Ndugu zanguni, wiki mbili zilizo pita nilileta uzi hum Jf lengo likiwa ni Kuomba /kuuliza namna ya kufika SA. Nilipata ushauri mwingi mno, mzuri, mbaya, wakunijenga, wakunikebehi Nk. Pamoja na hayo yote Mungu awabariki sana kwa ushauri wenu mzuri.
Safari nimeianza jana nikitokea Babati mtaa wa Nyunguu, leo ndio nimeanza safari tena nikitokea Dar. Nauli nimetoa elf 45 mpaka Tunduma. Kiukweli moyoni nina hofu yenye mchanganyiko na furaha, Johannesburg sijawahi kufika, ila najua Mungu atafanya tu.
Ombi langu kwenu kila mmoja asiogope kutoka. Mi leo nimethubutu, nikifika tu JoBeg Ntawapa picha, huko nimejipanga kufanya kazi yoyote ambayo ni halali, hata km ni kuosha vyombo hotelni. Mbarikiwe sana