Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,979
- 218,904
Huyu kijana alipewa madaraka akiwa duni sana ! hivi alizaliwa na kukulia wapi , mbona ushamba wake ni wa kutisha sana ?Mwaka jana mwishoni mfanyabiashara na mbunifu wa mavazi Jeffery Mmbungu maarufu kama @Speshoz alifungua kiwanda cha vinywaji vikali, wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro. Kiwanda hicho kinaitwa Daren Fabrics Industries Ltd kinazalisha kinywaji chenye jina Faru John.
Mwezi February mwaka huu, aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya alimpigia Jeff na kumwambia kuwa CCM itafanya maadhimisho ya miaka 44 tangu kuanzishwa, na yeye ni miongoni mwa wanakamati wanaoandaa maadhimisho hayo.
Akataka kiwanda hicho kichangie TZS 10M kufanikisha maadhimisho hayo. Jeff akamwambia hana uwezo wa kuchangia 10M, lakini akaahidi kuchangia 1M. Sabaya akamnanga kwamba serikali ya CCM ndiyo iliyomuwekea mazingira mazuri ya kibiashara hadi akaweza kufungua kiwanda, kwahiyo kuchangia 1M ni dharau kwa chama, anatakiwa achangie kiasi kisichopungua 10M.
Jeff akamwambia hana pesa hiyo. Sabaya akamwambia nimepitia transaction zako TRA najua unafanya mauzo ya mamilioni ya shilingi. Jeff akamwambia bado kiwanda ni kichanga na hakijaanza kujiendesha kwa faida kiasi cha kumpa Sabaya 10M.
Mwezi May mwaka huu Sabaya akavamia kiwanda hicho akiwa na mabaunsa wake. Wakawa-harass sana wafanyakazi waliokuwepo. Sabaya akiongozana na waandishi wa vyombo 11 vya habari akatangaza kukifunga kiwanda hicho kwa madai kinajiendesha bila vibali.
Vyombo vya habari vikaripoti kuwa kiwanda hicho kimefungwa kwa kufanya uzalishaji wa vinywaji vikali bila kuwa na kibali. Jeff akashangaa kwa sababu alikua na vibali vyote.
Ana leseni ya BRELA nambari 142255766 iliyotolewa July mwaka 2020. Ana leseni ya TRA nambari 142255766 iliyolewa July 2020. Ana leseni ya biashara nambari 03356294 iliyotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Hai tarehe 25 September 2020.
Ana Leseni ya mkemia mkuu wa serikali nambari B002C000255 iliyotolewa October mwaka 2020, pia ana Leseni ya TBS nambari 3082 iliyotolewa December 2020. Pia kabla ya kuanza uzalishaji alipewa barua ya ruhusa kutoka TBS yenye Kumbukumbu nambari QA/QCCA/3215/17.
Sasa akashangaa imekuaje kiwanda kifungwe kwa kukosa vibali wakati vibali vyote anavyo? Akampigia Sabaya kumuuliza. Akamwambia aende ofisini.
Alipofika ofisini, wakaongea na akamuonesha nakala za vibali. Sabaya akatoka ofisini na kumuacha ndani. Aliporudi akamnyang'anya simu zote, na kumuamuru akae chini. Akaita mabaunsa wake, wakamvua viatu na mkanda na kumpeleka rumande.
Taarifa za kukamatwa kwake zikafika kwa viongozi mbalimbali wa serikali. Wizara ya ya viwanda na biashara ikatoa tamko kuwa kiwanda hicho kinajiendesha kwa mujibu wa sheria. Wizara ya uwekezaje, ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali, Shirika la viwango (TBS), pamoja na ofisi ya BRELA wakaingilia kati na kueleza kuwa kiwanda hicho kinajiendesha kihalali.
Kesho yake Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro akafanya press na kutoa ufafanuzi kuwa kiwanda hicho kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Taarifa hiyo ikaeleza kuwa mwezi April kiwanda hicho kilipewa stika za 200M na kiliweza kuhuisha stika za 93M. Pia kwa siku chache za mwezi May (kabla hakijafungwa) kilikua kimehuisha stika za 13M.
Taarifa ya TRA ikaeleza kuwa kiwanda hicho hakijawahi kuwa na mgogoro wowote na serikali wala hakijawahi kujiendesha bila kuwa na vibali. Ikatangaza kukifungulia kiwanda hicho na kukiruhusu kiendelee na uzalishaji.
Media zote zilizoripoti kuwa kiwanda hicho kimefungwa zilialikwa kwenye Press ya TRA ili ziujulishe umma kwamba taarifa ya Sabaya haikua sahihi, na kwamba kiwanda hicho kimeruhusiwa kuendelea na uzalishaji.
Lakini Sabaya akazuia media hizo zisiripoti taarifa hiyo ya TRA. Ni ITV pekee walioamua kusimama katika misingi ya taaluma na kutoa ufafanuzi kwa umma. Media nyingine ziliamua kusimama na Sabaya. What a shame?
Tayari Jeff ameshaenda TAKUKURU kuwasilisha ushahidi wake. Pia atawasilisha malalamiko Baraza la habari nchini (MCT) ili media zilizomchafua na zikakataa kumsafisha zichukuliwe hatua, kwa sababu habari ya kiwanda hicho kufungwa imeathiri mauzo kwa kiasi kikubwa!