Mentor
JF-Expert Member
- Oct 14, 2008
- 20,334
- 23,940
Safari ya Rwanda…
Najua wengi mnatarajia kusoma hadithi nzuri na tamu juu ya wadada warembo wa Kinyarwanda…wabantu haswa Madame B weka chini...wenye maumbo ya nyigu…sura nyembamba inayopambwa na tabasamu lenye kumtoa pesa mbahili (sio notifeki)…rangi za kibantu haswa wenye kujua majambozi kunako 6*6 ( Natalia u gotta go for some lessons from these ladies ).
Warefu..kila umwonae mzuri kuliko uliyemwona dakika chache zilizopita..sauti nyororo na wapole kama binti aliyetoka kufundwa…ukitaka sample nzuri mtafute Elizabeth dominick ujue nnachoongelea…aliye mfupi basi mrembo kama FirstLady…aliye mwembamba basi kimodo cha ukweh kama bi Asnam.
Ni safari yangu ya Rwanda niliyoenda na bosi wangu. Ilikuwa safari yangu ya mwisho na bosi wangu..R.I.P na sasa nimekaa natafakari ni bosi gani mwingine nitampata nakosa jibu. Lakini wakati huu wa majonzi nimetafakari sana juu ya safari yangu ya Rwanda.
Of course yote hapo mwanzo au tuseme mengi kati ya hayo ni kweli lakini hiyo ni hadithi ya siku nyingine (naogopa kumwaga kuku penye mchele mwingi nsije kosa mke)
Background:
Mentor ni mfanyakazi wa serikali katika wizara moja hapa nchini. Mentor anafanya kazi muhimu sana ya kuhakikisha bosi wake anafika mahali anapotaka kwa muda anaotaka (Well, wakati mwingine Mentor huchelewa na kugombezwa sana). Ila mentor anafurahia sana kazi yake maana inampeleka sehemu mbalimbali nchini. Watu humuita Mentor, dereva.
Mentor alimaliza mafunzo ya elimu ya kidato cha nne mwaka 1998, mwaka ambao matokeo yalifutwa na mitihani kurudiwa (my classmates elmagnifico, Kipaji Halisi, KakaKiiza). Alifanya tena mitihani ile na kupata daraja la pili (div 2 20 points thanks to waalimu wangu gfsonwin na snowhite @neggirl na @evelyn salt ). Baadaye alienda kidato cha tano shule ufundi ya Moshi. Matokeo hayakuwa mazuri sana kwenda chuo kikuu. Alienda kusoma diploma ya mechanical and motor engineering.
Mwaka jana alipata fursa ya kwenda US kujifunza auto tire system..kiufupi elimu yake angeweza kuitumia katika many manufacturing plants/viwanda.
Anyway mwezi uliopita nilienda Rwanda
Huko nilikutana na warembo wa ukweh..si ndiyo kazi yangu ni udereva. Baada ya kumchukua bosi asubuhi na kumshusha kwenye kikao mimi niko free na gari na pesa ya mafuta si tumeshapewa, posho yangu kibindoni…ndiyo serikali yetu pendwa inamlipa bosi wangu pesa ya dereva sasa mnashangaa nini!
Nilishangazwa sana na mambo mawili;
Cha kwanza…Kilichonishangaza ni kukuta magari tofauti tofauti yamepakiwa eneo la mkutano tofauti na huku kwetu ambapo ni kawaida kukuta ma VX V8 na mengine wanayoita FUEL GUZZLERS yamepangwa ambapo ‘waheshimiwa sana' wanakutana.
Cha pili…ni kuwa ukitoa gari la bosi wangu ambalo nilikuwa mimi ndani mengine yote yalikuwa empty. Yaani hakuna dereva.
Kila waziri, katibu sijui mkuu wa kitengo..woooote walikuwa wanaendesha magari yao wenyewe. Nilipouliza nikaambiwa ndiyo sera ya nchi. Yaani ni watu wanne tu nchi nzima ambao madereva wao wanalipwa na serikali (Raisi, Waziri Mkuu, Chief Justice na Spika).
On top of that, Magari ya serikali ni hayo manne tu (excluding magari ya jeshi na polisi). Ila wanachofanya wao ni unanunua gari unapewa pesa ya mafuta na maintenance. Kama unajisikia sana kuwa na dereva utamlipa mwenyewe from your own pocket.
Mimi na bosi wangu hili halikutughasi. Tuliondoka jioni nikaenda maeneo ya karibu na Umutara Polytechnic nikamchukulia mzigo wa ukweh bosi wangu nikampelekea hotelini..si ndo kazi yangu dereva bana..maswali ya nini sasa (msiniulize mimi nlifanyaje..)
Siku ya mwisho ya kikao nikapata mshangao mwingine (na hata huu si wa mwisho)…alikuja IGP wa Rwanda yani anaonekana mshkaji sana very alert Bwana E. Gassana. Yeye aliletwa na Dereva wake ndani ya gari ya jeshi. Nilijaribu kuchungulia kuona ma-bodyguard wake lakini hola..hana bodyguards IGP wa Rwanda!!!! Nikashtuka sana nikasema hili si sahihi…nikangoja ashuke ili nikamuulize dereva wake huenda wako nyuma au somewhere..SHOCK ON ME!
Dereva naye anashuka na notebooks naye anaingia kwenye kikao..damn!!! yani naye anatoa mchango kama wadau wengine anachukua minutes na vitu kama hivyo (kama wafanyavyo makatibu wa vikao wengine). Sio kwamba kazi yake ni kulala kwenye gari kama mimi na kupiga miayo tu (heeey…ninapokuwa nimelala huwa natafakari mustakabali wa nchi..excuse me! Na nikipiga miayo ni kuwa nimepata solution..yaani nimefikia ‘Ahaa moment' hence the confusion with miayo)
Ikabidi niwaulize walinzi wa pale vipi bodyguards wa mkuu wako wapi? Wakaniambia hana. Kisa? Eti yeye kama mkuu wa usalama wa ndani wa nchi akiwa na bodyguards inadepict kuwa nchi yake mwenyewe haiko salama, askari wake hawafanyi kazi yao hence therefore ndo maana anahitaji extra ulinzi!
Nkaguna..malizia mwenyewe kushangaa..
Kabla mshtuko wangu haujaisha kikao kikaisha. Nashangaa sioni ving'ora vya kuwasindikiza mawaziri na IGP na wakuu wengine waliokuwepo pale. Believe me, kulikuwa na high profile leaders wa nchi ile kiasi kwamba ingekuwa ni hapa kwetu bongo basi barabara zingefungwa from Ferry to Ubungo I tell you…
Jioni tukaenda nyumbani kwa waziri wa wizara kama anayofanyia bosi wangu. Mh…anaishi kwake nyumba aliyojenga mwenyewe yani eti nyumba za serikali ni nne tu!!! These guys are crazy..nikafikiria nikaona government expenditure zao zitakuwa very low..nkawaonea wivu!!!
Basi safari yangu ya Rwanda kabla ya kurudi ofisini wizarani ikanipitisha Tanga. Ndiyoo lazima uonje ladha zote..sasa ulitaka kula ladha za nje tu bila kula za ndani #sina maana hiyooo…
Ukiwa unatoka Tanga mjini kuja Segera apo maeneo tu ya mjini kuna magofu ambayo kwa wale wa zamani (mzee Dark City unahusika) watakutajia sijui hapa kilikuwa kiwanda cha nini sijui pale cha nini yani mpaka basi. Alimradi vyote vimebadilishwa First names kuwa "kilikuwa…"
Nikawaza sana nikasema hivi zile diploma zangu si zingefaaga sana huku viwandani? Niliwaza sana nikampigia simu rafiki yangu Mtambuzi (yeye ni dereva wa Asprin, waziri wa ...ngoja nimuombe ruhsa yake kwanza!) nikamuuliza,
Mentor; "Hivi ni kwanini serikali yetu imefanya hivi? (baada ya kumuelezea ya Rwanda)"
Mtambuzi; "Unajua nini Mentor, serikali isipoajiri hawa watu itabidi bado iwalishe na kuwatunza. So ni afadhali tu wawatafutie viajira vya alimradi tu wawe bize."
Mentor; "Lakini Mtambuzi, ubize gani wa masaa mawili kwa siku? Ubize gani wa kumpeleka bosi club na gari la serikali? Ubize gani wakati napiga miayo kutwa kucha? Ubize gani?"
Mtambuzi; "Si ndo hivyo at least mwisho wa mwezi unapata mshahara! Yani hapo ulitakiwa tu ulipwe na serikali hata kama hungekuwa dereva."
Mentor; "Ivoee… huku sio sawa na kumpa mtu samaki badala ya kumfundisha kuvua?"
Mentor; "Hivi wakifufua maviwanda yale sisi wenye diplomas zetu za VETA na kwingineko si tutapata pesa na bado tutaiingizia nchi pato?"
Mtambuzi ; "heheh na kweli aisee maana iyo pesa ya kutulipa ingetosha kufufua maviwanda mangapi? Unakumbuka juzi Alhamisi bungeni. Ebu fikiria madereva wote wale na marupurupu yote..sijui lakini wanasemaga, ‘kazi mbaya unapokuwa nayo'"
Mentor; "Hehe alafu hadi mbunge mangi!! Mbunge naye ana V8 mbe! Mhh..acha ya mbunge..sijui mkuu wa wilaya eti mangi! Diwani naye ana hadi dereva sijui kwa pesa nyingi ipi tuliyonayo..Kule kwa wenzetu unanunua gari utakaloweza kuafford kuendesha after umetoka hiyo ofisi..."
Simu nilikata ghafla baada ya kumuona bosi amekuja ananituma niende Ubungo kumchukulia mkaa na mafuta ya alizeti aliyotumiwa na Yule mkuu wa wilaya wa wilaya moja kule Singida. Nivipeleke nyumbani niwaambie bado yupo kwenye kikao ila nikitoka hapo nimpitie Sinza kwenye kale ka nyumba kadogo anakoishi na ‘nambie mrembo' ili nimrudishe kwa ‘we mama Joni'
Basi nikaachia hapo nisijepatwa na hasira nkaacha kazi wakati sijapata kazi nyingine afu nikajiunge na wasio na kazi kutafuta kazi ndipo nitakapoona kazi kupata kazi!!!
Ila mpaka kesho nawaza mimi Mentor…
Nawaza sana mpaka nimekosa usingizi muda huu Monday, 02:25am 1[SUP]st[/SUP] April 2013…
Wasalaam wapendwa,
Mentor.
Last edited by a moderator: