Safari ya binadamu kutoka Afrika Mashariki

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Kisayansi inasemekana binadamu ali evolve kutoka kwenye mnyama anayefanana na sokwe. Mnyama huyu alikuwa na ngozi nyeupe na alikuwa na manyoya mengi. Aliishi kwenye misitu ya Afrika Mashariki.

Kutokana na shughuli za kutafuta chakula huyu bwana akahama kutoka msituni na kwenda kwenye nyika za EA kuwinda. Nyikani kuna jua kali na si baridi kama msituni hivyo hakuhitaji tena manyoya. Akapoteza manyoya. Ngozi nyeupe na jua kali huwa haviendani. Akaanza kutengeneza melanini na ngozi yake ikaanza kuwa nyeusi.

Kwenye kujitafutia msosi akaanza kuhama. Njia rahisi ya kuhama ilikuwa ni kupita pembezoni mwa bahari. Hii haina vikwazo(ni kama barabara tu) na pia aliweza kupata chakula toka baharini kila atakapo, akaanza kupita kando kando ya bahari kufika hadi kwenye pembe ya Africa, akavuka kuingia Yemen. Akaendelea hadi kufika India. Wengine wakaendelea kuishi hapo na ndiyo sababu hadi leo wahindi wengi wana weusiwesi. Wengine wakaendelea na safari.

Wakasambaa South east Asia yote. Wakavuka visiwa vya Indonesia na kuingia Australia. Ndiyo waaborigine wa Australia.

Baada ya miaka mingi wengine pia wakaanza kuhama. Uhamaji wa pili. Hawa hawakupita pwani bali nchi kavu. Hawa kulingana na mazingira waliyopita wakaanza kuwa weupe.

Wakafika Misri, wakavuka kuingia Mashariki ya kati. Wengine wakaenda mashariki wakatoa waarabu, wakaendele wengine wakatoa waIran. Wakazidi kusonga, wakafika sehemu wengine wakaenda kuwa wahindi wale weupe maana hawa waliingia kupitia kasakazini ya India. Wengine wakaenda kuwa wakazi wa Asia ya kati.

Hapo napo wakagawanyika wengine wakaenda kuwa kuwa wachina,wajapan, na wavietnam na wengine wakaenda maeneo ya baridi ya Siberia.

Hawa wakavuka mlango bahari wa Bering na kuingia Amerika. Wakaanza kushuka bara la Amerika hadi kufika Amerika kusini na kusambaa kote.

Walipofika mashariki ya kati wengine wakaingia wakaenda magharibi na kuingia ulaya na kuwa wazungu. Huko waliikuta jamii nyingine ya binadamu, wakazaliana nayo lakini wakaitokomeza. Hivyo ndivyo binadamu aliweza kusambaa dunia nzima.

Watu wamebadilika sana lakini jamii ya san kama wakhosa, wasandawe na wahadzabe bado wana DNA za binadamu wa kale kabisa.

Kutokana na binadamu kuanzia Africa,waafrika ndiyo watu wenye mchanganyiko mwingi sana wa DNA. Tofauti ya DNA kati ya muafrika mmoja na mwingine ni kubwa kuliko kati ya muafrika na mzungu.
 
Unafahamu kuwa wasan si weusi, ni watu weupe. Pamoja ya kuwa mbali sana na Asia lakini wana macho ya kichina. Wana DNA ya kale zaidi. Hawa na wasandawe na wadzabe ni jamii moja.

unnamed (2).jpg
khoi.jpg
unnamed.jpg
San-people-marczawel_com_1.jpg
unnamed (1).jpg
unnamed (3).jpg
 
Naamini Sana kuna stori iliyofichika Sana kuhusu asili ya binadamu sio hichi ulichotuambia hapa
 
Back
Top Bottom