Sabodo kumchangia mgombea wa CHADEMA milioni 500

Jembe Ulaya

JF-Expert Member
Oct 27, 2008
456
103
Mfanyabiashara maarufu wa nchini, Mustapha Sabodo, ameahidi kumuunga mkono mgombea urais atakayependekezwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu ujao.

Sabodo alitoa kauli hiyo jana nyumbani kwake Dar es Salaam, katika hafla ya kukabidhi msaada wa kujenga visima 200 vya maji katika maeneo yote nchini yanayowakilishwa na wabunge 48 wa Chadema.

Alisema anakusudia kukichangia chama hicho kiasi kikubwa cha pesa, kisichopungua milioni 500, kwa sababu anakunwa na siasa zinazofanywa na Chadema katika kutetea maslahi ya wananchi.

Mbali na msaada anaoutoa kwa chama hicho kikuu cha upinzani, alisema anakusudia kukienzi kwa kujenga shule ambayo ataiita Chadema ili iwe kumbukumbu yake ya kudumu.
 
DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,667
Ndie huyu mwenye kutetea Watanzania wenye asili ya Kiasia wa NHC au mwingine?,hakika mbele ya safari CDM mkiendelea na tabia ya kupokea Pesa za aina hiii,zile sifa zenu zote kama CHAMA MAKINI zitapotea huko mbele ya safari na ndio itakuwa mwanzo wa kununuliwa kusimamia haki.Tafuteni vyanzo vya umma kukusanya pesa ya kuendeshea chama ili mje kupata dhamana ya kukabidhiwa Nchi.

Watoa pesa nyingi kiasi hicho jueni zitaitajika kulipwa,mtaziludishaje hizo pesa,kwaa njia hipi,au ndio muwape nafasi wapinzain wenu kuwa mtalazimisha kwenda ikulu ili mlipe pesa za matajiri wa kiasia walio ingiza [Inject] kwenye chama chenu.Ninategemea chadema kuwa chama chenye mvuto na style ya aina yake na sio kucopy na kupaste namna ya kujitengenezea pesa.Chama kizuri ni kile chenye watu waliozamilia [Commited] na kujituma kwa hiali na moyo kufanya kazi ya kutumika chama kwa moyo wa hiali na sio kwa kununua mbinu za kuwapata wananchi wa kukiunga mkono chama.

Kwa kusudio kuwa Taifa linaitaji vyama viwili makini vya kupambanishwa katika kufukuzia nafasi ya kupewa madaraka ya kuchukua nafasi ya Urais na kutawala Taifa hili,basi CDM kama wao pia wako katika list hiyo basi hawana budi kujiandaa namna ya kumilki chama chenye mkakati wa kisayansi na sio chenye kucopy na kupaste hivyo kwa watu makini hakuna tofauti na kwingine hivyo basi wataona ni bora na kuendelea na chama kilichoko madarakani kulikoni kuwa na chama ambacho hakina tofauti na hawajui uwezo wake kama kweli kinaweza.Hivyo wataona ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili au heri ya zimwi likujualo halikuli likakwisha.

Kama chadema ni makini Watch Out.
 
Biohazard

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
2,186
1,403
Ndie huyu mwenye kutetea Watanzania wenye asili ya Kiasia wa NHC au mwingine?,hakika mbele ya safari CDM mkiendelea na tabia ya kupokea Pesa za aina hiii,zile sifa zenu zote kama CHAMA MAKINI zitapotea huko mbele ya safari na ndio itakuwa mwanzo wa kununuliwa kusimamia haki.Tafute vyanzo vya umma kukusanya pesa ya kuendeshea chama ili mje kupata dhamana ya kukabidhiwa Nchi.

Watoa pesa nyingi kiasi hicho jueni zitaitajika kulipwa,mtaziludishaje hizo pesa,kwaa njia hipi,au ndio muwape nafasi wapinzain wenu kuwa mtalazimisha kwenda ikulu ili mlipe pesa za matajiri wa kiasia walio ingiza [Inject] kwenye chama chenu.Ninategemea chadema kuwa chama chenye mvuto na style ya aina yake na sio kucopy na kupaste namna ya kujitengenezea pesa.Chama kizuri ni kile chenye watu waliozamilia [Commited] na kujituma kwa hiali na moyo kufanya kazi ya kutumika chama kwa moyo wa hiali na sio kwa kununua mbinu za kuwapata wananchi wa kukiunga mkono chama.

Kwa kusudio kuwa Taifa linaitaji vyama viwili makini vya kupambanishwa katika kufukuzia nafasi ya kupewa madaraka ya kuchukua nafasi ya Urais na kutawala Taifa hili,basi CDM kama wao katika list hiyo basi hawana budi kujiandaa namna ya kumilki chama chenye mkakati wa kisayansi na sio chenye kucopy na kupaste hivyo kwa watu makini hakuna tofauti na kwingine hivyo basi wataona ni bora na kuendelea na chama kilichoko madarakani kulikoni kuwa na chama ambacho hakina tofauti na hawajui uwezo wake kama kweli kinaweza.Hivyo wataona ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili au heri ya zimwi likujualo halikuli likakwisha.

Kama chadema ni makini Watch Out.

Kwani ukimhonga mwanamke pesa kwa malengo ya kupata penzi na mwisho wa siku akakunyima penzi,je atakua amefanya dhambi au utampiga?
Basi tafuta corelation mwenyewe katika taarifa hapo juu sio unakuja na mawazo kama mtu ambaye hajaenda shule.
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Binafsi sioni ubaya wa mchango wa Mzee Sabodo kwa chama anachokipenda,
zaidi anatia na kuongeza chachu ya demokrasia nchini

The guy amethubutu na ameweza kukata matisho ya CCM.Kasema kwa nini ana spend pesa zake na chachu kubwa ni Dr.Slaa now mwacheni awasaidie wananchi kupitia maelewano mazuri na Chadema .
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
Mkuu inaonekana hamjui huyu mzee. Jamaa alishawachangia cdm huko nyuma mkuu kabla ya uchaguzi wa 2005. Hii haitakuwa mara ya kwanza kwake kufanya hivi kwa opposition party, hasa cdm.

Ikumbukwe pia, huyu jamaa amejenga shule yenye thamani ya bilioni moja mkoani mtwara na lindi. yeye anajali zaidi maslahi ya watz wote na hasa wale wenye mlengo wa kuwatumikia walalahoi.

Fuatilia mambo ya huyu mzee utakubaliana na ukweli kuwa sio mtu wa kutaka madaraka mzee.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,830
Mfanyabiashara maarufu wa nchini, Mustapha Sabodo, ameahidi kumuunga mkono mgombea urais atakayependekezwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu ujao.
Sabodo alitoa kauli hiyo jana nyumbani kwake Dar es Salaam, katika hafla ya kukabidhi msaada wa kujenga visima 200 vya maji katika maeneo yote nchini yanayowakilishwa na wabunge 48 wa Chadema.
Alisema anakusudia kukichangia chama hicho kiasi kikubwa cha pesa, kisichopungua milioni 500, kwa sababu anakunwa na siasa zinazofanywa na Chadema katika kutetea maslahi ya wananchi.
Mbali na msaada anaoutoa kwa chama hicho kikuu cha upinzani, alisema anakusudia kukienzi kwa kujenga shule ambayo ataiita Chadema ili iwe kumbukumbu yake ya kudumu.

Sabado is a hero. Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana bila woga na kwa uwazi kabisa alitoa mchango wake kwa Chadema kusaidia kampeni. Wafanyabiashara wengine hufanya kwa kutaka sifa na kujipendekeza kwa wakuu wa nchi na chama tawala. Sijaona mfanyabiashara aliyetoa pesa kusaidia vyama vya upinzania ila sabato. Matajiri wengine wanahangaikia kwenda ikulu na mtaa wa Lumumba kwa malengo ya kurudishiwa fadhila yao kwa kuheshimiwa. Na hatujui niasi gani wanakitoa na kwa makusudio gani.

Sabado ameeleza sababu wazi kwamba anakunwa na sera za Chadema kutetea wanyonge. Na anayokusudia kufanya kuchimba visima 200 katika majimbo ya uchaguzi yanayoongozwa na wabunge wa chadema ni dalili njema za mzee huyu kujali maslahi ya wanyonge. Na kama kujenga shule ambazo ameshafanya kwa manufaa ya wananchi wote inanipa faraja, vinginevyo angejenga shule zake na kuzifanya kitegauchumi kitu ambacho wengi wanafanya, mpaka hapo hatujaelewa jitihada zake?

Uasili wake si hoja kwa vile hata wakati tunapata uhuru kulikuwa na wazungu ambao walikuwa bega kwa bega na Nyerere kutetea Utanganyika. Na Nyerere hakuwaweka kando kwani kumbukumbu zangu kwenye dayari zinaonyesha kwamba Tanganyika huru na baadaye Muungano wa Tanzania tulikuwa na Waziri wa Fedha mzungu ambaye kama sijakosea aliitwa Jenings. Huko Morogoro Bi Shamim ambaye alikuwa mwenye asili ya kiasia alikuwa mbunge wa Morogoro muda mrefu tu kuanzia awamu ya kwanza.

Jamani tusiwe na mtazamo mbaya katika mambo mengi hivyo, tujitahidi kuwa na mtazamo chanya vinginevyo tutakuwa tunatanguliza moyo zaidi badala ya ubongo. Tuachane na itikadi za uzawa, katika ulimwengu wa leo hazina nafasi na ni dalili ya upeo finyu.

dkslaa-na-sabodo.jpgKatibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa (kushoto)
akimsaidia Kada wa CCM, Mustafa Sabodo kunyanyuka
kwenye kiti nyumbani kwa kada huyo Upanga,
jijini Dar es Salaam.

Kada CCM atamani Chadema ishinde uchaguzi wa 2015
AMWAGA MABILIONI KUCHIMBA VISIMA, ASIFU MSIMAMO WA DK SLAA
KADA wa CCM, Mustafa Sabodo ameahidi kuchimba visima 200 katika majimbo yote ya wabunge wa Chadema nchini, huku akieleza kuwa angependa kuona upinzani unachukua nchi mwaka 2015.Sabodo ambaye ni kada wa CCM tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyarere, alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akipokea mpango wa uchimbaji visima hivyo kutoka kwa Katibu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.Kauli hiyo ya Sabodo ambaye tayari katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana aliisaidia Chadema Sh100 milioni za kampeni, imekuja kipindi ambacho CCM, inakabiliwa na mpasuko kutokana na siasa za makundi.
Wakati CCM ikikabiliwa na kipindi hicho kigumu kisiasa, jana Sabodo ambaye aliahidi kuendelea kukisaidia Chadema, alisema "Ningependa kuona upinzani ukichukua nchi mwaka 2015".

Jana Saa 4:00 asubuhi, Dk Slaa akiongozana na Mkurugenzi wa Mambo ya Bunge wa Chadema, John Mrema walifika nyumbani kwa Sabodo kwa lengo la kukabidhi mchakato wa utekelezaji wa mradi huo wa visima na pia kumshukuru kada huyo wa CCM kwa misaada yake kwa chama hicho.

Katika mazungumzo hayo, Sabodo alimhakikishia Dk Slaa kwamba ataendelea kusaidia chama hicho katika miradi mbalimbali, inayohusu wananchi hususani suala la maji na elimu.

Sabodo alisema elimu ni muhimu katika maisha ya binadamu, lakini maji pia ni uhai, kwakuwa bila maji hakuna mtu anayeweza kufanya chochote.​

Mradi wa Sh2.5 bilioni
Sabodo alisema ametenga Sh2.5 bilioni kwa ajili ya kuchimba visima vya maji virefu na vifupi 700 katika maeneo yenye ukame, huku visima 200 kati ya hivyo vikielekezwa katika majimbo 23 wanakotoka wabunge wa Chadema na Jimbo la Igunga. Chadema kina jumla ya wabunge 48 na 25 kati yao ni wa Viti Maalum.

Alifafanua kwamba anatoa msaada wa maji kwa sababu anatambua umuhimu wa huduma hiyo kwa jamii huku akisisitiza kwamba maji siyo anasa bali ni hitaji la lazima.

Kuhusu sababu ya kujenga urafiki na Dk Slaa Sabodo alisema: "Mimi siyo kwamba navutiwa na wewe Dk Slaa hata nikaona umuhimu wa kutoa msaada kwa Chadema, ninavutiwa na Principle (Kanuni) zako na chama chako,"alisema Sabodo.

Michango hiyo ya Sabodo kwa Chadema iliwahi kuibua manung'uniko kwa baadhi ya makada wa CCM, lakini aliyekuwa Katibu Mkuu, Yusuph Makamba, aliwahi kuliambia gazeti hili kwamba, "Siyo vibaya Mkristo kumsaidia Mwislam, ndiyo ubinadamu," hivyo haoni tatizo kwa Sabodo kusaidia upinzani.​

Dk Slaa anena
Kwa upande wake, Dk Slaa alisema chama hicho kinatarajia kuchimba visima vya maji 11 katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora ikiwa ni wiki takriban mbili tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika Oktoba 2.

Dk Slaa alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kukabidhi mchanganuo wa namna walivyogawa mradi wa utekelezaji wa visima 200, vilivyotolewa na Sabodo kwa lengo la kuchimbwa katika majimbo tofuati wanakotoka wabunge wa Chadema.

Alisema lengo la kutekeleza mradi huo wa maji katika Jimbo la Igunga limetokana na ziara aliyoifanya katika vijiji 98, vilivyopo katika jimbo hilo na kugundua wananchi wake wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji.

"Katika mpango kazi wetu, tumepanga kuchimba visima 11 katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, hii imetokana na ziara yangu katika vijiji 98 ambapo niligundua kuwa wakazi hao wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji,"alifafanua Dk Slaa.

Chadema kilishika nafasi ya pili katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, kwa aliyekuwa mgombea wake, Joseph Kashindye kupata kura 23,260 sawa na asilimia 44.3, nyuma ya mgombea wa CCM, Dalaly Kafumu aliyeshinda kwa kura 26,484 kati ya 52,487 halali zilizopigwa, sawa na asilimia 50.4.

Dk Slaa alimshukuru Sabodo kwa msaada wake wa kukusudia kuchimba visima vya maji katika maeneo mbalimbali nchini, yanayokabiliwa na uhaba akisema kitendo hicho ni cha utu kwa kuwa maji ni uhai.

"Nitoe shukrani kwa niaba ya wabunge ninaowawakilisha kufuatuia msaada wako wa kukusudia kuchimba visima 200 vya maji katika majimbo yao, ni maelfu ya watu watanufaika na msaada huu,"alisema Dk Slaa na kuongeza:,

"Sisi tumekuja kukushukuru kwa niaba ya wabunge wetu na wananchi, lakini pia wabunge wangu watakuja mmoja mmoja kukushukru wewe ni baba yao. Ushindi walioupata ulitokana pia na msaada wako mkubwa wa kifedha wakati wa kampeni,"alisema Dk Slaa.

Kwa upande wake, mchumba wa Dk Slaa, Mushumbushi, alishukuru msaada huo wa maji kutoka kwa Sabodo akisema utawasaidia wanawake na watoto.

"Watu wanaopatwana athari nyingi kutokana na tatizo la maji ni wanawake na watoto, ni wanawake ndio hupatwa na matatizo ya kubakwa wanapokwenda umbali mrefu kuteka maji. Pia ukame wa maji umevunja hata baadhi ya ndoa,"alisema Mushumbushi.​
Wamzungumzia Nyerere

Akizungumzia kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Nyerere, Sabodo alisema kwa miaka 12 Taifa limeshuhudia maadui wa taifa wakiongezeka."Baba wa taifa aliacha maadui wakuu watatu, ujinga, mardhi na umasikini. Lakini sasa badala ya kupungua, wameongezeka wawili na kufanya idadi hiyo kuwa watano,"alisema Sabodo.

Sabodo aliwataja maadui hao wapya kuwa ni wizi wa mali za umma wanaotokana na mmomonyoko wa maadili pamoja na ufisadi.

Katika mazungumzo yake, Sabodo hakusita kueleza kuwa hali ya sasa ya uadilifu kwa viongozi imeshuka kwa kiwango kikubwa na kusisitiza kwamba, vitendo hivyo ndivyo vinavyoliangamiza taifa.

Kwa upande wake, Dk Slaa alisema kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere inaadhimishwa kwa utani kutokana na viongozi wengi wakiwemo wenye mamlaka kushindwa kufuata maadili ya mwasisi huyo wa taifa.

Alisema kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere haipaswi kusherehekewa kama siku ya shamrashamra na badala yake, kwa kufuata maadili na msingi aliyosimamia.
 
hahoyaya

Member
Apr 24, 2011
89
11
The guy amethubutu na ameweza kukata matisho ya CCM.Kasema kwa nini ana spend pesa zake na chachu kubwa ni Dr.Slaa now mwacheni awasaidie wananchi kupitia maelewano mazuri na Chadema .
Haogopi coz ni mfanyabiashara halali na si fisadi tokea enzi za MWALIMU NYERERE,wanaogopa ni hawa mafisadi na wasiolipa kodi.Sabodo alikuwa ni rafiki wa karibu wa Mwalimu.
 
Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,582
755
Hongera sabodo.

Sabodo ameonyesha wazi wapi ataweka kura yake 2015 bado mimi na wewe. Kila Mtanzania anayeitakia haki Umma wa Mtanzania aandae hata Tsh.200 kama ndio uwezo wake kwa ajili Mgombea ambaye atakukomboa na kutuvusha katika mtu huu wenye mamba wengi wala watu.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,830
Hongera sabodo.

Sabodo ameonyesha wazi wapi ataweka kura yake 2015 bado mimi na wewe. Kila Mtanzania anayeitakia haki Umma wa Mtanzania aandae hata Tsh.200 kama ndio uwezo wake kwa ajili Mgombea ambaye atakukomboa na kutuvusha katika mtu huu wenye mamba wengi wala watu.

Sabado kishaona ngoma ilivyolia Bungeni Dodoma, ni dhahiri jitihada kubwa zinahitajika kuwabakisha wabunge waliopo kutoka Chadema bungeni, kuongeza wengine na control ya Ikulu.
 
Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,046
KADA wa CCM, Mustafa Sabodo ameahidi kuchimba visima 200 katika majimbo yote ya wabunge wa Chadema nchini, huku akieleza kuwa angependa kuona upinzani unachukua nchi mwaka 2015.

Natoa pongezi kubwa sana kwa Mzee Mustafa Sabodo kwa kutoa ahadi yenye matumaini kwa wananchi wa majimbo tunayoyashikilia na kuiombea dua CDM kuongoza nchi 2015. Wananchi wazalendo wajitoe pia kukisaidia chama hata kwa njia ya SMS ili kukijengea chama uwezo kwani safari ya ukombozi ni ndefu na inagharama kubwa. Tusiishie tu kushabikia chama na kutoana povu na magamba badala ya kuchangia chama kwa hali na mali. Ndugu zangu safari ya ukombozi ni ngumu lakini chonde chonde lengo letu libaki kuwa ni lile lile la kuikomboa nchi kutoka kwa mafisadi. Ndugu zangu kwa sasa chama pekee ambacho kinatoa upinzani wa kweli na ambacho kinapokelewa vizuri na wananchi walio wengi ni CDM, hivyo juhudi za kukijenga chama ili kiuzike zaidi liwe ni la kila mtakia nchi mema. Kwa mfano unaweza kwa nafasi yako huko ulipo ukakisaidia chama kwa kuwaamsha walio lala hasa vijijini kuwa CDM ni Tumaini jipya na kuwapa mawili matatu ya namna tunavyohujumiwa na Viongozi tuliowaamini na kuwapa dhamana ya kuongoza nchi. Huo ni mchango tosha kwa Chama. Peeeeooopleeeee's

Source: Mwananchi tar 13-14/10/2011
 
WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
2,920
1,226
Well done!! Ila inabidi CDM waendelee kuwa smart, nategemea ahadi zao zitatekelezwa kwa speed kubwa.
 
Mgongo wa paka

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
485
34
jambo zuri kabisa ila nivema yakaangaliwa maeneo mengine yenye matatizo zaidi kuliko kuangalia chama. Kwani maeneo ya wabunge wa Cdm kama kilimanjaro moshi hayana matatizo
 
Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
4,500
jambo zuri kabisa ila nivema yakaangaliwa maeneo mengine yenye matatizo zaidi kuliko kuangalia chama. Kwani maeneo ya wabunge wa Cdm kama kilimanjaro moshi hayana matatizo
Watanzania tuko zaidi ya mil.40 yeye kaanza na hayo kama kuna mwingine ataangalia yaliyobaki.
 
Mbugi

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,489
256
Haogopi coz ni mfanyabiashara halali na si fisadi tokea enzi za MWALIMU NYERERE,wanaogopa ni hawa mafisadi na wasiolipa kodi.Sabodo alikuwa ni rafiki wa karibu wa Mwalimu.

aisifuye mvua ujue imemnyea!!!!!
 
Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Chadema achaneni na misaada ya hawa wafanyabiashara, yatawakuta kama ya ccm.
 
Mponjori

JF-Expert Member
Feb 21, 2011
2,205
548
Huyu mzee ni jasiri 7bu 2mezoea wafanyabiashara kujpendekeza chama tawala.hatoi kisiri amejtangaza kabsa.kama wapo wengne nao waige..
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,563
7,141
Chadema achaneni na misaada ya hawa wafanyabiashara, yatawakuta kama ya ccm.

Hizi pesa zunaenda kwa wananchi moja kwa moja na sio za matumizi binafsi Kama wafanyavyo viongozi wa ccm.
 
Mpanzi

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
785
435
Ndie huyu mwenye kutetea Watanzania wenye asili ya Kiasia wa NHC au mwingine?,hakika mbele ya safari CDM mkiendelea na tabia ya kupokea Pesa za aina hiii,zile sifa zenu zote kama CHAMA MAKINI zitapotea huko mbele ya safari na ndio itakuwa mwanzo wa kununuliwa kusimamia haki.Tafuteni vyanzo vya umma kukusanya pesa ya kuendeshea chama ili mje kupata dhamana ya kukabidhiwa Nchi.

Watoa pesa nyingi kiasi hicho jueni zitaitajika kulipwa,mtaziludishaje hizo pesa,kwaa njia hipi,au ndio muwape nafasi wapinzain wenu kuwa mtalazimisha kwenda ikulu ili mlipe pesa za matajiri wa kiasia walio ingiza [Inject] kwenye chama chenu.Ninategemea chadema kuwa chama chenye mvuto na style ya aina yake na sio kucopy na kupaste namna ya kujitengenezea pesa.Chama kizuri ni kile chenye watu waliozamilia [Commited] na kujituma kwa hiali na moyo kufanya kazi ya kutumika chama kwa moyo wa hiali na sio kwa kununua mbinu za kuwapata wananchi wa kukiunga mkono chama.

Kwa kusudio kuwa Taifa linaitaji vyama viwili makini vya kupambanishwa katika kufukuzia nafasi ya kupewa madaraka ya kuchukua nafasi ya Urais na kutawala Taifa hili,basi CDM kama wao pia wako katika list hiyo basi hawana budi kujiandaa namna ya kumilki chama chenye mkakati wa kisayansi na sio chenye kucopy na kupaste hivyo kwa watu makini hakuna tofauti na kwingine hivyo basi wataona ni bora na kuendelea na chama kilichoko madarakani kulikoni kuwa na chama ambacho hakina tofauti na hawajui uwezo wake kama kweli kinaweza.Hivyo wataona ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili au heri ya zimwi likujualo halikuli likakwisha.

Kama chadema ni makini Watch Out.

Acha wivu wa kike, alichopinga Sobodo na suala la kuulizia asili ya wapangaji! Huo ni ubaguzi!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom