Safari ya South Africa ndio nimeanza

shibekijijini

JF-Expert Member
May 26, 2015
358
478
Ndugu zanguni,

Wiki mbili zilizo pita nilileta uzi kuhusu;
https://www.jamiiforums.com/threads/south-africa-nitafikaje.1198997/
South Africa nitafikaje?


Safari nimeianza jana nikitokea Babati mtaa wa Nyunguu, leo ndio nimeanza safari tena nikitokea Dar. Nauli nimetoa elf 45 mpaka Tunduma. Kiukweli moyoni nina hofu yenye mchanganyiko na furaha, Johannesburg sijawahi kufika, ila najua Mungu atafanya tu.

Ombi langu kwenu kila mmoja asiogope kutoka. Mi leo nimethubutu, nikifika tu JoBeg Nitawapa picha, huko nimejipanga kufanya kazi yoyote ambayo ni halali, hata kama ni kuosha vyombo hotelni.

Mbarikiwe sana
 
Back
Top Bottom