Saga la Makonda: My Take

Saga la Makonda: My Take

Nime mkumbuka marehemu kabwe pale darajani kigamboni wakati wa ufunguzi na namna makonda alivo mtuhumu tu na hapo hapo muheshimiwa akafanya maamuzi of coz tulimuonea saana lakini hatuna namna
 
Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?
Naona siku hizi umehitimu matusi. Na sio wote wanaotaka RC achukuliwe hatua ni wapinzani. Na sio wapinzani wote wanataka RC achukuliwe hatua. Kupaza sauti ni haki ya kila mmoja. Mwenye uamuzi achukue uamuzi wake lakini hiyo haitanyamazisha watu. Ni wengi tu ambao hawakutegemea Uncle Magu achukue hatua hata kama walipenda achukue hatua.
 
Naamini wengi wenu humu ndani leo mlitegemea mkuu wa mkoa wa Dar kutumbuliwa na mheshimiwa mtukufu rais wa JMT.

Imani hiyo naamini iliongezwa na utolewaji wa video ya usalama ya kituo cha habari na burudani cha Clouds ambapo mkuu wa mkoa alionekana akiingia na askari wenye bunduki kwenye ofisi za kituo hicho majira ya usiku.

Hilo la kutumbuliwa halijatokea na kusema ukweli mimi sikuwa nategemea litokee hapo Ubungo mbele ya kadamnasi [ingawa Magu na huyo Makonda wake wameshawahi kumtumbua mtu hadharani]. Sikutegema wao kwa wao watumbuane hadharani.

Kwa jinsi rais Magufuli alivyo na kwa jinsi suala zima la vita dhidi ya Makonda linavyoendeshwa hivi sasa [kiudaku udaku hususan huku mitandaoni] mimi sitegemei kuona wala kusikia kuwa Makonda atatumbuliwa hivi karibuni. Uwezekano wa kutumbuliwa upo ila uelekeo wake mimi siuoni.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nadhani Magufuli akifanya hivyo atakuwa kama kasalimu amri ya shinikizo linalotoka huku kwenye mitandao na sidhani yuko tayari aonekane kasalimu amri.

Naamini kabisa Magufuli naye anayaona makosa ya Makonda. Ila sidhani kama 'ego' yake itamruhusu kufanya vile ambavyo wengi, hususan huku kwenye mitandao, wanataka afanye. Akifanya hivyo itakuwa ni kama kawapa ushindi wapinzani wake.

Baada ya muda suala hili la Makonda litapoa tu. Sina hakika itachukua muda gani lakini naamini litapoa tu.

Likishapoa ni imani yangu pia kuwa hapo ndo utakuwa mwanya wa Magufuli 'kumpangia' Makonda shughuli nyingine.

Lakini kwa sasa jinsi mazingira yalivyo [mipasho madhabahuni, matusi mitandaoni, drama magazetini, n.k.] sidhani kama yanampa rais nafasi nzuri ya kufanya kile ambacho wapinzani wake wanamtaka afanye.

Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu. Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na Magufuli ni wapenzi....seriously?

Mtu mnamtukana hivyo halafu bado mnategemea afanye jambo la kuwasuuza nyonyo zenu? Acheni masikhara bana.

Ila muda utatuonyesha tu....tusubiri tuone.
Msukuma anatetea msukuma
 
Onyesha niliposema Makonda anaonewa.

US baby!
Mkuu haijalishi uahirishe mpaka mwakani kumtumbua lakini wambeya wanakuwa wameshashinda na hasa hili la uvamizi wa clouds studio ndiyo kaharibu. Mambo ya vyeti vilikuwa issue ndogo sana!
 
NN umeongea milivyowaza, akimtumbua anawapa wapinzani ushindi. Wapinzani wake ni; watu wa udaku mitandaoni, wanasiasa wa upinzani na wale waliotajwa hadharani kujihusisha na ngada.

Hata hivyo, raisi ana 'ego' kubwa, hawezi ku-surrender kirahisi hivyo.
 
Huu ni mchezo wa karata robo sitini, kuacha kucheza karata ambayo ingeweza kukupa ushindi ukabaki nayo kwa kisingizio tuu kwamba mwenzako kachungulia karata yako ni uzuzu mchezo utakulazimisha kucheza wakati ambao hiyo karata haitakusaidia tena! .mwacheni abaki na zero wake
 
Raisi huwa anapiga simu 360 leo mbona hajapiga kuwapa pole marafiki zake? si anasema anawapenda au?
 
Huyo ni muongo wa kutupa! Anawapenda halafu anaunga mkono uvamizi uliofanywa kwenye ofisi zao!

Uongo ni mwingi sana kiasi kwamba mtu huwezi kuchambua kipi cha ukweli au kipi cha uongo, au uongo asilimia ngapi?
Hivyo busara lazima itumike kwa kiongozi yeyote na muda ambao ni muafaka ndipo unaweza kuchukua hatua.
halafu, inaoneka Watanzania wanapenda sana umbea, majungu, uzushi ndiyo hatufikiria sana kwa undani mambo ya maendeleo kwa nchi badala yake tumekuwa wabinafsi.
 
Wananchi gani hao unaowaingelea? Wauza Madawa ya kulevya Mbowe, Tundu Lisu, & Co.?
Ha ha na cheka muuza madawa mbona ni mwenyewe makonda kwa msaada wa Magufuli ghi kwani hiyo nayo siri
 
Huyo ni muongo wa kutupa! Anawapenda halafu anaunga mkono uvamizi uliofanywa kwenye ofisi zao!
Kama alivamia mbona matangazo ya Redio na Television yaliendelea.
Jambazi akivamia sehemu yoyote shughuli za hapo lazima zisimame, hetu tutumie akili kidogo jamani
 
NN umeongea milivyowaza, akimtumbua anawapa wapinzani ushindi. Wapinzani wake ni; watu wa udaku mitandaoni, wanasiasa wa upinzani na wale waliotajwa hadharani kujihusisha na ngada.

Hata hivyo, raisi ana 'ego' kubwa, hawezi ku-surrender kirahisi hivyo.

Watu inabidi wabadili mbinu za kukabiliana na huyu ngosha.

Huyu ngosha si wa spoti spoti. Yuko tofauti sana na bwana dhaifu.

Mbinu zilizotumika dhidi ya bwana dhaifu kwa ngosha zitashindwa tu.

Ila naamini mwishowe Makonda atatumbuliwa kidiplomasia na si ki drama.

Watch this space....
 
Naamini wengi wenu humu ndani leo mlitegemea mkuu wa mkoa wa Dar kutumbuliwa na mheshimiwa mtukufu rais wa JMT.

Imani hiyo naamini iliongezwa na utolewaji wa video ya usalama ya kituo cha habari na burudani cha Clouds ambapo mkuu wa mkoa alionekana akiingia na askari wenye bunduki kwenye ofisi za kituo hicho majira ya usiku.

Hilo la kutumbuliwa halijatokea na kusema ukweli mimi sikuwa nategemea litokee hapo Ubungo mbele ya kadamnasi [ingawa Magu na huyo Makonda wake wameshawahi kumtumbua mtu hadharani]. Sikutegema wao kwa wao watumbuane hadharani.

Kwa jinsi rais Magufuli alivyo na kwa jinsi suala zima la vita dhidi ya Makonda linavyoendeshwa hivi sasa [kiudaku udaku hususan huku mitandaoni] mimi sitegemei kuona wala kusikia kuwa Makonda atatumbuliwa hivi karibuni. Uwezekano wa kutumbuliwa upo ila uelekeo wake mimi siuoni.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nadhani Magufuli akifanya hivyo atakuwa kama kasalimu amri ya shinikizo linalotoka huku kwenye mitandao na sidhani yuko tayari aonekane kasalimu amri.

Naamini kabisa Magufuli naye anayaona makosa ya Makonda. Ila sidhani kama 'ego' yake itamruhusu kufanya vile ambavyo wengi, hususan huku kwenye mitandao, wanataka afanye. Akifanya hivyo itakuwa ni kama kawapa ushindi wapinzani wake.

Baada ya muda suala hili la Makonda litapoa tu. Sina hakika itachukua muda gani lakini naamini litapoa tu.

Likishapoa ni imani yangu pia kuwa hapo ndo utakuwa mwanya wa Magufuli 'kumpangia' Makonda shughuli nyingine.

Lakini kwa sasa jinsi mazingira yalivyo [mipasho madhabahuni, matusi mitandaoni, drama magazetini, n.k.] sidhani kama yanampa rais nafasi nzuri ya kufanya kile ambacho wapinzani wake wanamtaka afanye.

Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu. Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na Magufuli ni wapenzi....seriously?

Mtu mnamtukana hivyo halafu bado mnategemea afanye jambo la kuwasuuza nyonyo zenu? Acheni masikhara bana.

Ila muda utatuonyesha tu....tusubiri tuone.

Watu Kama mtoa mada hii ndio wanaoweza kubeba dhana ya JF kuwa na great thinkers. Pongezi zako mkuu.
 
Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?
Tanzania urais sio taasis,ni jitu moja tu!
 
Wewe ndiyo tumia akili achana na ubashite wa kutetea yale ambayo hayastahili kutetea. Sasa unataka kumpinga hata Ruge! Halafu unajiona eti una akili!

Back
Top Bottom