Kama ilivyokuwa kwa Ethiopia, Misri imeanza cChokochoko na hujuma za kukwamisha ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme Sudan Kusini

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Nchi changa ya Sudan Kusini imelalamika kwamba Egypt inailetea Chokochoko na Figisu ili ikwame kuanza Ujenzi wa Mabwawa kadhaa ya Kuzalisha umeme mgwt 2,000 hususani bwawa la Wau ambalo linategemea Kuzalisha umeme ,kutoa maji ya Kilimo na Matumizi ya nyumbani.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Sudan Kusini amenukuliwa akisema Misri imekuwa ikihujumu Juhudi za kujenga mabwawa hayo kwenye Matawi ya Mito ambayo hujaza maji kwenye Mto Nile licha ya kwamba waliingia makubaliano ya ujenzi na Egypt walipitisha ila Sasa wanaleta vikwazo.

Licha ya vikwazo hivyo South Sudan imesema itasonga mbele na hatua ya ujenzi licha ya vikwazo vya Egypt.


View: https://twitter.com/ebczena/status/1734190498355827095?t=dd-q0h9-x0vvHhWU-hfBYA&s=19

My Take
Ujinga kama huu Egypt ilifanya Kwa Ethiopia ikiwemo vitisho lakini Walisonga Mbele.

Sudan Kusini komaeni na msikubali kupangiwa na Misri Kwa sababu hakuna mahala maji ya Mto Nile yamepungua Kwa Ethiopia kujengwa bwawa au Tanzania kutumia kwenye shughuli za Watu na Sasa tunayapeleka Dodoma kufanya irrigation farming.
 
Nchi za Africa Mashariki ziiunge mkono Sudan Kusini maana inaweza kuonewa na Egypt Kwa kuwa tuu Haina Misuki ya kijeshi ya kukabiliana na Misri.
 
Back
Top Bottom