Saga la Makonda: My Take

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
94,012
121,292
Naamini wengi wenu humu ndani leo mlitegemea mkuu wa mkoa wa Dar kutumbuliwa na mheshimiwa mtukufu rais wa JMT.

Imani hiyo naamini iliongezwa na utolewaji wa video ya usalama ya kituo cha habari na burudani cha Clouds ambapo mkuu wa mkoa alionekana akiingia na askari wenye bunduki kwenye ofisi za kituo hicho majira ya usiku.

Hilo la kutumbuliwa halijatokea na kusema ukweli mimi sikuwa nategemea litokee hapo Ubungo mbele ya kadamnasi [ingawa Magu na huyo Makonda wake wameshawahi kumtumbua mtu hadharani]. Sikutegema wao kwa wao watumbuane hadharani.

Kwa jinsi rais Magufuli alivyo na kwa jinsi suala zima la vita dhidi ya Makonda linavyoendeshwa hivi sasa [kiudaku udaku hususan huku mitandaoni] mimi sitegemei kuona wala kusikia kuwa Makonda atatumbuliwa hivi karibuni. Uwezekano wa kutumbuliwa upo ila uelekeo wake mimi siuoni.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nadhani Magufuli akifanya hivyo atakuwa kama kasalimu amri ya shinikizo linalotoka huku kwenye mitandao na sidhani yuko tayari aonekane kasalimu amri.

Naamini kabisa Magufuli naye anayaona makosa ya Makonda. Ila sidhani kama 'ego' yake itamruhusu kufanya vile ambavyo wengi, hususan huku kwenye mitandao, wanataka afanye. Akifanya hivyo itakuwa ni kama kawapa ushindi wapinzani wake.

Baada ya muda suala hili la Makonda litapoa tu. Sina hakika itachukua muda gani lakini naamini litapoa tu.

Likishapoa ni imani yangu pia kuwa hapo ndo utakuwa mwanya wa Magufuli 'kumpangia' Makonda shughuli nyingine.

Lakini kwa sasa jinsi mazingira yalivyo [mipasho madhabahuni, matusi mitandaoni, drama magazetini, n.k.] sidhani kama yanampa rais nafasi nzuri ya kufanya kile ambacho wapinzani wake wanamtaka afanye.

Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu. Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na Magufuli ni wapenzi....seriously?

Mtu mnamtukana hivyo halafu bado mnategemea afanye jambo la kuwasuuza nyoyo zenu? Acheni masikhara bana.

Ila muda utatuonyesha tu....tusubiri tuone.

NYONGEZA YA NUKUU

"Mimi huyu uniingilie..ukiniingilia ushapoteza kabisa"

"Mimi huwa sipangiwi mambo"

"Mimi ni rais ninayejiamini"

"Siwezi nikapangiwa mtu"

"Ninapanga mimi"

Video hii hapa chini.

Hizo nukuu za rais zinaipa nguvu hoja ya kwamba kwa sasa hizi kelele za watu kupitia mitandao ya kijamii hazitamfanya achukue uamuzi wa kumtumbua Makonda.

Ego tripping on steroids.
 
Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?
 
Mkuu hata nape nae amekuwa mpinzani
 
.....ata kama wangekaa kimya upinzani ..ishu ingekuwa vilevile.....huyu mzeee kiburi tu
 
Issue ya Makonda kuisha siyo rahisi sana ,maana kumbuka Makonda anapenda sifa mno,na anapenda aonekane anafanya kazi kuliko wenzake ndiyo kitu kinachomfanya Makonda atumbukie kwenye Mashimo ya makosa ya jinai.

Kwa alichofanya JPM sijui kama amemsaidia Makonda anyway Clouda na CCM ni wamoja.
 
Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?
kama upinzania hauna akili basi ccm ni majuha kabisa,kwani alidhani kazi ya uraisi ni lelemama na nirahisi tu kwakukaa na kuanza kufatilia shilawadu wakati wananchi wake hawana uhakika wa kesho wata kula nini..wewe ni bwege mwingine
 
Nyani, Bashite alikuwa amepita tuu pale ofisi za clouds na askari wake kuwasabahi watangazaji wa clouds, ule haukuwa uvamizi kabisa. Kwanza wale askari walikuwa mamebeba vibastola vya maji tu na waligonga mlango wakafunguliwa na kisha kukaribishwa kahawa na watangazaji.
 
Ngoja nikatopee kwenye jukwaa la MMU kwa muda kwanza kisha nitarudi siasani.
 
A fool will always get caught up in his own ego.

And Machiavelli once said something like; if an injury is to be caused to a man, it should be so severe that his revenge need not be feared. Time will tell.

Halafu Magu anavyosema tuache 'udaku', wakati wiki iliyopita tu katoka kusema ni shabiki wa SHILAWADU; How ironic is that???
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom