SAKATA LA DOWANS: Wanasheria wamuunga mkono Jaji Bomani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SAKATA LA DOWANS: Wanasheria wamuunga mkono Jaji Bomani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 18, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,794
  Trophy Points: 280
  *Wasema Hoja zake zimezingatia sheria si porojo za siasa
  *Wakerwa na wasomi wanafunzi kubeza maoni yake


  Na Mwandishi Wetu

  SIKU moja baada ya waliojiita wanafunzi wa kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, Profesa Mwesiga Baregu kupinga maoni ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Mark Bomani kuhusu malipo ya Kampuni ya Dowans, wanasheria kadhaa jijini Dar es Salaam wamemuunga mkono na kusisitiza kuwa maoni hayo ni sahihi kwani yamezingatia mtazamo wa kisheria.

  Wakizungumza na gazeti hili kwa sharti la majina yao kutoandikwa, wanasheria hao kwa nyakati tofauti jana walisema kwa mujibu wa sheria, kauli ya Jaji Bomani katika mahojiano maalum na gazeti hili juzi ni sahihi na kwamba alitumia uzoefu wake kisheria na huo ndio ukweli kuhusu malipo hayo.“Ukiangalia ukweli wa kisheria hoja zote alizozungumza

  Jaji Bomani kuhusu uhalali wa malipo ya Dowans na madhara yanayoweza kuikumba nchi endapo itakataa kulipa ni sahihi. Mimi kama mwanasheria mzoefu namuunga mkono, hawa wanaojaribu kupinga hoja zake
  naamini bado wachanga kisheria.

  Malipo ya Dowans kwa vigezo alivyotoa Jaji Bomani hayakwepeki japo waliohusika katika mkataba lazima wachukuliwe hatua,”alisisitiza mwanasheria mmoja wa kujitegemea jijini Dar es Salaam.

  Alisisitiza kuwa iwapo hukumu ya kesi dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Migogoro ya Kibiashara (ICC) ilitolewa na watu wenye sifa, Tanzania haiwezi kukwepa kuilipa Dowans kwa kutumia mabavu.

  Alishauri Watanzania kuacha ushabiki na kupoteza muda katika suala hilo badala yake watafute ufumbuzi wa tatizo la umeme kwani umeme si suala la kisiasa bali linagusa uchumi na maendeleo ya nchi.

  “Kumshambulia Jaji Bomani si sahihi, hoja alizotoa ni za kitaalamu zenye mtazamo wa kisheria. Maoni ya Jaji Bomani yanapaswa kuheshimiwa kwani kama mtaalamu na mkongwe wa fani ya sheria ana haki kutoa maoni yake kwa kuzingatia uzoefu wake, huyu ni mwanasheria anazungumza kwa kuitazama sheria si porojo za kisiasa,” alisema wakili mwingine jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa sheria ni utaalamu si ushabiki.

  Aliwashambulia waliojiita wanafunzi wa sheria mwaka wa tatu kwa kauli zao dhidi ya Jaji Bomani na kueleza kuwa wamekosa hoja kwani walipaswa kujibu kwa misingi ya hoja alizotoa Jaji Bomani badala ya kutoa majibu yasiyo na mantiki hatua inayoshusha hadhi na usomi wao.

  Naye Jaji Bomani akizungumza na gazeti hili jana, alieleza kusikitishwa na watu wanaomshambulia katika maoni yake kwa kutanguliza ushabiki bila kuzingatia ukweli na mantiki
  ya kisheria.

  “Mimi nilitoa maoni yangu kama mwanasheria mzoefu, Jaji na Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Serikali kwa kuzingatia sheria za nchi na za kimataifa na kwa maslahi ya heshima ya nchi katika jumuiya ya kimataifa. Sikutoa maoni hayo kisiasa kama wengi wanavyofanya. Inasikitisha kuwa tumefikia mahali hata mtu hawezi kutoa maoni yake bila kupachikwa maneno ya ovyo ovyo. Mimi ni mwanasheria ninayeheshimika haijawahi na haitatokea kurubuniwa na mtu yeyote. Inasikitisha sana,” alisema Jaji Bomani.

  Hivi karibuni katika mahojiano yake na gazeti hili, Jaji Bomani alisema kisheria malipo ya Dowans hayakwepeki kinyume na hapo taifa litaingia kwenye matatizo makubwa zaidi.Akaeleza kuwa ni vigumu Mahakama Kuu kutengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC Court) kama hakukuwa na kasoro zozote katika utoaji hukumu hiyo.

  “Kwa kesi za usuluhishi kama hii hukumu hii inaweza kutenguliwa tu kama hao wapatanishi hawakuwa na sifa za kuwa wapatanishi kitu ambacho hapa hakiwezi kutumiwa kwa kuwa katika suala hili, hawa walikubaliwa na pande zote,” alikaririwa akisema Jaji Bomani na kuongeza;

  “Hukumu hii inaweza kutenguliwa tu kama ikidhihirika kwamba wamepewa rushwa kwa kutoa hukumu ya namna hiyo. Vinginevyo Mahakama Kuu haijihusishi na kuingilia kesi yenyewe.” “Mimi kwa upande wangu kama nilivyokwisha kusema siku za nyuma jambo hili liishe ili mitambo hiyo itumike hapa nchini kuzalisha umeme tuondokane na hali ya mgawo na upungufu wa umeme na hilo ndilo jambo muhimu kwa uchumi wa nchi.

  Jaji Bomani aliyetumikia nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kati ya mwaka 1965- 1976 akirithi wadhifa huo kutoka kwa mwingereza Bw. Roland Brown,alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, haoni sababu za kukwepa kulipa fidia hiyo na kushauri kuwa kilichopo sasa ni kuzungumza na hao wanaodai ili kufikia muafaka wa namna ya malipo hayo.

  Alishauri kuwa kukataa kulipa kimabavu si sahihi hivyo serikali inapaswa kutafakari kwa makini jambo hilo kabla ya kufikia maamuzi.

  Alionya kwamba endapo serikali itatumia mabavu kugoma kulipa na Dowans ikasajili hukumu ya kesi hiyo nje ya Tanzania, kisheria kampuni hiyo inaweza kupewa uwezo kukamata mali za serikali huko ziliko.

  Novemba 15 mwaka jana,Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara ilipitisha hukumu dhidi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuilipa Dowans fidia ya sh. bilioni 94 kutokana na kuvunja mkataba.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,794
  Trophy Points: 280
  Hawa wanasheria wetu ni bomu........vibaya mno sijui hata hizo digrii walipewaje!!!!!!!!!!!............hawajibu hoja hizi za kimsingi na wanabakia kutetea ufisadi..................tena kwa lugha laini zilizosheheni siasa tupu na hakuna hata uchambuzi wowote ule wa mapungufu ya TUZO husika......yaani hata hawaonyeshi ya kuwa hiyo hukumu yenyewe wameisoma kwa sababu hawatoi uchambuzi wa aina yoyote ile...............

  Hoja nne hapa chini ndizo zinabatilisha uhalali wa malipo ya DOWANS nazo ni hizi zifuatazo:-

  a) Watumishi serikalini walipata kibali kutoka kwa Bunge lipi kukubali kuwa TUZO ya msuluhishi haiwezi kuhojiwa na Mahakama Kuu chombo ambacho kinatambuliwa na katiba yetu kuwa ndicho chenye mamlaka ya mwisho katika kutoa haki.

  b) Msuluhishi alipoamua kuhalalisha uvunjwaji wa sheria yetu ya manunuzi kwa kutumia visingizio vya matendo ya kifisadi ndani ya TANESCO, WIZARA MAMA na Ofisi wa Waziri Mkuu wakati wa Lowassa. Swali ni je watendaji hao wako juu ya sheria za nchi hii na hivyo kuwa na uhuru wa kufanya watakavyo?

  c) Msuluhishi kutumia mapungufu ya watendaji ndani ya Mamlaka ya kudhibiti manunuzi kwa kutochunguza kashfa ya DOWANS je ni mwanya wa kuzisigina sheria za nchi hii?

  d) Uhalali wa Richmond ambayo haitambuliki kisheria na kuhamishia miliki ya mkataba wake kwa DOWANS ambao ni batili ni suala ambalo Mahakama Kuu haiwezi kulifumbia macho hata kidogo. Ukichanganya na misingi aliyoitumia Msuluhishi kuhalalisha malipo hayo umejaa harafu kali ya kifisadi..............................

  Wanasheria hao wajibu hizi hoja na waache kutoa majibu ya kisiasa ili kuhalalisha mahusiano yao na watendaji serikalini kwa manufaa yao binafsi tu..............................
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Kwa nini hawataki majina yao kuandikwa kama wanaongea ukweli hao wanasheria? Wana ficha nini?
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tunachohoji wengi ni kuwa hii Mahakama ya Usuluhishi ilielezwa ukweli wote kuhusu mkataba feki wa Richmond ambao hatimaye alirithishwa DOWANS? Waliiona ile taarifa ya Bunge Tukufu la Tanzania?
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,794
  Trophy Points: 280
  Huu ni ukikwaji wa maadili kwa jaji Mkuu kstaafu kuanza kuongelea mambo ambayo tayari yanaelekea Mahakamani. Uhuru wa mahakama zetu unamkataza mheshimiwa huyu kutoa maoni ya aina yoyote yale yanayoashiria kuweka mashinikizo kwa mahakama zetu kuaamua jinsi yeye atakavyo..........................................
   
 6. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  kuna post ilisema watatokea wengi tu kutetea upuuzi huuuuuuu, bado subirini
   
 7. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Je nani aliiwakilisha nchi kwenye hiyo mahakama?
  na alitumwa na nani?
   
 8. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Hii stori imeandikwa na Gazeti gani?
  Hawa jamaa kwa nini wao hawataki majina yao yatajwe? Isije ikawa mwandishi kaaamua kujitengenezea habari na yupo kwenye account ya malipo ya fadhila ya RA na mafisadi wengine

  Dowans yenyewe ina utata wa uhalali wake achilia mbali Richmond ikumbukwe yule mwarabu alikiikana
   
 9. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Hizo pande mbili ziliwakilishwa na nani kuwakubali hao wasuluhishi?
  Ngeleja alikuwepo huko ICC,maana anatoa tamko kuwa serikali lazima ilipe,je; baraza la mawaziri limekaa lini kuijadili na kutoa tamko la pamoja ama niaje hapa?
   
 10. Innobwoy

  Innobwoy JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 980
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 60
  Tunapoelekea naomba wazee wapumzike.kwa aman wasijishushie heshima, watuachie vijana tuamue kuhusu taifa letu..
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee alishachakachuliwa integrity yake long time ago......yuko na akina Subash kule SBL....walewale na Rostam
   
 12. dkims

  dkims Senior Member

  #12
  Jan 18, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hao sio manasheria ni wasaniiiiii, kama wana uhakika na mawazo jao kwanini wanajificha??? mi nadhani hiyo ni siasa tu ya muandishi na kampeni ya kuipamba dowans
   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hivi kumbe hili swala la Dowans limeshafika mahakama kuu? nilikuwa sina taarifa thanks for the update.
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye RED naomba nikusahihishe, sio mahakama ni Hotel, hiyo kesi ilikuwa inaendeshwa pale kilimanjaro kempinski. mwenye macho na aone na mwenye masikio na asikie. ndio maana taifa kubwa kama marekani mahakama za kihuni kama hizi huwa haizitambuwi, na huwa haisaini protocal docs ya kuzitambuwa. ndio maana hata rais wa sudan haitambuwi mahakama ya ocampo, ni magenge tu ya wahuni ambao wantarget zao.
   
 15. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Swali la Msingi la Kujiuliza: Nchi hii ina wanasheria?
   
 16. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Si walipe wanangoja nini kama wanaona sheria zao zinaruhusu?????????????????
   
 17. comorado

  comorado Member

  #17
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 15
  tatizo sio kuwalipa dowans, tatizo hao dowans ni waakina nani! Kwasababu hakuna kitu kama hicho maana hata serikali ya costa rica hawaitambui iwaje sisi tuitambue! Pili kama hio kampuni ipo na inasthili hayo malipo kama jaji bomani anavyo itetea hamna shida sisi tunataka kulia naviongozi waliopelekea taifa ku sign mikataba mibovu ili kama 2kianzisha maandamano ni inchi nzima kuhakikisha wanajiuzulu wote na ikiwezekana kuchukuliwa hatua za kisheria...kwaio bomani ache na yeye kuongea kama mwanasiasa wa tanzania wameshaanza kuchoka na madudu ya viongozi..watu wanamshambulia kwasababu maoni yake hayajazingatia ukweli wa jambo analozungumzia na hili haitaji uwe jaji mstaafu au mwanasheria mkuu mstaafu unaweza liona tuu..
   
 18. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Jana niliongea na mzee mmoja ambaye ni mstaafu. Yeye alidai tatizo la msuluhishi wa jambo hili hakuzingatia chimbuko la tatizo hili bali ameelea tu kwenye contact ilivyoandikwa na namna sheria inyosema kuhusu mikataba. Huu siyo usuluhishi bali ni maamuzi ya kawaida sana ya kisheria ambayo mwanasheria yoyote angeweza kufanya.

  Usuluhishi siyo kuangalia vitabu vya sheria peke yake bali ni kuangalia na uzito wa jambo lenyewe pamoja na madhara yanayojitokeza na ukubwa wa athari zake. maamuzi ya iccc yanawaathiri wtanzania zaidi ya 40mil wakati dowans ni kikundi kidogo tu cha matapeli. Mzee huyu aliongelea uzoefu wake kwamba alishawahi kushiriki kwenye usulushishi kama huu na mara msuluhishi alipogundua kuwa kulikuwa na information alizokuwa hajaambiwa, alijitoa kulinda heshima yake.

  Tuna wasiwasi na integrity ya ujumbe wa ICC waliofanya usuluhishi huu pale movenpik. kinachoonekana hapa ni kwamba msuluhishi wa swala la dowans pengine hajui kama RICHMOND na DOWANS zilikuwa ni kampuni feki kitu ambacho kinafanya zile contract kuwa null and void.

  Kwa vile serikali inania ya kunufaisha mafisadi wachache basi tunadhani hawapotayari kuwaambia ICC ukweli juu ya uhalali wa makampuni haya na kama sheria za kimataifa zinakubaliana na contracts za aina hii. Hapa sheria imeshindwa kuwatendea haki wa tz ni yayale mtu anadhulumiwa kisa ameshindwa techniques za kisheria.

  Huu ni ujinga, hebu tufikirie kama nyerere alikataa kulipa madeni ambayo ni halali na hawakutufanyakitu, sembuse huu upuuzi. Hakuna cha maana hapa huu ni wizi mtupu wa ccm kama kawaida yake. Kila uchaguzi lazima watuibie fedha zetu kwa njia za kitoto, sasa hapatoshi na hata kama watalipa basi fedha hizo walipe waliotuingiza hasara hii na siyo kodi yetu.
   
 19. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Turejeeni kauli ya Mkulo kuhusiana na kutokuwa na fundu la kuwalipa Dowans. Walioshitakiwa ni Tanesco waache wao wawalipe matapeli/wezi wenzao na kama hawana fedha za kufanya hivyo basi mahakama itoe ridhaa ya mali zao kukamatwa na/au kuuzwa ili "deni" hili la kitapeli lilipwe. Nitafurahi sana kuona timu yote wa uozo pale Tanesco na Wizara husika zikiwekwa ndani, Tanesco kufilisiwa ili tujue moja. Sijawahi kuona shirika kero kama hili, ni vyema life.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280
  Rutashubanyuma, ule mkataba wa Dowans si uliuona ulipowekwa humu?. Maamuzi ya ICC pia si uliyaona humu?. Sasa hivi vipengele vyako a-d umeviona kwenye mkataba?.

  Mkataba ni makubaliano ya pande mbili na utekelezaji unahusu vifungu vya mkataba husika. Vipengele, issues zozote ambazo sio part of the deal, zinabaki nje ya mkataba husika.

  Jaji Mark Bomani amejibu kisheria, lazima tulipe japo morality ni issue nyingine. Kuna issue nyingi ambazo morarily ni wrong lakini kisheria sio kosa, ikiwemo kutembea nje ya ndoa, au kutembea na mke wa mtu. Vivyo hivyo kuna issue nyingi za kisheria ni right kisheria ingawa morally ni wrong, issue hii ya Dowans ndio moja ya issue hizo, kisheria, tumeshikwa pabaya, hakuna pa kutokea, Sitta na Mwakiembe wanapiga siasa tuu!.

  Take it from me, pesa zitalipwa, after all msiwe na wasiwasi, haziendi mbali, zitazunguka humu humu nchini kujenga mji wa kimataifa pale Mlingotini, mahoteli makubwa, kumbi kubwa kubwa za starehe na casino kwa wingi, dada zetu pia watapata ajira, baada ya buku buku za pale kinondoni makaburini. itakuwa ni kilo kilo kwa wazungu wa satelite city Mlingotini!.
   
Loading...