Safari ya South Africa ndio nimeanza

Safari ya South Africa ndio nimeanza

Kama nakujua vile mm nipo Majengo mapya kwa sasa , all da best master Mungu akuongeze.
Huwezi kunijua, Babati nimekaa miaka 2.5 tu, Lakin pia nilikuwa sishindi mjini, nikuwa napasua mawe kule Imbilili ndani ndani na kuyauza. Nimesota sana kaka, mpaka nahisi machozi, wala siamin km niko ndani ya Bus
 
Shibekijijini...we nenda kila kitu kinawezekana..ukiona mtu anasema hiki hakiwezekani jua yeye ndo hawezekani..
Mimi mwezi huu nitaenda Namibia kwanza
 
Shibekijijini...we nenda kila kitu kinawezekana..ukiona mtu anasema hiki hakiwezekani jua yeye ndo hawezekani..
Mimi mwezi huu nitaenda Namibia kwanza
Asante kwa kunitia Moyo. Nashukuru Mungu wengi wamesema watanifata, Hasa kulingana na view nitakayo iona huko.
 
Cape Town naona ni mbali Sana, Hasa nikiangalia umbali ulipo, Pritoria kidogo naona ni karibu, ila kadri ntakavyo kuwa mwenyeji naweza kwenda, km una neno lolote lonaloweza kuwa na faida au la kunijenga we niambie tu Bro, maisha ni safari ndefu, you never know about tomorrow (nimeanza kufanya mazoez ya Kingereza)

Wenyeji wenyewe hawaongei kiingereza kizuri ila chenye kuchanganyika na kizulu, usiwe na shaka aisee umefika wapi sasa hivi
 
Wenyeji wenyewe hawaongei kiingereza kizuri ila chenye kuchanganyika na kizulu, usiwe na shaka aisee umefika wapi sasa hivi
Ayse njia hii sio mwenyeji sana, ila tumesha pita morogoro, tupo ndani ndani huku, ntawajulisha tu, ila torch nyingi sana bara barani
 
Ukifika upambane kwelikweli...vinginevyo hata uliowaacha wanalima huku utawatamani. Otherwise all the very best
 
Naomba nikujibu kaka, kila mtu anakuwa na vision zake, mimi nyumbani sijafukuzwa wala Mtaani, japo nilikuwa siishi na wazazi, nikiona hakuna chochote ninacho ona cha kufanya ntarudi Tz. Sio lazima eti kwakua wengi wanauza Hayo MA uchafu eti na mimi lazima niuze km wao, kwanza mimi nimeokoka, nina ujuzi wa kupiga mziki, ni It, nk nitaosha hata vyombo kwa mama Ntilie wa Ki-kabulu, haaaaaaaa ili mradi tu maisha yasonge.
nimekupa tu angalizo kwamba kuna hiyo ishu na vijana wengi sana wa kitanzania wameingia. Kwa hiyo sijasema wewe utauza. Kama hutauza hiyo ni heri.
 
Mkuu sipendi nikukatishe tamaa, lakini kama maisha ya Tanzania yamekushinda, basi ku-win nje ya nchi ni kazi sana! i am talking with experience ndugu, kikubwa nenda ukijua sio rahisi sana, upambane sana
 
Ulishaenda nchi gani kutafuta hela utupe ushuhuda
 
Hakuna sehemu (nchi) ambayoRaia na Mgeni wanaweza kutumia nguvu na akili ya kupipatia kipato na mkono kwenda kinywani kama Tanzania....

Bongo ikikushinda ni bora ukubali matokeo.....
Au unakwenda kulala nje huko uendako...?!
 
Mkuu sipendi nikukatishe tamaa, lakini kama maisha ya Tanzania yamekushinda, basi ku-win nje ya nchi ni kazi sana! i am talking with experience ndugu, kikubwa nenda ukijua sio rahisi sana, upambane sana
Siwez kukubishia, huenda unajua unacho manisha, ila na wewe uelewe kwamba Tz sijafukuzwa, nikishindwa ntarudi tu. Lakini pia ingekuwa vzr km ungefafanua huo ugum wa kuwin utakuja vp ili nijue namna ya kupambana, km huwez basi kaa kimya ili isije ikawaonyesha watu kwamba una wivu.
 
Huwezi kunijua, Babati nimekaa miaka 2.5 tu, Lakin pia nilikuwa sishindi mjini, nikuwa napasua mawe kule Imbilili ndani ndani na kuyauza. Nimesota sana kaka, mpaka nahisi machozi, wala siamin km niko ndani ya Bus
Ukifika tu nijulishe nikuambie chimbo zuri la kukaa. Achana na J'burg wala Cape. Kuna province za wastaarabu wala hutaona wahuni wahuni. Ukifika tu na kuwa mwenyeji utajuta kupoteza muda
 
Mhimu ni passport, VISA na vibali vyako vinavyoonyesha unaenda kufanya nini angalau uwe na kahela kakuanzia.[/QUOTE
Kama ni MTZ hahitaji VISA kwenda SA labda passport, vyeti vya chanjo za kimatafa na nauli tu.
 
Hakuna kazi huko we kauze ndizi aka mgundi au kama una vyeti vyako kazi utapata
 
Hakuna sehemu (nchi) ambayoRaia na Mgeni wanaweza kutumia nguvu na akili ya kupipatia kipato na mkono kwenda kinywani kama Tanzania....

Bongo ikikushinda ni bora ukubali matokeo.....
Au unakwenda kulala nje huko uendako...?!
Huo ni mtazamo wako tu!!!
 
Ndugu zanguni, wiki mbili zilizo pita nilileta uzi hum Jf lengo likiwa ni Kuomba /kuuliza namna ya kufika SA. Nilipata ushauri mwingi mno, mzuri, mbaya, wakunijenga, wakunikebehi Nk. Pamoja na hayo yote Mungu awabariki sana kwa ushauri wenu mzuri.

Safari nimeianza jana nikitokea Babati mtaa wa Nyunguu, leo ndio nimeanza safari tena nikitokea Dar. Nauli nimetoa elf 45 mpaka Tunduma. Kiukweli moyoni nina hofu yenye mchanganyiko na furaha, Johannesburg sijawahi kufika, ila najua Mungu atafanya tu.

Ombi langu kwenu kila mmoja asiogope kutoka. Mi leo nimethubutu, nikifika tu JoBeg Ntawapa picha, huko nimejipanga kufanya kazi yoyote ambayo ni halali, hata km ni kuosha vyombo hotelni. Mbarikiwe sana

South Africa una kibali cha kukaa siku 90. Baada ya hapo utaishi kwa kibali gani, kama umeamua kenda bila kuwa na kibali cha kazi? Kumbuka ukizidisha siku zaidi ya 90 unapigwa marufuku kurudi South hadi miaka mitano.
 
Back
Top Bottom