Said Ntimizi akamatwa kwa mauaji

Said Ntimizi akamatwa kwa mauaji

Papamsofe amefutiwa shtaka la mauwaji na yuko nje kwa dhamana

Je huyu atafungwa

Nb:majaji wamekuwa n wahunisana hasa kesi kama hizi..hata kama n serikali wanaomshtaki inaishia porojo nn kifanyike wakiachiwa tumalize nje wenyewe??
 
Mmiliki Wa Shule ipi?

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya mmiliki wa shule ya Mtakatifu Zion iliyopo maeneo ya Ununio, Mbezi Beach wilaya ya kipolisi Kawe mkoa wa kipolisi wa Kinondoni aliyejulikana kwa jina la ANNA D/O MIZINGI, Miaka 48, Mfanyabiashara, Mkazi wa Boko.

Mnamo tarehe 02/02/2015 majira ya saa za mchana mtoa taarifa alifika kituo cha Polisi na kueleza kwamba marehemu ANNA D/O MIZINGI aliondoka tangu tarehe 26/12/2014 majira ya saa 1:00hrs akiwa na mmoja wa watuhumiwa wakitumia gari dogo aina ya Toyota Verosa ambayo namba zake hazikufahamika mara moja iliyokuwa inamilikiwa na marehemu na tangu wakati huo hakuwa ameonekana tena.

Kutokana na taarifa hizo Jeshi la Polisi lilifungua jalada la uchunguzi na kuanza uchunguzi mara moja. Wakati uchunguzi ukiendelea zilipatikana taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watuhumiwa hao huko Uchira Miwaleni, Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Watuhumiwa walipokamatwa na kuhojiwa mtuhumiwa mmoja kati ya hao watatu amekiri na kutoa maelezo kuwa siku ya tukio aliondoka na marehemu kuelekea katika shule ya Mt. Zion. Kwamba walipofika shuleni hapo walivamiwa na watu wapatao wanne na kuanza kupigwa lakini yeye alifanikiwa kutoroka na kujificha katika uzio wa shule hiyo. Amesema akiwa katika uzio huo aliwaona watu hao wakiendelea kumpiga marehemu ANNA D/O MIZINGI na kisha kumtupa katika shimo la choo. Baada ya kitendo hicho watu waliotenda uhalifu huo waliondoka na gari la marehemu na kutokomea kusikojulikana.

Tarehe 22/06/2015 mabaki ya mwili wa marehemu ANNA D/O MIZINGI yalipatikana eneo la Ununio baada ya Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Zima moto kubomoa shimo la choo cha shule hiyo.

Watuhumiwa waliokamatwa ni hawa wafuatao:
1. DANIEL S/O RANADHANI MKILINDI @ ABDALLA @ DULLA, Miaka 25, Mganga wa kienyeji, Mkazi wa Uchira Moshi – Kilimanjaro.

2. SAID S/O RASHID OMARY @ SAID NTIMIZI au DUVII, Miaka 34, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbweni JKT.

3. ERICK S/O MZIRAY, Miaka 40, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kurasini.

Watuhumiwa hawa wanaendelea kuhojiwa ili kupata undani wa tukio hili ikiwa ni pamoja na kuwatafuta na kuwakamata watuhumiwa wengine wanaohusiana na tukio hili.
Mara baada ya uchunguzi kukamilika jalada la shauri hili litapelekwa kwa mwanasheria wa serikali kwa hatua zake za kisheria.

http://issamichuzi.blogspot.com/2015/06/watatu-watiwa-mbaroni-jijii-dar-es.html?m=1
 
Umofia kwenu wana JF,

Mtoto wa aliyekuwa waziri wa zamani tatu Ntimizi, anakabiliwa na tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara wa shule ya unununio international.

Taarifa za awali zinasema kwamba jamaa alikuwa na mahusiano na Huyo mama, Huyo mama akamsaidia kupata mkopo bank kwa kumdhamini kiasi cha pesa, ni zaidi ya bilioni na ushee ndipo Saidi alipotumia Hiyo fedha kununua nyumba baharini Mbweni JKT na kununulia magari ya kifahari, baada ya mama kuanza kusumbuliwa na bank kuhusu marejesho ya aliyemdhamini ndipo jamaa na team yake walikula njama na kumuua Huyo mama ambaye alikuwa mpenzi wake.
 
Papamsofe amefutiwa shtaka la mauwaji na yuko nje kwa dhamana

Je huyu atafungwa

Nb:majaji wamekuwa n wahunisana hasa kesi kama hizi..hata kama n serikali wanaomshtaki inaishia porojo nn kifanyike wakiachiwa tumalize nje wenyewe??
Dawa ni kuwatandika tu hao majaji kama wanavyofanya misri
 
dah....dunia hii ...ama kweli pesa ni shetani.. this is too much... bana :shock:

plz Stop the World – I Want to Get Off
 
Mwenye picha yake tafadhari huyo Saidi Ntimizi
 
Ndio huyo
 
Attachments

  • 1435661782930.jpg
    1435661782930.jpg
    79.4 KB · Views: 563
Umofia kwenu wana JF,

Mtoto wa aliyekuwa waziri wa zamani tatu Ntimizi, anakabiliwa na tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara wa shule ya unununio international.

Taarifa za awali zinasema kwamba jamaa alikuwa na mahusiano na Huyo mama, Huyo mama akamsaidia kupata mkopo bank kwa kumdhamini kiasi cha pesa, ni zaidi ya bilioni na ushee ndipo Saidi alipotumia Hiyo fedha kununua nyumba baharini Mbweni JKT na kununulia magari ya kifahari, baada ya mama kuanza kusumbuliwa na bank kuhusu marejesho ya aliyemdhamini ndipo jamaa na team yake walikula njama na kumuua Huyo mama ambaye alikuwa mpenzi wake.

Binaadamu sasa kamuua ili asidaiwe na huyo muuwaji hatakufa akili zao fupi sana.
 
Heheheh shosti hilo nalo neno ujue

Ukizingatia ana zaidi ya ml 900(alizokopa akagoma kulipa na kum-rip-isha mdai wake)nina mashaka kama atafungwa.....

Kweli pesa ibilisi....

Thubutuuu!
Papaa msoffe kasanua, kesi imekuwa ya kughushi sijui nini. Na alex massawe anakula bata dubai

Iba wewe karanga za jirani yako tukunyooshe kwa rula.
 
Unaongelea deni tu shogar? Mama ana jina pia. Ulishawahi kuona muuaji anakamatwa na polisi wanaringa ringa kutoa tamko? Mwaka mmoja mrefu ushahidi utakosekana. Akiachiwa unistue mama, ndio nchi yetu hii. Tunaivumilia
Heheheh shosti hilo nalo neno ujue

Ukizingatia ana zaidi ya ml 900(alizokopa akagoma kulipa na kum-rip-isha mdai wake)nina mashaka kama atafungwa.....

Kweli pesa ibilisi....
 
Back
Top Bottom