Saga la Makonda: My Take

Saga la Makonda: My Take

Naamini wengi wenu humu ndani leo mlitegemea mkuu wa mkoa wa Dar kutumbuliwa na mheshimiwa mtukufu rais wa JMT.

Imani hiyo naamini iliongezwa na utolewaji wa video ya usalama ya kituo cha habari na burudani cha Clouds ambapo mkuu wa mkoa alionekana akiingia na askari wenye bunduki kwenye ofisi za kituo hicho majira ya usiku.

Hilo la kutumbuliwa halijatokea na kusema ukweli mimi sikuwa nategemea litokee hapo Ubungo mbele ya kadamnasi [ingawa Magu na huyo Makonda wake wameshawahi kumtumbua mtu hadharani]. Sikutegema wao kwa wao watumbuane hadharani.

Kwa jinsi rais Magufuli alivyo na kwa jinsi suala zima la vita dhidi ya Makonda linavyoendeshwa hivi sasa [kiudaku udaku hususan huku mitandaoni] mimi sitegemei kuona wala kusikia kuwa Makonda atatumbuliwa hivi karibuni. Uwezekano wa kutumbuliwa upo ila uelekeo wake mimi siuoni.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nadhani Magufuli akifanya hivyo atakuwa kama kasalimu amri ya shinikizo linalotoka huku kwenye mitandao na sidhani yuko tayari aonekane kasalimu amri.

Naamini kabisa Magufuli naye anayaona makosa ya Makonda. Ila sidhani kama 'ego' yake itamruhusu kufanya vile ambavyo wengi, hususan huku kwenye mitandao, wanataka afanye. Akifanya hivyo itakuwa ni kama kawapa ushindi wapinzani wake.

Baada ya muda suala hili la Makonda litapoa tu. Sina hakika itachukua muda gani lakini naamini litapoa tu.

Likishapoa ni imani yangu pia kuwa hapo ndo utakuwa mwanya wa Magufuli 'kumpangia' Makonda shughuli nyingine.

Lakini kwa sasa jinsi mazingira yalivyo [mipasho madhabahuni, matusi mitandaoni, drama magazetini, n.k.] sidhani kama yanampa rais nafasi nzuri ya kufanya kile ambacho wapinzani wake wanamtaka afanye.

Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu. Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na Magufuli ni wapenzi....seriously?

Mtu mnamtukana hivyo halafu bado mnategemea afanye jambo la kuwasuuza nyoyo zenu? Acheni masikhara bana.

Ila muda utatuonyesha tu....tusubiri tuone.
mkuu, Clouds tv/radion in mtandao? Nape naye ni mtandao?
by the way habari zake ziko kwenye print media already (Mwananchi etc), je nao huu ni mtandao mkuu wangu?
 
Nyani Ngabu katika ubora wake
 
mkuu, Clouds tv/radion in mtandao? Nape naye ni mtandao?
by the way habari zake ziko kwenye print media already (Mwananchi etc), je nao huu ni mtandao mkuu wangu?

Nadhani hata hao wapo kwenye mitandao ya kijamii pia, au hawapo?
 
Upo sahihi kabisa, hili suala nimeliangaia naona ni zaidi ya hayo tunayoyaona, I am so much disappointed kwa hili ila naona mkulu ameamua kukumbatia bomu ambalo litamlipukia. Mwache sababu anadhani siasa ni mchezo anaoucheza kirahisi namna hiyo. Leo nasikia wanaCCM wenzake wamejitoa kwenye uongozi wa kamati ya Bunge, hao atawadharau kama kawaida yake na kuwaita wasaliti. Kesho wataibuka wakina Kingu pia ambao walishatoa misimamo yao ila pia ataweka ego yake. Itafika wakati chama kitamegeka atabaki na huyo Mungu wa Darisalama na yule mvaa makaptura masaa yote, yeye badala ya kukaa na watu wenye uzoefu wa siku nyingi anaspend muda na shilawadu, sawa tu...

BTW itafika wakati hakuna atakayeongea kuhusu madudu yanayoendelea ili akose kioo cha kumsaidia kujiangalia hapo ndipo atakapoona natural demise yake kama hamuamini ila hii ni pale asipojiangalia na kukaa kurekebisha namna anavyotawala kwakweli sijui tutafika wapi..
 
Nadhani hata hao wapo kwenye mitandao ya kijamii pia, au hawapo?
wapo mkuu lakini not in the context ambayo JPM anataka kuwaaminisha watu (and I think you are one of his victims of manipulative hand).

come f.....g on, you cant stoop that low mkuu.
 
Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu. Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na Magufuli ni wapenzi....seriously?
Kwa kweli umeandika, Rais wetu hapangiwi huo ndio ukweli
 
BTW itafika wakati hakuna atakayeongea kuhusu madudu yanayoendelea ili akose kioo cha kumsaidia kujiangalia hapo ndipo atakapoona natural demise yake kama hamuamini ila hii ni pale asipojiangalia na kukaa kurekebisha namna anavyotawala kwakweli sijui tutafika wapi..
Kwani alivyomtumbua mama Malechela nani alimshinikiza Rais, alivyomtumbua Kitwanga ishu ya ulevi nani alimshinikiza Rais, alipomtoa Katibu mkuu wizara ya fedha, Likwelile nani alimshinikiza Rais.. Alipomuondoa mkurugenzi wa Mkinga, nani alimshinikiza Rais.. Wengi waliotumbuliwa hakuna alimshinikiza..
 
Nyani Ngabu Mimi leo nimekuelewa hata mimi nimeliona hilo jamaa hataki kuona anasalimu amri...ila ile hotuba ya leo acha tu
 
Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?
Uwezo wako kiakili ni mdogo sana. Lakini una haki ya kusikilizwa maoni yako
 
Cheleachelea utamkuta meana sio wako!kutumbuliwa kwake kupo palepale .hapa ni suala la muda tu,siku sio nyingi atarudia yale ditopile mzuzuri aliyo yatenda. Hapo kila mmoja atatafuta pakutokea sio yeye wala bwana wake watakao kuwasalama.
 
Naamini wengi wenu humu ndani leo mlitegemea mkuu wa mkoa wa Dar kutumbuliwa na mheshimiwa mtukufu rais wa JMT.

Imani hiyo naamini iliongezwa na utolewaji wa video ya usalama ya kituo cha habari na burudani cha Clouds ambapo mkuu wa mkoa alionekana akiingia na askari wenye bunduki kwenye ofisi za kituo hicho majira ya usiku.

Hilo la kutumbuliwa halijatokea na kusema ukweli mimi sikuwa nategemea litokee hapo Ubungo mbele ya kadamnasi [ingawa Magu na huyo Makonda wake wameshawahi kumtumbua mtu hadharani]. Sikutegema wao kwa wao watumbuane hadharani.

Kwa jinsi rais Magufuli alivyo na kwa jinsi suala zima la vita dhidi ya Makonda linavyoendeshwa hivi sasa [kiudaku udaku hususan huku mitandaoni] mimi sitegemei kuona wala kusikia kuwa Makonda atatumbuliwa hivi karibuni. Uwezekano wa kutumbuliwa upo ila uelekeo wake mimi siuoni.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nadhani Magufuli akifanya hivyo atakuwa kama kasalimu amri ya shinikizo linalotoka huku kwenye mitandao na sidhani yuko tayari aonekane kasalimu amri.

Naamini kabisa Magufuli naye anayaona makosa ya Makonda. Ila sidhani kama 'ego' yake itamruhusu kufanya vile ambavyo wengi, hususan huku kwenye mitandao, wanataka afanye. Akifanya hivyo itakuwa ni kama kawapa ushindi wapinzani wake.

Baada ya muda suala hili la Makonda litapoa tu. Sina hakika itachukua muda gani lakini naamini litapoa tu.

Likishapoa ni imani yangu pia kuwa hapo ndo utakuwa mwanya wa Magufuli 'kumpangia' Makonda shughuli nyingine.

Lakini kwa sasa jinsi mazingira yalivyo [mipasho madhabahuni, matusi mitandaoni, drama magazetini, n.k.] sidhani kama yanampa rais nafasi nzuri ya kufanya kile ambacho wapinzani wake wanamtaka afanye.

Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu. Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na Magufuli ni wapenzi....seriously?

Mtu mnamtukana hivyo halafu bado mnategemea afanye jambo la kuwasuuza nyoyo zenu? Acheni masikhara bana.

Ila muda utatuonyesha tu....tusubiri tuone.
Hebu mjifikirishe kidogo!
Kuna issues Zaidi ya 3 in one!
  1. Kuna mtu kafoji cheti
    • hili ni kosa kisheria, sheria inayompa power yeye ndio hiyohiyo inamuhukumu huyu bwana mdogo. iweje achague vipengere vya kuvikubali na kuvikataa katika sheria moja
  2. mtu ameibia/kadhulumu watu kwa kutumia madaraka yake, na the same sheria inatoa adhabu
  3. mtu amefanya uvamizi wa silaha kwenye chombo cha habari, na pia sheria hiyohiyo inakataza!
hakuna excuse kwa makosa ya mkuu aliyoyafanya leo, ameiponda na kudhalilisha sheria za jamhuri, amekuwa above sheria and amekosea wapiga kura wake wengi mno! ametamba kuchukua fomu, amesahahu kuwa kura yake ilikuwa moja tu, amesahau kuwa alituomba tena shingo upande tumchague!
huwezi kusema eti yeye halazimishwi, sisi ndio tunaompa kila haki aliyonayo, kwa umoja wetu sisi ndio tumemkasimisha madaraka na sheria hizi anazozifanyia faulo leo ndio zinazompa power!
 
Naamini wengi wenu humu ndani leo mlitegemea mkuu wa mkoa wa Dar kutumbuliwa na mheshimiwa mtukufu rais wa JMT.

Imani hiyo naamini iliongezwa na utolewaji wa video ya usalama ya kituo cha habari na burudani cha Clouds ambapo mkuu wa mkoa alionekana akiingia na askari wenye bunduki kwenye ofisi za kituo hicho majira ya usiku.

Hilo la kutumbuliwa halijatokea na kusema ukweli mimi sikuwa nategemea litokee hapo Ubungo mbele ya kadamnasi [ingawa Magu na huyo Makonda wake wameshawahi kumtumbua mtu hadharani]. Sikutegema wao kwa wao watumbuane hadharani.

Kwa jinsi rais Magufuli alivyo na kwa jinsi suala zima la vita dhidi ya Makonda linavyoendeshwa hivi sasa [kiudaku udaku hususan huku mitandaoni] mimi sitegemei kuona wala kusikia kuwa Makonda atatumbuliwa hivi karibuni. Uwezekano wa kutumbuliwa upo ila uelekeo wake mimi siuoni.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nadhani Magufuli akifanya hivyo atakuwa kama kasalimu amri ya shinikizo linalotoka huku kwenye mitandao na sidhani yuko tayari aonekane kasalimu amri.

Naamini kabisa Magufuli naye anayaona makosa ya Makonda. Ila sidhani kama 'ego' yake itamruhusu kufanya vile ambavyo wengi, hususan huku kwenye mitandao, wanataka afanye. Akifanya hivyo itakuwa ni kama kawapa ushindi wapinzani wake.

Baada ya muda suala hili la Makonda litapoa tu. Sina hakika itachukua muda gani lakini naamini litapoa tu.

Likishapoa ni imani yangu pia kuwa hapo ndo utakuwa mwanya wa Magufuli 'kumpangia' Makonda shughuli nyingine.

Lakini kwa sasa jinsi mazingira yalivyo [mipasho madhabahuni, matusi mitandaoni, drama magazetini, n.k.] sidhani kama yanampa rais nafasi nzuri ya kufanya kile ambacho wapinzani wake wanamtaka afanye.

Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu. Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na Magufuli ni wapenzi....seriously?

Mtu mnamtukana hivyo halafu bado mnategemea afanye jambo la kuwasuuza nyoyo zenu? Acheni masikhara bana.

Ila muda utatuonyesha tu....tusubiri tuone.
Kanda ya ziwa moko ile
 
Approach nzima inayotumika dhidi ya Makonda si nzuri maana imekaa kiudaku udaki na kulipiza kisasi.

Halafu watu wanapoanza kudokeza kuwa Magufuli na Makonda ni mashoga...halafu hapo hapo wanamtegemea Magufuli eti amtumbue Makonda!

Mtu mnamtukana halafu hapo hapo mnamtegemea afanye jambo la kuwafurahisha...come on now.

Wrong approach.
Kwa ufupi hicho unachokisema ni kweli, kama si kweli povu la Nini?? David Cameroon wakubwa nyie!
 
Kumtumbua ni uamuzi wake kama alivyomteua , hata hivyo kwa mambo yalivyowekwa hadharani juu ya mteule wake, busara zinasema alipaswa kunyamaza kimya kama ameamua kuendelea nae kuliko alichosema leo.

Mitandao ya kijamii kama ni udaku inakuaje ikukoseshe raha hadi uongee kwa hasira na jeuri hivyo! Nachelea kuamini kama mh anashauriwa vyema, vinginevyo hapokei ushauri ama anashauriwa na mkosaji huyo huyo.
 
Duh! Wewe si timu Bashite! Kila siku huishi kumsifia na kumsapoti humu Sasa leo vipi
 
Back
Top Bottom