Jielimishe kuhusu Israel na vita zinazomzunguka

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,555
41,065
Wayahudi, idadi yao ni ndogo sana, japo kuna wakati walikuwa wengi kidogo. Mwaka 1939, kabla ya vita kuu ya Dunia, idadi ya Wayahudi ilifikia 15.3 million Hitler aliwaua Wayahudi wapatao milioni 6. Wayahudi waliprudi Mashariki ya kati na kuanzisha Taifa la Israel mwaka 1948 walikuwa 0.806 milioni. Ifahamike kuwa mwaka 1933, idadi ya Watanganyika inakadiriwa kuwa watu milioni 5 tu, yaani Wayahudi walikuwa wengi mara 3 ya Watanganyika.

Kabla ya Wayahudi kuvamia na kutwaa eneo la Caanan ambalo ndiyo ardhi asilia ya Wayahudi, lilikuwa na ukubwa wa 50,000 kilometa za mraba. Israel ya leo ina ukubwa wa mita za kilometa za mraba 22,145.

Lakini hata kabla ya haya yaliyowapata baada ya Kristo, kabla yake walipitia madhira mengi kama vile kutengwa na Mungu (walipotenda kinyume na maagano), kuuawa na kutiwa utumwani mara kadhaa. Hivyo, kwa Wayahudi, kuuawa, kupigana vita na kushinda na hata kushindwa, kuishi kwa kumpendeza Mungu, kumkana, na kutenda kinyume cha mapenzi ya Mungu, imekuwa ndiyo mfumo wao wa maisha wakati wote. Na kiimani, tunaamini kuwa hayo yote ndivyo mpango wa Mungu ulivyo dhidi ya Israel na Ulimwengu mzima.

Israel imewahi kudhulumiwa na Wamisri, Wamaleki, Wafilisti, Wapersia, Wababiloni, Warumi, na nchi na makabila mengine mengi.

Kwa nini yote haya yanawatokea Waisrael?
Kwa kadiri ya biblia, ni kwa sababu, Mungu ana mpango na Taifa la Israel, na shetani yupo kwa sababu ya kuharibu mpango wa Mungu. Hivyo ni shetani anawatumia majirani zake, kuiangamiza Israel.

Kiimani, ni kwamba sijui awe ni Hitler, Iran, Wasyria, Hamas au Hizibollah, Wabogoni (Russia), hakuna aliyeweza au atakayeweza kuwaangamiza na kuwapoteza Waisrael. Maangamizi ya Waisrael yatakuja na kutoweka, na wala maangamizi hayo hayamaanishi kuwa tunaelekea siku za mwisho kama baadhi ya watu wanavyotaka kutuaminisha.

Nyakati hizi za mahangaiko ya Wayahudi inatajwa kuwa tribulation (Yeremia 30:7).

Lakini kuhusu siku za mwisho, kuhusiana na Israel, biblia inasema kuwa, makundi makubwa ya Wayahudi yatarejea kwenye ardhi ya Israel (Kumbukumbu la Torati 30:3; Isaya 43:6; Ezekiel 34:11-13; 36:24; 37:1-14). Ifahamike mpaka sasa hivi, Wayahudi wanaoishi Israel ni milioni 9 tu. Wayahudi wapatao 18 milioni wanaishi nje ya Israel, kwenye mataifa mbalimbali.

Kisha mpinga Kristo atafanya mkataba wa amani wa miaka 7 na Waisrael (Isaya 28:18; Daniel 9:27).

Hekalu lililovunjwa (bila shaka kutokana na vita) litajengwa upya mjini Yerusalem (Daniel 9:27; Matayo 24:15; 2 Watesolonike; 2:3-4; Ufunuo 11:1).

Mpinga Kristo atavunja mkataba wa amani uliosainiwa, na mauaji makubwa ya Wayahudi yatafanyika (Daniel 9:27; 12:1, 11; Zacharia 11:16; Matayo 24:15, 21; Ufunuo 12:13). Israel itavamiwa (Ezekiel 38-39).

Kisha Wayahudi watamtambua na kumkiri Yesu kuwa ndiye Masiha (Zacharia 12:10). Baada ya kumkiri Kristo, Israel mpya itazaliwa, itahuishwa, na itaungamishwa kama ilivyokuwa kale (Yeremia 33:8; Ezekiel 11:17; Warumi 11:26).

Andiko hili ni kwaajili ya wanaotaka kujifunza, wasio na nia hiyo, wasihangaishwe nalo.
 
kutwaa eneo la Caanan ambalo ndiyo ardhi asilia ya Wayahudi,
Mkuu wewe ni mtu makini sana jumu JF ila hii fact inanipa ukakasi!! Abraham hakutokea Canaan yeye alikuta watu wanaishi tayari na hata hao waisrael walikuta Canaanites yaani makabila kama Hivites, Jebusites, Amorites, Rephaites, na mpaka huko Gaza waliishi kabila zenye asili ya ugiriki yaani Caphtorites, casluh, na jamii zingine za Aegean.

Ni vizuri ieleweke kwamba Israelities walifanya genocide kama tu waliyofanya wazungu kuua American Indians au Wajerumani kuua wayahudi ndio wakatawala hapo CANAAN. So facts ziwekwe straight ili mjadala uwe objective.

Ni hayo tu but ill always respect your opinions.
 
Hekalu lililovunjwa (bila shaka kutokana na vita) litajengwa upya mjini Yerusalem (Daniel 9:27; Matayo 24:15; 2 Watesolonike; 2:3-4; Ufunuo 11:1).
Ningependa sana kukubaliana na hoja hii haraka sana kwa kulinganusha na Mandiko nukuliwa

Lakini kuna hili la kujifunza kuhusiana na hoja hii!

Kabla ya Ujio wa Yesu Kristo Duniani, Ilikuwa ni kawaida kwa wacha Mungu kupewa maelekezo ya namna ya kujenga hekalu ili kumwabudu Mungu

Ujio wa Yesu Kristo Duniani, haufundishi habari za hekalu la kujengwa na wanadamu

Hekalu linakuwa ni wewe mwenyewe!

Wayahudi wanaweza kulibomoa na kulijenga upya hekalu, lakini haiwapi faida yoyote katika ulimwengu wa Roho

Biblia ktk agano jipya, inakazia kwa namna ya kulijenga hekalu yaani wewe mwenyewe kwa maana ya kukulia wokovu na kuliishi

Nikipata nafasi nitakuja na maandiko
 
Kwa nini yote haya yanawatokea Waisrael?
Kwa kadiri ya biblia, ni kwa sababu, Mungu ana mpango na Taifa la Israel, na shetani yupo kwa sababu ya kuharibu mpango wa Mungu. Hivyo ni shetani anawatumia majirani zake, kuiangamiza Israel
Kama ni msomaji mzuri wa Bible utaelewa kwamba Laana ya Nuhu kwenda Kwa Canaan mjukuu wa Ham ndio ilipelekea haya kutokea.

Yaani Nuhu alitoa laana kwamba watoto wa Canaan watatawaliwa na watoto wa Shemu. Na hii ni sababu Ham alitembea na mke wa Nuhu.

So kwenye utekelezaji wa laana ikabidi Mungu amtoe Abraham huko alipo akaishi Canaan na hata Joshua aliambiwa achinje waCanaan wote asiache hata mmoja!! So kama sio laana ile tusingefika huku.

Na why Israel exactly sio watoto wengine ni Abraham!! Sababu biblia inasema walikua ndio weakest among nations so Mungu alitaka yakifanyika makubwa ajitwalie yeye utukufu na sio mataifa yenye nguvu yangejikweza.

Na mpango huo ulienda mpaka kuzaliwa kwa Yesu na relevance ya Israel kama taifa ukafia pale, na wao leo hii ni sawa tu na waha wenzangu kuliko Kakonko!! Hakuna uspecial wowote tena wala uteule.

Kibiblia sasa Taifa teule ni wale waliompokea Yesu na pia wanakua watoto wa kurithi baraka za Abraham. Reference Wagalatia 3 na Yohana 1:12-17 pia Mathayo 11:11....
 
Ningependa sana kukubaliana na hoja hii haraka sana kwa kulinganusha na Mandiko nukuliwa

Lakini kuna hili la kujifunza kuhusiana na hoja hii!

Kabla ya Ujio wa Yesu Kristo Duniani, Ilikuwa ni kawaida kwa wacha Mungu kupewa maelekezo ya namna ya kujenga hekalu ili kumwabudu Mungu

Ujio wa Yesu Kristo Duniani, haufundishi habari za hekalu la kujengwa na wanadamu

Hekalu linakuwa ni wewe mwenyewe!

Wayahudi wanaweza kulibomoa na kulijenga upya hekalu, lakini haiwapi faida yoyote katika ulimwengu wa Roho

Biblia ktk agano jipya, inakazia kwa namna ya kulijenga hekalu yaani wewe mwenyewe kwa maana ya kukulia wokovu na kuliishi

Nikipata nafasi nitakuja na maandiko
Aiseee safi sana, wewe umejaa neno la Mungu. Hata Yesu alisema mnaweza vunja hekalu na akalijenga ndani ya siku 3!! Wao wakashangaa unaweza jenga "jengo" kwa siku tatu bila kujua Yesu alimaanisha hekalu ni rohoni sio matofali. Hata 1 wakorintho 3 inasema hayo.
 
Mkuu wewe ni mtu makini sana jumu JF ila hii fact inanipa ukakasi!! Abraham hakutokea Canaan yeye alikuta watu wanaishi tayari na hata hao waisrael walikuta Canaanites yaani makabila kama Hivites, Jebusites, Amorites, Rephaites, na mpaka huko Gaza waliishi kabila zenye asili ya ugiriki yaani Caphtorites, casluh, na jamii zingine za Aegean.

Ni vizuri ieleweke kwamba Israelities walifanya genocide kama tu waliyofanya wazungu kuua American Indians au Wajerumani kuua wayahudi ndio wakatawala hapo CANAAN. So facts ziwekwe straight ili mjadala uwe objective.

Ni hayo tu but ill always respect your opinions.
Upo sahihi kabisa.

Kumbukumbu za kiimani, siyo za kistoria, zinasema, "Mungu aliwaambia Waisrael wakaivamie Caanan na kuitwaa baada ya kuwaua watu wote wa nchi hiyo kwa sababu wamefanya machukizo mbele yake (Mungu), wazazi wanalala na watoto wao, kaka na dada zao, wanaume na wanaume wenzao. Nao Waisrael wakafanya kama walivyoagizwa na bwana, kisha wakaitwaa nchi.
 
Ningependa sana kukubaliana na hoja hii haraka sana kwa kulinganusha na Mandiko nukuliwa

Lakini kuna hili la kujifunza kuhusiana na hoja hii!

Kabla ya Ujio wa Yesu Kristo Duniani, Ilikuwa ni kawaida kwa wacha Mungu kupewa maelekezo ya namna ya kujenga hekalu ili kumwabudu Mungu

Ujio wa Yesu Kristo Duniani, haufundishi habari za hekalu la kujengwa na wanadamu

Hekalu linakuwa ni wewe mwenyewe!

Wayahudi wanaweza kulibomoa na kulijenga upya hekalu, lakini haiwapi faida yoyote katika ulimwengu wa Roho

Biblia ktk agano jipya, inakazia kwa namna ya kulijenga hekalu yaani wewe mwenyewe kwa maana ya kukulia wokovu na kuliishi

Nikipata nafasi nitakuja na maandiko
Hekalu siyo wewe bali ni mifano tu ya Paulo katika kuwatakatifuza wakristo,kumbuka kuwa Hekalu la Mungu ni nyumba ya sala.
 
Hekalu lililovunjwa (bila shaka kutokana na vita) litajengwa upya mjini Yerusalem (Daniel 9:27; Matayo 24:15; 2 Watesolonike; 2:3-4; Ufunuo 11:1).
Mambo ya hekalu hayana impact tena kasome waebrania 6,7,8 utaona jinsi Kuhani Mkuu kwa wakristo amekuwa Yesu sio tena mahukani. Sasa hata wakijenga kuna impact gani wakati Mungu hakai tena hekaluni kama miaka ya kale?

Biblia usiitafsiri literally maana ipo figuratively.... kasome habari za melchizedek ndio utaelewa why hatutafsiri Biblia literally.
 
Ningependa sana kukubaliana na hoja hii haraka sana kwa kulinganusha na Mandiko nukuliwa

Lakini kuna hili la kujifunza kuhusiana na hoja hii!

Kabla ya Ujio wa Yesu Kristo Duniani, Ilikuwa ni kawaida kwa wacha Mungu kupewa maelekezo ya namna ya kujenga hekalu ili kumwabudu Mungu

Ujio wa Yesu Kristo Duniani, haufundishi habari za hekalu la kujengwa na wanadamu

Hekalu linakuwa ni wewe mwenyewe!

Wayahudi wanaweza kulibomoa na kulijenga upya hekalu, lakini haiwapi faida yoyote katika ulimwengu wa Roho

Biblia ktk agano jipya, inakazia kwa namna ya kulijenga hekalu yaani wewe mwenyewe kwa maana ya kukulia wokovu na kuliishi

Nikipata nafasi nitakuja na maandiko
Upo sahihi. Maandiko mengi, haya yanayoonesha upekee wa Israel yapo zaidi katika Agano la kale.

Lakini kwenye Agano jipya, kwa kiasi kikubwa, Yesu anafundisha kwa mithali akielezea jinsi Wayahudi walivyomkataa mteule wa Mungu, kiasi cja Mungu (Bwana wa Karamu) kuyageukia mataifa. Na hilo linadhihirika, pale ambapo wakuu wa Wayahudi wanapotimiza hatma yao ya kumtundika Kristo aliyetabiriwa na manabii, juu msalabani, kwa mashtaka bandia ya uchochezi, eti anawachochea watu wasimpe Kaizari kodi.
 
Mkuu wewe ni mtu makini sana jumu JF ila hii fact inanipa ukakasi!! Abraham hakutokea Canaan yeye alikuta watu wanaishi tayari na hata hao waisrael walikuta Canaanites yaani makabila kama Hivites, Jebusites, Amorites, Rephaites, na mpaka huko Gaza waliishi kabila zenye asili ya ugiriki yaani Caphtorites, casluh, na jamii zingine za Aegean.

Ni vizuri ieleweke kwamba Israelities walifanya genocide kama tu waliyofanya wazungu kuua American Indians au Wajerumani kuua wayahudi ndio wakatawala hapo CANAAN. So facts ziwekwe straight ili mjadala uwe objective.

Ni hayo tu but ill always respect your opinions.

Ni sahihi Kabisa.
Ibrahim, Lutu, Isaka na Yakobo wote walikuwa Walowezi na wavamizi
 
Upo sahihi kabisa.

Kumbukumbu za kiimani, siyo za kistoria, zinasema, "Mungu aliwaambia Waisrael wakaivamie Caanan na kuitwaa baada ya kuwaua watu wote wa nchi hiyo kwa sababu wamefanya machukizo mbele yake (Mungu), wazazi wanalala na watoto wao, kaka na dada zao, wanaume na wanaume wenzao. Nao Waisrael wakafanya kama walivyoagizwa na bwana, kisha wakaitwaa nchi.
It's okay lakini usiseme ni eneo la asili, Abraham alitokea ilipo Syria/Iraq ya sasa. Na kama umesoma Bible vizuri nchi ya ahadi inaanzia Misri, Saudia, Syria, Iraq, Jordan cha ajabu wameng'ang'ania Palestina. Why wasiende Saudia wawaambie wapishe?
 
Mambo ya hekalu hayana impact tena kasome waebrania 6,7,8 utaona jinsi Kuhani Mkuu kwa wakristo amekuwa Yesu sio tena mahukani. Sasa hata wakijenga kuna impact gani wakati Mungu hakai tena hekaluni kama miaka ya kale?

Biblia usiitafsiri literally maana ipo figuratively.... kasome habari za melchizedek ndio utaelewa why hatutafsiri Biblia literally.
Wakati nakubaliana nawe kifalsafa, lakini natofautiana nawe katika uhalisia.

Yakumbuke maneno ya Mtume Paulo:

"Agano la kale ni kivuli cha Agano jipya"

Yaani kila lilitokea au kunenwa katika agano la kale, utimilifu wake katika maisha ya kiroho, upo katika agano jipya.

Agano la kale, lilishughulika na mwili, wakati agano jipya linashughulika na roho. Kwenye agano la kale ukiambiwa hekalu, ujue ni hekalu physical object. Katika agano jipya, hekalu ni roho yako ambayo ni hekalu la Roho Mtakatifu. Ila hilo hekalu physical object ni kivuli cja hekalu kamili ambalo ni maisha ya kiroho.

Kwenye agano la kale ukiambiwa wayahudi walikula mwanakondoo, walikula kondoo mnyama kamili, lakini katika agano jipya Kristo yeye anasema ni mwanakondoo na ni chakula cha uzima, anazungumzia uzima wa roho, siyo uzima wa tumbo. Na hakuna nyama ya yesu physical object.

Lakini pia vipo vitu physical vinavyotajwa katika Agano jipya ambavyo ni physical ila vinavyoashiria matukio ya kiroho. Kama vile tunaambiwa, kutakuwa na magonjwa, vita, n.k. Hivi ni vitu physical siyo magonjwa ya kiroho wala vita si vita vya kiroho.
 
Wayahudi, idadi yao ni ndogo sana, japo kuna wakati walikuwa wengi kidogo. Mwaka 1939, kabla ya vita kuu ya Dunia, idadi ya Wayahudi ilifikia 15.3 million Hitler aliwaua Wayahudi wapatao milioni 6. Wayahudi waliprudi Mashariki ya kati na kuanzisha Taifa la Israel mwaka 1948 walikuwa 0.806 milioni. Ifahamike kuwa mwaka 1933, idadi ya Watanganyika inakadiriwa kuwa watu milioni 5 tu, yaani Wayahudi walikuwa wengi mara 3 ya Watanganyika.

Kabla ya Wayahudi kuvamia na kutwaa eneo la Caanan ambalo ndiyo ardhi asilia ya Wayahudi, lilikuwa na ukubwa wa 50,000 kilometa za mraba. Israel ya leo ina ukubwa wa mita za kilometa za mraba 22,145.

Lakini hata kabla ya haya yaliyowapata baada ya Kristo, kabla yake walipitia madhira mengi kama vile kutengwa na Mungu (walipotenda kinyume na maagano), kuuawa na kutiwa utumwani mara kadhaa. Hivyo, kwa Wayahudi, kuuawa, kupigana vita na kushinda na hata kushindwa, kuishi kwa kumpendeza Mungu, kumkana, na kutenda kinyume cha mapenzi ya Mungu, imekuwa ndiyo mfumo wao wa maisha wakati wote. Na kiimani, tunaamini kuwa hayo yote ndivyo mpango wa Mungu ulivyo dhidi ya Israel na Ulimwengu mzima.

Israel imewahi kudhulumiwa na Wamisri, Wamaleki, Wafilisti, Wapersia, Wababiloni, Warumi, na nchi na makabila mengine mengi.

Kwa nini yote haya yanawatokea Waisrael?
Kwa kadiri ya biblia, ni kwa sababu, Mungu ana mpango na Taifa la Israel, na shetani yupo kwa sababu ya kuharibu mpango wa Mungu. Hivyo ni shetani anawatumia majirani zake, kuiangamiza Israel.

Kiimani, ni kwamba sijui awe ni Hitler, Iran, Wasyria, Hamas au Hizibollah, Wabogoni (Russia), hakuna aliyeweza au atakayeweza kuwaangamiza na kuwapoteza Waisrael. Maangamizi ya Waisrael yatakuja na kutoweka, na wala maangamizi hayo hayamaanishi kuwa tunaelekea siku za mwisho kama baadhi ya watu wanavyotaka kutuaminisha.

Nyakati hizi za mahangaiko ya Wayahudi inatajwa kuwa tribulation (Yeremia 30:7).

Lakini kuhusu siku za mwisho, kuhusiana na Israel, biblia inasema kuwa, makundi makubwa ya Wayahudi yatarejea kwenye ardhi ya Israel (Kumbukumbu la Torati 30:3; Isaya 43:6; Ezekiel 34:11-13; 36:24; 37:1-14). Ifahamike mpaka sasa hivi, Wayahudi wanaoishi Israel ni milioni 9 tu. Wayahudi wapatao 18 milioni wanaishi nje ya Israel, kwenye mataifa mbalimbali.

Kisha mpinga Kristo atafanya mkataba wa amani wa miaka 7 na Waisrael (Isaya 28:18; Daniel 9:27).

Hekalu lililovunjwa (bila shaka kutokana na vita) litajengwa upya mjini Yerusalem (Daniel 9:27; Matayo 24:15; 2 Watesolonike; 2:3-4; Ufunuo 11:1).

Mpinga Kristo atavunja mkataba wa amani uliosainiwa, na mauaji makubwa ya Wayahudi yatafanyika (Daniel 9:27; 12:1, 11; Zacharia 11:16; Matayo 24:15, 21; Ufunuo 12:13). Israel itavamiwa (Ezekiel 38-39).

Kisha Wayahudi watamtambua na kumkiri Yesu kuwa ndiye Masiha (Zacharia 12:10). Baada ya kumkiri Kristo, Israel mpya itazaliwa, itahuishwa, na itaungamishwa kama ilivyokuwa kale (Yeremia 33:8; Ezekiel 11:17; Warumi 11:26).

Andiko hili ni kwaajili ya wanaotaka kujifunza, wasio na nia hiyo, wasihangaishwe nalo.
Maelezo umetoa ila point Moja hujagusia ,kuhusu damu ya wayahudi ktk vipimo vya DNA ni kuwa ,hawa wazayuni SI wayahudi Kwa damu Bali wao ni Turks wa Eastern Europe walioingia ktk dini ya uyahadu.
Wenye Asili ya damu Kwa mujibu wa vipimo ya DNA ni watu walioko mashariki ya kati na maeneo ya jirani miongoni mwao ni wafuasi wa Torati 'orthodox , waislamu na wakristo.
Screenshot_2023-11-12-12-01-53-968_com.twitter.android.jpg
 
Achana na hizo hadithi zisizo na kichwa wala miguu.

Hakuna kitu kinaitwa ardhi ya waisraeli eti waliyopewa na Mungu, hakuna kitu kama hicho.

Waisraeli walivamia ardhi ya wapalestina mwaka 1948 na wanaikalia kwa nguvu kwa misaada ya nchi za ulaya na Marekani.
 
Hata ukiachana na rejea za kwenye vitabu vya dini, unaamini kuwa Wayahudi hawakuwahi kuwa na ardhi yoyote katika Ulimwengu huu?
 
Wakati nakubaliana nawe kifalsafa, lakini natofautiana nawe katika uhalisia.

Yakumbuke maneno ya Mtume Paulo:

"Agano la kale ni kivuli cha Agano jipya"

Yaani kila lilitokea au kunenwa katika agano la kale, utimilifu wake katika maisha ya kiroho, upo katika agano jipya.

Agano la kale, lilishughulika na mwili, wakati agano jipya linashughulika na roho. Kwenye agano la kale ukiambiwa hekalu, ujue ni hekalu physical object. Katika agano jipya, hekalu ni roho yako ambayo ni hekalu la Roho Mtakatifu. Ila hilo hekalu physical object ni kivuli cja hekalu kamili ambalo ni maisha ya kiroho.

Kwenye agano la kale ukiambiwa wayahudi walikula mwanakondoo, walikula kondoo mnyama kamili, lakini katika agano jipya Kristo yeye anasema ni mwanakondoo na ni chakula cha uzima, anazungumzia uzima wa roho, siyo uzima wa tumbo. Na hakuna nyama ya yesu physical object.

Lakini pia vipo vitu physical vinavyotajwa katika Agano jipya ambavyo ni physical ila vinavyoashiria matukio ya kiroho. Kama vile tunaambiwa, kutakuwa na magonjwa, vita, n.k. Hivi ni vitu physical siyo magonjwa ya kiroho wala vita si vita vya kiroho.
Nakubali 100%
 
Wayahudi, idadi yao ni ndogo sana, japo kuna wakati walikuwa wengi kidogo. Mwaka 1939, kabla ya vita kuu ya Dunia, idadi ya Wayahudi ilifikia 15.3 million Hitler aliwaua Wayahudi wapatao milioni 6. Wayahudi waliprudi Mashariki ya kati na kuanzisha Taifa la Israel mwaka 1948 walikuwa 0.806 milioni. Ifahamike kuwa mwaka 1933, idadi ya Watanganyika inakadiriwa kuwa watu milioni 5 tu, yaani Wayahudi walikuwa wengi mara 3 ya Watanganyika.

Kabla ya Wayahudi kuvamia na kutwaa eneo la Caanan ambalo ndiyo ardhi asilia ya Wayahudi, lilikuwa na ukubwa wa 50,000 kilometa za mraba. Israel ya leo ina ukubwa wa mita za kilometa za mraba 22,145.

Lakini hata kabla ya haya yaliyowapata baada ya Kristo, kabla yake walipitia madhira mengi kama vile kutengwa na Mungu (walipotenda kinyume na maagano), kuuawa na kutiwa utumwani mara kadhaa. Hivyo, kwa Wayahudi, kuuawa, kupigana vita na kushinda na hata kushindwa, kuishi kwa kumpendeza Mungu, kumkana, na kutenda kinyume cha mapenzi ya Mungu, imekuwa ndiyo mfumo wao wa maisha wakati wote. Na kiimani, tunaamini kuwa hayo yote ndivyo mpango wa Mungu ulivyo dhidi ya Israel na Ulimwengu mzima.

Israel imewahi kudhulumiwa na Wamisri, Wamaleki, Wafilisti, Wapersia, Wababiloni, Warumi, na nchi na makabila mengine mengi.

Kwa nini yote haya yanawatokea Waisrael?
Kwa kadiri ya biblia, ni kwa sababu, Mungu ana mpango na Taifa la Israel, na shetani yupo kwa sababu ya kuharibu mpango wa Mungu. Hivyo ni shetani anawatumia majirani zake, kuiangamiza Israel.

Kiimani, ni kwamba sijui awe ni Hitler, Iran, Wasyria, Hamas au Hizibollah, Wabogoni (Russia), hakuna aliyeweza au atakayeweza kuwaangamiza na kuwapoteza Waisrael. Maangamizi ya Waisrael yatakuja na kutoweka, na wala maangamizi hayo hayamaanishi kuwa tunaelekea siku za mwisho kama baadhi ya watu wanavyotaka kutuaminisha.

Nyakati hizi za mahangaiko ya Wayahudi inatajwa kuwa tribulation (Yeremia 30:7).

Lakini kuhusu siku za mwisho, kuhusiana na Israel, biblia inasema kuwa, makundi makubwa ya Wayahudi yatarejea kwenye ardhi ya Israel (Kumbukumbu la Torati 30:3; Isaya 43:6; Ezekiel 34:11-13; 36:24; 37:1-14). Ifahamike mpaka sasa hivi, Wayahudi wanaoishi Israel ni milioni 9 tu. Wayahudi wapatao 18 milioni wanaishi nje ya Israel, kwenye mataifa mbalimbali.

Kisha mpinga Kristo atafanya mkataba wa amani wa miaka 7 na Waisrael (Isaya 28:18; Daniel 9:27).

Hekalu lililovunjwa (bila shaka kutokana na vita) litajengwa upya mjini Yerusalem (Daniel 9:27; Matayo 24:15; 2 Watesolonike; 2:3-4; Ufunuo 11:1).

Mpinga Kristo atavunja mkataba wa amani uliosainiwa, na mauaji makubwa ya Wayahudi yatafanyika (Daniel 9:27; 12:1, 11; Zacharia 11:16; Matayo 24:15, 21; Ufunuo 12:13). Israel itavamiwa (Ezekiel 38-39).

Kisha Wayahudi watamtambua na kumkiri Yesu kuwa ndiye Masiha (Zacharia 12:10). Baada ya kumkiri Kristo, Israel mpya itazaliwa, itahuishwa, na itaungamishwa kama ilivyokuwa kale (Yeremia 33:8; Ezekiel 11:17; Warumi 11:26).

Andiko hili ni kwaajili ya wanaotaka kujifunza, wasio na nia hiyo, wasihangaishwe nalo.
Unaongelea Ashkenazi.

Tembelea uzi huo hapo chini uoate darsa:

Maelezo umetoa ila point Moja hujagusia ,kuhusu damu ya wayahudi ktk vipimo vya DNA ni kuwa ,hawa wazayuni SI wayahudi Kwa damu Bali wao ni Turks wa Eastern Europe walioingia ktk dini ya uyahadu.
Wenye Asili ya damu Kwa mujibu wa vipimo ya DNA ni watu walioko mashariki ya kati na maeneo ya jirani miongoni mwao ni wafuasi wa Torati 'orthodox , waislamu na wakristo.View attachment 2811692
Sijalifuatilia hilo, lakini inawezekana. Ifahamike kuwa Wayahudi tunaowaona Ulaya, wengine vizazi vyao vya mwanzo vimekuwepo huko kwa zaidi ya miaka 1,000. Katika muda mrefu namna hiyo lazima kuna mwingiliano mkubwa sana . Na hata hao wanaoitwa Waarabu, sitashangaa kama baadhi yao, asili yao yawezekana ni Wayahudi.

Ndiyo maana naamini kuwa kama laiti kungekuwa na wenye hekima, Wayahudi na Wapalestina wangeweza kuishi kwa amani, maana asili yao, uwezekano mkubwa ni ndugu. Hawa ni ndugu walioamua kuwa mahasimu wakubwa.

Labda tuamini tu kuwa hekima yao imefishwa ili maandiko yatimie (tukiamini katika mafundisho ya dini, dini zote zinazuia kuhoji maandiko matakatifu)
 
Back
Top Bottom