Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch

Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakini ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu nyingi.

Henoko anayedhaniwa kuwa alikuwa ndio mwandishi wa kitabu hiki ni Yule mtoto wa Yaredi na baba wa Metuselah, ambaye akaja kuwa babu wa Nuhu MWANZO 5:21-23, Ni Moja ya Mtu anayetajwa kuwa na Mwisho wa Ajabu kwani hakufa, bali alitwaliwa mbinguni YOSHUA BIN SIRA 44:16, WAEBRANIA 11:5. Maswala Kama haya hupaswi kujadili na Wale wenye Canon Ya Vitabu 66 kwani watakwambia vitabu hivi havifai "Wanaviita Apokrifa" Wasijue Hata Baadhi ya Sura za Kitabu cha Zaburi ni Apokrifa na katika Biblia yao zimo.

TUANZE....
Hiki kitabu cha Henoko Hukataliwa na Kanisa Katoliki la Magharibi (Latin Church) kwa Sababu zake za Msingi Moja ya Sababu ni Kitabu Kukosa Jina la Mwandishi hakika, Lakini kanisa Katoliki la Mashari la Ethiopia (Orthodox) katika Orodha yao wanakitumia kama Kitabu cha Muhimu sana. Ni kama Wayahudi wanavyokitumia kitabu kinachoitwa YASHARI au JASHAR kinachotajwa 2SAMWELI 1:18, Vitabu hivi vina mambo fulani ya kipekee ambayo wataalamu husema ni siri..... (Ngoja Tuendelee)

BASI......
Kitabu Cha Henoko Hutajwa kwa hypingwa Vikali kwa sababu Ndio huonyesha Mtu mweupe alipata wapi Ujuzi, Pia huonyesha Chanzo cha Mapepo na Wanefili.

Ukisoma Kitabu cha HENOKO 6:1-8 ni sawa na Ukisoma MWANZO 6:1-8 lakini kuna utofauti wa Stori za malaika zaidi, Inaonekana katika zama za YAREDI babaye na HENOKO kuna malaika kama 200 walikubaliana kushuka duniani na Kujichanganya na wanadamu, hapo ndipo ambapo YUDA alinakili maelezo ya YUDA 1:6 Malaika walipoona kuna mabinti wa wanadamu wanavutia/Wazuri MWANZO 6:2 Ndipo wakashauriana "Mwaonaje Tujitwalie tuwaoe, tuzae nao watoto?" Malaika Kiongozi aliyeitwa SAMYAZA akahofia Labda malaika wenzie wanaweza Kumsaliti katika mpango huu, Akahimiza malaika kuapa, Wakaapa kutekeleza. (Henoko 7:3-6)

Kitabu Cha Henoko kinawataja kabisa kwa Majina Viongozi wa Malaika hao waliokuwa katika Mlima HERMON kwamba ni SEMIAZAZ, ARAKIBA, RAMEEL, KOKABIEL, TAMIEL, RAMIEL, DANEL, EZEQEEL, BARAQIJAL, ASAEL, ARMAROS, BATAREL, ANANEL, ZAQIEL, SAMSAPEEL, SATAREL, TUREL, JOMJAEL, SARIEL.

Ikumbukwe hawa hawakuwa malaika Watiifu kwa Mungu, Ni wazi kuwa walikuwa sehemu Katika wale Walioasi pamoja na shetani, Katika MWANZO 6:2-4 Imewataja kama "WANA WA MUNGU" hili jina lisikuchanganye maana malaika wote huitwa wana wa Mungu ndio maana hata Biblia ya asili ya Kiyunani imewaita malaika "ANGELUS ES DEUS" ikimaanisha malaika wa Mungu No matter Watiifu au Sivyo, Sasa mstari wa 4 katika MWANZO 6 unasema "Basi walikuwepo Wanefili duniani(NEPHILIM THE FALLEN ANGELS) hapo jiulize kwa nini aseme "DUNIANI" ni kwasababu hapakuwa mahali pao pa asili (2Petro 2:4,YUDA 1:6) Ni lazima waliyaacha makao yao...

Tuendelee...
Kitabu cha HENOKO 7:1-6 tunaona haya yafuatayo, Malaika wale 200 Wakiongoza na SEMJAZA baada ya Kiapo, wanaoa mabinti wanadamu Na Kuwapa Mimba, Hawakuishia hapo, Katika Sura ya 7 Mstari wa 10 tunaona Malaika hawa waliwafundisha binadamu Uchawi "sorcery" Wakafundisha Orodha ya Maneno ya Kufufua wafu "incantations" Wakawafundisha Jinsi ya Kutengeneza Dawa za Kuwatibu kutumia Mitishamba (pharmacology).

Ilipofika kipindi cha wale mabinti kuzaa Katika sura ya 7:11-14 tunaambiwa Walizaliwa Viumbe wakubwa kupita hata Binadamu na Malaika (Giants), Walizaliwa wengi Mpaka Binadamu walichoka Kuwahudumia chakula, Wakaanza kula Wanyama, Ndege na Samaki, Baadae wakaanza kuwala Binadamu, na Mwisho wakalana wao kwa Wao.

Basi katika Sura ya 8 tunaona Malaika AZAZEL anawaonea huruma Binadamu, Anaanza kuwafundisha Kutengeneza Silaha, Mapanga (Swords) , Visu, Ngao na Ngao za Vifuani (BREASTPLATED) hapa ndipo zana za chuma zilipogunduliwa (MWANZO 4:22) TUBALI-KAINI akiwa wa kwanza kuchukua Ujuzi.

BASI..... Kupitia Malaika Azazel ndipo Binadamu alipojua Kupigana Vita, Malaika hawakuishia hapo, Malaika hawa ndio Walifundisha Dada zetu kuvaa Vikuku na Bangili (BRACELETS) Pia wakafundisha dada zetu kupaka Rangi Kope (BEAUTIFYING OF EYELIDS) na hapa ndipo Dhambi ya Kuzini kwa matamanio ilianza

Malaika waliendelea Kutoa siri nyingi na Kumpa Binadamu uwezo Ulioshindikana, Kila malaika alikuwa na Kitengo chake.

Malaika aliyeitwa SEMJAZA huyu aliwafundisha Binadamu kumiliki Nguvu za Maajabu kufanya Mambo makubwa, Pia Kutumia Mizizi ya Miti kama Tiba, Kemia Kiujumla. Malaika ARMAROS alifundisha jinsi ya Kutatua Tatizo litokanalo na Uchawi wa mtu mwingine. Malaika BARAQIEL huyu aliwafundisha binadamu elimu ya vitu vya Angani "ASTROLOGY" Malaika kwa jina la KOKABEL akawafundisha binadamu elimu ya Anga ihusuyo mipaka ya Nyota na maumbo yake "CONSTELLATION" Malaika EZEQEEL akawafundisha Binadamu Juu ya Mawingu. Malaika ARAQIEL akawafundisha Alama za Kidunia (zodiac elemental rulerships) ambazo tunaziita Libra, Virgo, Capricon nakadhalika. Malaika SHAMSIEL akafundisha alama za Jua Na Malaika SARIEL akawapa Kozi za Elimu ya Mwezini.

Kwahiyo Ujuzi wa Binadamu na Mambo machafu yalianzia Juu ya Hawa malaika Bila Ujio wao Binadamu Angekuwa "Kilaza Mmoja hivi" Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na malaika duniani, Hata Mungu aliona wameipa Mbingu aibu, na Alishindwa Kuwasamehe na aliwafunga vifungo vya milele chini ya Giza wakingojea hukumu.

CATHOLIC THEOLOGICAL REFLECTION.

Wanateolojia Wakanisa Husema wazi kuwa inawezekana huu ulikuwa ni mpango wa Shetani kuharibu Mpango wa Mungu wa MWANZO 3:15 kwa Sababu Mungu alisema Mkombozi wa Wanadamu atakuwa binadamu Pure na si Malaika na Atazaliwa Pasipo Dhambi, Na Atazaliwa na Mwanamke, Basi Shetani alipanga kuharibu Vinasaba (Gene) za Binadamu kwa kuzichanganya na za Malaika Basi basi Kuzaliwa Kwa Mkombozi kungeshindikana.

Lakini Mungu anajua Zaidi (AN OMNISCIENT) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na Kubakiza Wanadamu 8 tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kitabu kuwepo ndani ya biblia au kutokuwepo mimi sioni kama ni issue.
Issue ni kuangalia maudhui ya kitabu chote kizima cha biblia na kama yanaumana bila kukinzana. Sababu nijuavyo maandiko matakatifu hayakuwa hapo kabla katika mpangilio tunaouana leo. Watu waliandika kuhusu mfano maisha ya Yesu, kile walichosikia akisema au kuagiza nk.

Lakini Yesu hajui kama maneno yake yamewekwa fungu fulani kuwa ni Matayo moja mlango wa kwanza sijui mstari wa ngapi nakuendelea.
Hii ilikuwa ni taratibu tu ya waandishi kuyaweka katika mfumo wa kurahisisha kiufuatiliaji.

Kitabu cha biblia kina kusudi moja kuu nalo ni anguko la mtu na namna au hatua alizopitia hata ukombozi wake ulioahidiwa na Mungu mwenyewe. Na kama kitabu cha Henoko kipo kama mtoa post alivyojaribu kunukuu baadhi ya vifungu mie naona hata hii biblia yenye vitabu 66 inazungumza jambo lile lile.

Katika mtu(Adamu) kumekuwepo na zao mbili yaani uzao wa nyoka na uzao wa mwanamke. Huu uzao wa nyoka umekuwepo baada ya anguko na kwamba kuna mwingiliano kati ya wana wa Mungu kwa binti za binadamu ambayo matokeo yake ni kuzaliwa Mijitu(giants).

Kwa hiyo anguko la uzao wa Adam ni katika damu. Habili kwa ufunuo tunajuzwa kuwa alitoa dhabihu ya mnyama na hii ndio Mungu aliitoa kwa wazazi wake kwani wakiisha anguka aliwafunika uchi wao kwa ngozi ya mnyama. Ngozi hiyo ingetoka wapi pasipo kumwaga damu?

Hata injili ya waebrania inashuhudia hilo kwamba hapana upatanisho bila damu.

Tunaweza kujiuliza je malaika wa kimbingu ni roho, je waweza kupata uzao kwa binadamu?

Jibu ni hapana! Kiumbe yule shetani ambae ni roho alipitia kwa mnyama nyoka. Na kwa sasa hivi haiwezekani ila kwa wakati ule iliwezekana maana nyoka yule aliyemdanganya hawa alikuwa hajabadilishwa maumbile. Katika hukumu ya Mungu kwa nyoka baada ya kumdanganya Hawa ni kuenda kwa tumbo na chakula chake kuwa mavumbi. Ni wazi kuwa hakuwa na umbile hilo la kwenda kwa tumbo ila ni mabadiliko ya kimaumbile yaliyotokana na laana ya kuasi.

Hapa ndipo palipo na ile missing link kati ya mwendelezo wa uzao wa nyoka na binadamu.

Ukiifuatilia biblia kwa umakini utagundua kuwa kusa la shetani kuuchangaya uzao wa kibinadamu na mnyama ulipitia kwa hayawani yule aliekuwa mwerevu sana yaani nyoka na jambo hili lilitokea kwa Hawa mke wa Adamu.

Sasa ukiendeleza huu ufuatiliaji utaona kuwa uzao wa Kaini ndio ulioitwa uzao wa nyoka na kwamba kizazi hiki cha kaini kilipojichukulia wake kutoka kizazi cha Seth ndipo walipozaliwa mijitu(giants).

Malaika waliowekwa katika vifungo vya giza kama utosoma vizuri utagundua sii malaika roho bali watu kwa sababu hadi sasa malaika wa kimbingu walioasi wapo katika anga la roho wa pepo wachafu wakiendeleza kazi yao ya ushawishi dhidi ya neno la Mungu(asili).

Naamini kuna mengi ya kujifunza nami binafsi ni muumini wa kujifunza.
 
Nimesoma kitabu hicho cha Yuda.

Lakini point yangu itabaki pale pale, ni mafundisho yapi ya Henoko unayoyalilia wewe ukitaka yawekwe kwenye biblia.

Manabii wa zamani walitoa unabii kuwaonya watu wa kipindi kile, si henoko peke yake alifanya hivo, wapo manabii wengi tu.

Lakini swali linakuja wewe uliyesoma kitabu cha henoko unanizidi nini mimi ambae sijakisoma. ?

Na kama waliounganisha vitatu vilivyounda Biblia waliona hakifai Roho mtakatifu aliwaonesha kuwa kimechakachuliwa ? Au si cha muhimu.
Utalazimisha kiwepo kwenye Biblia ?

Kama henoko anamafundisho muhimu sana, tuambie.
Maana mimi najua hata vitabu vya Solomon si vyote vilichukuliwa na kuwekwa kwenye biblia.
Kwa biblia hakuna kuzidiana kiimani ila ntakuzidi kimaarifa tu na kuelewa mistari zaidi..... Mfano hiyo Yuda 6 kwa wewe utaona ni vague ila kwangu ntaunganisha dots na Book of Enoch maana imeongelewa kwa undani zaidi.

Ngoja nikupe na huu mstari

Mwanzo 4
23 Lameki akawaambia wake zake,Sikieni sauti yangu, Ada na Sila;Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu;Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha;Kijana kwa kunichubua;
24 Kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba,Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba

Hapa umeelewa nini?
 
Mkuu hauja katazwa kusoma hicho kitabu utata unakuja pale unapotaka kile ulicho soma basi kiwepo na kama kisipo kuwepo basi ni tatizo

Umetilia mashaka kitabu cha waebrania ila cha kushangaza umetumia kitabu hicho hicho pia kutoa maelezo ya hoja kadhaa.
 
Hivi kitabu cha waebrania kimeandikwa na nani?
Mimi ninaamini mwandishi ni paulo japo kuna baadhi ya wanaopinga ila hawaleti mwandishi
 
Kwa biblia hakuna kuzidiana kiimani ila ntakuzidi kimaarifa tu na kuelewa mistari zaidi..... Mfano hiyo Yuda 6 kwa wewe utaona ni vague ila kwangu ntaunganisha dots na Book of Enoch maana imeongelewa kwa undani zaidi.

Ngoja nikupe na huu mstari

Mwanzo 4
23 Lameki akawaambia wake zake,Sikieni sauti yangu, Ada na Sila;Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu;Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha;Kijana kwa kunichubua;
24 Kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba,Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba

Hapa umeelewa nini?
Hahaaaa ety maarifa.
Haya bhana mimi nimekubari mkuu utakua unajua vingi kuliko mimi.

Niseme kitu.

Mimi sio mkatoliki wala sijui msabato.
Mimi najiita mkristo safi kabisa.

Naomba unipe tofauti ilioko kwawa orthodox na wakristo wa leo.
Tofauti yao iko wapi ?
Ukinipa tofauti nitaelewa kama wewe ni mnafiki kama mafarisayo au nawe pia ni mkristo safi.
 
Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakini ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu nyingi.

Henoko anayedhaniwa kuwa alikuwa ndio mwandishi wa kitabu hiki ni Yule mtoto wa Yaredi na baba wa Metuselah, ambaye akaja kuwa babu wa Nuhu MWANZO 5:21-23, Ni Moja ya Mtu anayetajwa kuwa na Mwisho wa Ajabu kwani hakufa, bali alitwaliwa mbinguni YOSHUA BIN SIRA 44:16, WAEBRANIA 11:5. Maswala Kama haya hupaswi kujadili na Wale wenye Canon Ya Vitabu 66 kwani watakwambia vitabu hivi havifai "Wanaviita Apokrifa" Wasijue Hata Baadhi ya Sura za Kitabu cha Zaburi ni Apokrifa na katika Biblia yao zimo.

TUANZE....
Hiki kitabu cha Henoko Hukataliwa na Kanisa Katoliki la Magharibi (Latin Church) kwa Sababu zake za Msingi Moja ya Sababu ni Kitabu Kukosa Jina la Mwandishi hakika, Lakini kanisa Katoliki la Mashari la Ethiopia (Orthodox) katika Orodha yao wanakitumia kama Kitabu cha Muhimu sana. Ni kama Wayahudi wanavyokitumia kitabu kinachoitwa YASHARI au JASHAR kinachotajwa 2SAMWELI 1:18, Vitabu hivi vina mambo fulani ya kipekee ambayo wataalamu husema ni siri..... (Ngoja Tuendelee)

BASI......
Kitabu Cha Henoko Hutajwa kwa hypingwa Vikali kwa sababu Ndio huonyesha Mtu mweupe alipata wapi Ujuzi, Pia huonyesha Chanzo cha Mapepo na Wanefili.

Ukisoma Kitabu cha HENOKO 6:1-8 ni sawa na Ukisoma MWANZO 6:1-8 lakini kuna utofauti wa Stori za malaika zaidi, Inaonekana katika zama za YAREDI babaye na HENOKO kuna malaika kama 200 walikubaliana kushuka duniani na Kujichanganya na wanadamu, hapo ndipo ambapo YUDA alinakili maelezo ya YUDA 1:6 Malaika walipoona kuna mabinti wa wanadamu wanavutia/Wazuri MWANZO 6:2 Ndipo wakashauriana "Mwaonaje Tujitwalie tuwaoe, tuzae nao watoto?" Malaika Kiongozi aliyeitwa SAMYAZA akahofia Labda malaika wenzie wanaweza Kumsaliti katika mpango huu, Akahimiza malaika kuapa, Wakaapa kutekeleza. (Henoko 7:3-6)

Kitabu Cha Henoko kinawataja kabisa kwa Majina Viongozi wa Malaika hao waliokuwa katika Mlima HERMON kwamba ni SEMIAZAZ, ARAKIBA, RAMEEL, KOKABIEL, TAMIEL, RAMIEL, DANEL, EZEQEEL, BARAQIJAL, ASAEL, ARMAROS, BATAREL, ANANEL, ZAQIEL, SAMSAPEEL, SATAREL, TUREL, JOMJAEL, SARIEL.

Ikumbukwe hawa hawakuwa malaika Watiifu kwa Mungu, Ni wazi kuwa walikuwa sehemu Katika wale Walioasi pamoja na shetani, Katika MWANZO 6:2-4 Imewataja kama "WANA WA MUNGU" hili jina lisikuchanganye maana malaika wote huitwa wana wa Mungu ndio maana hata Biblia ya asili ya Kiyunani imewaita malaika "ANGELUS ES DEUS" ikimaanisha malaika wa Mungu No matter Watiifu au Sivyo, Sasa mstari wa 4 katika MWANZO 6 unasema "Basi walikuwepo Wanefili duniani(NEPHILIM THE FALLEN ANGELS) hapo jiulize kwa nini aseme "DUNIANI" ni kwasababu hapakuwa mahali pao pa asili (2Petro 2:4,YUDA 1:6) Ni lazima waliyaacha makao yao...

Tuendelee...
Kitabu cha HENOKO 7:1-6 tunaona haya yafuatayo, Malaika wale 200 Wakiongoza na SEMJAZA baada ya Kiapo, wanaoa mabinti wanadamu Na Kuwapa Mimba, Hawakuishia hapo, Katika Sura ya 7 Mstari wa 10 tunaona Malaika hawa waliwafundisha binadamu Uchawi "sorcery" Wakafundisha Orodha ya Maneno ya Kufufua wafu "incantations" Wakawafundisha Jinsi ya Kutengeneza Dawa za Kuwatibu kutumia Mitishamba (pharmacology).

Ilipofika kipindi cha wale mabinti kuzaa Katika sura ya 7:11-14 tunaambiwa Walizaliwa Viumbe wakubwa kupita hata Binadamu na Malaika (Giants), Walizaliwa wengi Mpaka Binadamu walichoka Kuwahudumia chakula, Wakaanza kula Wanyama, Ndege na Samaki, Baadae wakaanza kuwala Binadamu, na Mwisho wakalana wao kwa Wao.

Basi katika Sura ya 8 tunaona Malaika AZAZEL anawaonea huruma Binadamu, Anaanza kuwafundisha Kutengeneza Silaha, Mapanga (Swords) , Visu, Ngao na Ngao za Vifuani (BREASTPLATED) hapa ndipo zana za chuma zilipogunduliwa (MWANZO 4:22) TUBALI-KAINI akiwa wa kwanza kuchukua Ujuzi.

BASI..... Kupitia Malaika Azazel ndipo Binadamu alipojua Kupigana Vita, Malaika hawakuishia hapo, Malaika hawa ndio Walifundisha Dada zetu kuvaa Vikuku na Bangili (BRACELETS) Pia wakafundisha dada zetu kupaka Rangi Kope (BEAUTIFYING OF EYELIDS) na hapa ndipo Dhambi ya Kuzini kwa matamanio ilianza

Malaika waliendelea Kutoa siri nyingi na Kumpa Binadamu uwezo Ulioshindikana, Kila malaika alikuwa na Kitengo chake.

Malaika aliyeitwa SEMJAZA huyu aliwafundisha Binadamu kumiliki Nguvu za Maajabu kufanya Mambo makubwa, Pia Kutumia Mizizi ya Miti kama Tiba, Kemia Kiujumla. Malaika ARMAROS alifundisha jinsi ya Kutatua Tatizo litokanalo na Uchawi wa mtu mwingine. Malaika BARAQIEL huyu aliwafundisha binadamu elimu ya vitu vya Angani "ASTROLOGY" Malaika kwa jina la KOKABEL akawafundisha binadamu elimu ya Anga ihusuyo mipaka ya Nyota na maumbo yake "CONSTELLATION" Malaika EZEQEEL akawafundisha Binadamu Juu ya Mawingu. Malaika ARAQIEL akawafundisha Alama za Kidunia (zodiac elemental rulerships) ambazo tunaziita Libra, Virgo, Capricon nakadhalika. Malaika SHAMSIEL akafundisha alama za Jua Na Malaika SARIEL akawapa Kozi za Elimu ya Mwezini.

Kwahiyo Ujuzi wa Binadamu na Mambo machafu yalianzia Juu ya Hawa malaika Bila Ujio wao Binadamu Angekuwa "Kilaza Mmoja hivi" Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na malaika duniani, Hata Mungu aliona wameipa Mbingu aibu, na Alishindwa Kuwasamehe na aliwafunga vifungo vya milele chini ya Giza wakingojea hukumu.

CATHOLIC THEOLOGICAL REFLECTION.

Wanateolojia Wakanisa Husema wazi kuwa inawezekana huu ulikuwa ni mpango wa Shetani kuharibu Mpango wa Mungu wa MWANZO 3:15 kwa Sababu Mungu alisema Mkombozi wa Wanadamu atakuwa binadamu Pure na si Malaika na Atazaliwa Pasipo Dhambi, Na Atazaliwa na Mwanamke, Basi Shetani alipanga kuharibu Vinasaba (Gene) za Binadamu kwa kuzichanganya na za Malaika Basi basi Kuzaliwa Kwa Mkombozi kungeshindikana.

Lakini Mungu anajua Zaidi (AN OMNISCIENT) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na Kubakiza Wanadamu 8 tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kilifichwa, wewe umekitoa wapi?
Au ndo wafichaji?
 
Back
Top Bottom