Saed Kubenea amesafirishwa leo kwa ndege kwenda mkoani Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge

Haya mambo ukiyafatilia sana utasikitika sana, inabidi kuwepo external force itakayo act upon the system kusudi kuchange the position of the system.
 
Huyu spika hafai kabisa!Hawa wabunge wamekopeshwa magari,wanalipwa posho na mishahara mikubwa kwa nini asitumie usafiri wake mwenyewe kwenda huko Dodoma ambako ndio kazini kwake?
 
Haya ni mojawapo ya matumizi mabovu kabisa ya fedha za umma, hivi Mh mbunge si anaweza kupigiwa tu simu na akaenda mwenyewe !
 
Kodi zetu znatumiwa hovyo sana na hawa 'wazalendo' wetu
Na akimaliza kuhojiwa akitaka kutoka ataulizwa unakwenda wapi? Akijibu naenda nyumbani kwangu Area D kupumzika, Ndugai atamwambia uje Dodoma kwa gharama zako mwenyewe. Watamrejesha Dar kwa escort kuhakikisha kafika mpaka Dar kwa ndege!
 
Mimi ndio maana nikinunua bidhaa sidai risiti,bora mwanakijiji mwenzangu mwenye duka atajirike kuliko nidai risiti serikali ipate kodi na kumsafirisha mtu asiye na hatia kisa tu spika ana chuki naye

Wakati huo huo kuna mtoto au mama Mja mzito anakufa kwa kukosa laki moja,serikali inasafirisha mtu kwa milioni tano!

TV zimejaa matangazo ya watu wenye magonjwa wanahitaji laki tano,serikali inachezea pesa kwenye mchezo ya kisiasa
MTU ASIE NA HATIA ...... yaani tayari ushatoa maamuzi katika jambo ambalo huna hakika nalo
 
Sawa,ila tusisahau kumchangia TL na kumwombea eh,Hizi drama nazo zitapita tu.Pole Kubenea.
 
Huu ni ujinga wa hali ya juu sana issue yenyewe ni ya kijinga eti wanabishana idadi ya risasi, huyu spika and akili kweli? nadhani karibu atachanganyikiwa.

Then wakimhoji watamuweka mahabusu stupidity of a century.
 
Back
Top Bottom