Safari yangu ya dhahabu Botswana

Midnight

JF-Expert Member
Apr 24, 2021
229
675
Kama ilivyo kwa wengine wapenda kusafiri kama mimi, daima tunapenda ku- share some stories na watu wengine ili nao angalau wapate kidogo mwanga wa maisha ya sehemu nyingine za mbali kidogo na nyumbani Tanzania.

Miaka kadhaa iliyopita kulikuwa na wimbi kubwa sana la vijana wa kitanzania kutamani kuondoka nchini na kukimbilia nchini Afrika ya kusini almaarufu bondeni kwa wakati huo. Nakumbuka sikuwa muhanga wa matamanio hayo yaliyokuwa sehemu kubwa ya vijana vijiweni kote huko, kuanzia temeke hadi kinondoni.

Nakumbuka rafiki zangu wengi tuliokuwa tukikaa pamoja pale maeneo ya Abbas club kama sikosei wakati huo miaka ya 2000 mwanzoni kabisa. Enzi za uwanja wa ugimbi na vita vya marefa na mashabiki...acha kabisa yaani, ukitoa matumizi ya bange kulikuwa na kubeli zilizotumiwa bila idadi maeneo hayo ya pembezoni mwa viwanja hivyo vyenye mchanga kibao. Kwa wakaazi wa kurasini, maeneo yote ya keko, zamkago kule na beach yetu pendwa ya Sava mtakuwa mnanipata vyema hapa.

Basi kipindi ndio safari za magendo zikiwa zimepamba moto huku waliokuwa washkaji kipindi hicho, maana kama kuna waliopo hai wakati huu wa sasa sio vijana tena. Mipango mingi ya kutafuta pesa za nauli za safari ilikuwa ikifanyikia nyuma ya kuta za bandari...aisee wizi wa mafuta ulipamba moto kweli kweli, kuna jamaa mmoja maarufu miaka hiyo aliita Jongo.

Kwa sasa ni marehemu kama walivyolala washkaji wengine wengi tu waliojihusisha na maswala ya wizi wa mafuta na vitu mbali mbali, kama unamfahamu Jongo na habari zake saluti kwako mkuu.

Huyu jamaa na genge lake walikuwa ni watu wakukaa nao mbali kabisa. Wakati mwingine unaweza kusema ni bora kushirikiana na wachuna ngozi wa mbeya huko kuliko hao jamaa.

Acha. Tusonge mbele sasa, baada ya vijana wengi kunogewa na habari za south na baadhi ya nchi nyingine za ulaya, ndipo safari za kuzamia meli zikaanza kwa Fuji sana na bila mpangilio na plan nzuri.
Nakumbuka kuna jamaa kadhaa waliobahatika kuzamia meli na hatukupata tena habari zao tena, hatujui kama walifanikiwa kufika walipo kusudia au la.

Kuna waliopitia njia za barabara kuelekea south Afrika ambapo ndio nchi pekee pendwa zaidi wakati ule.

Baadhi walizamia omani na kutokomea huko huko hadi hii leo tukiwa tunakisubili kwa hamu kimbunga chetu Jobo sijui nani.
Sasa wakati huo nchi kama Msumbiji, Kenya, sijui Uganda na huu upuuzi mwingine wote wa Afrika mashariki na kati sijui kama vijana walikuwa wanazifahamu kama zipo duniani hapa. Issue kubwa ilikuwa bondeni, Ulaya au angalau Arabuni kidogo kujipanga na kisha kuingia nchi za ulaya, na hata South Afrika ilikuwa ni kama njia tu au kituo cha kuelekea Italian, Finland, na kwingineko huko mbele kwa mbele.

Kwa upande wangu nilikuwa mwoga sana na ikizingatiwa makuzi na mazingira ya nyumbani yalivyokuwa. Maana kulikuwa na matabaka ya vijana kati ya watoto wa kota, watoto wa changanyikeni huko keko machungwa, keko mwanga, Tandika na viunga vyote vya wilaya ya Temeke (TMK) wilaya yetu ngumu na ya wagumu haswaaa.
Mwanzoni sikuwa na mawazo ya kusafiri nje kabisaaa, kwangu ilikuwa ngumu sana kushiriki katika mipango na plan za kutoroka nyumbani huku ukiwa umewaachia hasara kubwa ya wizi wa fedha, deki VHS kwa wale mnaozijua, TV Hitachi ya chogo, na vikorokolo kibao ilimradi tu upate kianzio cha safari.

Mwishoni mwa miaka ya 1999 kuelekea 2000 hivi kipindi kama sikosei ndio watu wengi wanaanza kumiliki simu za mkononi na zile vocha zetu pendwa zilizoitwa Dollar. Zilikuwa mtindo wa karatasi hivi, unalichana katikati na tarakimu unazikuta ndani kisha mkononi una Nokia yako kubwa 30410 jeneza full vibration, au Philips kidole juu.

Basi baada ya stori nyingi za marafiki waliofanikiwa kuescape manyumbani kwao kutufikia kuwa wanakula bata mbele huko, ndipo na mimi nilipo amua kujilipua na kuondoka na jamaa zangu wawili.


Kusoma sehemu ya pili tembelea - Safari yangu ya dhahabu Botswana - Sehemu ya pili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom