Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,621
- 46,267
Janjaweed ni kundi la wanamgambo Waarabu lililoundwa kwa msaada wa serikali ya Sudan ya wakati huo ya Omar Al-Bashir kupambana na uasi wa kujitenga wa Darfur, inayokaliwa na watu weusi.
Janjaweed wanakadiriwa kuua karibia robo hadi nusu milioni ya watu weusi wakazi wa Darfur katika mauaji ya kimbari, walifanya ubakaji, ulawiti, ujambazi na kila aina ya dhulma dhidi ya binadamu. Pia vita vyao hivyo vilisababisha wakimbizi zaidi ya milioni 2 kutoka eneo hilo.
Wakati haya yote yanafanyika Africa Kusini haijawahi kujigusa hata Umoja wa Africa(AU) kuinyooshea kidole Serikali ya Sudan ya Omar Al-Bashir achilia mbali kufungua kesi katika mahakama ya kimataifa ya ICJ kutetea weusi wenzao wa huko Darfur waliokuwa wakiishi katika mazingira ambayo wakati mmoja yalijulikana kama nusu ya Jehanamu.
Huu ni unafiki mkubwa nchi hii inafanya huko ICJ katika hii kesi yake dhidi ya Israel.
Fadhila huanzia nyumbani na Darfur ni nyumbani zaidi kwa Africa ya Kusini kuliko Palestina.