye mkanda . Hivyo picha limeanza kuonekana , na kwa taarifa zaidi ni kuwa polisi wana video yenye dakika 27.06 na maneno yanatofautiana sana na yaliyoko kwenye You tube iliyowekwa kwenye mitandao .

Sasa polisi nao waliulizwa ni kwanini hawajamkamata aliyeweka hiyo you tube kwenye mitandao walitoa majibu yao na mawakili wanaendelea na uchunguzi wao.
 
Nilijua tangu awali, kwamba kama mpango huu haukupangwa na Lwakatare na Ludovick kwapamoja, basi lazima mmoja wapo alishiriki.... Mwisho wa siku tutaujua tu ukweli. Na kwa hatua hii hawawezi kumkana Ludovick tena, kama kweli wangekuwa hawajuani, angemruhusu vipi kwenda nyumbani kwake na kuzungumza waliyozungumza?

Utam kolea... wameanza kukubali wenyewe kwamba mkanda ule una ukweli ndani yake ee? haya na tuwe wapole tusubiri majibu ya polisi. Ha ha ahaaaa

Tangu uzaliwe, ulishawahi kukiona kitu kinachoitwa "UWONGO MTUPU"?. TUAMBIE KAMA KINA EXIST KIKOJE? TENA UTOE MFANO. BAADA YA HAPO UTAELEWA UNACHOTAKA KUKISAHAU HAPA.
 
Swala la nani aliyeko kwenye video na mahali gani ulichukuliwa hilo limeishapata ufumbuzi.

KEY POINT.
Kwa sasa misuguano iliyopo ni kama video itakuwa EDITED au La. Na kama EDITED kwa kiasi gani (minutes).

mtu wa kwanza kudhalilika mpaka hapa tulipo ni Dr. Slaa aliyesema video ni fake.
 
Kama ni kweli mazungumzo yakupanga mission yalifanyika basi ViJANA wa CHADEMA hata hapa JF kelele ni nyingi kumbe zinachagizwa na kusumbuliwa na njaa. Kiboko chao, weka pesa mezani. Kelele zote zinaisha.
TAARIFA ni pesa,kama huna pesa huwezi kupata TAARIFA,hawa vijana wanapewa pesa,hata wakina Juliana Shonza na Mtela Mwampamba tumewoana wakiwa na hao wakina Mwigulu kwenye maeneo fulani,kikubwa walikuwa wanapewa MPUNGA.ACHANA NA HELA BWANA HAINA ADABU HATA MKEO ANAWEZA KUKUSALITI KWA SABABU YA HELA!
 
Tundu Lissu siku ile alijidhalilisha sana pale mahakamani mpaka akachekwa na umati wa watu!!!

Ngoja utabadilika tu, moyo unauma kusema uongo,ukweli upendeza sanaa....nilikuwa beanch la 2 sikuona upuuzi huu labda kwako na mkeo.( zaid ni wakili wa serikar kuchekwa na watu baada ya kuonesha hati ya mashitaka kakipande kadogo....
 
Maelezo ya Wanasheria hapa yanakuwa na CONTRADICTION kama Ludovick ndiye aliye record au alikuwa masterlminder wa hii saga otherwise kama Ludovick ni mtu wa TISS.

Haiwezekani mtu wa TISS akarecord bila kumshirikisha Ludovick kama kweli Ludovick alikuwa ana mission hiyo na Mh. Mwigulu.
Issa Michuzi Mpiga picha wa Rais alikuwa akipongezana na watu wa Ikulu wenzake kuwa TISS (Usalama wa Taifa) wamefanya kazi nzuri kwa kurekodi ile video. Kisheria usalama wa taifa hawatakiwi wala hawaruhusiwi kurekodi au kuvifanyia ushushu vyama vya siasa kwa maslahi ya Chama tawala.
Ludovick baada ya kukutana na Rwakatale tarehe 28Dec saa 5 muda mfupi baadae yaani saa 5:59 alimpigia simu Mwigulu Nchemba kwa kutumia namba ya simu ya Mwigulu ambayo ameiandikisha kwenye kumbukumbu na vitabu vya Bunge Lissu anadai wana rekodi ya mazungumzo yao.
 
Huyu dada aliyepitisha mgongo kwenye video imeshindikana na yeye kuhojiwa? Kutokana na mshitakiwa kusema photo ni sawa ila sauti. Nadhani huyu dada ana weza akaeleza hili tukio lilikuwa na harufu gani isije ikawa alikuwa anachukuwa kijiko cha kukorogea chai? na watu anahangaika kujua ukweli. Jaribuni kuchungua mwenendo wa huyu Dogo Ludovick na ma met zake wa Chuo. Kwanini amefanya recording? Siku zote mpiga picha haonekani kwenye picha
 
Maelezo ya Wanasheria hapa yanakuwa na CONTRADICTION kama Ludovick ndiye aliye record au alikuwa masterlminder wa hii saga otherwise kama Ludovick ni mtu wa TISS.

Haiwezekani mtu wa TISS akarecord bila kumshirikisha Ludovick kama kweli Ludovick alikuwa ana mission hiyo na Mh. Mwigulu.
What if huyo Ludo naye ni uwt!
 
Back
Top Bottom