Bado nipo nipo sana kaka Lyagwa...saaana!!!
Naona ushuhuda juu ya mazingira yako ya kazi yamekuwezesha sana kukutana na vipusa vya kila aina, na hii inanikumbusha tena story ya mwalimu wangu mmoja wakati nikiwa sekondari yeye aliwahi kusema (nanukuu) "
Siwezi kununua ng`ombe wa maziwa ili hali maziwa bado yanapatikana" (mwisho wa nukuu). Hii ni nje na mada ya msingi kwa leo.
Ukikaa na kutafakari kwa kina sana juu ya Tanzania yetu kama utakuwa na japo dalili za kuwa ugonjwa wa moyo, hakika unaweza kujikuta jina lako limebadirika (unakufa), kuna mengi ya ajabu hasa sehemu mbalimbali za kazi serikalini. Pesa za umma zinajuta huko kwenye serikali kuu, mitaa nk japo haziwezi kusema jambo.
Mkuu mentor kwa fani yako umeona magofu ya viwanda ukatamani wewe mwenye diploma flani na mwenye fani fulani toka Veta mngeweza kupata ajira hapo, lakini hakika hapo kila taaluma ingeingia hapo na hata mfagiaji na mpika chai na mama & baba ntilie wote wangeingia hapo na kufaidika kwa namna moja ama nyingine, lakini yamebaki magofu. Ili ninyi mfanye kazi hapo mngehitaji mhasibu, storekeeper, driver, mafundi kwa fani zote i.e umeme, welding, plumbing, civil, na siku hizi tena computer n.k, angalia idadi ya ajira zilizopotea hapo, eti mpaka mwekezaji atoke China ama India aje tumuuzie na kwa bahati mbaya naye akija anakuja na watu wake ama anafanya kiwanda chetu kuwa godauni/store, aibu hii tutaificha wapi. hii ni moja tu
Kuna kwenye madini, maliasili, nk.