Kwenye maiaka ya 80 karibia na 90, kwenye halmashauri fulani ya wilaya moja iliyo mahali fulani ndani ya JMT, kule Kanda ya Ziwa, ulizuka mtindo wa wafanyabiashara kuibiwa maduka yao kwa kubomolewa. Hali hii mwishowe ilipelekea siku moja kuitishwa mkutano wa hadhara na watu kuombwa kumtaja mtu yeyote ambaye wanadhani kuwa anaweza kuwa ni mhusika
Watu wengi walichangia kwenye mkutano huo siku hiyo lakini hayupo hata mmoja aliyejitokeza kutaja jina la mtu. Kwa bahati nzuri au mbaya, alikuwepo bwana fulani ambaye akili yake haikuwa sawa, alikuwa kama nusu chizi hivi ila hakuwa chizi completely. Ilitokea baada ya watu kuwa wameongea lakini pasipo kuwa wametaja jina lolote, hatimaye "nusu chizi" naye alinyoosha mkono ili aongee
"Nusu chizi" aliporuhusiwa, alisimama kwenye hadhara ya mkutano huo ambao ulikuwa ni mkubwa mno. Baada ya kusimama aliwauliza swali makutano hao akisema "NITOBOE SIRI?" watu wote wakaitikia "TOBOAAAAA!!!!"; akarudia tena akauliza " NITOBOE SIRI" safari hii watu wakaitikia kwa sauti ya juu kabisa na kwa nguvu zaidi kuliko mwanzo wakisema "TOBOAAAAA!!!!"; huku wakiwa na imani kabisa kuwa kwa sababu jamaa ni "nusu chizi" lazima tu atataja angalau jina la mtu mmoja na baada ya hapo watakuwa wamepata pa kuanzia
Baada ya makutano kumuitikiwa "nusu chizi" kwa mara ya pili, "nusu chizi" huyo alifikiria kidogo halafu akasema " NALIUNGA MKONO LILE LIFIJANA LIMEKAA"; akiwa anamaanisha kuwa anaunga mkono hoja ya mzunguzaji wa mwisho kijana aliyekuwa amepewa nafasi ya kuongea kabla yeye (nusu chizi) hajaruhusiwa kuongea
Baada ya hapo, watu karibia wote waliinamisha vichwa chini huku wakiwa wamegubikwa na nyuso zilizokosa matumaini juu ya ufumbuzi wa tatizo lililokuwa limewakusanya kwenye mkutano huo.
Aliyeanzisha thread hii amezirudisha kumbukumbu zangu kwenye tukio hilo