Sakata la Escrow: Kigogo wa Ikulu (Shaaban Gurumo) ahojiwa na Baraza la Maadili

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,023
144,381
Baraza la Maadili leo limeendelea kuhoji viongozi wa umma wanaotuhumiwa kupata mgao wa fedhza kutoka katika akaunti ya Tegeta Escrow ambapo leo hii mtumishi wa Ikulu,bwana Shabani Gurumo nae amehojiwa.

attachment.php

Mnikulu wa Ikulu, Shaban Gurumo akitoa utetezi wake mbele ya Kamati ya Maadili ya Watumishi wa Umma

Akijitetea Mnikulu huyo bwana Gurumo, alikiri kupokea sh milioni 80 kutoka kwa bwana Rugemarila lakini alidai kuwa amekuwa na mahusiano ya kijamii na bwana Rugemarila kwa karibu miaka 10 na amesema anadhani bwana Rugemarila alimuwekea fedha hizo katika akaunti yake iliyokuwa Mkombozi bank kama msaada wa matibabu kwani alikuwa na mgonjwa wa kansa.

Bwana Gurumo alisema alifungua akaunti hiyo katika benki ya Mkombozi kama alivyotakiwa kufanya hivyo na bwana Rugemarila na mpaka mwezi December mwaka jana alikuwa ameshatoa kiasi cha shilingi milioni 70.

CHANZO: Channel 10/Star tv

My take:
Hivi kweli inaingia akilini mtu kusema eti "anadhani" bwana Rugemarila alimpa fedha hizo kwasababu tu alikuwa na mgonjwa wa kansa?!!

Utetezi kama huu unaweza kweli kutolewa na "mnikulu" wa Ikulu?

It is a very pathetic excuse!

MAJIBU tata ya Mnikulu, Shabani Gurumo mbele ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yalizua mshangao kwa wananchi waliokuwepo.
Pia utetezi huo ulizua mvutano mkubwa kati ya Gurumo na wanasheria wa sekretarieti ya maadili, kwa upande mmoja, na pia mvutano kati ya wanasheria hawa na wakili wa Gurumo, kwa upande mwingine.

Mwanasheria: Majina yako kamili ni yapi kiongozi?

Gurumo: Naitwa Shaban Rajab Gurumo.

Mwanasheria: Kiongozi, unaweza ukaliambia Baraza hili unafanya kazi gani?

Gurumo: Kazi yangu ni mnikulu. Nasimamia watumishi wote wa ndani ya Ikulu; nasimamia ukarabati wa majengo yote ya Ikulu; naratibu ikulu ndogo zote nchini; napokea mabalozi wapya kutoka nchi za nje; na ninaandaa tafrija zote za ikulu zinazomhusisha rais.

Mwanasheria: Kiongozi, akaunti namba 00110102645401 iliyofunguliwa Benki ya Mkombozi 04 Februari mwaka 2014 ni ya nani?

Gurumo: Akaunti hiyo ni yangu. Niliifungua baada ya rafiki yangu James Rugemalira kunielekeza nifungue akaunti katika benki hiyo?

Mwanasheria: Kiongozi, tarehe 05 Februari 2014 akaunti hiyo ilipokea shilingi 80,850,000. Hiyo fedha ni mali ya nani?

Gurumo: Hiyo fedha ni mali yangu halali.

Mwanasheria: Kiongozi, hiyo fedha ulipewa na nani?

Gurumo: Nilipewa na rafiki yangu aitwaye James Rugemalira.

Mwanasheria: Kiongozi, wewe na James Rugemalira mlifahamiana vipi na tangu lini?

Gurumo: Sikumbuki vizuri. Lakini nadhani nilimfahamu tangu zamani kupitia daktari wa familia yangu aitwaye Fred Limbanga, ambaye nimekuja naye hapa leo kama shahidi.

Mwanasheria: Kiongozi, kwenye nakala ya Ankara za benki uliyowasilisha katika ofisi za sekretarieti ya maadili inaonekana fedha hizo zilitoka kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd na sio kwa James Rugemalira. Unasemaje kuhusu jambo hili?

Gurumo: (Anatazama nakala ya ankara kwanza). Ndio leo nimeligundua jambo hili. Hapo kabla sikuwa nimechukua muda kuisoma ankara hii. Muda wote nilijua fedha zimetoka kwa James Rugemalira.

Mwanasheria: Kiongozi, hiyo fedha ulipewa kwa ajili gani na ziliambatana na masharti gani?

Gurumo: Sikuambiwa ni kwa sababu gani na hakuna masharti yoyote niliyopewa kuhusu matumizi yake. Naomba akaulizwe James Rugemalira.

Mwanasheria: Kiongozi, James Rugemalira alikuingizia fedha hizo kwa sababu uliziomba au hapana?

Gurumo: Sikumwomba James Rugemalira fedha. Na sijui kwa nini aliniwekea fedha hizo. Hata aliponiambia nifungue akaunti benki ya Mkombozi ili aniwekee fedha sikumwuliza fedha hizo ni za nini. (Kicheko kutoka kwa wananchi).

Mwanasheria: Kiongozi, kwa sasa karibu fedha yote umekwisha kuitumia. Uliitumia katika mambo gani na kwanini?

Gurumo: Niliitumia katika matumizi mbalimbali yakiwemo matibabu ya ugonjwa wa kansa uliokuwa unamsumbua mke wangu.

Mwanasheria: Kiongozi, fedha hizo ambazo umekiri ni mali yako, uhalali wake unatokana na nini. Ni mshahara, posho, faida katika biashara, urithi, kuokota, zawadi au kitu gani?

Gurumo: Sio mshahara, posho, faida katika biashara, urithi, au zawadi. Pia hazikuokotwa. Ni fedha nilipewa tu. (Kicheko kutoka kwa wananchi).

Mwanasheria: Kiongozi, unawezaje kutumia fedha nyingi kiasi hicho bila kwanza kutafiti sababu fedha hizo kuingizwa katika akaunti yako?

Gurumo: Sikuwa na hofu yoyote kwani James Rugemalira ni rafiki yangu kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

Mwanasheria: Kiongozi, kwa mujibu wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma, umewahi kutoa taarifa ya fedha hizi kwenye sekretarieti ukionyesha kwamba ni miongoni mwa mali yako mpya?

Gurumo. Tayari. Nilifanya hivyo tangu 29 Desemba, 2014 kupitia fomu maalum. Fedha hizi zimetajwa kwenye ukurasa wa kumi na saba. (Anaonyesha nakala ya fomu aliyoijaza).

Kwa upande wake, Gurumo alisema neno hilo halina fasili rasmi katika sheria za Tanzania. Lakini, wanasheria wa shekretarieti walikuwa na maoni tofauti.

Walisema, "Gurumo amekiri kwamba fedha zile ni mali yake. Mali inaweza kupatikana kupitia mshahara, posho, biashara, urithi, kuokota, au zawadi. Gurumo amekanusha yote haya. Kwa hiyo fedha hizo anazimiliki kwa mujibu wa kanuni gani?," walihoji.

"Fedha zile alizipokea kama zawadi na kinyume cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma na atatiwa hatiani na Baraza," walihitimisha.
 

Attachments

  • Shaban Gurumo.jpg
    Shaban Gurumo.jpg
    26 KB · Views: 3,328
Pia taarifa hiyo imesema wataitwa tena tarehe 13 ili kutoa hukumu
 
nimeona chanel 10,jamaa ana jeuri sana,amesema alikuta ml 80 kwenye ac yake akaanza kuitumia,hakuona haja ya kujua kapewa za nini na mwenye kutaka kujua hilo amfuate Rugemalila!
 
Ukituhumiwa lazima uhojiwe siyo vinginevyo then ukweli utafahamika.
 
nimeona chanel 10,jamaa ana jeuri sana,amesema alikuta ml 80 kwenye ac yake akaanza kuitumia,hakuona haja ya kujua kapewa za nini na mwenye kutaka kujua hilo amfuate Rugemalila!

Ana kiburi kwasababu alitumwa na mkulu.
 
Pia taarifa hiyo imesema wataitwa tena tarehe 13 ili kutoa hukumu
Msaada tafadhari kwani hao Maadili na utumishi mipaka yao ni ipi, namanisha kama wahusika watapatikana na hatia watachukuliwa hatua gani.?
 
Chadema mnamiliki kiwanda cha kutengeneza uongo

Unaishi katika pori gani wewe au waajiri wako wa lumumba wamekuondoa akili? Maana unabisha hadi mambo halisi. Na kama ni maagizo ya waajiri wako wa buku saba per day basi wamekuvuruga vibaya huwezi rudi katika hali ya kawaida hata ukipelekwa india kwa matibabu
 
Back
Top Bottom