Jembe Ulaya
JF-Expert Member
- Oct 27, 2008
- 456
- 104
Ndie huyu mwenye kutetea Watanzania wenye asili ya Kiasia wa NHC au mwingine?,hakika mbele ya safari CDM mkiendelea na tabia ya kupokea Pesa za aina hiii,zile sifa zenu zote kama CHAMA MAKINI zitapotea huko mbele ya safari na ndio itakuwa mwanzo wa kununuliwa kusimamia haki.Tafute vyanzo vya umma kukusanya pesa ya kuendeshea chama ili mje kupata dhamana ya kukabidhiwa Nchi.
Watoa pesa nyingi kiasi hicho jueni zitaitajika kulipwa,mtaziludishaje hizo pesa,kwaa njia hipi,au ndio muwape nafasi wapinzain wenu kuwa mtalazimisha kwenda ikulu ili mlipe pesa za matajiri wa kiasia walio ingiza [Inject] kwenye chama chenu.Ninategemea chadema kuwa chama chenye mvuto na style ya aina yake na sio kucopy na kupaste namna ya kujitengenezea pesa.Chama kizuri ni kile chenye watu waliozamilia [Commited] na kujituma kwa hiali na moyo kufanya kazi ya kutumika chama kwa moyo wa hiali na sio kwa kununua mbinu za kuwapata wananchi wa kukiunga mkono chama.
Kwa kusudio kuwa Taifa linaitaji vyama viwili makini vya kupambanishwa katika kufukuzia nafasi ya kupewa madaraka ya kuchukua nafasi ya Urais na kutawala Taifa hili,basi CDM kama wao katika list hiyo basi hawana budi kujiandaa namna ya kumilki chama chenye mkakati wa kisayansi na sio chenye kucopy na kupaste hivyo kwa watu makini hakuna tofauti na kwingine hivyo basi wataona ni bora na kuendelea na chama kilichoko madarakani kulikoni kuwa na chama ambacho hakina tofauti na hawajui uwezo wake kama kweli kinaweza.Hivyo wataona ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili au heri ya zimwi likujualo halikuli likakwisha.
Kama chadema ni makini Watch Out.
Binafsi sioni ubaya wa mchango wa Mzee Sabodo kwa chama anachokipenda,
zaidi anatia na kuongeza chachu ya demokrasia nchini
Mfanyabiashara maarufu wa nchini, Mustapha Sabodo, ameahidi kumuunga mkono mgombea urais atakayependekezwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu ujao.
Sabodo alitoa kauli hiyo jana nyumbani kwake Dar es Salaam, katika hafla ya kukabidhi msaada wa kujenga visima 200 vya maji katika maeneo yote nchini yanayowakilishwa na wabunge 48 wa Chadema.
Alisema anakusudia kukichangia chama hicho kiasi kikubwa cha pesa, kisichopungua milioni 500, kwa sababu anakunwa na siasa zinazofanywa na Chadema katika kutetea maslahi ya wananchi.
Mbali na msaada anaoutoa kwa chama hicho kikuu cha upinzani, alisema anakusudia kukienzi kwa kujenga shule ambayo ataiita Chadema ili iwe kumbukumbu yake ya kudumu.
Sabado is a hero. Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana bila woga na kwa uwazi kabisa alitoa mchango wake kwa Chadema kusaidia kampeni. Wafanyabiashara wengine hufanya kwa kutaka sifa na kujipendekeza kwa wakuu wa nchi na chama tawala. Sijaona mfanyabiashara aliyetoa pesa kusaidia vyama vya upinzania ila sabato. Matajiri wengine wanahangaikia kwenda ikulu na mtaa wa Lumumba kwa malengo ya kurudishiwa fadhila yao kwa kuheshimiwa. Na hatujui niasi gani wanakitoa na kwa makusudio gani.
Sabado ameeleza sababu wazi kwamba anakunwa na sera za Chadema kutetea wanyonge. Na anayokusudia kufanya kuchimba visima 200 katika majimbo ya uchaguzi yanayoongozwa na wabunge wa chadema ni dalili njema za mzee huyu kujali maslahi ya wanyonge. Na kama kujenga shule ambazo ameshafanya kwa manufaa ya wananchi wote inanipa faraja, vinginevyo angejenga shule zake na kuzifanya kitegauchumi kitu ambacho wengi wanafanya, mpaka hapo hatujaelewa jitihada zake?
Uasili wake si hoja kwa vile hata wakati tunapata uhuru kulikuwa na wazungu ambao walikuwa bega kwa bega na Nyerere kutetea Utanganyika. Na Nyerere hakuwaweka kando kwani kumbukumbu zangu kwenye dayari zinaonyesha kwamba Tanganyika huru na baadaye Muungano wa Tanzania tulikuwa na Waziri wa Fedha mzungu ambaye kama sijakosea aliitwa Jenings. Huko Morogoro Bi Shamim ambaye alikuwa mwenye asili ya kiasia alikuwa mbunge wa Morogoro muda mrefu tu kuanzia awamu ya kwanza.
Jamani tusiwe na mtazamo mbaya katika mambo mengi hivyo, tujitahidi kuwa na mtazamo chanya vinginevyo tutakuwa tunatanguliza moyo zaidi badala ya ubongo. Tuachane na itikadi za uzawa, katika ulimwengu wa leo hazina nafasi na ni dalili ya upeo finyu.
Kada CCM atamani Chadema ishinde uchaguzi wa 2015 |
Haogopi coz ni mfanyabiashara halali na si fisadi tokea enzi za MWALIMU NYERERE,wanaogopa ni hawa mafisadi na wasiolipa kodi.Sabodo alikuwa ni rafiki wa karibu wa Mwalimu.The guy amethubutu na ameweza kukata matisho ya CCM.Kasema kwa nini ana spend pesa zake na chachu kubwa ni Dr.Slaa now mwacheni awasaidie wananchi kupitia maelewano mazuri na Chadema .
Hongera sabodo.
Sabodo ameonyesha wazi wapi ataweka kura yake 2015 bado mimi na wewe. Kila Mtanzania anayeitakia haki Umma wa Mtanzania aandae hata Tsh.200 kama ndio uwezo wake kwa ajili Mgombea ambaye atakukomboa na kutuvusha katika mtu huu wenye mamba wengi wala watu.
Watanzania tuko zaidi ya mil.40 yeye kaanza na hayo kama kuna mwingine ataangalia yaliyobaki.jambo zuri kabisa ila nivema yakaangaliwa maeneo mengine yenye matatizo zaidi kuliko kuangalia chama. Kwani maeneo ya wabunge wa Cdm kama kilimanjaro moshi hayana matatizo
Haogopi coz ni mfanyabiashara halali na si fisadi tokea enzi za MWALIMU NYERERE,wanaogopa ni hawa mafisadi na wasiolipa kodi.Sabodo alikuwa ni rafiki wa karibu wa Mwalimu.
Chadema achaneni na misaada ya hawa wafanyabiashara, yatawakuta kama ya ccm.
Ndie huyu mwenye kutetea Watanzania wenye asili ya Kiasia wa NHC au mwingine?,hakika mbele ya safari CDM mkiendelea na tabia ya kupokea Pesa za aina hiii,zile sifa zenu zote kama CHAMA MAKINI zitapotea huko mbele ya safari na ndio itakuwa mwanzo wa kununuliwa kusimamia haki.Tafuteni vyanzo vya umma kukusanya pesa ya kuendeshea chama ili mje kupata dhamana ya kukabidhiwa Nchi.
Watoa pesa nyingi kiasi hicho jueni zitaitajika kulipwa,mtaziludishaje hizo pesa,kwaa njia hipi,au ndio muwape nafasi wapinzain wenu kuwa mtalazimisha kwenda ikulu ili mlipe pesa za matajiri wa kiasia walio ingiza [Inject] kwenye chama chenu.Ninategemea chadema kuwa chama chenye mvuto na style ya aina yake na sio kucopy na kupaste namna ya kujitengenezea pesa.Chama kizuri ni kile chenye watu waliozamilia [Commited] na kujituma kwa hiali na moyo kufanya kazi ya kutumika chama kwa moyo wa hiali na sio kwa kununua mbinu za kuwapata wananchi wa kukiunga mkono chama.
Kwa kusudio kuwa Taifa linaitaji vyama viwili makini vya kupambanishwa katika kufukuzia nafasi ya kupewa madaraka ya kuchukua nafasi ya Urais na kutawala Taifa hili,basi CDM kama wao pia wako katika list hiyo basi hawana budi kujiandaa namna ya kumilki chama chenye mkakati wa kisayansi na sio chenye kucopy na kupaste hivyo kwa watu makini hakuna tofauti na kwingine hivyo basi wataona ni bora na kuendelea na chama kilichoko madarakani kulikoni kuwa na chama ambacho hakina tofauti na hawajui uwezo wake kama kweli kinaweza.Hivyo wataona ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili au heri ya zimwi likujualo halikuli likakwisha.
Kama chadema ni makini Watch Out.