Asha Abdala
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 1,130
- 46
Jasusi,
Pamoja na yote hayo nyie wanachama (wajumbe) mnayajua yaliyotokea hadi viongozi hawa kunyang'anywa maradaka yao? kama hamjui huoni kuna umuhimu wa nyie kuelezwa ikiwa nyie dio mlowachagua watu hao..
Bi.Asha nakusoma sana bibie ila nachojaribu kusema hapa ni UWAZI.. tunahitaji kuweka uwazi pale ambapo panatakiwa hata kama kuna machungu.Mkandara,
Maofisa hawachaguliwi, wanateuliwa. Mamlaka iliyowaajiri ndiyo hiyo imewatengua. Ni tofauti na viongozi wa kuchaguliwa ambao wanachama ni muhimu waelezwe wanapoondolewa
Asha
Bi.Asha nakusoma sana bibie ila nachojaribu kusema hapa ni UWAZI.. tunahitaji kuweka uwazi pale ambapo panatakiwa hata kama kuna machungu.
Binafsi huyo Kafulila, atakuwa kafulia kweli ikiwa tutafahamishwa madhambi yake ili kesho mtu mwingine asije yarudia lakini pasipo kuyajua inatupa picha tofauti na mawazo mengi yanajengwa kiasi kwamba hata hizi tuhuma hazikutakiwa kuwepo iwapo tu utaratibu huu ungekuwa wazi na huru.
Binafsi nazungumza hivi kwa kuchelea zaidi jinsi Wadanganyika tulivyo, kesho huyo Kafuylila akiamua kuondoa Chadema anaweza kukipata chama hata kisitamanike kwa sababu tu chama kiliamua kuficha ukweli kwa maufaa ya huyo Kafulila au mtu mwingine...
Trust me hoja zangu, hujaribu kufikiria kama mtu aliyeko nje ya chama (out of the box).. na ndipo tunapo tofautiana kimawazo.
Shukran sana kwa kunifumbua macho sikuliona hilo.. haya huyu Jamaa alichokisema ni kipi haswa! maanake sikumsoma...au nacho ni siri!Babaa, mbona Dr Slaa ameeleza kuwa ametengua uteuzi wao kutokana na wao kukiuka maadili na utendaji kutokana na matamashi waliyoyatoa kwenye vyombo vya habari?
Slaa amesema aliwaita wamejieleza kwa masaa manne na baadaye akaamua kuchukua hatua.
Au haijatosha? Nadhani kwa kuwa Kafulila alisema amepewa barua ni vizuri akatueleza nini kimeandikwa kwenye barua ambayo amepewa.
Lakini kumwambia Slaa aseme ni kulikuza tu hili jambo bila sababu, hawa na maofisa tu mwajiri wao aliyewateua ametengua utuezi wao.
Asha
Babaa, mbona Dr Slaa ameeleza kuwa ametengua uteuzi wao kutokana na wao kukiuka maadili na utendaji kutokana na matamashi waliyoyatoa kwenye vyombo vya habari?
Asha
Shukran sana kwa kunifumbua macho sikuliona hilo.. haya huyu Jamaa alichokisema ni kipi haswa! maanake sikumsoma...au nacho ni siri!
Matamshi gani hayo waliyotoa?
Je ina maana kila anayetoa matamshi tofauti na Mwenyekiti/Katibu inabidi afukuzwe uongozi/uachama?
Walipewa onyo kabla au adhabu yao haina onyo?
Something is definitely wrong here. Zitto tungeomba na wewe utupe maoni yako maana hapo awali ulitupa mtazamo tofauti juu ya hili suala.
Waberoya,
Kwa ajili ya Tanzania njema usijiunge na Chadema kutafuta cheo. Jiunge na Chadema kama njia ya uhakika ya kuleta mabadiliko yanayohitajika Tanzania. Ni ushauri tu.
Mkuu maneno haya Ghetto meeting aliyasema wakati kikao kinaendelea Dodoma kuwajadili watu hawa hawa ina maana kulikuwa na makosa kabla ya kikao hicho kuitishwa!...Haya ndio makosa nayotaka kuyasikia maanake kesho kesho kutwa huyu Kafulila anaweza sema vinginevyo.Viongozi wa CHADEMA walikuwa na GHETO Meeting, yaani afisa habari aongee matusi kama haya halafu aachwe?
soma alichozungumza na gazeti la majira, then toa hukumu.Bi.Asha nakusoma sana bibie ila nachojaribu kusema hapa ni UWAZI.. tunahitaji kuweka uwazi pale ambapo panatakiwa hata kama kuna machungu.
Binafsi huyo Kafulila, atakuwa kafulia kweli ikiwa tutafahamishwa madhambi yake ili kesho mtu mwingine asije yarudia lakini pasipo kuyajua inatupa picha tofauti na mawazo mengi yanajengwa kiasi kwamba hata hizi tuhuma hazikutakiwa kuwepo iwapo tu utaratibu huu ungekuwa wazi na huru.
Binafsi nazungumza hivi kwa kuchelea zaidi jinsi Wadanganyika tulivyo, kesho huyo Kafuylila akiamua kuondoa Chadema anaweza kukipata chama hata kisitamanike kwa sababu tu chama kiliamua kuficha ukweli kwa maufaa ya huyo Kafulila au mtu mwingine...
Trust me hoja zangu, hujaribu kufikiria kama mtu aliyeko nje ya chama (out of the box).. na ndipo tunapo tofautiana kimawazo.
kubwa jinga soma na hizo pia, unajua kiongozi wa chama kuwatuhumu wenzake kuwa wanataka kumfukuza uanachama ni jambo kubwa sana , inawezekana huyo Kafulila aliweza ama alishindwa kujitetea pia juu ya hilo. Im trying to think aloud.Chadema sasa hali si shwari waendesha vikao vya siri kuwajadili wanachama
Na Fidelis Butahe
HALI ya kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inaonekana kuyumba baada ya Mwananchi kupata habari kwamba Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe juzi aliongoza kikao cha siri mjini Dodoma kilicholenga kuwajadili baadhi ya wanachama akiwemo mama mzazi wa Zitto Kabwe, Shida Salum.
Habari hizo kutoka ndani ya chama hicho, zilieleza kuwa waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa, Hemed Sabula, John Mrema, Erasto Tumbo, Benison Kigaila, Halima Mdee, Lucy Owenya na Anna Komu.
Habari hizo zilifafanua kuwa Mbowe aliwasilisha ajenda ya kufukuzwa uanachama kwa afisa habari wa chama hicho, David Kafulila, mama mzazi wa Zitto Kabwe, Shida Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na Danda Juju ambaye ni afisa Mwandamizi kwa kuwa wanakichafua chama kwa kuchochea mgogoro kutokana na kuvujisha siri za chama kwenye vyombo vya habari.
Habari hizo, zilieleza kwamba baada ya Mbowe kuwasilisha hoja yake, ilipingwa na wajumbe wa kikao hicho kwa maelezo kuwa, Zitto Kabwe hatakubaliana na jambo hilo na kusisitiza kuwa linaweza kukipasua chama, lakini katika majumuisho Mbowe alisisitiza kuwa hataweza kufanya kazi na Kafulila hivyo alisisitiza kuwa Kafulila apewe barua ya kufutwa uanachama.
Kutokana na kusimamia uamuzi huo, ilidaiwa kuwa wajumbe wa mkutano huo walikubali kwa shingo upande umauzi huo.
Baada ya tarifa hizo Mwananchi liliwatafuta wahusika ambao walikiri kuwepo kwa taarifa za kikao hicho na kusisitiza kuwa wanasubiri kuona kama watapatiwa barua za kufutwa uanachama au la.
"Mimi hizo taarifa nimezisikia na nilikuwa najua kuwa kulikuwa na kikao kisicho rasmi kilichokaa Dodoma ila mpaka sasa sijapata barua yeyote, nasikia kuwa wanataka kunitimua uanachama, lakini ngoja tusubiri tuone wakinipatia barua kila kitu kitakuwa wazi," alisema Kafulila ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kuwania Ubunge mwaka 2010 Kigoma Kusini
Kafulila pia aliwahi kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama hicho, (Bavicha) katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa Agosti mwaka huu, lakini mshindi hakupatikana baada ya mpinzani wake, John Heche kupinga matokeo kwa madai kuwa kura 20 zilikuwa zimeongezeka.
Naye Danda Juju alisema taarifa hizo, amezisikia ingawa hana uhakika nazo na kusisitiza kuwa kwa kiasi fulani anaweza kuziamini kwa kuwa alikuwa na taarifa kuwa Mbowe anafanya kikao kisicho rasmi mkoani Dodoma. Mama mzazi wa Zitto, Shida Salum hakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hilo.
Wakuu zangu, Mimi sidhani kama kuna mgogoro kati ya Zitto na Mbowe.. Haukuwepo toka miaka yote ile isipokuwa kuna watu ndio wanachonga ili mradi tu kuharibu ukaribu wa Zitto na Mbowe..
Nijuavyo mimi Zitto na Mbowe wapo karibu zaidi ya mtu mwingine yeyote Chadema nje ya maswala ya chama yaani kuna urafiki na ushikaji. Hilo linaweza pia kuwa sumu kwa baadhi ya watu.
Hizo ni Wishfull thinking, hiyo Mimba imesubiriwa sana lakini hamna mtoto, kama mafisadi wameamua kutungisha Mimba then sperm count zao ni chacheMimba haifichiki, muda wake utakapofika kichanga kitajitokeza tu, hata kama wahusika wakisingizia ubikira.
Mazingaombwe gani mkuu?Kama Kafulila kaachishwa uongozi kwa sababu za kimazingaombwe za Mbowe, basi tusubiri tu tuone hii mimba inayokataliwa kuwepo itaishia wapi? Yetu macho lakini wachawi wetu tushawaona kutokana na historia ya migogoro ndani ya CHADEMA.
Hamna lolote mnajifanya mnampeeenda Zitto! Roho inawauma kwa sababu lengo lenu halitimii, mnataka mkimalizana na Zitto na Mbowe mje kwa Zitto na Slaa! Ha ha ha Janja ya Nyani kula Indi bichiMbowe na Mzee Mtei ndio wachawi. They have to go if the party is to progress.