OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,191
- 103,715
Habari wakuu!!
Kama mnavyofahamu Mwanasheria Mkuu ni sehemu ya bunge,kunapotaka kufanyika maazimio magumu huwa ni lazima kamati zifanye cosultation kwake na hata wakati wa bunge ni lazima awepo ili kutoa ufafanuzi na kupangua hoja za wabunge wabishi kina Mnyika na Lissu. Nadhani mnakumbuka enzi za Jaji Werema na Masaju wakihenyeshwa na nguli wa sheria Tundu Lissu.
Nimekuwa nikijiuliza sana wakati maamuzi ya Azimio dhidi ya CAG,mwanasheria mkuu alikuwa wapi? Je,nchi hii inayo mwanasheria mkuu?Anaitwa nani? Amejificha wapi,na anajifichia nini? Kwa sababu maamuzi yenye mkanganyiko kama yale yasingeweza kutokea katika uwepo wa AG.
Kingine,napenda kujua wapo wapi manguli wa sheria za katiba kina Prof. Kabudi, Dr.Bashiru nk. Je,haya ni maamuzi ya bunge au ni maamuzi ya CCM,mbona hatujaisikia CCM ikishangazwa na Azimio kama general public ilivyohamaki?
Hii inadhibitisha unafiki wa kiwango cha juu cha wasomi wa nchi hii. Kabla ya kupata vyeo walikuwa mstari wa mbele kufafanua na kukemea uvunjifu wa katiba.