Jembe Ulaya
JF-Expert Member
- Oct 27, 2008
- 456
- 104
Mfanyabiashara maarufu wa nchini, Mustapha Sabodo, ameahidi kumuunga mkono mgombea urais atakayependekezwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu ujao.
Sabodo alitoa kauli hiyo jana nyumbani kwake Dar es Salaam, katika hafla ya kukabidhi msaada wa kujenga visima 200 vya maji katika maeneo yote nchini yanayowakilishwa na wabunge 48 wa Chadema.
Alisema anakusudia kukichangia chama hicho kiasi kikubwa cha pesa, kisichopungua milioni 500, kwa sababu anakunwa na siasa zinazofanywa na Chadema katika kutetea maslahi ya wananchi.
Mbali na msaada anaoutoa kwa chama hicho kikuu cha upinzani, alisema anakusudia kukienzi kwa kujenga shule ambayo ataiita Chadema ili iwe kumbukumbu yake ya kudumu.