Saed Kubenea amesafirishwa leo kwa ndege kwenda mkoani Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mbunge Saed Kubenea (CHADEMA) amesafirishwa leo kwa ndege kwenda mkoani Dodoma, kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.
----------------------------
Mh. Kubenea amepelekwa Hospital ya bunge baada ya kamati kuona afya yake sio nzuri.

Kamati hiyo imesema Kubenea ataitwa tena kuhojiwa baada ya kujiridhisha kuwa afya yake imeimarika.

Ikumbukwe jana jeshi la polisi lilimtia nguvuni Mh. Kubenea akiwa hospital ya Aghakhan ambako alikuwa anapatiwa matibabu.


kubenea.jpg
 
Kuuliza sio ujinga:
1. Hivi spika wa bunge kumuita mbunge kwenye kamati za bunge ni jinai inayopaswa kushughulikiwa na polisi!?
2. Je, kamati ikishamuhoji na (either) kumkuta na makosa au la inamkabidhi kwa polisi kumfungulia mshitaka!?
Atakayenisaidia kunipa mwanga hapa itanisaidia kujua hizo gharama walizotumia polisi kuanzia kumkamata hadi kulipia ndege zinatoka fungu gani la matumizi katika bajeti aliyoisoma Mh. Dr. Mpango mwezi Julai .
 
Mimi ndio maana nikinunua bidhaa sidai risiti,bora mwanakijiji mwenzangu mwenye duka atajirike kuliko nidai risiti serikali ipate kodi na kumsafirisha mtu asiye na hatia kisa tu spika ana chuki naye

Wakati huo huo kuna mtoto au mama Mja mzito anakufa kwa kukosa laki moja,serikali inasafirisha mtu kwa milioni tano!

TV zimejaa matangazo ya watu wenye magonjwa wanahitaji laki tano,serikali inachezea pesa kwenye mchezo ya kisiasa
 
Kwa mwendo huu, ajiangalie watakuja kumuua! Inakera sasa. Ajali, risasi vinamnyemelea, ...... Huyu siyo criminal, ni kuwa alitoa maoni tofauti na spika, basi! Mapolisi wa nini?
 
Back
Top Bottom