Saga la Makonda: My Take

Saga la Makonda: My Take

NN

Mh Rais asingeliongelea leo ingesaidia zaidi, kwasasa limepapalia curiosity

1. Kitwanga alitmbuliwa hadharani
2. Wilson Kabwe (RIP) hadharani hadi mauti
3. Wakurugenzi kama akina Rashed Badi Hadharani
4. Anne Kilango , hadharani
5. Kila siku Gery analeta barua za waliotumbuliwa

Orodha ni ndefu sana. Watu wanajiuliza hata kama si kutumbuliwa ni upi ukweli kuhusu Makonda? Kwanini anakingiwa kifua tofauti na wengine?

Sula litapoa, lakini makovu yake yatabaki yakivuja damu kila siku
Leo nani mwenye uthubutu wa kuongelea uhakiki wa vyeti?
Credibility ya Rais kuinyosha nchi ipo wapi?
Kwanini cheti cha Luhende kilikuwa hadharani, vya Makonda iwe siri?
Waliotumbuliwa kwa vyeti feki wanalitazamaje hili jambo? fair au kuna double std

Hili si la Makonda tena, linaigusa serikali na credibility yake. Mbaya sana
Leo zigo la Makonda anabebeshwa Rais!

Kuna tatizo gani wakitoka na kueleza wanachojua?
 
Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?

"walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?"

Tunategemea amuwajibishe kwa kuwa katiba,sheria, kanuni na maadili ya uongozi wa nchi yetu Tanzania vimesha ainisha hivyo.
 
Tumeitikia wito wa kusafisha na kuwafichua wenye vyeti feki...ametuacha Msamvu.
Tumeambatana nae kufuatilia shilawadu na umbra wa mitandaoni... Ametukana kwani tumezidisha ubuyu.hakuna jipya kwani Hata yesu alitolewa akasurubiwe badala ya mnyanganyi na mhalifu baraba miaka 2000 iliyopita.
Wengi wa watu wanaofuga majini huwa yanawageuka.
 
NN

Mh Rais asingeliongelea leo ingesaidia zaidi, kwasasa limepapalia curiosity

1. Kitwanga alitmbuliwa hadharani
2. Wilson Kabwe (RIP) hadharani hadi mauti
3. Wakurugenzi kama akina Rashed Badi Hadharani
4. Anne Kilango , hadharani
5. Kila siku Gery analeta barua za waliotumbuliwa

Orodha ni ndefu sana. Watu wanajiuliza hata kama si kutumbuliwa ni upi ukweli kuhusu Makonda? Kwanini anakingiwa kifua tofauti na wengine?

Sula litapoa, lakini makovu yake yatabaki yakivuja damu kila siku
Leo nani mwenye uthubutu wa kuongelea uhakiki wa vyeti?
Credibility ya Rais kuinyosha nchi ipo wapi?
Kwanini cheti cha Luhende kilikuwa hadharani, vya Makonda iwe siri?
Waliotumbuliwa kwa vyeti feki wanalitazamaje hili jambo? fair au kuna double std

Hili si la Makonda tena, linaigusa serikali na credibility yake. Mbaya sana
Leo zigo la Makonda anabebeshwa Rais!

Kuna tatizo gani wakitoka na kueleza wanachojua?

Umejenga hoja nzuri sana kuhusu suala la imani [credibility].

Hapa nilipo najiandaa kuleta mada kuhusu suala zima la uchunguzi-usuli [background checks] unaofanywa kwa viongozi wa umma na watumishi wa umma kwa ujumla kabla hawajapewa kazi.

Nitaliunganisha na suala zima la mfumo na jinsi suala hili [la mfumo] ulivyolizungumzia kipindi kile ambapo wachache kati yetu ndiyo tulikuelewa vyema.

Nadhani sasa somo la mfumo linaweza kueleweka zaidi kupitia hili sakata la Makonda.
 
Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?
Neno upinzani unalitumia vibaya...sio kila anaejadili hili jambo ni upinzan. Fanyia kazi tafiti yako.
 
We si ulikuwa unasema makonda anaonewa leo ume surrender

Unafiki uache nyani ngabu
Huyu jamaa mnafiki kweli utafikiri hapo mwanzo alikuwa haoni makosa ya huy Mr. Zero brain, na usiishangae kesho akimtetea tena maana watu wenye mtindio wa ubongo wana kawaida ya kufanya mambo bila kumbukumbu
 
Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?

Magufuli anatakiwa "amtumbue" Makonda sio kwasababu wapinzani wake na watu wa "mitandaoni" wanataka hivyo. Ni kwasababu, maadili (udanganyifu wa vyeti vya elimu), sheria (udanganyifu wa vyeti na kupora kwa kutumia silaha), na ukosefu wa busara wa Makonda katika kutekeleza kazi zake, unamtaka rais amtumbue. Akifanya hivyo, atakuwa ameonyesha kwamba yeye ni rais makini, mtenda haki, na hapendelei mtu yoyote. Huo utakuwa ni ushindi wa rais na serikali yake, na sio wapinzani na mitandao inayomsaidia tu kutekeleza wajibu wake huo.
 
Naamini wengi wenu humu ndani leo mlitegemea mkuu wa mkoa wa Dar kutumbuliwa na mheshimiwa mtukufu rais wa JMT.

Imani hiyo naamini iliongezwa na utolewaji wa video ya usalama ya kituo cha habari na burudani cha Clouds ambapo mkuu wa mkoa alionekana akiingia na askari wenye bunduki kwenye ofisi za kituo hicho majira ya usiku.

Hilo la kutumbuliwa halijatokea na kusema ukweli mimi sikuwa nategemea litokee hapo Ubungo mbele ya kadamnasi [ingawa Magu na huyo Makonda wake wameshawahi kumtumbua mtu hadharani]. Sikutegema wao kwa wao watumbuane hadharani.

Kwa jinsi rais Magufuli alivyo na kwa jinsi suala zima la vita dhidi ya Makonda linavyoendeshwa hivi sasa [kiudaku udaku hususan huku mitandaoni] mimi sitegemei kuona wala kusikia kuwa Makonda atatumbuliwa hivi karibuni. Uwezekano wa kutumbuliwa upo ila uelekeo wake mimi siuoni.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nadhani Magufuli akifanya hivyo atakuwa kama kasalimu amri ya shinikizo linalotoka huku kwenye mitandao na sidhani yuko tayari aonekane kasalimu amri.

Naamini kabisa Magufuli naye anayaona makosa ya Makonda. Ila sidhani kama 'ego' yake itamruhusu kufanya vile ambavyo wengi, hususan huku kwenye mitandao, wanataka afanye. Akifanya hivyo itakuwa ni kama kawapa ushindi wapinzani wake.

Baada ya muda suala hili la Makonda litapoa tu. Sina hakika itachukua muda gani lakini naamini litapoa tu.

Likishapoa ni imani yangu pia kuwa hapo ndo utakuwa mwanya wa Magufuli 'kumpangia' Makonda shughuli nyingine.

Lakini kwa sasa jinsi mazingira yalivyo [mipasho madhabahuni, matusi mitandaoni, drama magazetini, n.k.] sidhani kama yanampa rais nafasi nzuri ya kufanya kile ambacho wapinzani wake wanamtaka afanye.

Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu. Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na Magufuli ni wapenzi....seriously?

Mtu mnamtukana hivyo halafu bado mnategemea afanye jambo la kuwasuuza nyoyo zenu? Acheni masikhara bana.

Ila muda utatuonyesha tu....tusubiri tuone.

NYONGEZA YA NUKUU

"Mimi huyu uniingilie..ukiniingilia ushapoteza kabisa"

"Mimi huwa sipangiwi mambo"

"Mimi ni rais ninayejiamini"

"Siwezi nikapangiwa mtu"

"Ninapanga mimi"

Video hii hapa chini.

Hizo nukuu za rais zinaipa nguvu hoja ya kwamba kwa sasa hizi kelele za watu kupitia mitandao ya kijamii hazitamfanya achukue uamuzi wa kumtumbua Makonda.

Ego tripping on steroids.

That's Very True Mkuu.
Kuhusu Ego..
 
Mtu mwenye akili anajua Makonda atatumbuliwa tu. It's a matter of time.
 
Rais anatuonyesha tabia yake,hajui maana ya kuwa rais na urais ni taasis
 
Upinzani wa Tanzania hawana Akili na ni wote, kudili na Raisi Magufuli ni rahisi sana kama mtu una uwezo wa kumsoma mtu na kumuelewa, kwenye hii ishu wao wangekaa kimya tu na kuacha na nina uhakika wangefika mbali zaidi kuliko kushinda siku nzima kumtukana, kumkejeli, kumchora katuni halafu hapo mnategema afanye mnavyotaka? Hata yeye Raisi Magufuli ni Binadamu pia na anaumia kwa matusi yenu/yao!
Yaani kwa akili yao walitegemea Raisi amfukuze kazi Mkuu wa Mkoa kwa kuwa wametaka wao iwe hivyo?
Kumbe wanaotaka RC wa DSM achukuliwe hatua ni wapinzani? Kumbe wapinzani wa nchi hii ndio wamesoma kwa shida na kihalali hivyo kuwa na uchungu na elimu kuliko wale wa chama tawala?
 
Kwanini Makonda aliandaa ile video na akalazimisha irushwe??
 
Naamini wengi wenu humu ndani leo mlitegemea mkuu wa mkoa wa Dar kutumbuliwa na mheshimiwa mtukufu rais wa JMT.

Imani hiyo naamini iliongezwa na utolewaji wa video ya usalama ya kituo cha habari na burudani cha Clouds ambapo mkuu wa mkoa alionekana akiingia na askari wenye bunduki kwenye ofisi za kituo hicho majira ya usiku.

Hilo la kutumbuliwa halijatokea na kusema ukweli mimi sikuwa nategemea litokee hapo Ubungo mbele ya kadamnasi [ingawa Magu na huyo Makonda wake wameshawahi kumtumbua mtu hadharani]. Sikutegema wao kwa wao watumbuane hadharani.

Kwa jinsi rais Magufuli alivyo na kwa jinsi suala zima la vita dhidi ya Makonda linavyoendeshwa hivi sasa [kiudaku udaku hususan huku mitandaoni] mimi sitegemei kuona wala kusikia kuwa Makonda atatumbuliwa hivi karibuni. Uwezekano wa kutumbuliwa upo ila uelekeo wake mimi siuoni.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu nadhani Magufuli akifanya hivyo atakuwa kama kasalimu amri ya shinikizo linalotoka huku kwenye mitandao na sidhani yuko tayari aonekane kasalimu amri.

Naamini kabisa Magufuli naye anayaona makosa ya Makonda. Ila sidhani kama 'ego' yake itamruhusu kufanya vile ambavyo wengi, hususan huku kwenye mitandao, wanataka afanye. Akifanya hivyo itakuwa ni kama kawapa ushindi wapinzani wake.

Baada ya muda suala hili la Makonda litapoa tu. Sina hakika itachukua muda gani lakini naamini litapoa tu.

Likishapoa ni imani yangu pia kuwa hapo ndo utakuwa mwanya wa Magufuli 'kumpangia' Makonda shughuli nyingine.

Lakini kwa sasa jinsi mazingira yalivyo [mipasho madhabahuni, matusi mitandaoni, drama magazetini, n.k.] sidhani kama yanampa rais nafasi nzuri ya kufanya kile ambacho wapinzani wake wanamtaka afanye.

Naona labda hataki kuweka precedent ya kuyumbishwa na kelele za watu. Tena watu wanaomtukana hadi matusi ya nguoni. Watu wanaomzushia kila aina ya uzushi. Watu wamefikia hadi hatua ya kudokeza kwamba Makonda na Magufuli ni wapenzi....seriously?

Mtu mnamtukana hivyo halafu bado mnategemea afanye jambo la kuwasuuza nyoyo zenu? Acheni masikhara bana.

Ila muda utatuonyesha tu....tusubiri tuone.

NYONGEZA YA NUKUU

"Mimi huyu uniingilie..ukiniingilia ushapoteza kabisa"

"Mimi huwa sipangiwi mambo"

"Mimi ni rais ninayejiamini"

"Siwezi nikapangiwa mtu"

"Ninapanga mimi"

Video hii hapa chini.

Hizo nukuu za rais zinaipa nguvu hoja ya kwamba kwa sasa hizi kelele za watu kupitia mitandao ya kijamii hazitamfanya achukue uamuzi wa kumtumbua Makonda.

Ego tripping on steroids.

Mkuu hizo kelele ni za watu wa upande wa pili hasa wanaohusika na madawa ya kulevya,mbona hapo nyuma Makonda alifanya maamuzi mengi yenye kutia shaka na hatusikia hizi kelele .Kuna watu wanataka Makonda asurubiwe kwa kuwagusa wauza unga na hiyo inaonyesha kweli kwamba Makonda amefanya kazi nzuri na amewashika pabaya wauza unga hasa hao wauza unga madhahabuni na kwenye siasa na wengine waowatetea dada zao kwa sababu wanazozijua wao wenyewe hadi wanjitoa ufahamu eti kwa kuwa wengine ni brand zilizojengwa kwa muda mrefu.
 
Kikubwa hapo akimuondoa kwa cheti feki, wapinzani watarudi na PHD yake inaweza kuwa tatizo
 
Naamini watu hawatataka tena Makonda/Daud atumbuliwe kwani wanajua Makonda hajakosea chochote kile ila anatekeleza majukumu aliyopewa na waliomuweka hapo.
Watu walichojifunza na walichonufaika nacho ni kutowaamini wanasiasa tena, na ukitaka kumuadhibu mwanasiasa acha vita ya maneno dhidi yake, msubirie tu kwenye box la kura tena usimuonyeshe dalili yoyote ya kumkataa ili asije akastuka na kuja na mbinu nyingine.
Rais wetu hawezekani kwa vita ya maneno ila ni kumuacha aendeshe mambo anavyoona inafaa, akikwama huwa anarudi kimya na kuomba msaada wa mawazo.
Kwa hiyo vyeti katafutiwa na aliyemuwea?LB7 mmekosa cha kuandika
 
Hatomtumbua bcz serikali ina inteligency system. Rais anajua yote kuhusu makonda kupitia information system .
Kinachonishangaza ni tabia ya nyumbu kuamin na kushadadia haya mambo huku wakikiamin kinywa cha Gwajima na video clip ya sekunde 3.
Hv nyinyi NYUMBU kwann amreason.
 
Rais anawaongoza wananchi,na waliopo mitandaoni ni wananchi sasa unakataa maoni ya watanzania kwasababu wanasemea mitandaoni.
Mitandaoni ndiyo njia nyepesi ya kutoa maoni kwa wananchi wengi.
 
Back
Top Bottom