Yule Jamaa etu aliyekwenda South Africa mbona hatupi Mrejesho tena

Tuwaseme

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
645
1,191
Kuna yule mwenzetu anaitwa Shibe Kijijini alisema anakwenda South.. Sijui alifika au hajafika maana kimya sana..

Nilikuwa navutiwa sana na simulizi yake. Kama hupo njoo bana uendelee kutupa Mrejesho..

Mrejesho wake wa mwisho ulikuwaga hivi


Habari za asubuhi ndugu zangu wa hapa Wengi najua mmengoja kupata habari au report ya mwendelezo wa safari yangu ya SA. Kuna changamoto nyingi sana njiani, usumbufu wa hapa na pale, leo ni siku ya 4 tangu nianze safari yangu ya Kutokea Nyunguu - Babati, to Johannesburg.Kwanza kabisa nimeambiwa hela pale kwenye mpaka wa Tunduma. Kuna jamaa walikimbia kugongewa mhuri ni hela sh elfu 30, ila wao wakasema watanisaidia kupeleka Migration office kwa 20 nikawapa, kumbe ni bureee kabisa, nikasema poa. Kwa sasa niko Zimbabwe ila hatujafika Harare bado sana. 1. Kila Border ni kushuka na mzigo yote wanakagua hadi kwenye buti, wengine nimeona wakikaguliwa hadi kwenye Madela (wamama), wababa hadi kwenye soks wanakagua Ngada. Muda mwingi utapotea kwa sababu ya ukaguzi.2. Hadi sasa nimeshatumia zaidi ya $160, Harare to Johannesburg nimeambiwa itanigharim Usd 70$ hiyo ni Transport peke ake.3. Nimekutana na hela ambazo nilikuwa sijui wala kuzisikia MF Kwacha, hivyo nimeonekana Mshamba maana hunilazimu kuisoma kila upande ili nijue ni sh ngapi?4. Nilikuwa sijawahi kushika $$$$ ila kwenye safari hii ndio natumia.5. Kuhusu vinywaji na vyakula njiani ni vingi km Kawaida. Ila tu Bia ndio haziruhusiwi ndani ya Bus.6. Nilisahau document yangu ya chanjo ya manjano kwahiyo imenisababishia usumbufu kwenye mipaka.NB: Usumbufu njiani upo kabisa ila km una Valid document (nyaraka halali) ni km unakwenda kwenu.Kwa atakaekuja huku usisahau kadi ya mpiga kura na vitambulisho vingine hata kama ni cha mkazi n.k.Mwisho, kadri Bus linavyozidi kusonga mbele ndivyo Lugha zinazidi kubadilika, hapa tulipo kiswahili sikisikii tena km juzi.Changamoto nyingine ni mawasiliano ya Simu ila nimeshanunua line nyingine ya South Africa MTN, ina rangi ya njano.Nilichogundua kabla ya kuanza safari maneno ni mengi mno ila kumbe ni kawaida tu. Document ni muhimu sana +$$ hakuna shida.Mungu awabariki.
 
daaah ata mimi kuna siku nilijiuliza jamaa vp au wamemfanya kitu mbaya kwa mugabe apo

ila all in all tumuombee mema na tuhisi kma yuko salama ugeni uko na mambo mengi anajipanga may be

Allah amfanyie wepesi katika kila jambo lake uko aliko...............amin
 
Nendeni Angola, Namibia au Botswana kwa mfanyakazi kumekaa vizuri Sana. Ninavyosikia kwa watu. Kwa South mm ninakujua kwa imekaa kama miaka saba .
 
Back
Top Bottom