Safari yangu "Kitchanga" mji uliotekwa M23

Sehemu iliyonisisimua ni hapo maelfu na maelfu ya ng'ombe wanaolindwa na watutsi. Yani mleta mada wamesafiri kilomita 100 nikupita tu katikati ya ng'ombe. Dah 100 km siyo mchezo very interesting.

Watakuwa tu ng'ombe wa kagame jamaa anapenda ng'ombe.

Hao chini ni Inyambo cows fahari ya Rwanda. Watutsi wanawapenda sana.

ankole-long-horned-cows-1.jpg
FB_IMG_1674920600327.jpg

Arovera
 
.
Katika harakati zangu za kujikomboa na umasikini, niliamua kufanya ziara ya kusaka fursa Mpya nchini Congo. Nilikua tayari nimeshapata masimulizi mengi ya upatikanaji wa madini ya dhahabu na Rubi.

Ni mnamo mwaka Juzi mwanzoni nikiwa mji wa Uvira amabapo jilikutana najamaa Akiwa na jiwe alilo dai kuwa ni Rubi

View attachment 2497370
Baada ya mazungumzo marefu jamaa alikubali kunipa jiwe Moja ambalo alisema kuwa alishawahi kulipeleka Kigali Rwanda lakini katika vipimo ilitoa majibu yanayo Changanya. Ilisoma upande Moja ni Rubi na wakati mwingine inasoma Spinel. Sasa akanionesha ndoo imekaa mawe ya Kila namna. Kazi yangu nilitakiwa kwanza kwenda Tanzania kupima jiwe hilo ili tujue ni aina Gani ya jiwe Kisha nitafute mteja wa Uhakika ambaye tutakuwa tunampa Mzigo.

Kazi hiyo nikaichukua na kuanza safari, sikuhiyo nililala Bujumbura na keshoyake nikalala Kigoma. Asubuhi nilianza safari mpaka Arusha. Pamoja na kuzongwa na matapale na kashkash nyingi nilifanikiwa kufanya vipimo na bahati mbaya jiwe lilikua feki .
Pale Arusha nilikutana na wadau wengi sana na kupewa michongo nankutiwa moyo sana. Nilianza kuiona Dunia ya dealers. Sasa kazi ilaanza kutafuta connection ili nikasake Mzigo. Hapo ndipo safari wa Kivu kaskazini ikaanza.

Kiukweli sikuwa najua mawazo yangu ni hatari kiasi gani lakini laiti ningelijua pengine ningeanza kuungama dhambi zangu kwanza kabla ya kuanza safari katika ukanda wa damu mbichi.

Wakati ukawadia na safari ikaanza, niliambiwa nitafute biashara ya kwenda mayo ili nizugie kuingia mayo maeneo ya ndani na machimboni. Kwanza nikawaza kupeleka Nguo za kiume Jeans za masela na Viatu moka za Bakulutu na Kisha nikafikiria kupeleka Mchele. Baada tathmini jikapeleka Jeans Viatu na Samaki. Nilidhamilia kukutana na kamii ya Kila namna nanjinsia zote nilidhamilia kufa au kurudi na Mali. Militia taarifa za AWALI kujua hata mavazi ninayotakiwa kuvaa nikiwa huko. Nilihakikisha ninachukua kilataarifa Kwa uzito unao stahili.

Nilijifunza kuhisabu na kutaja pesa Kwa kifaransa, ndani ya wiki Moja nilijua kuhesabu Moja mpaka Milioni na kutaja pesa na maneno muhim ya kibiashara. Mfano Congo neno Kuuza wao linamaana ya kununua kuuu. Nipatie, kombola, mbasela na maneno mengine kama kutaja rangi na kusalimia. Bahati ni kwamba Kiswahili Cha Kivu kinafanana sana na Kiswahili Cha Tanzania Bara tofauti na hawachanganyi sana french kama wale wa Lubumbashi na Kinshasa.
View attachment 2497368
Safari ilianza Kwa kupitia Burundi Kisha kuingia mji wa Uvira. Hapo nililala na kesho nikapanda Hiache kwenda Mji wa Bukavu. Nilikua na machaguo mawili aidha kupitia Barabara ya ndani ya Congo au kupitia Rusizi Kisha Rwanda na kurudi tena Congo.
Barabara ya ndani ya Congo ni mbaya sana na hatari sana, wanapita watu wahalifu na wanao ogopa ukaguzi wa Rwanda na ukifika unafanyiwa sherehe yaani makorongo na magari kuanguka sio habari tena, kutekwa na kuuwawa ni kawaida kuliko kusaliklmiana. Hii inaitwa Barabara ya Ngomo(Kaburi wazi)

Changamoto ya kupitia Rwanda, ukiwa na Visa ya Dola 50 basi ukiingia Rwanda Visa ya Congo imeisha na ukitaka tena kuingia Congo Kwa kutokea Barabara mchepuko ya Rwanda basi utalazimika kulipia Visa tena, kwahiyo kupitia njia hiyo utalipa Dola 200 kwenda na kurudi.

Suluhisho ni Visa ya Dolar100 ambayo unapewa miezi mitatu na unaweza kutoka Congo na kuingia kadili uwezavyo. Hilo nilisha lifuatilia mapemaa, nikawa na Visa ya Dola100 nikapita Rwanda. Kuna mengi hapa Rwanda lakini kwakua sio mada ya Leo itoshe kusema ni Dunia tofauti sana. Tuishi bongo tu, amani inatosha .

Sasa niliingia mjini Bukavu kupitia mpaka wa Rusizi. Pale Bukavu wakati nimeingia nikakuta watu wanafunga maduka na kukimbia kujificha, nilipojaribu kuuliza wakasema Kuna vita imetangazwa M23 wanaingia Leo.

Hapo nilitetemeka sana, nikawaza nirudi Rwanda lakini ukaguzi na Mahojiano ya Rwanda yalinipa hofu, maana ilifika wakati nashuhswa kwenye gari nafanyiwa Mahojiano maalum . Nilishangaa Kila yulipopita nakuta askari wanajua Kuna Mtanzani Yuko kwenye gari.

Nilikuwa nahojiwa Kwa muda mrefu mpaka abiria wanalalamika, abiria Wote walikua Wakongo na karoko mswahili Mimi, askari wa Rwanda hawamuelewi wanashangaa Mtanzani kupitia pale.

Sasa Hali Ile ilinipa hofu ya kurudi Rwanda na nikakumbuka adhima yangu Bado, safari yangu Bado na lazima nifike.

Hapo nilisajili lakini ya Simu na kuweka vocha niajiunga mitandao yote na kupata dakika 3 Kwa Buku...

Haraharaka nikapita mtu wa toroli wao wanapita shareti, nikapakia mizigo tukaelekea Bandarini. Kutoka Bukavu kwenda Guma Kuna ziwa Kivu hapo unapanda meli usiku Kucha unafika kesho Asubuhi. Lengo langu niondoka Bukavu na usiku niwe kwenye meli ili hata vita ikitokea Mimi nakua kwenye meli. Bandarini nilikuta Meli nyingi ila nikaamua kupanda "Emanele04" waniita Emauele katre, hii Bei yake Iko juu na wanapanda watu wenye uwezo na mabishoo.

Lengo langu nilitaka kuanza kukutana na watu ambao wanaweza kunipa michongo ya machimbo au kupata connection za dealer wazuri. Katika safari yangu nilikua mkimya sana kwani Kila nilipo jaribu kuongea watu waligeuka kunitazama, nikagindua Kiswahili changu kinaniumbu jambo ambalo sikulitaka hasa kulingana na treatment ya Wanyarwanda.

Usiku niliingia Club na kukaa Kwa muda Kisha nikarudi, mpaka wakati huo sikupata mtu wa kuanza mazungumzo naye. Tukiwa njiani upande Moja nchi kavu kulikuwa Giza huko ni Congo kisiwa kinaitwa Idjwi na upande mwingine Kuna mataa sana, huko ni Rwanda na mataa yale ni miji na vijiji.
Asubuhi tulifika Bandarini Goma.

Hapo nilikuwa makini kuangalia watu wenye mizigo kama yangu hasa samaki ili nijue wanako wapeleka. Kuna dada Moja alikua na Samaki mwengi. Niliadhimia kujiweka karibu yake.

Wakati anapakia kwenye gari kupeleka stoo ndipo nikasogea na kumuomba anipakilie Mzigo wangu nitachangia garama, dada yule alikubali na Alipo niuliza napeleka wapi nikamwambia Kuna mtu tutamkuta hapo mbele ndiye anajua stoo ilipo, lakini haikua kweli..

Tulienda mpaka nakoenda yeye, na tukiwa njiani nilikwambia ukweli kuwa sina stoo Bali nimekuja tujaribu biashara. Alipo niuliza Bei za Samaki Tanzania nilimdanganya nikamwambia Bei ya chini sana kiasi akawa anatamani nimpeleke huko chimbo. Leongo langu lilitimia na tulipo fika stoo kitu Cha kwanza alimueleza mume wake kuhusu Bei za Samaki Tanzania na kuanzia hapo hao wakawa weneji wangu.

Kesho yake nilizunguka mjini Goma mpaka sehem inaitwa Bireree hapo ni mjini na ndipo mpakani na Gisenyi Rwanda, yaani border Ile Iko kama ilivyoisha Tunduma na Nakonde Zambia.

Nyumba zimeungana za Rwanda na Congo. Soko na mishe nyingi ziko upande wa Congo . Asubuhi Wanyarwanda wanavuka kufungua biashara zao huko Goma ni jioni kurejea kwao.

View attachment 2497412
Hapo ni katikati ya mji wa Goma. Sanamu la Chukudu kama alama za vijana kuchapa kazi.

Nilitumia siku tatu nilizo Kaa hapo Goma ili kukusanya intelijensia muhim Kwa safari yangu. Nilioewa masimulizi ya vita na uharifu. Mji wa Goma mpaka Sasa uko Chini ya utawala wa Kijeshi.

Pale hakuna mbunge wala mkuu wa Mkoa. Niuongizi wa Kijeshi, hii ni sababu mji wa Goma na wilaya zake ni ukanda wa Vita na machafuko Kila wakati.

Pale nilishuhudia kusikia Simulizi za YouTuber wa Tanzania Denis Mpagaze zikipigwa redioni akisikuli mambo ya uzalendo Kwa Afrika.

Pia Kuna redio ya watu wanajiita Kimbanguist hao wanarusha hotuba za Magufuli na kumtaja kama shujaa wa Afrika. Wakati huo Stori za Magufuli zilivutia sana na nikama ukimzungumzia vizuri tu, hapo niliwasoma mapema Wakongo nikawa namsifia Magufuli basi wakanipenda na kupata marafiki.

Nilianza kuoneshwa askari waasibwa maimai wakiwa mtaani kama raia wa kawaida tu.

Mji wa Goma umefimikwa na mawe ya Volcano na nyumba karibu zote zimejengwa Kwa mawe ya Volcano au mbao.

Nilifanya intelijensia yangu na kukamilisha Sasa safari ikawa ni kuelekea sehem inaitwa Walikale.

Mwanzo nilitaka kwenda semem inaitwa Beni au Butembo huko mnako sikia vita Kila siku lakini kilikua kumepigwa vita Kali sana na ADF wamechinja watu.

Pia kilikua na taarifa za watanzania kukutwa kwenye jeshi la ADF na wakatekwa. Hii ilinipa hofu nikajua huku Watanzania hautuaminiki tena na kwakua ni ukanda wa Vita wanaweza kunikamata Kwa kushakia usalama wao tu. Pia ilitakiwa nipitie mji wa Rutchuru huko M23 waliko ondoka baada ya Kenya kupeleka majeshi.

Niliambiwa tungepita Virunga na huko tunapata escort ya jeshi lakini kikinuka majeshi wanakimbia mnaachwa porini na kutekwa. Wanaume mnalazimisha kujiunga na jeshi la waasi na wanawake wanaolewa na ADF au M23. Hiyo ikatosha kiua mpango wangu.

Sasa uslekeo ni Walikale na nisafari ya wiki Moja na Sio Chini ya siku Tano. Huko wakaniambia wanafanya butter trade yaani unawapa samaki.

Pia masela wakipenda jeans hasa zile zenye mapichapicha basi wanakupa Madini hasa dhahabu na hapo mnakadiliaana tu.

Huko ikawa changua Bora. Kitu ambacho sikuzingatia ni usalama wa Barabara na aina ya usafiri. Mawazo yangu yalikua kwenye Madini tu. Safari ikawadia nikiwa na yule dada wa samaki mwenyeji wangu. Wakati huo Wote sikuwa nimemueleza lengo la safari yangu, yeye alikua anafurahi kuja Tanzania kuzoa samaki Kwa Bei Chee. Alinipa Kila msada ilimradi tu niwe na amani.
Siku ya safari Tulienda sehem inaitwa KwaAroxii , hapo tulikuta Maroli mengi aina ya Mercedes Benz Actros yakiwa yanapakia. Magari yalikua wazi Kwa Nyuma na hayana Bomba.
Hapo mizigo inapakiwa mapaka juuu, Kisha watu wanagombania kukaa juu ya mizigo. Nilijaribu kupya sehem nzuri lakini nilishindwa. Nilijibana Kwa mbele hapo nilikaa kwenye body huku miguu ukiwa juu ya Cabin juu ya dereva. Gari likinesa miguu inaning'inia na kutua juu ya Cabin, napo nimekalia tako Moja. Nilijibana sana nikakaa katikati. Safari ikaanza na hapo sikujua kumbe tulikua tunaingia Dunia ya wafu, huko kufa ni kawaida kuliko kuishi, Wanasema Zone rujhe yaani Red zone au Ukanda wa Damu.
Baada ya safari ya kama kilomita 50 tulikua nje ya mji wa Goma na hapo tulikuta Kuzuizi Cha jeshi. Hapo wanakagua Kila mtu kujua anakoenda na anaenda kufanya nini. Nilijaribu sana kukwepa lakini ilitoka amri ya wanaume Wote kushuka Chini.
Yule dada alinisogele na akasema ukiulizwa waambie Mimi ni mke wako tunakwenda kusalimia ukweni. Ikafika zamu yangu kupekuliwa, pesa nilikua na karobia Dola 500 nimezificha kwenye begi ambalo yukonalo yule dada.
"Peti yakawa,...... , Hapo ilimwagija lingala ya vitisho na walipooona sijibu Moja alikua pembeni alikoki silaha yake. Na kusogea pembeni, moyo ukienda mbio nikajua anataka kunifyatulia risasi. Niliamua kuongea Kiswahili Cha Tanzania pure, na hapo wakajua Mimi ni mbongo. Yule askari akamzuwia mwenzie nabkumuita. Jamaa alikua ananuka Bangi na pombe, gwanda zimechoka vibaya. Taarifa kuwa Kuna Mtanzani zikasambaa wakaanza kukusanyika. Dakika mbili mbele ikatoka amri nikaonane na Mkuu wako "Weye kuya hapa Kwa shefu" kilikua na Banda la turubai pembeni huko yupo boss wao. Nikaingia Kwa kuinama. Huko nilimkuta jamaa mstaaarabu Akiwa amezungukwa na walizi.
Pembeni kulikuwa na vijana wanne watusi na walikua wameshakiwa kuwa ni M23. Simu zao zilikiua Inapekuliwa nankukutwa picha zao wakiwa na kombati za jeshi la Rwanda. Gafla wakatolewa nje, nikiwa mle ndani nikihojiwa gafla ilisikika mlio wa risai. Yule boss aligundua hufu yangu, akaniuliza "weye mtanzania unaenda huko huyo bibi yako hayakuambia kama kule ni fasi ya mubaya?" Mikamwambia kuwa ninajua lakini titawahi kurudi haraka. Jamaa aliniomba Hela ya bia nikampa Franga 2000. Kitu inatakiwa kujua ni Askari wa Congo hawaombi Hela nyingi.
Nilipotoka nikakuta nasubiriwa Mimi peke yangu. Wale M23 sikujua nini kimewakuta zaidi ya ule mshindo wa chuma.
Safari ikaendea mpaka mji wa Masisi hapo ni kama mwisho wa kuona majumba, Sasa tunaanza milima na maporomoko ya msitumi. Huko utakuta vibanda vya Nyasi Kandi ya Barabara na askari wa Serikali wako hapo wanafanya doria. Baada ya kutembea kama kilomita 200 tulikua uwanda wa juu sana, baridi na upepo mkali. Nilianza kuona makundi makubwa ya ng'ombe wanao lindwa na walizi wa kitusi. Nilipo uliza nikaambiwa kuwa hao ni ng'ombe wa Raia Joseph Kabila. Wengine walisema ng'ombe wa Kagame. Tumesafiri zaidi ya kilomita 100 tukiwa katika ya makundi ya ng'ombe. Safari iliendelea mpaka kufika saa tatu usiku tulifika katika mji wa KITCHANGA, mji huu ambao M23 Leo wameuteka. Hao ni mji muhim sana kwani unaunganisha miji ya Goma na Bukavu Kwa upande wa magharibi na ni mji unao pitisha huduma ya chakula kwenda miji mingi sana. Mji huu ni kama roho ya maisha ya watu na uchumi.
Tulifika na kulala kwenye mgahawa wa mbao na wengine walilala nje. Hapo Kuna baridi Kali sana. Ilipofika usiku wa manane ilitoka amri ya kuzima mataa na kukaa kimya. Tulishangaa bila kujua kinachowndelea. Yule mama mmiliki wa mgahawa alijisahau kuzima taa chumbani mwake, kumbe wajuba waliona mwanga Kwa nje. Dakika chache baadae vilisikika vishindo vikumbwa sana na sauti za kiume ambazo ni kama walikua wakiimba huku wamefunga midomo. Wakiimba na kupiga vishindo Kwa pamoja na kuitikia Kwa kuunguruma. Tulipata hofu sana. Walikuja na kuzunguka Ile mgahawa wa mbao. Yule mama akatueleza kulala Chini sakafuni na tusikijitikise Kisha akajitosa yeye kuokoa maisha yetu. Wakamuamuru kuzima taa Kisha wakondoka naye kusikojulikana. Yulikaa mpaka asubuhi tukiwa na hofu sana.
Ilipofika asubuhi yule mama alikuja na kuomba tumchangie pesa ili anunue mbuzi wawili wa faini. Akatueleza kuwa wale walikua ni wazee wa Mila wanafanya tambiko la mji ule na kukutwa hajazima taa ni kosa na wangejua mule Kuna wageni basi tunguwawa. Anasema wale wajuba walikua na vichwa vya watu vimetungwa kwenye miti na kule walipo mpeleka alishuhudia wanazika mtu Akiwa hai inagwa hakumjua yule mtu. Yeye walimzuwia wakasema atakesha nao na kesho saa sita apeleke mbuzi wawili Kwa chifu wao. Tulipo muuliza akasema ni kawaida kufanya Tambiko Kila ifikapo mwisho wa mwaka. Na sikuile ilikua siku ya Tambiko.
Hapo KITCHANGA Kuna sananu la mwanamke linaabudiwa na linabadilishwa Nguo Kila mwaka.
Safari iliendelea na huko mbele kadili tulivyokua tukisogea ndivyo tulikua tunazidi kukiendea kifo. Hapo KITCHANGA ndio mwisho wa kupata internet na mpaka hapo sikuwa na mawasiliano na Ndugu zangu nilipiga simu za mwisho na kutoa malekekezo Kwa kina katika Kila jambo langu. Nilikua kama naaga au kutoa wosia wa mwisho bila ndugu zangu kujua. Nilikata tamaa ya kurudi hai, tulikua tayari katikati ya makundi zaidi ya 20 ya waasi na magenge ya watekaji. Wenyeji walionekana kuwa na hofu huku Mimi nikiwa hoitaabani. Masimulizi ya ujambazi na vita yalitawala, tulipita maeneo yenye Kila kumbukumbu ya mauaji. Jambo la kushangaza ni kuwa huko ni kama tulikua tumevuka mpaka na kuingia Rwanda, watu wanao ongea Kiswahili walizidi kupugua na wengi walibaki waliokua kwenye gari. Tulianza kupitia vijiji vya Watusi na vijiji vya wahutu Wote kutoka Rwanda. Hofu ilizidi kutanda.Tulifika sehem inaitwa Mweso, hapo ni Kambi wa wakimbizi wa Rwanda ambao wameshafanya Kijiji na Kuna Kambi ya Majeshi ya MUNOSCO na ofisi za nji nyingi zenye Operation zao Congo. Mabango ya UN,UNICEF , USaid na Japan aid na Kila shirika la kimataifa basi liko hapo. Pomoja na hivyo haizuwii kitu sababu hao Wote hawaingilii mapigano yoyote.
Tulipumzika hapo kidogo Kisha safari iliendelea.
Kabla ya kukiacha hiki Kijiji dereva alisisimama sehem watu wakashuka kuchimba dawa na Kisha wakakusanyika na kuanza kuomba Mungu. Kitendo hicho kilinipa hafu ambayo sijawahi kuipata na kwamara ya Kwanza nikatamani kurudi Nyuma , niliuliza kama naweza kupata usafiri lakini wakasema mpaka gari hilo lirudi hivyo hakuna kurudi Nyuma. Yake maombi sikutaka hata kuuliza maana waliomba Kwa Kiswahili na ni kama ilikua Sala ya toba na kukabidhi roho Kwa Muumba...
Itandelea
 
nilikua na project moja maeneo ya Gisenyi, nje ya mji huu na kuja asubuhi kufanya shughuli zangu kule juu milimani kwenye volcano zilizokufa,ile tunafika asubuhi kuendelea na shughuli zetu tukaambiwa kuna maiti zimezagaa mtaani kwakua jamaa wa M23 wamepita alfajiri na mara nyingi wanakuja chukua vyakula au kuteka watu na kuwafanya askari wao, tunaambiwa kila ikifika saa 11 jioni tunasitisha kufanya kazi tunaondoka kabisa mji huo, vizuizi vya ukaguzi vilikuwepo ila sikupata changamoto yoyote kwa askari/wanajeshi wa Rwanda na hasa nilipokua naonyesha passport yangu wanafurahia sana kuja TZ and kupiga story then wanakuachia, marehemu (mola amrehemu) Magu wanampenda sana tena mno kule.
 
Msukuma anakuambia hakuna Ng'ombe hapo kuna Mapembe.
Sehemu iliyonisisimua ni hapo maelfu na maelfu ya ng'ombe wanaolindwa na watutsi. Yani mleta mada wamesafiri kilomita 100 nikupita tu katikati ya ng'ombe. Dah 100 km siyo mchezo very interesting.

Watakuwa tu ng'ombe wa kagame jamaa anapenda ng'ombe.

Hao chini ni Inyambo cows fahari ya Rwanda. Watutsi wanawapenda sana.

View attachment 2498506View attachment 2498507

Arovera
 
Justine Marack nikung'ate sikio yakuwa ukidhamiria kuleta mada jf basi jitahidi kufanya likamilike kama uliamua kushare Yale muhimu hapa tafadhali Fanya hima watu waelimike na kuburudika hv unavyochelewa kuendelea kusimulia aisee unakaribisha kudhihakiwa, kupewa maneno yasiyopendeza na baadae unaeza Iona jf chungu.

USHAURI - unaposimulia hapa inamaanisha wewe unajua hicho na Kuna watu watakoment watasema vile basi nawe utakuwa umeongeza maarifa ama kuburudika.

Usikae Kila muda unachungulia Uzi wako umefika page ngap Bali lete stori tujifunze/kuburudika wote wewe na sisi.

Usiku mwema.
 
Write your reply...kule kuna vita mara kwa mara sababu ya madini ya vitu n mengi,hku katanga shwari tu.
 
Ikiendelea ni tag please
 
Asee
 
Kuna watu mnatukana bila sababu. Sio lazima usome. Kazi sio kuandika tu tunamajukumu mengine. So tuwe na staha kidogo wengine Sio wavumilivu wa kutukanwa bila aababu
Ukija na jambo humu jaribu kujifanya chiz humu watu wanakuchokonoa maksud Ili uzire tuu au umjalii tuu ndio mana nilikushauri jaribu kukitoa mana jf arosto ya stori kama Hz wanazo wengi sana.

Wapuuze shusha kipande muda huu Mzee kesho wakutane nacho
 
Sehemu iliyonisisimua ni hapo maelfu na maelfu ya ng'ombe wanaolindwa na watutsi. Yani mleta mada wamesafiri kilomita 100 nikupita tu katikati ya ng'ombe. Dah 100 km siyo mchezo very interesting.

Watakuwa tu ng'ombe wa kagame jamaa anapenda ng'ombe.

Hao chini ni Inyambo cows fahari ya Rwanda. Watutsi wanawapenda sana.

View attachment 2498506View attachment 2498507

Arovera
Vp pembe zao nazo zinauzwa au akisha chinjwa zinatupwa dampo? Pia naomba kufahamishwa utofauti wa pembe za hao ng'ombe na zile za ndovu na faru
 
Very interesting story..... Bila ya mwendelezo.
Nina mpango wa kuitembelea Congo hasa Yale maeneo ya Kivu kusini au Goma kwa ujumla, mpaka sasa naendelea kukusanya taharifa za kiintelejensia kuhusu ayo maeneo, ingawa naambiwa kuna watu makatili sana lkn Mimi uwa napenda sana awo watu makatili kwa maana ndiyo watu ambao ukiibahatika kuzoeana nao wakakubali basi utakuwa unaweza kutimiza lengo lako kiuraisi sana,Congo ni taiga ambalo limejaa rasilimali kibao unaambiwa kuna maeneo nyumba zimekandikiwa udongo wa dhaabu ukiweka Mashine kwenye kuta zao ngoma inasoma PPM za kutosha, na kwa wale wazee wa Carbon uko ndo balaa unaambiwa mkamuo moja tu wa tani moja ya Carbon unaweza toka na 1.5 kg ya gold...unaambiwa mzigo upo wa kutosha.
Vijana tupunguze uoga, twende tukapambane....
 
Back
Top Bottom