Mrejesho wa safari yangu ya South Africa

shibekijijini

JF-Expert Member
May 26, 2015
358
478
Habari za asubuhi ndugu zangu wa hapa JF

Wengi najua mmengoja kupata habari au report ya mwendelezo wa safari yangu ya SA.

Kuna changamoto nyingi sana njiani, usumbufu wa hapa na pale, leo ni siku ya 4 tangu nianze safari yangu ya Kutokea Nyunguu - Babati, to Johannesburg.

Kwanza kabisa nimeambiwa hela pale kwenye mpaka wa Tunduma. Kuna jamaa walikimbia kugongewa mhuri ni hela sh elfu 30, ila wao wakasema watanisaidia kupeleka Migration office kwa 20 nikawapa, kumbe ni bureee kabisa, nikasema poa. Kwa sasa niko Zimbabwe ila hatujafika Harare bado sana.

MATATIZO

1. Kila Border ni kushuka na mzigo yote wanakagua hadi kwenye buti, wengine nimeona wakikaguliwa hadi kwenye Madela (wamama), wababa hadi kwenye soks wanakagua Ngada. Muda mwingi utapotea kwa sababu ya ukaguzi.

2. Hadi sasa nimeshatumia zaidi ya $160, Harare to Johannesburg nimeambiwa itanigharim Usd 70$ hiyo ni Transport peke ake.

3. Nimekutana na hela ambazo nilikuwa sijui wala kuzisikia MF Kwacha, hivyo nimeonekana Mshamba maana hunilazimu kuisoma kila upande ili nijue ni sh ngapi?

4. Nilikuwa sijawahi kushika $$$$ ila kwenye safari hii ndio natumia.

5. Kuhusu vinywaji na vyakula njiani ni vingi km Kawaida. Ila tu Bia ndio haziruhusiwi ndani ya Bus.

6. Nilisahau document yangu ya chanjo ya manjano kwahiyo imenisababishia usumbufu kwenye mipaka.

NB: Usumbufu njiani upo kabisa ila km una Valid document (nyaraka halali) ni km unakwenda kwenu.

Kwa atakaekuja huku usisahau kadi ya mpiga kura na vitambulisho vingine hata kama ni cha mkazi n.k.

Mwisho, kadri Bus linavyozidi kusonga mbele ndivyo Lugha zinazidi kubadilika, hapa tulipo kiswahili sikisikii tena km juzi.

Changamoto nyingine ni mawasiliano ya Simu ila nimeshanunua line nyingine ya South Africa MTN, ina rangi ya njano.

Nilichogundua kabla ya kuanza safari maneno ni mengi mno ila kumbe ni kawaida tu. Document ni muhimu sana +$$ hakuna shida.

Mungu awabariki.

- Rejea mwanzo wa safari yangu kwenye Minakasha hii miwili > South Africa nitafikaje? | Safari ya South Africa ndio nimeanza..
 
Kuwa makini Johannesburg. Kuwa makini zaidi endapo utaingia Johannesburg usiku. Kwa Kifupi Johannesburg sio rafiki kwa wageni. Hakikisha unalala Hotel kama ikibidi.
Kuna jamaa tumekutana nae, anaongea English mbovu mbovu, ananiambia kwamba eti Guest house za Jobeg huwa niza ku share, sasa eti ananiomba tukifika huko tuweze ku share room. Ila nimemwambia mimi nina mwenyeji wangu, SA japo sina, naogopa asije akanitanua somewhere.
 
Back
Top Bottom