Saga la Makonda: My Take

Saga la Makonda: My Take

Najaribu kujiingiza ndani ya kichwa cha huyu dogo ndani ya muda huu. Sijui anapoingia kazini ofisini kwake anawatazamaje wafanyakazi wote walio chini yake.

Uso umeumbiwa aibu na kauli ya jana ya JPM ni nzito sana. Inafaa kabisa kuambatana na barua ya termination.
 
Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?
Mkuu upinzani umetoka wapi hapa? mbona unaandika kwa mihemko? wanaomsakama makonda ni wapinzani tu? mbona wengi ni ndani ya ccm? siku ukianza kutumia akili zako ndogo ulizojaaliwa itapendeza. acha kutumia akili za barabarani na udaku!
 
Najaribu kujiingiza ndani ya kichwa cha huyu dogo ndani ya muda huu. Sijui anapoingia kazini ofisini kwake anawatazamaje wafanyakazi wote walio chini yake.

Uso umeumbiwa aibu na kauli ya jana ya JPM ni nzito sana. Inafaa kabisa kuambatana na barua ya termination.
Ukifanikiwa kuingia kichwani mwa Bashite na ukitoka salama basi uje utusimulie hayo mazingira ya humo ndani yapo vipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini wengi wenu humu ndani leo mlitegemea mkuu wa mkoa wa Dar kutumbuliwa na mheshimiwa mtukufu rais wa JMT.

Imani hiyo naamini iliongezwa na utolewaji wa video ya usalama ya kituo cha habari na burudani cha Clouds ambapo mkuu wa mkoa alionekana akiingia na askari wenye bunduki kwenye ofisi za kituo hicho majira ya usiku.

Hilo la kutumbuliwa halijatokea na kusema ukweli mimi sikuwa nategemea litokee hapo Ubungo mbele ya kadamnasi [ingawa Magu na huyo Makonda wake wameshawahi kumtumbua mtu hadharani]. Sikutegema wao kwa wao watumbuane hadharani.

Kwa jinsi rais Magufuli alivyo na kwa jinsi suala zima la vita dhidi ya Makonda linavyoendeshwa hivi sasa [kiudaku udaku hususan huku mitandaoni] mimi sitegemei kuona wala kusikia kuwa Makonda atatumbuliwa hivi karibuni. Uwezekano wa kutumbuliwa upo ila uelekeo wake mimi siuoni.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nadhani Magufuli akifanya hivyo atakuwa kama kasalimu amri ya shinikizo linalotoka huku kwenye mitandao na sidhani yuko tayari aonekane kasalimu amri.

Naamini kabisa Magufuli naye anayaona makosa ya Makonda. Ila sidhani kama 'ego' yake itamruhusu kufanya vile ambavyo wengi, hususan huku kwenye mitandao, wanataka afanye. Akifanya hivyo itakuwa ni kama kawapa ushindi wapinzani wake.

Baada ya muda suala hili la Makonda litapoa tu. Sina hakika itachukua muda gani lakini naamini litapoa tu.

Likishapoa ni imani yangu pia kuwa hapo ndo utakuwa mwanya wa Magufuli 'kumpangia' Makonda shughuli nyingine.

Lakini kwa sasa jinsi mazingira yalivyo [mipasho madhabahuni, matusi mitandaoni, drama magazetini, n.k.] sidhani kama yanampa rais nafasi nzuri ya kufanya kile ambacho wapinzani wake wanamtaka afanye.

Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu. Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na Magufuli ni wapenzi....seriously?

Mtu mnamtukana hivyo halafu bado mnategemea afanye jambo la kuwasuuza nyoyo zenu? Acheni masikhara bana.

Ila muda utatuonyesha tu....tusubiri tuone.

NYONGEZA YA NUKUU

"Mimi huyu uniingilie..ukiniingilia ushapoteza kabisa"

"Mimi huwa sipangiwi mambo"

"Mimi ni rais ninayejiamini"

"Siwezi nikapangiwa mtu"

"Ninapanga mimi"

Video hii hapa chini.



Hizo nukuu za rais zinaipa nguvu hoja ya kwamba kwa sasa hizi kelele za watu kupitia mitandao ya kijamii hazitamfanya achukue uamuzi wa kumtumbua Makonda.

Ego tripping on steroids.


Shule muhimu sana. Bashite ni bichwa wazi, debe tupu. Litaibua shida nyingine kubwa. Yetu macho. Mzee baba atashindwa kuendelea kumvumilia.
 
Shule muhimu sana. Bashite ni bichwa wazi, debe tupu. Litaibua shida nyingine kubwa. Yetu macho. Mzee baba atashindwa kuendelea kumvumilia.

Hapo kwa Makonda alikosea sana kumteua.
 
Back
Top Bottom