Said Mtanda: Dhana ya haki na amani haziwezi kutenganishwa katika ujenzi wa taifa imara, ni pande mbili za sarafu moja

Said Mtanda: Dhana ya haki na amani haziwezi kutenganishwa katika ujenzi wa taifa imara, ni pande mbili za sarafu moja

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
351
Reaction score
1,028

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amesisitiza kuwa dhana ya haki na amani haziwezi kutenganishwa katika ujenzi wa taifa imara, akizitaja kuwa ni pande mbili za sarafu moja.

Akizungumza jana, Machi 4, 2026, katika Maadhimisho ya Siku ya Maridhiano (Maridhiano Day) nchini Tanzania, Mtanda ambaye alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mtanda amebainisha kuwa bila amani, hakuna mazingira yanayoruhusu taasisi na mifumo ya kisheria kufanya kazi ya kutoa haki na amekiri kuwa bila haki, amani inayokuwepo inakuwa haina msingi imara wa kudumu.

Pia soma: Mzee Butiku: Tukubali tunaye Rais

“Kwa hiyo hatuwezi kuzungumza kuhusu amani kama hakutakuwa na haki. Lakini pia ili haki iweze kupatikana ni lazima amani iwepo ndani ya taifa. Kwa hiyo amani ni jamvi la kuelekea upatikanaji wa haki na haki nayo ni jamvi kuelekea upatikanaji wa amani”, ameeleza.
 
Neno haki limetamalaki siku hivi karibuni!

Je ni shinikizo la TFF!!?au!!?

Hadi kuwe na tishio la kutekwa ndio mnakumbuka haki!!?

Mbona tumehubirinkazi na utu kwenye mikutano lakini mambo yamekua vile vile!!?
 
Mkuu wa mkoa hapa ameamua kutufunga kamba za kisasa. AMANI na HAKI kamwe sio pande mbili za sarafu. Hizi ni dhana mbili tofauti zenye nguvu tofauti zinazojitegemea. HAKI ni sheria ya kimkataba, AMANI ni moja tu ya matunda ya mkataba na sio chanzo cha HAKI.

Ebu fikiria wanyama wa mwituni hawana Mkataba kwa maana ya katiba na hii ni moja ya sababu kubwa ya wao kukosa AMANI. Katiba ndio ingempa haki panya asiliwe na nyoka, nguruwe asiliwe na simba nk nk.

AMANI baina ya Simba na Nguruwe kamwe haitoshi kumfanya simba asimle nguruwe wala amani baina ya panya na nyoka haimfanyi nyoka aache kumla panya.

HAKI inayopatikana kwa mkataba/katiba na kulindwa na kutekelezwa na vyombo vya usimamizi wa katiba ndiyo inayoleta AMANI. Kamwe AMANI haijileti yenyewe bali inaletwa na HAKI kupitia mkataba/katiba kati ya mwanadamu na mwanadamu au Mungu na mwanadamu au yote mawili. AMANI haileti haki kwasababu AMANI ni kipengele (cha HIYARI) tu katika mkataba/katiba inayogawa HAKI kwa kila mmoja. AMANI inaombwa (mara nyingi kwenye nyumba za ibada kwa Mungu) HAKI aiombwi makanisani wala misikitini kwasababu ipo kwa kila mtu KISHERIA.

Turudi kwenye hii sarafu anayeisema mkuu wa mkoa. Sarafu ya AMANI na HAKI. Ebu tazama, nikikupa sarafu iliyogeukia upande wa AMANI na wewe ukadai nikupe iliyogeukia upande wa HAKI ni dhahiri sarafu hiyo HAIBEBI thamani sawa kwa kila pande. IMEKOSEWA katika matengenezo na ina haki ya kukataliwa na watumiaji. HAIFAI.

Hivyo kelele za kudai haki zisidunishwe au kuondolewa na hoja kwamba haki na amani ni pande mbili za sarafu. Hoja ya msingi ni Katiba mpya itakayogawa HAKI kwa kila mmoja na usimamizi madhubuti wa haki hizo. Haki isiwe tena chini ya madaraka ya mtu au watu. HAKI isiwe HISANI ya mtu au chombo cha dola. Muhimu zaidi AMANI isiwe shariti la HAKI, HAki iwe shariti la kikatiba.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amesisitiza kuwa dhana ya haki na amani haziwezi kutenganishwa katika ujenzi wa taifa imara, akizitaja kuwa ni pande mbili za sarafu moja.

Akizungumza jana, Machi 4, 2026, katika Maadhimisho ya Siku ya Maridhiano (Maridhiano Day) nchini Tanzania, Mtanda ambaye alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mtanda amebainisha kuwa bila amani, hakuna mazingira yanayoruhusu taasisi na mifumo ya kisheria kufanya kazi ya kutoa haki na amekiri kuwa bila haki, amani inayokuwepo inakuwa haina msingi imara wa kudumu.

Pia soma: Mzee Butiku: Tukubali tunaye Rais

“Kwa hiyo hatuwezi kuzungumza kuhusu amani kama hakutakuwa na haki. Lakini pia ili haki iweze kupatikana ni lazima amani iwepo ndani ya taifa. Kwa hiyo amani ni jamvi la kuelekea upatikanaji wa haki na haki nayo ni jamvi kuelekea upatikanaji wa amani”, ameeleza.
Ndani ya Biblia Takatifu "haki" imenukuliwa na kusisitizwa mara kadhaa.
 
Back
Top Bottom