Sababu za ngao (push bumper) kupigwa marufuku baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Ngao, kama zinavyojulikana na wengi au kwa kiingereza bull bar, au push bumper, brush guard, moose bumper, etc, ni vyuma vinavyowekwa mbele ya uso wa gari au wengine husema bampa la mbele ya gari, kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupendezesha muonekano wa gari. Hata hivyo, jina lenyewe bull bar linaashiria chanzo au mwanzo wa matumizi ya vyuma hivyo. Kihistoria, vyuma hivyo vilikuwa vinawekwa mbele ya magari hasa makubwa yanayopita kwenye maeneo yenye changamoto za wanyama wanaokatisha barabarani, hasa ng’ombe au nyati. Na vile vile gari zinazokwenda mbugani, ili kuweza kuikinga gari na waliomo ndani dhidi ya madhara ya kugongana na wanyama. Lakini pia ngao hizo zilikuwa zimewekwa ili kusaidia pale inapotokea ajali gari ikagonga mti. Sawa na kazi inayofanywa na roll bars.

Kuenea kwa matumizi ya ngao hadi kwenye magari yanayobeba abiria ambayo hayana safari za kwenda mbugani wala misituni kulikuja kuonekana kuwa na madhara makubwa hasa inapotokea ajali. Lakini hata hivyo, ngao hizo wakati Fulani zilikuwa zinasababisha ubabe (road rage) kwa watu wenye magari yenye ngao dhidi ya wasio nazo, au wenye ngao kubwa dhidi ya magari madogo. Hata hivyo, sababu kubwa ya kupigwa marufuku ngao ni za kiusalama zaidi kama zinavyoelezwa hapa chini:

Madhara ya Ngao Yaliyosababisha Zizuiwe
1. Ngao husababisha sehemu laini ya mbele au ya nyuma ya gari iliyojengwa kwa ajili ya kuharibiwa (crumple zone) na ajali ili kunyonya mshindo(impact) wa ajali unaotokana na nishati mwendo (kinetic energy), ili kuzuia mshindo kwenda kwenye bodi, iharibike na hivyo kusababisha majeraha au vifo kwa waliomo kwenye gari. Kama ulikuwa hufahamu hii ndoa sababu magari mengi sasa hivi bodi zake zinatengenezwa kwa “fibre” na vyuma vichache hasa maeneo ya mbele, na kuachwa nafasi kati ya injini na bodi;

2. Ngao huweza kuingilia ufanyaji kazi wa mifuko ya hewa (air bags) wakati wa ajali na kufanya zisifumuke ili kumkinga dereva au abiria;

3. Ngao ni hatari kwa waendesha pikipiki, baiskeli na waenda kwa miguu. Kiasi magari yameundwa kupunguza madhara kwa watumiaji wengine wa barabara, ngao zinaongeza madhara hayo, hasa ukizingatia watumiaji tajwa hapo juu hawana bodi.

4. Ngao Husababisha uharibifu wa chesesi wakati wa ajali kutokana na ugumu wake. Kisayansi ule mshindo wa kugongana(impact) haugawanywi kisawa sawa, na hivyo kupelekea nishati mwendo kulazimika kwenda kwenye bodi na hivyo kutembea hadi kwa abiria.

Ripoti ya Mamlaka ya Usafiri ya Australia, yaani Australian Transport Safety Bureau(ATSB) ya 2020, inasema kwamba ngao zinaongeza hatari zaidi ya madhara kwa binadamu waenda kwa miguu na watumiaji barabara wanyonge( vulnerable road users). Utafiti huu unaungwa mkono na utafiti uliofanywa na Desapria na wenzake (Ediriweera Desapriya, et al, Bull Bars and Vulnerable Road Users, Traffic Injury Prevention, 13:1, 86-92, DOI: 10.1080/15389588.2011.624143). Nchini India kosa la kukutwa umefunga ngao ni kuanzia Rupia 1000 hadi 5000.
F1535356-4990-434B-BC2B-9654657E3B03.jpeg
 
View attachment 2509015
Bodaboda wanaheshima sana wakiona gari yako ina ngao
 
Daladala wanatuchomekea watakavyo wenye magari madogo..
Ngao zimepigwa marufuku lkn bado traffic wanaangalia tu
 
Back
Top Bottom