Sakata la Bandari: Spika Tulia atoa ufafanuzi

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,894
109,227
Spika anasema wacheni kupotosha:



--
Spika wa Bunge, Dr Tulia Ackson ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizosambaa zikidai kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari limesharidhia Azimio la Bunge kuhusu pendekezo la mkataba wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ambapo amesema Bunge bado halijaridhia.

Spika Dr. Tulia amesema taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na mitandao kuwa azimio hilo limesharidhiwa na Bunhe si za kweli kwani azimio husika kwa sasa bado lipo katika ngazi ya kamati ya pamoja kwa mujibu wa kanuni na mara baada ya kamati kumaliza kazi yake azimio hilo limepangwa kuingia Bungeni tarehe 10 June 2023 kwa ajili ya mjadala.
 
Siku si nyingi nchi itarudi kwa wenyewe

Sent from my CPH2217 using JamiiForums mobile app
Kwa sasa subiri, usipotoshe:

 
Tulia ni Tippu Tipu wa zama zetu kuwaswaga Watanganyika na kuwapeleka utumwani Falme za Kiarabu

tippu-tip-african-slave-trader-T81N3C.jpg

Muhammad Bin Said Al Murjabi lala unono mzee lala unono umeacha Legacy ya kuuzana sisi kwa sisi.
 
"Narudia kusema kwamba, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na (anatajwa wadhifa na jinale) Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza uchumi na maendeleo ya Watanzania ..."

Kwa matamshi hayo, ikichukuliwa kwamba sekta ya bandari ni sehemu ya maendeleo ya nchi...
 
Kupotosha kupi wakati Mkataba Kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DPW ya Emirates Dubai unaacha maswali mengi.

Ni mkataba ambao ulisainiwa kwa mwendokasi bila kuchukua tahadhari juu ya madhara yake yaliyo dhahiri. Mkataba huu haukubaliki kwa sababu nyingi Sana.

1. Mkataba ni wa milele kwa sababu hauna ukomo. Najua wapo waliosema ni wa miaka 100 na wapo waliosema ni wa miezi 12.

Hawa wote sijui wametoa wapi huo muda wa mkataba. Ibara ya 23 ya mkataba na randama zake (appendixes) hakuna popote zinaonyesha mkataba huu ni wa muda gani. Hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kudumu.

Ni kweli unaweza kuwa miaka mia lakini pia hakuna Cha kuzuia uwe wa miaka 1000.


2. mkataba huu una nguvu kuliko Sheria za Tanzania pamoja na Sheria za kimataifa (Takes precedent over national and international law)

Mathalani Ibara 23(4) hairuhusu kuvunja mkataba huu hata pakiwa na ukiukwaji mkubwa (material breach) au kukitokea hali inayopelekea mkataba usitekelezeke (fundamental change of circumstances) ambalo ni Takwa la mkataba wa kimataifa uitwao Vienna Convention on the Law of Treaties,1969 ambao Tanzania imejifunga nao.

Sasa hii tafsiri yake ni kwamba baada ya kusaini mkataba huu hata Dubai wakikiuka kabisa hatuwezi kujitoa. Hicho ni kitu Cha ajabu mno dunia itatushangaa.

Mbaya zaidi mkataba hausemi je una nafuu ili mbadala ukiachilia mbali kuvunja mkataba.

Kifungu Cha 23(4) kinaenda mbali zaidi na kusema ikitokea sababu yeyote inayotambulika kwenye Sheria za kimataifa ya kupelekea kuvunja mkataba bado mkataba huu hautavunjwa.Tafsiri yake ni kwamba tumeingia kwenye shimo ambalo halina pa kutokea (coup de sac) .

3. Mawanda (scope) ya mkataba pia ni mapana, ni Kama hayana ukomo. Ibara ya 2(1) itaruhusu muwekezaji kujenga na kuendesha miradi ya bandari za Bahari na maziwa yote.

Mkataba unakwenda mbali zaidi hata kwenye kile kinachoitwa logistic parks na trade corridors ambazo bahati mbaya hazijatafisiriwa kwenye mkataba.

Kwa namna mkataba huu ulivyo sisi tutakuwa tumepoteza udhibiti wa bandari zote za bahari na maziwa yote.

Mkataba ungeweka wazi ni bandari zipi hasa kwa sababu kwa namna ya Sasa hata usalama wa nchi unaweza kuwekwa rehani.

4. Mkataba hausemi sisi tutapata nini (consideration) kwa maana ya faida za mradi. Je, sisi tutakusanya Kodi tu? Au tutakuwa wabia?

5. Mkataba hauonyeshi nafasi ya mamlaka ya bandari (TPA) ni ipi katika uendeshaji wa mkataba. Kumbuka kwa mujibu wa sheria TPA ndo chombo chenye mamlaka ya kuendesha bandari zote. Sasa je mkataba huu umefuta sheria hiyo? Kwa mamlaka gani?

Mkataba hauelezei kuhusu usalama wa mapato yetu bandarini na nafasi ya vyombo vya ulinzi na usalama kwaajiri ya usalama wa nchi yetu hasa kwenye marine.

Nafasi pekee ya TPA kwa mujibu ya randama ya kwanza imeachiwa kuendesha na kusimamia " DHOW AND WHARF TERMINAL" ya bandari ya Dar es Salaam.

6. Pamoja na kuweka kipengele Cha local content ili kunufaisha wazawa kwenye ajira na manunuzi kwenye Ibara 13( 2) ambayo haina maana yoyote.
•Kwanza kwa sababu haiweki wazi kwamba "threshold" ya wazawa kwenye ajira itakuwaje.
• Pili hata procurement (manunuzi) ya vitu au "items" au huduma zinazopatikana ndani hailindwi na mkataba kwa sababu kwa mujibu wa bara ya 6(2) ya mkataba huu serikali yetu hauruhusiwi kufanya usumbufu wowote (interference) hata kwenye manunuzi yanayokiuka Sheria isipokuwa tu Kama yanahatarisha usalama (safety and security).

Sasa je wakiamua kuagiza mbao Dubai wakati hapa nchini zipo utawazuia kwa kigezo Cha usalama?

7. Mkataba hausemi nani atawajibika kulipa fidia yoyote inayotokana na utekelezaji wa mradi pamoja na watumishi ambao ajira zao zinaweza athiriwa na mradi.

8. Pamoja na kwamba Ibara ya 26 ya mkataba inaelekea kuruhusu "reservation" utagundua kwa namna Ibara ya 24 ilivyo imepoka kwa mkono mwingine haki ya "reservation" iliyopo kwenye Ibara ya 26 hivyo sioni uwezekano wa nchi yetu kufanya "reservation" kwenye makubaliano bila kukwaza mkataba.

Kwa namna ya mkataba huu tukifanya "reservation" sasa hivi inaweza kupelekea nchi iingie kwenye mgogoro wa kukiuka mkataba.

9. Hata kuridhiwa kwa mkataba huu na Bunge tayari umefanyika nje ya muda. Ibara ya 25(2) ilitaka mkataba uridhiwe ndani ya siku 30 tu na leo ni zaidi ya miezi Saba.

10. Kwa mujibu wa Ibara ya 8(3) (c ) mkataba huu ni kama unatoa umiliki wa ardhi kwa mwekezaji kinyume na Sheria ya ardhi. Kwa mujibu wa sheria ya Ardhi Sura ya 113 Kampuni ya kigeni hairuhusiwi kumiliki ardhi Tanzania. Tulitegemea mkataba useme ardhi zitakuwa chini ya TPA au mamlaka nyingine za serikali na wao watapata "derivative rights" badala ya kuwapa ardhi kwa mgongo wa "lease hold".
 
Back
Top Bottom