Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch

Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakini ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu nyingi.

Henoko anayedhaniwa kuwa alikuwa ndio mwandishi wa kitabu hiki ni Yule mtoto wa Yaredi na baba wa Metuselah, ambaye akaja kuwa babu wa Nuhu MWANZO 5:21-23, Ni Moja ya Mtu anayetajwa kuwa na Mwisho wa Ajabu kwani hakufa, bali alitwaliwa mbinguni YOSHUA BIN SIRA 44:16, WAEBRANIA 11:5. Maswala Kama haya hupaswi kujadili na Wale wenye Canon Ya Vitabu 66 kwani watakwambia vitabu hivi havifai "Wanaviita Apokrifa" Wasijue Hata Baadhi ya Sura za Kitabu cha Zaburi ni Apokrifa na katika Biblia yao zimo.

TUANZE....
Hiki kitabu cha Henoko Hukataliwa na Kanisa Katoliki la Magharibi (Latin Church) kwa Sababu zake za Msingi Moja ya Sababu ni Kitabu Kukosa Jina la Mwandishi hakika, Lakini kanisa Katoliki la Mashari la Ethiopia (Orthodox) katika Orodha yao wanakitumia kama Kitabu cha Muhimu sana. Ni kama Wayahudi wanavyokitumia kitabu kinachoitwa YASHARI au JASHAR kinachotajwa 2SAMWELI 1:18, Vitabu hivi vina mambo fulani ya kipekee ambayo wataalamu husema ni siri..... (Ngoja Tuendelee)

BASI......
Kitabu Cha Henoko Hutajwa kwa hypingwa Vikali kwa sababu Ndio huonyesha Mtu mweupe alipata wapi Ujuzi, Pia huonyesha Chanzo cha Mapepo na Wanefili.

Ukisoma Kitabu cha HENOKO 6:1-8 ni sawa na Ukisoma MWANZO 6:1-8 lakini kuna utofauti wa Stori za malaika zaidi, Inaonekana katika zama za YAREDI babaye na HENOKO kuna malaika kama 200 walikubaliana kushuka duniani na Kujichanganya na wanadamu, hapo ndipo ambapo YUDA alinakili maelezo ya YUDA 1:6 Malaika walipoona kuna mabinti wa wanadamu wanavutia/Wazuri MWANZO 6:2 Ndipo wakashauriana "Mwaonaje Tujitwalie tuwaoe, tuzae nao watoto?" Malaika Kiongozi aliyeitwa SAMYAZA akahofia Labda malaika wenzie wanaweza Kumsaliti katika mpango huu, Akahimiza malaika kuapa, Wakaapa kutekeleza. (Henoko 7:3-6)

Kitabu Cha Henoko kinawataja kabisa kwa Majina Viongozi wa Malaika hao waliokuwa katika Mlima HERMON kwamba ni SEMIAZAZ, ARAKIBA, RAMEEL, KOKABIEL, TAMIEL, RAMIEL, DANEL, EZEQEEL, BARAQIJAL, ASAEL, ARMAROS, BATAREL, ANANEL, ZAQIEL, SAMSAPEEL, SATAREL, TUREL, JOMJAEL, SARIEL.

Ikumbukwe hawa hawakuwa malaika Watiifu kwa Mungu, Ni wazi kuwa walikuwa sehemu Katika wale Walioasi pamoja na shetani, Katika MWANZO 6:2-4 Imewataja kama "WANA WA MUNGU" hili jina lisikuchanganye maana malaika wote huitwa wana wa Mungu ndio maana hata Biblia ya asili ya Kiyunani imewaita malaika "ANGELUS ES DEUS" ikimaanisha malaika wa Mungu No matter Watiifu au Sivyo, Sasa mstari wa 4 katika MWANZO 6 unasema "Basi walikuwepo Wanefili duniani(NEPHILIM THE FALLEN ANGELS) hapo jiulize kwa nini aseme "DUNIANI" ni kwasababu hapakuwa mahali pao pa asili (2Petro 2:4,YUDA 1:6) Ni lazima waliyaacha makao yao...

Tuendelee...
Kitabu cha HENOKO 7:1-6 tunaona haya yafuatayo, Malaika wale 200 Wakiongoza na SEMJAZA baada ya Kiapo, wanaoa mabinti wanadamu Na Kuwapa Mimba, Hawakuishia hapo, Katika Sura ya 7 Mstari wa 10 tunaona Malaika hawa waliwafundisha binadamu Uchawi "sorcery" Wakafundisha Orodha ya Maneno ya Kufufua wafu "incantations" Wakawafundisha Jinsi ya Kutengeneza Dawa za Kuwatibu kutumia Mitishamba (pharmacology).

Ilipofika kipindi cha wale mabinti kuzaa Katika sura ya 7:11-14 tunaambiwa Walizaliwa Viumbe wakubwa kupita hata Binadamu na Malaika (Giants), Walizaliwa wengi Mpaka Binadamu walichoka Kuwahudumia chakula, Wakaanza kula Wanyama, Ndege na Samaki, Baadae wakaanza kuwala Binadamu, na Mwisho wakalana wao kwa Wao.

Basi katika Sura ya 8 tunaona Malaika AZAZEL anawaonea huruma Binadamu, Anaanza kuwafundisha Kutengeneza Silaha, Mapanga (Swords) , Visu, Ngao na Ngao za Vifuani (BREASTPLATED) hapa ndipo zana za chuma zilipogunduliwa (MWANZO 4:22) TUBALI-KAINI akiwa wa kwanza kuchukua Ujuzi.

BASI..... Kupitia Malaika Azazel ndipo Binadamu alipojua Kupigana Vita, Malaika hawakuishia hapo, Malaika hawa ndio Walifundisha Dada zetu kuvaa Vikuku na Bangili (BRACELETS) Pia wakafundisha dada zetu kupaka Rangi Kope (BEAUTIFYING OF EYELIDS) na hapa ndipo Dhambi ya Kuzini kwa matamanio ilianza

Malaika waliendelea Kutoa siri nyingi na Kumpa Binadamu uwezo Ulioshindikana, Kila malaika alikuwa na Kitengo chake.

Malaika aliyeitwa SEMJAZA huyu aliwafundisha Binadamu kumiliki Nguvu za Maajabu kufanya Mambo makubwa, Pia Kutumia Mizizi ya Miti kama Tiba, Kemia Kiujumla. Malaika ARMAROS alifundisha jinsi ya Kutatua Tatizo litokanalo na Uchawi wa mtu mwingine. Malaika BARAQIEL huyu aliwafundisha binadamu elimu ya vitu vya Angani "ASTROLOGY" Malaika kwa jina la KOKABEL akawafundisha binadamu elimu ya Anga ihusuyo mipaka ya Nyota na maumbo yake "CONSTELLATION" Malaika EZEQEEL akawafundisha Binadamu Juu ya Mawingu. Malaika ARAQIEL akawafundisha Alama za Kidunia (zodiac elemental rulerships) ambazo tunaziita Libra, Virgo, Capricon nakadhalika. Malaika SHAMSIEL akafundisha alama za Jua Na Malaika SARIEL akawapa Kozi za Elimu ya Mwezini.

Kwahiyo Ujuzi wa Binadamu na Mambo machafu yalianzia Juu ya Hawa malaika Bila Ujio wao Binadamu Angekuwa "Kilaza Mmoja hivi" Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na malaika duniani, Hata Mungu aliona wameipa Mbingu aibu, na Alishindwa Kuwasamehe na aliwafunga vifungo vya milele chini ya Giza wakingojea hukumu.

CATHOLIC THEOLOGICAL REFLECTION.

Wanateolojia Wakanisa Husema wazi kuwa inawezekana huu ulikuwa ni mpango wa Shetani kuharibu Mpango wa Mungu wa MWANZO 3:15 kwa Sababu Mungu alisema Mkombozi wa Wanadamu atakuwa binadamu Pure na si Malaika na Atazaliwa Pasipo Dhambi, Na Atazaliwa na Mwanamke, Basi Shetani alipanga kuharibu Vinasaba (Gene) za Binadamu kwa kuzichanganya na za Malaika Basi basi Kuzaliwa Kwa Mkombozi kungeshindikana.

Lakini Mungu anajua Zaidi (AN OMNISCIENT) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na Kubakiza Wanadamu 8 tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa sijaelewa mtu mweupe alipata ujuz viip
 
Mam
Mimi naujua umuhimu wa agano la kale na muhubiri anatakiwa kulitumia vipi agano la kale kufundisha neno la Mungu,
Agano jipya pia.

Sasa kama kuna kitu cha muhimu mwanadamu kukijua na hakipo ndani ya biblia kiseme.

Kwasababu biblia inasema laiti kama biblia ingeandika kila alilolifanya Yesu kipindi chake isinge wezekana ?
Yohana 21:25
[25]Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
sio kweli! Mambo gani aliyofanya yesu na hayaandikwa? Mbona Yesu kaandkwa na wahubiri wanne (matayo, marco, luka na yohana) lakin wote wanaeleza yale yale tu.. apo si ndo kila mmoja angeandika ambayo mwenzie hajaandika.

kama wameandika hadi alivokwenda kwa zakayo sasa wameacha jambo gan la muhimu?
 
Mam

sio kweli! Mambo gani aliyofanya yesu na hayaandikwa? Mbona Yesu kaandkwa na wahubiri wanne (matayo, marco, luka na yohana) lakin wote wanaeleza yale yale tu.. apo si ndo kila mmoja angeandika ambayo mwenzie hajaandika... kama wameandika hadi alivokwenda kwa zakayo sasa wameacha jambo gan la muhimu?
Bishana na maandiko sasa.

Yohana 21:25
[25]Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
 
Sawa Sawa

Musa mwandishi wa vitabu vitano maarufu vya kwenye Biblia, inasemwa aliandika jumla vitabu Tisa. Vitabu vinne havimo kwenye Bible.

Swali lako mujarabu, iweje kulazimisha maandishi yaliyotupwa yaingizwe kwenye Bible? Anyway, hili ni la kuendelea kujifunza
Hivyo vitabu 4 vinapatikana wapi?
 
Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakini ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu nyingi.

Henoko anayedhaniwa kuwa alikuwa ndio mwandishi wa kitabu hiki ni Yule mtoto wa Yaredi na baba wa Metuselah, ambaye akaja kuwa babu wa Nuhu MWANZO 5:21-23, Ni Moja ya Mtu anayetajwa kuwa na Mwisho wa Ajabu kwani hakufa, bali alitwaliwa mbinguni YOSHUA BIN SIRA 44:16, WAEBRANIA 11:5. Maswala Kama haya hupaswi kujadili na Wale wenye Canon Ya Vitabu 66 kwani watakwambia vitabu hivi havifai "Wanaviita Apokrifa" Wasijue Hata Baadhi ya Sura za Kitabu cha Zaburi ni Apokrifa na katika Biblia yao zimo.

TUANZE....
Hiki kitabu cha Henoko Hukataliwa na Kanisa Katoliki la Magharibi (Latin Church) kwa Sababu zake za Msingi Moja ya Sababu ni Kitabu Kukosa Jina la Mwandishi hakika, Lakini kanisa Katoliki la Mashari la Ethiopia (Orthodox) katika Orodha yao wanakitumia kama Kitabu cha Muhimu sana. Ni kama Wayahudi wanavyokitumia kitabu kinachoitwa YASHARI au JASHAR kinachotajwa 2SAMWELI 1:18, Vitabu hivi vina mambo fulani ya kipekee ambayo wataalamu husema ni siri..... (Ngoja Tuendelee)

BASI......
Kitabu Cha Henoko Hutajwa kwa hypingwa Vikali kwa sababu Ndio huonyesha Mtu mweupe alipata wapi Ujuzi, Pia huonyesha Chanzo cha Mapepo na Wanefili.

Ukisoma Kitabu cha HENOKO 6:1-8 ni sawa na Ukisoma MWANZO 6:1-8 lakini kuna utofauti wa Stori za malaika zaidi, Inaonekana katika zama za YAREDI babaye na HENOKO kuna malaika kama 200 walikubaliana kushuka duniani na Kujichanganya na wanadamu, hapo ndipo ambapo YUDA alinakili maelezo ya YUDA 1:6 Malaika walipoona kuna mabinti wa wanadamu wanavutia/Wazuri MWANZO 6:2 Ndipo wakashauriana "Mwaonaje Tujitwalie tuwaoe, tuzae nao watoto?" Malaika Kiongozi aliyeitwa SAMYAZA akahofia Labda malaika wenzie wanaweza Kumsaliti katika mpango huu, Akahimiza malaika kuapa, Wakaapa kutekeleza. (Henoko 7:3-6)

Kitabu Cha Henoko kinawataja kabisa kwa Majina Viongozi wa Malaika hao waliokuwa katika Mlima HERMON kwamba ni SEMIAZAZ, ARAKIBA, RAMEEL, KOKABIEL, TAMIEL, RAMIEL, DANEL, EZEQEEL, BARAQIJAL, ASAEL, ARMAROS, BATAREL, ANANEL, ZAQIEL, SAMSAPEEL, SATAREL, TUREL, JOMJAEL, SARIEL.

Ikumbukwe hawa hawakuwa malaika Watiifu kwa Mungu, Ni wazi kuwa walikuwa sehemu Katika wale Walioasi pamoja na shetani, Katika MWANZO 6:2-4 Imewataja kama "WANA WA MUNGU" hili jina lisikuchanganye maana malaika wote huitwa wana wa Mungu ndio maana hata Biblia ya asili ya Kiyunani imewaita malaika "ANGELUS ES DEUS" ikimaanisha malaika wa Mungu No matter Watiifu au Sivyo, Sasa mstari wa 4 katika MWANZO 6 unasema "Basi walikuwepo Wanefili duniani(NEPHILIM THE FALLEN ANGELS) hapo jiulize kwa nini aseme "DUNIANI" ni kwasababu hapakuwa mahali pao pa asili (2Petro 2:4,YUDA 1:6) Ni lazima waliyaacha makao yao...

Tuendelee...
Kitabu cha HENOKO 7:1-6 tunaona haya yafuatayo, Malaika wale 200 Wakiongoza na SEMJAZA baada ya Kiapo, wanaoa mabinti wanadamu Na Kuwapa Mimba, Hawakuishia hapo, Katika Sura ya 7 Mstari wa 10 tunaona Malaika hawa waliwafundisha binadamu Uchawi "sorcery" Wakafundisha Orodha ya Maneno ya Kufufua wafu "incantations" Wakawafundisha Jinsi ya Kutengeneza Dawa za Kuwatibu kutumia Mitishamba (pharmacology).

Ilipofika kipindi cha wale mabinti kuzaa Katika sura ya 7:11-14 tunaambiwa Walizaliwa Viumbe wakubwa kupita hata Binadamu na Malaika (Giants), Walizaliwa wengi Mpaka Binadamu walichoka Kuwahudumia chakula, Wakaanza kula Wanyama, Ndege na Samaki, Baadae wakaanza kuwala Binadamu, na Mwisho wakalana wao kwa Wao.

Basi katika Sura ya 8 tunaona Malaika AZAZEL anawaonea huruma Binadamu, Anaanza kuwafundisha Kutengeneza Silaha, Mapanga (Swords) , Visu, Ngao na Ngao za Vifuani (BREASTPLATED) hapa ndipo zana za chuma zilipogunduliwa (MWANZO 4:22) TUBALI-KAINI akiwa wa kwanza kuchukua Ujuzi.

BASI..... Kupitia Malaika Azazel ndipo Binadamu alipojua Kupigana Vita, Malaika hawakuishia hapo, Malaika hawa ndio Walifundisha Dada zetu kuvaa Vikuku na Bangili (BRACELETS) Pia wakafundisha dada zetu kupaka Rangi Kope (BEAUTIFYING OF EYELIDS) na hapa ndipo Dhambi ya Kuzini kwa matamanio ilianza

Malaika waliendelea Kutoa siri nyingi na Kumpa Binadamu uwezo Ulioshindikana, Kila malaika alikuwa na Kitengo chake.

Malaika aliyeitwa SEMJAZA huyu aliwafundisha Binadamu kumiliki Nguvu za Maajabu kufanya Mambo makubwa, Pia Kutumia Mizizi ya Miti kama Tiba, Kemia Kiujumla. Malaika ARMAROS alifundisha jinsi ya Kutatua Tatizo litokanalo na Uchawi wa mtu mwingine. Malaika BARAQIEL huyu aliwafundisha binadamu elimu ya vitu vya Angani "ASTROLOGY" Malaika kwa jina la KOKABEL akawafundisha binadamu elimu ya Anga ihusuyo mipaka ya Nyota na maumbo yake "CONSTELLATION" Malaika EZEQEEL akawafundisha Binadamu Juu ya Mawingu. Malaika ARAQIEL akawafundisha Alama za Kidunia (zodiac elemental rulerships) ambazo tunaziita Libra, Virgo, Capricon nakadhalika. Malaika SHAMSIEL akafundisha alama za Jua Na Malaika SARIEL akawapa Kozi za Elimu ya Mwezini.

Kwahiyo Ujuzi wa Binadamu na Mambo machafu yalianzia Juu ya Hawa malaika Bila Ujio wao Binadamu Angekuwa "Kilaza Mmoja hivi" Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na malaika duniani, Hata Mungu aliona wameipa Mbingu aibu, na Alishindwa Kuwasamehe na aliwafunga vifungo vya milele chini ya Giza wakingojea hukumu.

CATHOLIC THEOLOGICAL REFLECTION.

Wanateolojia Wakanisa Husema wazi kuwa inawezekana huu ulikuwa ni mpango wa Shetani kuharibu Mpango wa Mungu wa MWANZO 3:15 kwa Sababu Mungu alisema Mkombozi wa Wanadamu atakuwa binadamu Pure na si Malaika na Atazaliwa Pasipo Dhambi, Na Atazaliwa na Mwanamke, Basi Shetani alipanga kuharibu Vinasaba (Gene) za Binadamu kwa kuzichanganya na za Malaika Basi basi Kuzaliwa Kwa Mkombozi kungeshindikana.

Lakini Mungu anajua Zaidi (AN OMNISCIENT) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na Kubakiza Wanadamu 8 tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hicho kitabu enoki aliagizwa aandike na kuhifadhi kwa vizazi vijavyo,kizazi kilicholengwa ni hichi cha sasa ambacho kila kitu kitajulikana.

Na alivihifadhi ndani ya pyramid of giza, wana theologia walivikuta huko, ndio pyramid kubwa ambayo enoki aliijenga yeye mwenyewe sio wamisri.
 
Habari mkuu. Naomba unipe siri 3 tu ambazo hazijulikani ulizozisoma humo kitabuni.
1. Mwanadamu kuzaa na Malaika

2. Kifo cha Cain na jinsi laana ya kisasi ilipoishia.

3. Evolution na milestones za melchizedek ambaye kwenye Biblia ya kawaida ni mysterious figure.

4. Nuhu kama mtu mweupe wa kwanza kwenye kizazi cha Adam. Ikabidi wamuite Methuselah kushangaa binadamu mweupe (Blonde)

And such interesting topics kma uwepo wa 7 heavens.

Kuzimu ya Euphrates walipofungwa malaika wachafu..... Uwepo wa fallen angels kama zamzammim na azazel na role yao kwenye maisha ya binadamu. Silaha,uchawi, usomaji wa nyota ma vitu vingi vilianza Kipindi hiki
 
"Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na malaika duniani" kwahiyo unataka kusema bila malaika kumwambia Mungu asingejua matendo ya hao malaika?

"Lakini Mungu anajua Zaidi (AN OMNISCIENT) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na Kubakiza Wanadamu 8 tu"

Kupitia hizo paragraph 2 inaonekana kama kuna ukomo wa kuona au kujua mambo Kwa Mungu, kama anajua zaidi hadi akafuta kizazi cha Nuhu nazani lengo lilikuwa ni kuondoa kizazi kiovu cha Nuhu na kuleta kizazi kizuri Ila cha ajabu hiki kizazi ndio kibaya kuliko ata cha Nuhu hivo sidhani kama alijua na hiki kizazi kitakuwa hivi

Kuendelea kumuacha shetani uraiani ili binadamu apambane nae mwenyewe ni Sawa na kujitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe, kama Baba huwezi kuwatakia mema watoto wako Kwa kuwaweka chumba kimoja na Nyoka, kuendelea kutuweka zizi moja na shetani na kutegemea tutakuwa tofauti na kina Nuhu inabidi uwe na akili za Wanyonge kuamini hili, Kamata shetani funga huko dunia iwe sehemu salama easy tu
Labda nikumegee kidogo namna hao malaika walivyowakilisha ujumbe wao kwa Mwenyezi Mungu.

Katika sura ya 9 ya Kitabu cha Enoch hicho kipande unachozungumzia kinasema hivi.."Na Michael, Uriel, Rafael, Gabriel wakatazama chini na kuona damu inavyomwagika na uovu wote unaoendelea duniani..wakaambizana wakisema dunia iliumbwa bila vilio,mbona tunasikia sauti za wanadamu zikitulilia na kuomba tufikishe vilio vyao kwake Mwenyezi Mungu?...wakamwendea Mwenyezi Mungu na kumwambia eeh Mungu mwenye haki,uliyeumba yote,Mwenye enzi yote..hakuna kinachojificha mbele yako..umeyaona yote aliyoyafanya Azazel...lakini upo kimya..hujatuambia la kufanya..."

Katika Kitabu cha Matayo Bwana Yesu Kristo alikuwa akiwaombea mitume na wote watakaoamini kile wanachohubiri mitume hao hapa duniani.Kuna mstari Yesu anasema.."siombi uwatoe duniani bali uwalinde dhidi ya yule mwovu.."

Kitabu cha Luka 17 Bwana Yesu anasema "makwazo hayana budi kuja lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa ajili yake".😀

2 wathesalonike 2;3-6 ikizungumzia kuhusu siku ya hukumu ya mwisho(kiama) inasema "mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote;maana haiji,usipokuja kwanza ule ukengeufu,akafunuliwa yule mtu wa kuasi,mwana wa uharibifu,yule mpingamizi ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa, hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndio Mungu...na sasa limzuialo mwalijua,apate kufunuliwa kwa wakati wake".

Ukisoma hiyo verse juu utapata kitu,kwamba kuna sababu Mungu kuacha uasi uendelee.Haimdisqualify yeye kama Mungu ila itamthibitisha zaidi kuwa Mungu mkuu muweza wa yote.Pia itawathibitisha wote katika viumbe wake walio watiifu kwake.

Kulielewa hili vizuri unahitaji kujifunza zaidi juu ya uhusiano wa free will,choice and judgement.

Ukielewa juu ya hayo matatu na context yake katika ulimwengu wa roho na mahusiano ya Mungu na viumbe wake,then utaelewa kwanini Mungu akijua kabisa shetani ataasi ila bado alimuumba, hakumzuia kuasi, kamwacha hata sasa na yote yanayoendelea yuko kimya mpaka WAKATI FULANI UKIFIKA.

Ikumbukwe WAKATI huo ni wetu sisi viumbe,sio wake,maana yeye hana wakati,yuko nje ya jedwali,hafungwi na time limit,kwake wakati wote ni mmoja,so ameyaona,anayajua yote,ameshayathibitisha na yako perfect😊..what about you?

ushathibitisha hiyo perfection?ushathibitisha God is love?ushathibitisha you are right or wrong..saint or..?umefika mwisho ukajumlisha hesabu yote?!No..you need TIME..lakini mwenyewe mwenye mali zake katika kitabu cha Luka 12;6,7 anasema anajua idadi hadi ya wale njiwa na shomoro wote uliowapiga manati ukaua enzi zile na nywele zako zote ulizonyoa tangu uzaliwe..😂😂Pole kaka!
 
Pia Mungu anaweza taka wewe ukakisome hicho kitabu.
Ndio sikatai
Lakini usiseme biblia inamapungufu.
Ilivyo ndivyo Mungu ametaka biblia iwe.
Mtalitafuta neno lakini hamtalipata

Hii biblia tunayotumia sasa ni tofauti na zile biblia za zamani walizotumia babu zetu et wanadai wanaziboresha

Yaani unaboresha neno la mungu???

Shetani Katia mizizi kwenye kila jambo la mungu nyie endeleeni kumtetea
 
Screenshot_20210718-150228_Gallery.jpg
 
Wanadamu wa kwanza hawakuwa weupe(wazungu) kama wengi tunavyo amin bali nuhu ndio.alikiwa mtu mweupe (mzungu) wakwanza duniani
Chapter 105 ndio inaelezea hvyo.
Hiyo chapter aloandika Nani?
 
Back
Top Bottom