Saed Kubenea amesafirishwa leo kwa ndege kwenda mkoani Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge

Nalipa kodi ya nymba kila mwaka elf kumi kwa ajili ya upupu kama huu?magufuli ulitokea wapi unanipa BP kila kukicha!
 
Nitaanza kudai kodi yangu.

Naona haifanyi kazi.

From this month, mshahara wangu usikatwe PAYE.
 
Sheikh wangu Ramadhan Rajabu,hayo siyo maadili tuliyofundishwa,ungetumia lugha nzuri kuonesha kukasirishwa kwako ungeeleweka na wala usidanganyike kwamba neno MPUMBAVU siyo tusi.Hilo neno ni tusi ORIGINAL.
Kama hilo nine ndilo linaloeleza wasifu wa mtu huyo, wewe ulitaka atumie neno gani lingine mbadala lakini maana ibaki ile aliyoikusudia!
 
Kuuliza sio ujinga:
1. Hivi spika wa bunge kumuita mbunge kwenye kamati za bunge ni jinai inayopaswa kushughulikiwa na polisi!?
2. Je, kamati ikishamuhoji na (either) kumkuta na makosa au la inamkabidhi kwa polisi kumfungulia mshitaka!?
Atakayenisaidia kunipa mwanga hapa itanisaidia kujua hizo gharama walizotumia polisi kuanzia kumkamata hadi kulipia ndege zinatoka fungu gani la matumizi katika bajeti aliyoisoma Mh. Dr. Mpango mwezi Julai .

Ukijibiwa utanitag mkuu
 
Huyu spika hafai kabisa!Hawa wabunge wamekopeshwa magari,wanalipwa posho na mishahara mikubwa kwa nini asitumie usafiri wake mwenyewe kwenda huko Dodoma ambako ndio kazini kwake?
Daktari alitoa tahadhari Kubenea ana tatizo hawezi kupanda gari kwa safari ndefu
 
Duuh unasafirishwa na ndege kweli awamu ya raha hii,bdo vibaka wataanza nao kusafirishwa na chopa kutoka segerea
 
Haya matumizi mengine ni kukatishana tamaa kulipa kodi, yani kodi yangu inatumika kwenye mambo ya kipumbavu namna hii????!!!!! naenda hospital nakosa huduma nzuri kutokana na uhaba wa dawa, wataalamu, majengo bora, vifaa afu leo kodi yangu inatumika kulipia mambo ya kiseng.... namna hii, haaaaaaaaaaaaaaaaah inakera mno, ukute angeweza hata kuhojiwa Dar kwenye ofisi za bunge. Yeyote aliyehusika kwenye huu ulofa ajue anatuumiza sana walipa kodi, anatusononesha moyoni mwetu, anatukera, pesa zetu za kodi zitumike kutuletea maendeleo na sio kwenye mambo yao yakipuuzi puuzi kama haya.
 
Wamemsafirisha hadi Dodoma Alf wameishia kumpeleka hospital tena, na kamati imesema itamhoji itakapojiridhisha afya yake imeimarika mambo mengine ya nchi ni kizunguzungu tu
 
Kuuliza sio ujinga:
1. Hivi spika wa bunge kumuita mbunge kwenye kamati za bunge ni jinai inayopaswa kushughulikiwa na polisi!?
2. Je, kamati ikishamuhoji na (either) kumkuta na makosa au la inamkabidhi kwa polisi kumfungulia mshitaka!?
Atakayenisaidia kunipa mwanga hapa itanisaidia kujua hizo gharama walizotumia polisi kuanzia kumkamata hadi kulipia ndege zinatoka fungu gani la matumizi katika bajeti aliyoisoma Mh. Dr. Mpango mwezi Julai .


Hiyo pesa iliyotumika kumkatia tiketi ingenunulia watoto wa chekechea pencils. nchi yangu nchi yangu, kuna nini ulichomkosea Mungu?
 
Back
Top Bottom