Safarini Dar: Msaada wa hoteli nzuri bei ya wastani

Safarini Dar: Msaada wa hoteli nzuri bei ya wastani

kwa dodoma lodge zipo nyingi sana,nashauri nenda mtaa unaitwa mji mpya,huo mtaa umechangamka chakula unapata na kwa lodge tuu zimejaa.
 
Hahhahahaaaa ngoja tusibishane bure tafuta siku nikuchukue ziara
Serious speaking mambo yanapinduka siku hizi huku kunakuwa kule na kule kunakuwa huku
Hizi zote nilizotaja ziko pembeni ya morogoro Rd na zinafikika kwa urahisi sana lakini hebu niambie kule Sinza mfano ukitaka kwenda Namnani
Hii Namnani ingali ipo kitambo sana, ni kama miaka 26 iliopita kama sikosei ilikua bar, na guest house. Mshana Jr?
 
Kumbe ndio maana...Manzese ya 2006 ndio sinza ya leo [emoji23] [emoji23] [emoji23] trust me fanya ziara ya kushtukiza siku moja hutajuta
Ni kweli, mwaka huu nilifika manzese mitaa ya tip top ndani kidogo sikuamini km niko manzese, hotel nzuri na tulivu zimesheni na kwa bei poa kabisa na mitaa ina utulivu tofauti na hisia nilizokuwa nazo kuhusu manzese
 
Ni kweli, mwaka huu nilifika manzese mitaa ya tip top ndani kidogo sikuamini km niko manzese, hotel nzuri na tulivu zimesheni na kwa bei poa kabisa na mitaa ina utulivu tofauti na hisia nilizokuwa nazo kuhusu manzese

Ni kweli kabisa mimi nilitumiaga miaka ya 2010 huko tip top,aisee kuna vitu vya hatari huduma safi,ac safi heater bafuni ukitaka maji moto maji baridi asubuhi breakfast yaani nilishangaa hako ka hotel nilikuta wageni wa Uganda na Kenya kibao nikajidharau sana nikasema kweli wa Tz hatujui vitu vizuri , parking safi wahudumu wazuri ,wa kike ila nilikuwa na kidemu changu,uwezi amini kipindi hicho ilikuwa Tsh 15,000 sijui sasa hivi
 
Elfu 30 IPO pale pale Ubungo terminal upande Wa pili ukifuata ile njia inayienda mabibo, hatua chache kuna hotel pale ya ghorofa, vyumba visafi pia
 
Mimi nadhani nimeathiriwa na tabia nchi, nitakwenda kinondoni lakini siyo Manzese, huu ndio ukweli wangu.

Mimi hata Magomeni nimeanza kwenda juzijuzi tu baada mchizi wangu mmoja kupata mjengo wa bei nafuu pande hizo.

Unaweza usinielewe, hata kariakoo mimi ndio tofauti kabisa siku nikipita kariakoo basi kuna kitu muhimu sana siwezi kukipata sehemu nyingine zaidi ya Kariakoo.
Mkuu yaonekana Manzese anayoisema mshana jr na siye, ni tofauti sana na ya ziku zile, anyway wewe tembelea tu, nenda kanywe hata bia na nyama choma hizo sehemu za TipTop, kwanza ni tulivu kuliko hata sinza, wale Wachaga wameleta ustaarabu wa ajabu kule..Mimi shahidi..
 
Back
Top Bottom