SAKATA LA DOWANS: Wanasheria wamuunga mkono Jaji Bomani

SAKATA LA DOWANS: Wanasheria wamuunga mkono Jaji Bomani

hao wanasheria nguli ambao wanaogopa majina yao kutajwa ni nguli kweli au njaa/minyoo ya tumbo! Ebu watuwekee hapa hiyo hukumu nasi tuisome, ili nasi tutoe mawazo ya uchanga wetu. Kwa kuangalia mantiki ya Rich monduli ilivyokuja kisha hili li-muzimu la Dwans, hahitaji cheti cha sheria ili kuweza kupitisha maamuzi ya kutomlipa huyo zimwi.
Acha wakasajili, huko nje ya nchi na wakamate chochote watakachokamata, kuliko kulipa kwa kuridhia. Haya malipo nina imani hata shetani anashangaa kwa nini tumlipe huyo zimwi na mazingira yake yote, yaliyokwisha jidhihirisha kuwa ni ya kizimwi zimwi; labda nyiye wanasheria msokuwa na majina mtusaidiye kuelewa mantiki ya hili suala ili tuweze kusheherekea hii move ya malipo.
 
Jaki angezingatia kwanza uhalali wa Dowans kisheria. Then atoe maoni yake baada ya kueleza ukweli huo. Otheewise hana tofauti na Ngeleja . Tunajua hata hao wahusika walitumia sheria hizo hizo ammbazo anadai ana uzoefu nazo
 
Turejeeni kauli ya Mkulo kuhusiana na kutokuwa na fundu la kuwalipa Dowans. Walioshitakiwa ni Tanesco waache wao wawalipe matapeli/wezi wenzao na kama hawana fedha za kufanya hivyo basi mahakama itoe ridhaa ya mali zao kukamatwa na/au kuuzwa ili "deni" hili la kitapeli lilipwe. Nitafurahi sana kuona timu yote wa uozo pale Tanesco na Wizara husika zikiwekwa ndani, Tanesco kufilisiwa ili tujue moja. Sijawahi kuona shirika kero kama hili, ni vyema life.


You're kidding yourself, it's you who pay through electric bill, not TANESCO.
 
Hivi Sheria iliposema watu weusi hawana haki ya kupiga kura kwanini kina Martin Luther King na wenzake waliipinga? Pale Sheria ilipowatenganisha watu weupe na weusi kule Afrika ya Kusini kwanini kina Mandela walipinga wakati ilikuwa ni sheria kweli? Hivi uhalali wa kutii sheria unatokana na kuwa ni kwa "vile ni sheria imesema" au kutokana na kitu gani? Maana kama sheria ikisema tu basi tusihoji - sijui ni nchi gani ingepata uhuru!
 
Swali la Msingi la Kujiuliza: Nchi hii ina wanasheria?
Nchi imejaa wanasheria wazuri tu ila wengi wao wana ugonjwa wa kufikiri ki CCM CCM kama Bomani. Utamwambia nini Bomani wakati yeye ni mmoja wa 'Walezi' wa chama ambacho kwa dalili zilizopo kiini macho hiki cha Dowans kinalenga kukinufaisha?
Hapa kuna pendekezo; kama kweli malipo ya Dowans hayaepukiki kisheria, wahusika woote wa Richmond, Dowans na takataka zake wafikishwe kwenye Mahakama maalum itakayoundwa ambapo hukumu ya juu itakuwa kifo.
Mimi naona ni salama kuwaondoa duniani wahalifu wachache ili kuinusuru nchi na madhara wanayoisababishia sasa na kwa vizazi vyetu vijavyo.
 
kuna post iliandikwa hapa jf tukawa tunajiandaa kupata maoni ya huyu mzee na ndivyo ilivyokuwa wajameni na bado wengi watajitokeza sana kutetea haya kwa sababu rostam aziz ameshawapa ulaji
 
Wote hawa wamestaafu wanakula pesa ya walipa kodi na JK ndiye msimamizi wanaogopa mafao yao yatakatwa hakuna madhara yoyote tutakayopata. Ikumbukwe nchi kama China, nk miaka 20/30 iliyopita zilikuwa zinapigwa vita sana hivi sasa zipo juu sana wasitutishe hawa vilaza. Tatizo lililopo ni kwamba Dowans ni mali ya rais Mwizi.
 
Guys kuwa na hasira, kuwaita watu vibaraka haisaidii kitu, na ukiangalia thread nzima hamna any professional input ya sheria, bali politics.

Sheria ni professional wote tunajua, na kamwe si kila mtu ni wakili au hakimu!!sheria ni sheria na ndio maana kuna mahakama

kama mtu ulizaliwa dunia hii na kuzikuta system za kidunia zinafanya kazi basi sheria ni system iliyopo tena very active kuliko engineers or doctors.

System za sheria kwa ujumla wako ziko KIONEVU, HAZIJALI MASLAHI, NDIYO UTAKUTA WATU WAKO RADHI KUTETEA JAMBAZI AN AKASHINDA KESI

UKIENDA KWENYE SYSTEM ZA MAHAKAMA NA SHERIA UTAKUTA HAKI kama Haki ya kweli ni asilimia 5 ya matokeao yote ya kisheria

Dowans is not first time!! jamani kuna kesi kibao wanafungwa innocent na kuachiliwa majambazi, chengemmeona JUZI

Mark Bomani anavyosema kisheria wako sahihi kabisa, japo tunajua sheria hizo hazileti HAKI!!! the argument here should be more pholosophical and not JUST eti ''amepewa hela na Rostam ili kumtetea'' what a childish argument!!! simply tuonekane tuna hasira na Dowans!!

kazi ipo!!
 
kuna post iliandikwa hapa jf tukawa tunajiandaa kupata maoni ya huyu mzee na ndivyo ilivyokuwa wajameni na bado wengi watajitokeza sana kutetea haya kwa sababu rostam aziz ameshawapa ulaji

nyie ndio mnaharibu jamvi! wamepewa ulaji wangapi sasa?? jengeni hoja na sio vihoja, YAANI UMEFUNGUA JAMII FORUMS NA KUJA KUSEMA BOMANI KAPEWA FEDHA NA ROSTAM!!! umemaliza! where is your intelectual inputs???
 
Nchi imejaa uchafu kila upande. Bidhaa zinachakachuliwa, wasomi wanapatikana kwa uchakachuaji, viongozi nao wanapatikana kwa uchakachuaji na wananchi wa ujumla wanaishi kwa kuchakachua. Hao wanaojiita wanasheria lazima degree zao zilichakachuliwa ndiyo maana wanongea mambo ya aibu.

.
 
Tunapoelekea naomba wazee wapumzike.kwa aman wasijishushie heshima, watuachie vijana tuamue kuhusu taifa letu..

Hawa jamaa wananukuu gazeti gani? Nina wasiwasi kwamba hili ni gazeti la fisadi RA
 
Wakishika mali zetu nje na sisi si tunashika zao hapa? After all na wao wamewekeza kwetu huku. Wasitutishe bana. Tena tutaanza kwa kushika za Rostam Aziz. Ajaribu aone. Tutatumia upalestina.
 
Kadiri muda unavyokwenda ndivyo ukweli unaendelea kuonekana. Tatizo letu watanzania ni kuwa tunaongozwa na fikra za watu wengine bila kufikiri kwa kina. Suala la kulipwa Dowans halikwepeki. Mh Zito alipoeleza madhara ya kutokulipa mkambeza sana. Leo wataalamu wa sheria wanapita mulemule mnakejeli nao hao pia. Sijajua vyuo mlivyosomea. Si kila mtu ana haki ya kusema chochote hata kama sio taaluma yake?. Pale makamba aliponukuu vifungu vya Biblia maaskofu wakasema hana haki hiyo nanyi mkawasapoti. Leo ndio nyie haohao mnaosema mambo ya kisheria wakati taaluma hiyo hamna. Ajabu kweilikweli? Hao ndio intellectuals wa kibongo. Domo kaya.
Halafu mwisho wa siku Tunalipa! Viumbe wa ajabu sana! Hivi ni nani ametuloga?
I hate to deal with intellectual fools! Mlikuwa wapi wakati Bunge linashauri Serikali ivunje Mkataba miezi mitatu kabla haujaisha???
Kama nilivyosema humu ndani ya JF muhimu ni kulipa.
 
Back
Top Bottom