Mara nyingi zaidi napenda kutumia wakati huu wa usiku kujumuika nanyi katika masimulizi yangu haya.
Sina shaka ya kuwa mu wazima wa afya na amani tele. Mungu awabariki sana na awazidishie uvumilivu na mioyo safi.
Tunaendelea pamoja.....
Kutoka Lusaka Zambia hadi kufika Botswana wakati huo hakukuwa na usafiri wa moja kwa moja na wa kuaminika. Bahati nzuri kulikuwa na gari moja la dharura lililokuwa likielekea moja kwa moja Gaborone kupitia mji wa Francis town na sisi kama tungefanikiwa Francis town, ingetupasa pia kuabili treni hadi Gaborone kwa kuwa lile gari ilikuwa inachukua muda mwingi kuanza tena safari kutoka Francis town hadi Gaborone ambako ndio mji mkuu na mji wa kibiashara kwa Botswana kama ilivyo Dar es salaam.
Tulilipia kiasi kingi cha pesa ili kuweza kuhitimisha safari hii ya kuelekea rasmi Botswana.
Kama kawaida yetu matatizo yetu yote tuliwaachia wenyenye wayamalize kila tuendapo ikiwa kama kutatokea kizuizi chochote. Na njia hii ilitufanya sasa tuishiwe kabisa pesa ambazo kwa uchache wake na ile hali ya kuzibadili kienyeji enyeji ilituletea hasara kubwa na kubambikwa bambikwa tu.
Safari ilianza mapema tu kuelekea katika mpaka wa Kazungura kisha tube tuchukue high way kuelekea Francis town. Kutokana na uzoefu wa wenyeji wetu tulifanikiwa kupanda kivuko na kuvuka bila shida sana pale kwenye MTO Chobe. Wakati huo kulikuwa na kivuko mithili ya panton, lakini chenye kubeba magari makubwa na mizigo mbali mbali.
Afrika bila rushwa ingekuwa tajiri sana aisee.
Ngoja niweke sawa hapa. Gari tuliyopanda ilikuwa imesajiriwa Botswana na ilikuwa ni mali ya kampuni fulani hivi ya kitalii talii, hivyo wakati huo ilikuwa imetokea Zambia kwa shughuli zao za utalii, na ilikuwa inarejea Botswana katika kituo chao cha kazi kisha ikiwezekana baada ya siku kadhaa ingeenda Gaborone kuwapokea wageni. Ndani ya gari tulikuwa sisi wa Tz wawili, wafanya biashara watatu wa kizambia na dereva Mbotswana jina lake Boipelo, Boipelo alikuwa mcheshi na huku kwao majina ya Boipelo ni mengi kuliko wakina Musa wote waliopo DSM.
Wale wa Zambia walikuwa wanaonekana ni watu wa magendo magendo sana, ni kana kwamba wanafanya mabiashara ya haramu haramu hivi, maana japo lugha ilikuwa inatuchenga chenga sana lakini tuliwasoma sana na hata tulidhani wanaweza kutuchoma. Kifupi ni kuwa wao walikuwa hawatuelewi, hawatuamini na sisi hatuwaelewi na hatuwaamini kabisa yaani ni mwendo wa kuhisiana hisiana vibaya.
Wao hawakufika Francis town, Luna sehemu waliishia na kulikuwa hakuna mji maeneo hayo, bali Boi alituambia wale ni wafanyabiashara wa nyama pori na bidhaa nyingine za magendo huko maporini, hivyo kunakuwa na vi camp vyao huko ndani ndani.
Tuliendelea kunasa neno moja moja hivyo hivyo maana lafudhi ya Boi ilikuwa imekaa sana ki- tswana tswana sana hivyo hata yeye alipata tabu kutuelewa ijapo kuwa mwenzetu kiingereza alikizungumza vizuri kutokana na kazi yake na pia nchi yake kutumia kiingereza kama lugha yao pia.
Basi unaambiwa kule Botswana mzee hakuna bahari, sehemu mkubwa ni jangwa na unaweza ukatembea na gari mamia ya makirometa katika ardhi tambalale isiyokuwa na kimlima chochote. Lugha yao mkubwa ni tswana na kiingereza na kukuta MTU anatembea barabarani huku akiwa amevaa mavazi ya kijadi ni kawaida sana.
Pia jambo nililojifunza kwao ni kuwa mgeni kamwe hauwezi kujificha kwao. Yaani usijulikane!!! hio sahau labda uwe m-Namibia, au kutokea nchi fulani nimeisahau ipo ukanda ule ndio kidongo wanafanana fanana.
Maajabu ya Mungu ni kuwa kama walivyo tofauti wanyarwanda wengi na watu wengine ndivyo hivyo hivyo walivyo wa-Karanga wa Botswana au Basarwa , tswana, Basubiya n.k na kuna wahindi kule, hawa jamaa wapo kila unapopajua.
Watu wa kule wanajali sana tamaduni zao, na ukitaka kuishi nao vizuri wewe onyesha tu kuwa unapenda mitindo yao ya maisha na kufanya kila kitu kama wanavyofanya wao, hapa utawamaliza hakuna uchawi tena aisee
Basi safari iliendelea na mfukoni sasa hatukuwa na fedha, hatukuwa na nguo za ziada, hatukuwa na pakufikia hata jina la yule uncle wa mwenzetu aliyekwamia Tunduma hatukuwa tunalikumbuka.. Ilikuwa ni kichwa kichwa tu bora mzigo ufike na chaajabu kabisa tulivyokuwa tunatengeneza taswira vichwani mwetu ya jinsi tungepokelewa na majumba mazuri ya kifahari na kujionea mijengo mikali, lakini haikuwa hivyo bali tuliendelea kuesabu miti ya miiba kote njiani na ardhi kame name kamo tupo Dodoma tu hapo.
Njaa ilikuwa inatupiga sana lakini hakuna cha kufanya, na Boi kutokana na kuelewana kwa shida shida aliamua kuwa kimya kwa umbali mrefu.
elimu yetu ya Jkt mgulani iliishia Tunduma pale, huku kote kulikuwa tunajaralibu jaribu
upepo na kutumia uzoefu
Japo kwa shida lakini yule