Safari yangu ya dhahabu Botswana

Safari yangu ya dhahabu Botswana

Mwisho wa siku isije kuangukia kuwa "kule gaborone nilipata demu mkali Sana mwenye tako" kama stori ya kina konda na keagan, yan sisi vijana wa Tz huwa malengo yetu yanaharibiwa sana kwa kupenda uchi
 
Habari..., matumaini yangu nyote humu mu wazima wa afya tele.
Kwanza kabisa mniwie radhi kwa upotevu wangu mkuu hapa.
Kwa siku kadhaa sikuwa mtandaoni kabisa kutokana na kadhia ya kuibiwa simu yangu, pia napenda kuwapa tahadhali muwe makini sana na maeneo yenye foleni kunakuwa na hawa waendesha pikipiki wenye tabia mbovu ya kupokonya simu janja hasa za wale waliokuwa ndani ya magari
.

Tulikaa pale mpakani kwa zaidi ya mwezi mmoja na siku kadhaa, lengo kuu likiwa kupata uzoefu, kupata pesa, connection na kufahamu zaidi juu ya huko tunakotaka kwenda.
Kwa bahati mbaya zaidi yule mwenzetu alie kuwa na ndugu yake kule Botswana aliamua kughailisha safari baada ya kunogewa na maisha ya pale hasa baada ya kukutana na binti mrembo kutoka mbeya.
Ukweli ni kwamba alikuwa kigeugeu sana, mpenda wanawake, pombe na mpungufu sana wa mipango na mwogopa matatizo.

Baada ya kujua in and out, moja na mbili za maujanja ya njiani kama wazamiaji wengine wenye ndoto kibao.
Tulifahamiana na jamaa mmoja mtanzania lakini alikuwa anafanyia mishe zake nyingi Zambia huko. Yeye alikuwa anafanya kazi katika kampuni moja hivi, jina lake kidogo limenitoka ijapokuwa kwa sasa nikiunganisha doti inaweza kuwa ndio iliyokuwa inatumia jina la Kobil. Lakini wakati huo huku Tz hakukuwa na kampuni ya usafirishaji mafuta yenye jina Kobil, Bali huko Zambia lakini ni kwa jina tofauti.

Nasi kutokana na uzoefu wake alituunganisha na madereva fulani hivi anaojuana nao na kwa kuwapa pesa kidogo tulifanikiwa kusonga mbele, japo wakati huo kila mmoja alienda tofauti na mwingine.
yaani mimi sikuweza kuandamana na yule mwenzangu.
Ilipowadia siku ya safari, mishare ya jioni kabisa nilijipakia ndani ya gari ya usafirishaji mafuta, safari kuingia Zambia ikaanza huku nikiwa kama turn boy wa gari hiyo.
kila kitu kilikuwa juu ya deleva.
kama akiamua kuniuza, kunichoma, kunikamatisha au chochote ni yeye tu, maana nilikuwa mweupe sana sifahamu mengi hata maswala ya rushwa

Kama ilivyokuwa kwangu na kwa upande wa mwenzangu ilikuwa vivyo hivyo, tofafauti yangu na yake ilikuwa siku za safari zilitofautiana, mimi nilitangulia kwa siku mbili zaidi, huku kwenye gari tukiwa wawili tu, yaani mimi na dereva.
Yeye alichelewa kwa siku mbili nyuma, huku kwenye gari walikuwa watu wa tatu.
Jambi zuri lililoenda sawa ilikuwa pale nitakaposhukia ndio hapo hapo atakaposhukia. Issue ngumu ilibaki kuwa mawasiliano tu ndio tatizo.
Safari ya kuelekea Zambia ilianza na ikumbukwe wakati huo tunaondoka hakukuwa na magari mengi yanayoelekea Botswana na hata watu walitushangaa kwanini tunaenda Botswana

Gari ilichapa mwendo na kuanza kuimaliza Nakonde, hapo sasa nilikaa mbele kwa amani kidogo na yule dereva aliniambia kuwa kwa muda wote wa safari nitakuwa kama turn boy wake ili tusisumbuliwe njiani, basi alinionyesha nguo flani hivi zilikuwa kwenye mfuko akaniambia nizivae hizo wakati wote tukiwa safarini.
baadae nilikuja kugundua umuhimu wa zile nguo baada ya kusimamishwa na maafande, maana hawakuwa hata na muda na mimi walinitambua kama walivyozoea kuona ma- turn boy vijana kama mimi tu wakati mwingi.
Tulisogea hadi sehemu moja inaitwa Kabwe kama sikosei. Kalikuwa kamji mji tu wakati huo.
Kuna mzigo ulikuwa unashushwa hapa kabwe, nusu ya mzigo ilifikia hapo na baada ya siku moja ya kulala ndani ya gari tuliendelea mbele tukiitafuta Lusaka ambapo ndipo itakapokuwa mwisho wa safari.

(Kuanzia hapo sikuwa na wasiwasi tena, taratibu niliingiwa na maujasili ya ajabu ajabu)

Nakumbuka hadi tunafika Lusaka Zambia pale nilishakuwa kama mzoefu tu wa njia hiyo. Na jambo la maana kabisa nililolifanya ni kutuma salamu za uzima wangu na matarajio yangu huko nyumbani nilikotoroka.
Yule dereva aliniunganisha na dereva mwingine anayekuja Dar na kupitia yule dereva niliweza kuwataarifi ndugu zangu wapi nilipo.
Nilijua watapata taarifa japo kwa kuchelewa lakini hivyo ndivyo ilivyo hakuna namna. Yule dereva alikuwa anarejea nyumbani Tanzania, tena karibu kabisa na maeneo yangu ya kujidai, maana mizigo yake alikuwa akipakilia bandari na kazi zake zote ni maeneo ya huko huko Costume.

Kimbembe sasa ilikuwa hapa Lusaka. Kwanza nilitakiwa kumsubili yule mwenzangu, pili jinsi ya kuendelea na safari hadi kule kwenye mji wa mpakani kati ya Zambia na Botswana huku ikipakana kabisa na Zimbabwe na Namibia.
Ukweli ni kwamba ukiwa na viakiba vya pesa japo kidogo tu hapa Afrika utaishi popote pale bila taabu saaana na kama utakuwa umetokea kwenye nchi rafiki na nchi hiyo au watu wa ulikotoka wanasifika kwa Tabia nzuri na ukalimu hapo utaishi kama nyumbani tu huku ukijibusti kidogo na ndugu corruption ili kuongeza kidogo ujamaa.

Nilikaa pale kibosi kabisa hadi alipowasili jamaa yangu. Jambo lingine muhimu watu mnalopaswa kuzingatia, siku zote wekeza katika kutengeneza connection, MTU mwenye connection ateseki sana kuliko asiyekuwa na ma-connection. Kwanza mimi kutokana na kutokea eneo ambalo hata wenyeji wa kule nje ukiwauliza wakutajie maeneo wanayoyajua kwa huku Tz ilikuwa ni lazima wataje Dar es salaam kariakoo.
Sehemu waliyodhani itakuwa bora kabisa katika ukanda huo wa Afrika mashariki. Na pia kujua kwangu mambo mbalimbali kuhusiana na shughuli za bandalini kule iyo nayo ilinipa point kwa madereva pale nilipofikia na wenyeji wa pale niliwapa mipango na mastory kibao ya downtown DSM...
Nikawa kama afisa wa habari wa muda pale kwenye yard ndogo nilipo fikia kwa siku mbili.

Hadi anawasili jamaa yangu, mimi tayari nilishakuwa na ramani nzima ya tunakoelekea na jinsi gani tutafika kwa urahisi huko.
Japo kuwa niliona kutakuwa na ugumu kweli kweli kufika Gaborone moja kwa moja kutokana na umbali nilioambiwa na wenyeji wa pale na huku ukizingatia pesa tulizokuwa nazo hazikuwa nyingi, na nadhani nilipigwa pia wakati wa kubadili fedha maana wajanja huko ni kila kona. Yaani kwenye pesa watu hawataki utani kabisa.

(Nitaendelea. Ahsanteni na mchukue tahadhari na vibaka waliojiajiri kwa wingi nyakati hizi)

Mkuu pole kwa yote ndio harakati za kimaisha hzo.
Kama unavotuahid mkuu tafadhali jitahd usiachie njiani huu uzi wako mana naamini unamafundisho ndani yake na wengi tutapata fursa ya kujifunza kupitia kwako.
 
Chembeza imezidi mishikaki. Mpaka unamaliza sijajua story inahusu nini na wapi
 
" Huwezi kumfanyia jambo jipya msafiri au mtu aliyepitia misukosuko ya kila namna.
Ni sawa na bure kabisa kumlewesha aliyelewa"

Nitazingatia mawazo yenu, kama mlivyojichagulia hapa, ijapokuwa najua mtakosa mambo mengi muhimu na nyeti zaidi niliyopanga kuwafunulia hapa.
Namaanisha kila kitu mtaambulia juu kwa juu tu na hakuna mtakachojifunza zaidi ya makapi ya kawaida tu.
" HEKIMA NA SIRI ZITAKUFA NA WENYE BUSALA"

Tunaendelea. (Ufupi wa habari umezingatiwa.)

Baada ya kuchelewa kwa usafiri asubuhi ya siku ya kwanza pale Mafinga. Kesho yake tulifanikiwa kufika maeneo ya panapoitwa Songwe kwa sasa.

Tuliishia hapa kwa sababu ya mtindo wetu wa kuunga unga safari. Na kuna mengi muhimu yaliyotusibu wakati wa safari ya kipande hiki cha kati ya Mafinga na hapo Songwe.

Miaka hiyo hakukuwa na maendeleo sana Tanzania, maeneo mengi hayakuwa na vitu kama vilivyopo nyakati hizi.
Kuna mtu ameuliza swali kwenye komenti, akitaka kujua kiasi cha pesa tulizokuwa nazo na je? tuliifadhi vipi?
Nasikitika sita andika hapa kila kitu, ili tu wale wenye mashauri tofauti tusiwakwaze.

Kule Botswana, watu ni wakalimu sana. Watu wanaheshimu mawazo na hisia za wengine mara elfu zaidi ya ujuavyo.
Ni sawa na kutomshangaa Mtanzania mlevi aliyelowea Urusi.
Tabia zetu zinabadilishwa na mazingira tuliyopo.

Tulifanikiwa kufika border ya Nakonde. Haikuwa nzuri na salama kama sasa.
Tunduma ilitupasa tukae sana, maana kwanza hatukuwa na nyaraka zozote, pili hatukuwa na moja wala mbili kuhusu namna ya kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha yoyote ng'eni zaidi ya kiswahili, tatu pesa yetu haikuwa nyingi na kuibadili haikuwa kazi rahisi.
Nne tulipaswa kuwa na connection na wazamiaji wengine zaidi ili iwe rahisi kwetu kutimiza azma yetu.

Mipango si ukuta, mwenzetu mmoja baada ya kunogewa na mji na watoto wa karii pale border, aliamua kabisa kughaili safari na kutekwa na mtoto wa kinyakyusa.
Almanusura tukwame wote pale Nakonde one stop border. Haikuwa sehemu salama kabisa kama wewe sio mjanja mjanja.
Chief acha masihala, unawasikilizaje hao machizi wachache??

Wanakulipia bando na muda unaitumia??

Noooooo.

Andika TU wakisoma wamesoma wasiposoma Ni juu Yao.

Narudia we andikaaaa unavyojisikia asitokee ndezi yoyote akakupangia namna ya kuandika hapa.

Nakusihi Sana simama kwenye nafasi yako.

Kwanza server za jf hasijai Sasa unajibana Nini?

Tulio wengi tuna hamu Sana na hii simulizi yako we andika TU narudia andikaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Habari..., matumaini yangu nyote humu mu wazima wa afya tele.
Kwanza kabisa mniwie radhi kwa upotevu wangu mkuu hapa.
Kwa siku kadhaa sikuwa mtandaoni kabisa kutokana na kadhia ya kuibiwa simu yangu, pia napenda kuwapa tahadhali muwe makini sana na maeneo yenye foleni kunakuwa na hawa waendesha pikipiki wenye tabia mbovu ya kupokonya simu janja hasa za wale waliokuwa ndani ya magari
.

Tulikaa pale mpakani kwa zaidi ya mwezi mmoja na siku kadhaa, lengo kuu likiwa kupata uzoefu, kupata pesa, connection na kufahamu zaidi juu ya huko tunakotaka kwenda.
Kwa bahati mbaya zaidi yule mwenzetu alie kuwa na ndugu yake kule Botswana aliamua kughailisha safari baada ya kunogewa na maisha ya pale hasa baada ya kukutana na binti mrembo kutoka mbeya.
Ukweli ni kwamba alikuwa kigeugeu sana, mpenda wanawake, pombe na mpungufu sana wa mipango na mwogopa matatizo.

Baada ya kujua in and out, moja na mbili za maujanja ya njiani kama wazamiaji wengine wenye ndoto kibao.
Tulifahamiana na jamaa mmoja mtanzania lakini alikuwa anafanyia mishe zake nyingi Zambia huko. Yeye alikuwa anafanya kazi katika kampuni moja hivi, jina lake kidogo limenitoka ijapokuwa kwa sasa nikiunganisha doti inaweza kuwa ndio iliyokuwa inatumia jina la Kobil. Lakini wakati huo huku Tz hakukuwa na kampuni ya usafirishaji mafuta yenye jina Kobil, Bali huko Zambia lakini ni kwa jina tofauti.

Nasi kutokana na uzoefu wake alituunganisha na madereva fulani hivi anaojuana nao na kwa kuwapa pesa kidogo tulifanikiwa kusonga mbele, japo wakati huo kila mmoja alienda tofauti na mwingine.
yaani mimi sikuweza kuandamana na yule mwenzangu.
Ilipowadia siku ya safari, mishare ya jioni kabisa nilijipakia ndani ya gari ya usafirishaji mafuta, safari kuingia Zambia ikaanza huku nikiwa kama turn boy wa gari hiyo.
kila kitu kilikuwa juu ya deleva.
kama akiamua kuniuza, kunichoma, kunikamatisha au chochote ni yeye tu, maana nilikuwa mweupe sana sifahamu mengi hata maswala ya rushwa

Kama ilivyokuwa kwangu na kwa upande wa mwenzangu ilikuwa vivyo hivyo, tofafauti yangu na yake ilikuwa siku za safari zilitofautiana, mimi nilitangulia kwa siku mbili zaidi, huku kwenye gari tukiwa wawili tu, yaani mimi na dereva.
Yeye alichelewa kwa siku mbili nyuma, huku kwenye gari walikuwa watu wa tatu.
Jambi zuri lililoenda sawa ilikuwa pale nitakaposhukia ndio hapo hapo atakaposhukia. Issue ngumu ilibaki kuwa mawasiliano tu ndio tatizo.
Safari ya kuelekea Zambia ilianza na ikumbukwe wakati huo tunaondoka hakukuwa na magari mengi yanayoelekea Botswana na hata watu walitushangaa kwanini tunaenda Botswana

Gari ilichapa mwendo na kuanza kuimaliza Nakonde, hapo sasa nilikaa mbele kwa amani kidogo na yule dereva aliniambia kuwa kwa muda wote wa safari nitakuwa kama turn boy wake ili tusisumbuliwe njiani, basi alinionyesha nguo flani hivi zilikuwa kwenye mfuko akaniambia nizivae hizo wakati wote tukiwa safarini.
baadae nilikuja kugundua umuhimu wa zile nguo baada ya kusimamishwa na maafande, maana hawakuwa hata na muda na mimi walinitambua kama walivyozoea kuona ma- turn boy vijana kama mimi tu wakati mwingi.
Tulisogea hadi sehemu moja inaitwa Kabwe kama sikosei. Kalikuwa kamji mji tu wakati huo.
Kuna mzigo ulikuwa unashushwa hapa kabwe, nusu ya mzigo ilifikia hapo na baada ya siku moja ya kulala ndani ya gari tuliendelea mbele tukiitafuta Lusaka ambapo ndipo itakapokuwa mwisho wa safari.

(Kuanzia hapo sikuwa na wasiwasi tena, taratibu niliingiwa na maujasili ya ajabu ajabu)

Nakumbuka hadi tunafika Lusaka Zambia pale nilishakuwa kama mzoefu tu wa njia hiyo. Na jambo la maana kabisa nililolifanya ni kutuma salamu za uzima wangu na matarajio yangu huko nyumbani nilikotoroka.
Yule dereva aliniunganisha na dereva mwingine anayekuja Dar na kupitia yule dereva niliweza kuwataarifi ndugu zangu wapi nilipo.
Nilijua watapata taarifa japo kwa kuchelewa lakini hivyo ndivyo ilivyo hakuna namna. Yule dereva alikuwa anarejea nyumbani Tanzania, tena karibu kabisa na maeneo yangu ya kujidai, maana mizigo yake alikuwa akipakilia bandari na kazi zake zote ni maeneo ya huko huko Costume.

Kimbembe sasa ilikuwa hapa Lusaka. Kwanza nilitakiwa kumsubili yule mwenzangu, pili jinsi ya kuendelea na safari hadi kule kwenye mji wa mpakani kati ya Zambia na Botswana huku ikipakana kabisa na Zimbabwe na Namibia.
Ukweli ni kwamba ukiwa na viakiba vya pesa japo kidogo tu hapa Afrika utaishi popote pale bila taabu saaana na kama utakuwa umetokea kwenye nchi rafiki na nchi hiyo au watu wa ulikotoka wanasifika kwa Tabia nzuri na ukalimu hapo utaishi kama nyumbani tu huku ukijibusti kidogo na ndugu corruption ili kuongeza kidogo ujamaa.

Nilikaa pale kibosi kabisa hadi alipowasili jamaa yangu. Jambo lingine muhimu watu mnalopaswa kuzingatia, siku zote wekeza katika kutengeneza connection, MTU mwenye connection ateseki sana kuliko asiyekuwa na ma-connection. Kwanza mimi kutokana na kutokea eneo ambalo hata wenyeji wa kule nje ukiwauliza wakutajie maeneo wanayoyajua kwa huku Tz ilikuwa ni lazima wataje Dar es salaam kariakoo.
Sehemu waliyodhani itakuwa bora kabisa katika ukanda huo wa Afrika mashariki. Na pia kujua kwangu mambo mbalimbali kuhusiana na shughuli za bandalini kule iyo nayo ilinipa point kwa madereva pale nilipofikia na wenyeji wa pale niliwapa mipango na mastory kibao ya downtown DSM...
Nikawa kama afisa wa habari wa muda pale kwenye yard ndogo nilipo fikia kwa siku mbili.

Hadi anawasili jamaa yangu, mimi tayari nilishakuwa na ramani nzima ya tunakoelekea na jinsi gani tutafika kwa urahisi huko.
Japo kuwa niliona kutakuwa na ugumu kweli kweli kufika Gaborone moja kwa moja kutokana na umbali nilioambiwa na wenyeji wa pale na huku ukizingatia pesa tulizokuwa nazo hazikuwa nyingi, na nadhani nilipigwa pia wakati wa kubadili fedha maana wajanja huko ni kila kona. Yaani kwenye pesa watu hawataki utani kabisa.

(Nitaendelea. Ahsanteni na mchukue tahadhari na vibaka waliojiajiri kwa wingi nyakati hizi)

Pole sana mkuu,karibu tena...tushushie nondo
 
Hii stori haiwez kufika mwsho naona dalili ya mtu kulala mbele kama alivyo fanya yule keagan paul
 
Back
Top Bottom