ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,115
- 49,837
Wakati mjadala wa uhalali wa mkatabva wa uwekezaji katika bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ukiendelea, Mwandishi nguli nchini Jenerali Ulimwengu, amesema Serikali imepoteza imani ya wananchi.
Mwandishi huyo nguli anaibua hoja hiyo wakati watanzania na wadau mbalimbali wamekuwa wakiupinga mkataba huo wa uboreshaji wa bandari wakisema, una harufu ya unyonyaji kwa kile walichobaini mkataba huo hauna ukomo na umekiuka sheria za nchi.
“Tanzania ni moja, haigawanyiki wala haiuziki. Kwa hiyo ndugu zangu mama ni Mtanzania, maendeleo yetu ndiyo muhimu, kila linalofanyika ni kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania,”amesema Rais Samia mara baada ya kuwasili mkoani Mwanza Juni 14 kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo.
Kwenye mjadala ulioendeshwa leo Juni 19,2023 na Taasisi ya Media Brains jijini Dar es Salaam, ukijadili “Kulinda na kuendeleza umoja wa kitaifa wakati wa mageuzi ya kisiasa na kiuchumi”
Ulimwengu amesema kutokana na usiri ambao umekuwepo wananchi wana haki ya nini kimetokea.
Amesema kwa watu wanaofikiri vizuri na kudodosa mambo Serikali haina ‘Trust’ kubwa ya wananchi. “kuna mtu mmoja alimkaribisha ndugu yake chakula cha mchana akamwambia atamchinjia jogoo, yule bwana akaenda anajua anachinjiwa jogoo bahati mbaya ana ulemavu wa macho haoni, Akaingiza mikono kwenye bakuli akagusa mguu wa kwanza na wapili akasema, yeye kipofu amepewa viwili wao wamekula vingapi,”amesema.
Akizungumzia suala la ubinafsishaji amesema hakuna ukinzaji wa moja kwa moja kati ya ubinafsishaji na utaifishaji kama wale ambao wanachukua mali chini ya Serikali ni raia waliopo ndani ya taifa husika.
Hoja hiyo imekuwa ikipingwa na Serikali huku ikisema huo ni upotoshaji kwani mkataba uliosainiwa ni wa msingi nab ado mikataba ya utekelezaji huku Rais Samia Suluhu Hassan akienda mbali zaidi kujibu kauli za wanaodai Serikali inauza bandari akisema bandari haiuzwi.
Maana yake mali itakuwa imetoka kwenye mikono ya serikali na kuingia kwenye mikono ya wananchi na hiyo ndio maana ya shirika la umma, Ili mashirika yawe ya umma yapewe umma ambao ndio wananchi wenye nguvu ya kufanya kazi na kuendeleza nchi yao kwa mali walizopata.
Amesema suala la uwekezaji wa bandari ya Tanzania si suala la kukataa au kukubali bali ni aina ya uwekezaji unaotakiwa kufanyika.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Kanisa Katoliki Tanzania TEC Padri Dk Charles Kitima amehoji pamoja na aina mbalimbali za uwekezaji uliowahi kufanyika nchini ni kwanini sasa uwekezaji wa bandari unapigiwa kelele…?.
Chanzo: Mwananchi
===
My Take
Serikali achaneni na hili suala, Wadanganyika hawataki regardless of how important privatisation is!