Nebukadreza
Member
- Dec 31, 2007
- 24
- 50
Hapa nazungumzia wale ambao hawali nyama kiimani na si wale ambao hawali kwasababu za kiafya tofauti na ukristo na uislam, dini kama buddhism, krishna nk wanaamini sana katika karma ya kila kiumbe na uwepo wake katika uso wa dunia, kwamba bata, mbuzi, samaki, punda na chochote chenye uhai kuna sababu maalum ya kuwa hivyo kilivyo.
Kwahiyo huwezi kutoa uhai wake kwa ajili ya shibe yako, utakuwa unajitengenezea karma mbaya, yani leo ukimuu mnyama ukala nyama yake next reincarnation yeye atazaliwa binadamu na wewe mnyama halafu atatenda kama wewe ulivyotenda imani hii imezama mno mioyoni mwao kiasi kwamba ni ngumu mno kuwakuta wanakula nyama. Kuna mazingira ambayo yanaweza kuwafanya wale nyama nayo ni
1.hawakushuhudia mnyama akichinjwa/akiuliwa
2. Hakuchinjwa kwa ajili yao
3. Isiwe ni nyama kwa ajili ya biashara, hapo anaweza kula na karma isimdhuru kila imani ina uchizi wake, kuna mavegetarian ambao kwa compassion kwa viumbe hufagia kabla ya kukanyaga ili wasiwadhuru viumbe
Dunia inaelimu za kila aina, wasiokula nyama kwa sababu za kiimani ukiwasikiliza wana maelezo yanayo onekana yana logic kibinadamu,kiafya na kiumbaji. wapo kiroho zaidi na wanaujua mfumo wa mahitaji ya mwili, mfumo wa uyeyushaji chakula, mfumo wa upumuaji. Wanasababu nyingi ikiwemo za kukataa kutoa uhai lakini pia wanasema.
Mfumo wa taya na meno ya binadamu haujaumbwa kula nyama, pia
Inachelewa kusagwa mwilini hivo kutengeneza sumu. Japo baadhi ya hoja zina ukweli, lakini kama issue ya uhai hata mimea na matunda ina uhai isipokuwa haina roho. Na kwa Elimu yao mwisho wa Siku wanaishia kwenye Miungu yao kama krishna, n.k
Tunaokula nyama tunazo sababu za kula nyama kama ifuatavyo.
Kwa wakristo aliyewaumba aliwapa muongozo na mipaka (haramu na halali) katika nyanja za chakula, kuoana, mavazi, n,k.(rejea kitabu cha torati, mambo ya malawi). Jambo lolote kama halikufanywa kwa kiasi litaleta madhara. hata kama ni vegetarian kama hukula kwa kiasi pia litaleta madhara. na nyama ukila kwa kiasi na yenye ubora unaotakiwa haiwezi kuleta madhara



