Safari yangu ya dhahabu Botswana

Safari yangu ya dhahabu Botswana

Jamaa alileta story ipi
 
Naipenda sana Botswana.siishi kuizungumzia..na wala sipajui...wale waswana nikiwaona wangejua ninavyowapenda..wee acha tu
 
" Huwezi kumfanyia jambo jipya msafiri au mtu aliyepitia misukosuko ya kila namna.
Ni sawa na bure kabisa kumlewesha aliyelewa"

Nitazingatia mawazo yenu, kama mlivyojichagulia hapa, ijapokuwa najua mtakosa mambo mengi muhimu na nyeti zaidi niliyopanga kuwafunulia hapa.
Namaanisha kila kitu mtaambulia juu kwa juu tu na hakuna mtakachojifunza zaidi ya makapi ya kawaida tu.
" HEKIMA NA SIRI ZITAKUFA NA WENYE BUSALA"

Tunaendelea. (Ufupi wa habari umezingatiwa.)

Baada ya kuchelewa kwa usafiri asubuhi ya siku ya kwanza pale Mafinga. Kesho yake tulifanikiwa kufika maeneo ya panapoitwa Songwe kwa sasa.

Tuliishia hapa kwa sababu ya mtindo wetu wa kuunga unga safari. Na kuna mengi muhimu yaliyotusibu wakati wa safari ya kipande hiki cha kati ya Mafinga na hapo Songwe.

Miaka hiyo hakukuwa na maendeleo sana Tanzania, maeneo mengi hayakuwa na vitu kama vilivyopo nyakati hizi.
Kuna mtu ameuliza swali kwenye komenti, akitaka kujua kiasi cha pesa tulizokuwa nazo na je? tuliifadhi vipi?
Nasikitika sita andika hapa kila kitu, ili tu wale wenye mashauri tofauti tusiwakwaze.

Kule Botswana, watu ni wakalimu sana. Watu wanaheshimu mawazo na hisia za wengine mara elfu zaidi ya ujuavyo.
Ni sawa na kutomshangaa Mtanzania mlevi aliyelowea Urusi.
Tabia zetu zinabadilishwa na mazingira tuliyopo.

Tulifanikiwa kufika border ya Nakonde. Haikuwa nzuri na salama kama sasa.
Tunduma ilitupasa tukae sana, maana kwanza hatukuwa na nyaraka zozote, pili hatukuwa na moja wala mbili kuhusu namna ya kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha yoyote ng'eni zaidi ya kiswahili, tatu pesa yetu haikuwa nyingi na kuibadili haikuwa kazi rahisi.
Nne tulipaswa kuwa na connection na wazamiaji wengine zaidi ili iwe rahisi kwetu kutimiza azma yetu.

Mipango si ukuta, mwenzetu mmoja baada ya kunogewa na mji na watoto wa karii pale border, aliamua kabisa kughaili safari na kutekwa na mtoto wa kinyakyusa.
Almanusura tukwame wote pale Nakonde one stop border. Haikuwa sehemu salama kabisa kama wewe sio mjanja mjanja.
bora uache tu maana porojo zimekuwa nyingi...stori haileweki mara wanyakyusa mara botwana ...
 
Kama ilivyo kwa wengine wapenda kusafiri kama mimi, daima tunapenda ku- share some stories na watu wengine ili nao angalau wapate kidogo mwanga wa maisha ya sehemu nyingine za mbali kidogo na nyumbani Tanzania.

Miaka kadhaa iliyopita kulikuwa na wimbi kubwa sana la vijana wa kitanzania kutamani kuondoka nchini na kukimbilia nchini Afrika ya kusini almaarufu bondeni kwa wakati huo. Nakumbuka sikuwa muhanga wa matamanio hayo yaliyokuwa sehemu kubwa ya vijana vijiweni kote huko, kuanzia temeke hadi kinondoni.

Nakumbuka rafiki zangu wengi tuliokuwa tukikaa pamoja pale maeneo ya Abbas club kama sikosei wakati huo miaka ya 2000 mwanzoni kabisa. Enzi za uwanja wa ugimbi na vita vya marefa na mashabiki...acha kabisa yaani, ukitoa matumizi ya bange kulikuwa na kubeli zilizotumiwa bila idadi maeneo hayo ya pembezoni mwa viwanja hivyo vyenye mchanga kibao. Kwa wakaazi wa kurasini, maeneo yote ya keko, zamkago kule na beach yetu pendwa ya Sava mtakuwa mnanipata vyema hapa.

Basi kipindi ndio safari za magendo zikiwa zimepamba moto huku waliokuwa washkaji kipindi hicho, maana kama kuna waliopo hai wakati huu wa sasa sio vijana tena. Mipango mingi ya kutafuta pesa za nauli za safari ilikuwa ikifanyikia nyuma ya kuta za bandari...aisee wizi wa mafuta ulipamba moto kweli kweli, kuna jamaa mmoja maarufu miaka hiyo aliita Jongo.

Kwa sasa ni marehemu kama walivyolala washkaji wengine wengi tu waliojihusisha na maswala ya wizi wa mafuta na vitu mbali mbali, kama unamfahamu Jongo na habari zake saluti kwako mkuu.

Huyu jamaa na genge lake walikuwa ni watu wakukaa nao mbali kabisa. Wakati mwingine unaweza kusema ni bora kushirikiana na wachuna ngozi wa mbeya huko kuliko hao jamaa.

Acha. Tusonge mbele sasa, baada ya vijana wengi kunogewa na habari za south na baadhi ya nchi nyingine za ulaya, ndipo safari za kuzamia meli zikaanza kwa Fuji sana na bila mpangilio na plan nzuri.
Nakumbuka kuna jamaa kadhaa waliobahatika kuzamia meli na hatukupata tena habari zao tena, hatujui kama walifanikiwa kufika walipo kusudia au la.

Kuna waliopitia njia za barabara kuelekea south Afrika ambapo ndio nchi pekee pendwa zaidi wakati ule.

Baadhi walizamia omani na kutokomea huko huko hadi hii leo tukiwa tunakisubili kwa hamu kimbunga chetu Jobo sijui nani.
Sasa wakati huo nchi kama Msumbiji, Kenya, sijui Uganda na huu upuuzi mwingine wote wa Afrika mashariki na kati sijui kama vijana walikuwa wanazifahamu kama zipo duniani hapa. Issue kubwa ilikuwa bondeni, Ulaya au angalau Arabuni kidogo kujipanga na kisha kuingia nchi za ulaya, na hata South Afrika ilikuwa ni kama njia tu au kituo cha kuelekea Italian, Finland, na kwingineko huko mbele kwa mbele.

Kwa upande wangu nilikuwa mwoga sana na ikizingatiwa makuzi na mazingira ya nyumbani yalivyokuwa. Maana kulikuwa na matabaka ya vijana kati ya watoto wa kota, watoto wa changanyikeni huko keko machungwa, keko mwanga, Tandika na viunga vyote vya wilaya ya Temeke (TMK) wilaya yetu ngumu na ya wagumu haswaaa.
Mwanzoni sikuwa na mawazo ya kusafiri nje kabisaaa, kwangu ilikuwa ngumu sana kushiriki katika mipango na plan za kutoroka nyumbani huku ukiwa umewaachia hasara kubwa ya wizi wa fedha, deki VHS kwa wale mnaozijua, TV Hitachi ya chogo, na vikorokolo kibao ilimradi tu upate kianzio cha safari.

Mwishoni mwa miaka ya 1999 kuelekea 2000 hivi kipindi kama sikosei ndio watu wengi wanaanza kumiliki simu za mkononi na zile vocha zetu pendwa zilizoitwa Dollar. Zilikuwa mtindo wa karatasi hivi, unalichana katikati na tarakimu unazikuta ndani kisha mkononi una Nokia yako kubwa 30410 jeneza full vibration, au Philips kidole juu.

Basi baada ya stori nyingi za marafiki waliofanikiwa kuescape manyumbani kwao kutufikia kuwa wanakula bata mbele huko, ndipo na mimi nilipo amua kujilipua na kuondoka na jamaa zangu wawili.


(Tukutane leo jioni hapa hapa)
Sawa
 
Mkuu Midnight Mbona umetuacha njia panda tupo hapa tumeweka Kambi tunasubiria muendelezo
 
Mkuu Midnight Mbona umetuacha njia panda tupo hapa tumeweka Kambi tunasubiria muendelezo
Kwa moyo safi kabisa na taadhima nitaurudia upya huu mkasa wangu katika nyuzi mpya. Kaa tayari mkuu.
 
Acheni ubwege baadhi ya watu humu. Hivi hamuwezagi kutulia hata kwa kidogo? mwanaume mwenzenu anatoa story lakini nyie wanaume ndo wakwanza kumzonga zonga kama vipi si muanzishe zenu?? Yani mnakera mnoo sisi tunataka kila kitu asiache hata kama alikohoa sehemu aseme alikohoa. Kuna vitu vinasisimua kama story zile za kule kwao kabla hawajaondoka. Hebu mtupishe mnawashwa kama mmetiwa pilipili
JF siku hizi imejaa utoto na ujuaji mwingi
 
Back
Top Bottom