SAKATA LA DOWANS: Wanasheria wamuunga mkono Jaji Bomani

SAKATA LA DOWANS: Wanasheria wamuunga mkono Jaji Bomani

Ni sheria gani hizo zisizo na maadili wala haki ambazo Justice Bomani anadhani zinastahili kutekelezwa?

Dowans kama Richmond ni aibu kwa Tz.

Mbona asitie shinikizo wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Africa Mashariki wanaodai haki zao miongo kadhaa saas, tena wengi ni wagonjwa na wengine wamefariki, walipwe?

Sheria za Tz zinasemaje juu ya madai halali ya wallimu, wauguzi, madaktari nk ambayo yana miaka meingi yakipigwa dana dana kutekelezwa na serikali il-hali mahakama zilshatoa hukumu?

Ni kwa nini Dowans inatakiwa ilipwe fasta?

Mbona Justcie Bomani, mnachagua na kubagua wakati gani na vipi mtekeleze sheria fulani kwa watu fulani? ?

Ungenyamaza labda ungehifadhi heshima kidogo.
 
Hao wastaafu nao inabidi waanze kuzikamata Mali za serikali na kuzipiga mnada labda itawalipa mapema maana Mali kukamatwa ndo kitu kinachoogipewa sana na watetezi wa Dowans!
 
Hii story ni ya uongo. Ni ya kupikwa kabisa, wanasheria gani hao "Wakizungumza na gazeti hili kwa sharti la majina yao kutoandikwa." Huu ni uongo kabisa, wanasheria gani wasijiamini mpaka watake majina yao yasitajwe. Wanaficha nini? Ni dhahiri kuwa hii story ni uongo mtupu.

Imeelezwa kwenye thread nyingine kuwa Rostam Aziz amepanga kutumia vyombo vya habari kueneza propaganda ili kuwatisha serikali wailipe Dowans haraka kable ya kikao cha Bunge cha Februari. Hii story ya kupikwa ya Majira na nyingine zitakazotoka kwenye magazeti mengine ni ushahidi wa njama hizo za Rostam.

 
Huyu Jaji Bomani ni retired AG. Ana interest gani na malipo ya Dowans yeye akiwa kama mstaafu mpaka ajidai kuwa kasoma kwa makini hukumu ya ICC na sheria za nchi na kuona kuwa serikali lazima iwalipe Dowans. Kazi zake Serengeti Breweries, TEITI, uwakili binafsi na biashara zake zote hizo anapata wapi muda na motivation ya kufuatilia suala la Dowans na kutoa unsolicited legal advice?

Kwanza nani alimpa huyu retired AG hiyo hukumu kamili ya ICC, maana so far it has not been made public mpaka ipelekwe Mahakama Kuu. Ni vipande tu vya hukumu ya ICC ndiyo vimewekwa humu JF na kwingineko.

Jibu ni rahisi: Jaji Mark Bomani yuko kwenye listi ya watu waliopewa rushwa na Rostam Aziz ili kutetea malipo kwa Dowans. Tusubiri wengine wengi watajitokeza. Maadili nchi hii kwa wastaafu na walio serikalini hakuna kabisa kutokana na njaa kali walizokuwa nazo. Rushwa imeshamiri kila kona.
 
Huyu Jaji Bomani ni retired AG. Ana interest gani na malipo ya Dowans yeye akiwa kama mstaafu mpaka ajidai kuwa kasoma kwa makini hukumu ya ICC na sheria za nchi na kuona kuwa serikali lazima iwalipe Dowans. Kazi zake Serengeti Breweries, TEITI, uwakili binafsi na biashara zake zote hizo anapata wapi muda na motivation ya kufuatilia suala la Dowans na kutoa unsolicited legal advice?

Jibu ni rahisi: Jaji Mark Bomani yuko kwenye listi ya watu waliopewa rushwa na Rostam Aziz ili kutetea malipo kwa Dowans. Tusubiri wengine wengi watajitokeza. Maadili nchi hii kwa wastaafu na walio serikalini hakuna kabisa kutokana na njaa kali walizokuwa nazo. Rushwa imeshamiri kila kona.

Kwani wewe ulipata wapi nafasi ya kuisoma au huna kazi?
 
Ninaamini kuwa mtu wa tatu au serikali ina haki ya kupinga uamuzi huu. Kama nilivyosema katika kipindi cha Kipima Joto kuna nafasi ya kisheria ya kupinga uamuzi huu kwani ulifikiwa kinyume cha sera za kitaifa ambazo zinazuia unyonyaji. Hivyo maoni ya Mzee Bomani na hao Wanasheria ambao hawataki kutajwa majina yao si sahihi. Nilichofanikiwa kukipata ni kuwa hata yule aliyepewa jukumu la kumshauri Mwanasheria Mkuu kama serikali ingeweza kukata rufaa ni mtu wa karibu wa Rostam. Hivyo jibu lilikuwa ni dhahiri.
 
Kwani wewe ulipata wapi nafasi ya kuisoma au huna kazi?

You are missing the point. Jaji Bomani anajidai ana all the facts za hukumu ya ICC wakati it is not in public domain. Yeye ni mstaafu, amepata wapi access ya hiyo hukumu na huo muda wa kuisoma na kupitia sheria za Tanzania then akafanya ruling yake yeye kama jaji kuwa serikali lazima iwalipe Dowans. Bomani kawekwa sawa na Rostam tu.
 
Watanzania kwa blah blah! kweli ndio wenyewe; nina uhakika 2015 bado tutakuwa tunajadili Dowans.
 
hii story ni ya uongo. Ni ya kupikwa kabisa, wanasheria gani hao "wakizungumza na gazeti hili kwa sharti la majina yao kutoandikwa." huu ni uongo kabisa, wanasheria gani wasijiamini mpaka watake majina yao yasitajwe. Wanaficha nini? Ni dhahiri kuwa hii story ni uongo mtupu.

Imeelezwa kwenye thread nyingine kuwa rostam aziz amepanga kutumia vyombo vya habari kueneza propaganda ili kuwatisha serikali wailipe dowans haraka kable ya kikao cha bunge cha februari. Hii story ya kupikwa ya majira na nyingine zitakazotoka kwenye magazeti mengine ni ushahidi wa njama hizo za rostam.

hata humu jf ra ameingiza mamluki wengi sana ili kukatisha tamaa watu wasijadili kutoilipa dowans. Kazi ipo nguvu ya umma na mafisadi
 
Swali la Msingi la Kujiuliza: Nchi hii ina wanasheria?

Ndugu yangu Tanzania ina wanasheria wengi sana waliobobea kwenye taaluma yao, lakini wengi wao ni wezi kupindukia yaani ni wezi mno. Wanashirikiana na wageni kuihujumu nchi. Mikataba yoote mibovu, kuanzia mikataba ya madini, umeme na mingine mingi, wanasheria wetu ndiyo waliohusika kuiandika. Pia huwaambia wageni sheria zetu zina mapungufu (lacuna) sehemu gani na kiasi gani. Halafu wana tumia mianya hiyo kuhujumu watanzania wenzao. Wanasheria wetu hawana uchungu na uzalendo hata chembe kuelekea nchi yao. Mikataba yote mibovu imesukwa na wanasheria wa nchi hii.
Lo, ni huzuni kweli na inauma sana.
 
Inaonekana kuna list ndefu sana ya watakaofaidika na malipo HARAMU kwa DOWANS . Nahisi hata mzee Bomani yupo kwenye listi kwa hiyo anaona serikali inachelewesha kulipa akaona aihimize kulipa kwa kupitia mgongo wa kutoa ushauri au maoni kwa serikali. Hii habari ya wanasheria kumuunga mkono kwa kuficha majina imetungwa tu (maana sidhani kama wapo wanasheria wa aina hiyo) katika jitihada ya kuhalalisha malipo. Kweli RA ni kiboko ya Tanzania maana ana uwezo wa kumnunua yeyote ili mradi afanikishe masilahi yake.
 
Hii stori imeandikwa na Gazeti gani?
Hawa jamaa kwa nini wao hawataki majina yao yatajwe? Isije ikawa mwandishi kaaamua kujitengenezea habari na yupo kwenye account ya malipo ya fadhila ya RA na mafisadi wengine

Dowans yenyewe ina utata wa uhalali wake achilia mbali Richmond ikumbukwe yule mwarabu alikiikana


Mie pia nina mashaka na habari hii. Kama kweli mwandishi angeongea na wanasheria isingewezekana wote waunge mkono upuuzi huo wa Bomani. Nahisi mwandishi ametumika tu kutengeneza habari hii kwa manufaa ya mafisadi. Huwezi kuandika habari sensitive kama hii halafu ukajifanya eti wanasheria ambao hawakutaka majina yao yaandikwe. Sijui huyo mwandishi ameenda chuo gani cha uandishi wa habari? Najua RA amekuwa akitumia kila hila kuhakikisha anapata support ktk kuhakikisha malipo ya Dowans yanafanywa haraka. Sitashangaa kusikia baadhi ya waandishi wa habari nao wanatumika.
 
Kwa nini hawataki majina yao kuandikwa kama wanaongea ukweli hao wanasheria? Wana ficha nini?


Hakuna mwanasheria anayeweza kuchangia suala nyeti kama hilo akakataa kutaja jina, hao waseme wameichakachua hiyo stori kuaccomodate malalamiko ya Mzee Bomani, inaonekana alikasirishwa na maneno makali waliyoyatumia katika habari ya kwanza sasa wanawazuga watanzania. Ukiisoma hiyo habari ni sawa Majira wanamsafisha Mzee Bomani-hakuna uandishi siku hizi wamejaa wahandisi wa habari tu katika newsrooms.

Hakuna kitu muhimu kama sourcing katika habari. Unahoja eti wanasheria kadhaa jijini Dar es Salaam halafu wote wakatae kutajwa majina-kitaaluma hao wote wasingepaswa kuhusishwa katika habari kwa sababu hapo hakuna suala la kuficha nyuso zao (kama ni kweli walihojiwa).
 
huyu mzee amesha UZA na KUOZA nafsi yake, si mzalendo ni fisadi affiliate, associate & beneficiary too, hana lolote
wale wale wakina Chenge, Werema, he has no reputation infront of TZans eyes anymore
 
Hii stori imeandikwa na Gazeti gani?
Hawa jamaa kwa nini wao hawataki majina yao yatajwe? Isije ikawa mwandishi kaaamua kujitengenezea habari na yupo kwenye account ya malipo ya fadhila ya RA na mafisadi wengine

Dowans yenyewe ina utata wa uhalali wake achilia mbali Richmond ikumbukwe yule mwarabu alikiikana

Gazeti lenyewe lisije likawa Habari Leo jamani!!!!! Na huyu mzee naye si apumzike atuachie nchi ituozee wenyewe? Maana yeye muda uliobaki ni mfupi kuliko muda alioishi, hivyo ni busara zaidi kama angenyamaza kimya kabisaa!!!!!!! Hawaoni wenzake kina Nkapa wametulia kimya kama maji mtungini!! Tunamwomba sana anyamaze, mbona wanasheria wenzake wazoefu kama akina Sitta wanasema DOWANS tusiwalipe kwa vile ni kikundi cha wajanja wachache wanataka kutuibia na wanacheza na makaratasi ili kufanikisha wizi huo??
 
Hivi ukijiuliza DOWANS mliki wake ni nani kisheria na kimajina?(achilia mbali akina EL,RA,JK n.k tunao wajua katika nafsi zetu)
-Serikali inasema ni Costorica jamaica na Singapore!Ripot ya Mwakyembe inasemaje kuhusu DOWANS costorica Jamaica?(Haipo)
-Richmond si ni kampuni hewa kwa mujibu wa bunge?ika iuziamitambo kampuni hewa ya DOWANS!
Ni nani(mtu) alisimama kizimbani kuitetea Dowans?Hivi serikali kwanini inatudanganya hivi?
-Dowans ni jina la kampuni!Meneja,mkurugenzi na wamiliki ni akina nani mbona hamtutajii?
-JAJI MAKIBOMANI hayaoni haya?
@Ilikupata hao watu wa Dowans costorica na Singapore tusiwalipe iliwajitokeze hadharani kudai haki yao..Ili tujue sura zao.
-Hizi kesi za makaratasi ni unyonyaji wa haki za watanzania.
 
Huu ni ukikwaji wa maadili kwa jaji Mkuu kstaafu kuanza kuongelea mambo ambayo tayari yanaelekea Mahakamani. Uhuru wa mahakama zetu unamkataza mheshimiwa huyu kutoa maoni ya aina yoyote yale yanayoashiria kuweka mashinikizo kwa mahakama zetu kuaamua jinsi yeye atakavyo..........................................
hawa wazee ndio maana Nyerere alianza kuwatosa mwishoni mwa uhai wake,wanasheria wantunia sheria kuua haki,sheria zinatungwa kwa nia nzuri lakini wajanja huzitutumia vibaya na kuhalalisha mabaya hayo kuwa halali
 
Najiuliza, mbona wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki hawalipwi na hatusikii watu wakiwatetea? Au hawajatushika pabaya? Mbona Vambai hakulipwa? Yeye alitushika pazuri? Mbona walimu hawalipwi mishahara na mafao yao? Tumewashika pazuri?

Ni vyema mahakama ikaachiwa kuamua. Hilo suala limeshafikishwa mahakamani na mtu yeyote anayejiita mwanasheria atatambua umuhimu wa kutokuongelea masuala ambayo yako mahakamani! Jaji na mahakama ni vitu viwili tofauti!
 
Back
Top Bottom