Sensa ya 2002 hakuna mtu au kikundi kilichogomea sensa lakini hadi leo hii hatujui hizo takwimu ziliiisaidiaje serikali kupanga maendeleo ya nchi - maana , mfano mdogo, leo hii katika kipindi cha sensa ya 2012 baadhi ya watoto wa shule za msingi mijini na vijijini bado wanasomea skafuni kama sio chini ya miti au katika vibanda vya makuti (picha zimekuwa kibandikwa humu humu JF). Sasa kama serikali haikuweza kutumia takwimu za sensa ya 2002 angaa kuboresha mazingira ya kuwapatia watoto wadogo elimu, SIONI FAIDA YO YOTE YA SENSA. Hayo madai kuwa takwimu zinaisaidia serikali kupanga na kuleta maendeleo ni political slogans tu kama zilivyo za 'maisha bora kwa kila mtanzania', 'kilimo kwanza', 'malaria haikubaliki', nk. Ninawapongeza wote waliogomea sensa.