Sababu za kufeli kwa zoezi sensa

Johnsecond

JF-Expert Member
May 4, 2010
1,076
211
1. Mgomo wa walimu, wametumia walimu waliogoma na wameenda kupata pesa tu na sio sensa
2. Serikali kandamizi, ingeweza kuongea na waislamu wakakubaliana. mabavu sio suluhu
3. Mgawanyiko wa wanajamii, raia wengi hawaiamini serikali
4. Ahadi nyingi walizoahidiwa hazijatekelezwa iweje leo uwaambie sensa itawasaidia

wadau zoezi limefeli ongezeeni sababu hapo chini za kufeli kwa hili zoezi.
 
Udini uliochochewa na unaoendelea kuchochewa na baadhi ya Wanasiasa kwa faida yao wenyewe..Hili CCM hatutalikwepa maana tumekuwa tukifikiria ni mtaji kumbe ni janga la taifa kipindi kifupi kijacho!!!
 
Hizi ni hisia zako tu; maana bila kufanya utafiti huna haki ya kuzungumza! Je wewe umetumia vigezo gani kutufanya tuamini sensa imefeli?!
Ni kweli kumekuwa na mapungufu ya hapa na pale na wameweka margin of error kwa sababu kazi hii inafanywa na binadamu sio malaika! lakini sidhani kama mapungufu hayo na changamoto zake zinakidhi kutoa "hukumu ya kifo" kufeili jumla!
 
Jamani mie kulingana na kazi yangu natoka asubuhi na kurudi jioni na naishi pekeyangu so alipokuja karani wa sensa akanikosa. Wakaacha maswali matatu tu kwa jirani;
1. Jina kamili
2. Tarehe ya kuzaliwa
3. Kiwango cha elimu
Hii imekaa vizuri kweli, kwani kulingana na mkurugenzi wa Takwimu alisema kuna aina mbili ya dodoso;
1. Fupi, yenye maswali 32 na
2. Dodoso ya pili ina maswali zaidi ya 60
 
Nimetumia vyombo vya habari redio, tv, magazeti. hata hivi tunavyoongea kuna watu wengi sana wameshikwa na polisi kwa kukataa kuhesabiwa. Walimu waligoma kwa kusema hawajapewa vitambulisho na sare. wewe uko tz?
 
Hizi ni hisia zako tu; maana bila kufanya utafiti huna haki ya kuzungumza! Je wewe umetumia vigezo gani kutufanya tuamini sensa imefeli?!
Ni kweli kumekuwa na mapungufu ya hapa na pale na wameweka margin of error kwa sababu kazi hii inafanywa na binadamu sio malaika! lakini sidhani kama mapungufu hayo na changamoto zake zinakidhi kutoa "hukumu ya kifo" kufeili jumla!

hapo hakuna mapungufu ya kawaida ya kibinadamu, na ingekuwa hivyo watu wasingefungiwa polisi. Watu kujifungia misikitini unasema mapungufu ya kawaida?? Kuna wengine amjui kufanya kazi zenu zikafanikiwa kwa kiwango kinachotakikana na ndio maana mnakimbilia kwenye mapungufu ya kibinadamu
 
ndo hao wakifumaniwa husema SHETAN ALINIPITIA
 
kwani lile la vitambulisho si lingetosha!!

wana interijensia wa serikali walifeli sana. kwani toka mwanzo tu walivyoona tayari kuna hoja, wangeweza kusitisha zoezi la sensa na kusema litafanyika mwakani wako wanafanya mabadiliko ya dodoso baada ya hapo wao wange komaa only na vitambulisho vya taifa na hapo wangehakikisha vitambulisho wanaandikishwa wote hata wa miezi. That could be simple and clear for them. sasa wao wakaendelea na pumbaziko kuwa watatumia vitisho.
VITISHO VILIWAFANYA HATA AMBAO HAWAKUWA NA MPANGO WA KUGOMEA ZOEZI KUGOMEA. wanasheria waseme ni sheria ipi inamfunga mtu aliyekataa kuhesabiwa bila kumpiga karani wala kumchania karatasi zake? wakuu wa wilaya na polis wanaiua CCM mchana kweupe.
 
watakuja kusema zoezi limefanikiwa kwa asilimia 95%. sababu ni moja tu, serikali haiungwi mkono wa wananchi
 
wana interijensia wa serikali walifeli sana. kwani toka mwanzo tu walivyoona tayari kuna hoja, wangeweza kusitisha zoezi la sensa na kusema litafanyika mwakani wako wanafanya mabadiliko ya dodoso baada ya hapo wao wange komaa only na vitambulisho vya taifa na hapo wangehakikisha vitambulisho wanaandikishwa wote hata wa miezi. That could be simple and clear for them. sasa wao wakaendelea na pumbaziko kuwa watatumia vitisho.
VITISHO VILIWAFANYA HATA AMBAO HAWAKUWA NA MPANGO WA KUGOMEA ZOEZI KUGOMEA. wanasheria waseme ni sheria ipi inamfunga mtu aliyekataa kuhesabiwa bila kumpiga karani wala kumchania karatasi zake? wakuu wa wilaya na polis wanaiua CCM mchana kweupe.

Kaka nimekugongea like, zoezi lilipaswa liahirishwe ili wamalize mvutano kwanza ni janga hili. Polisi wakasema wamejipanga nikajiuliza kwa lipi sasa??? Mpaka sasa hivi makarani wa sensa wawili wameuawa kwa kunyanganywa pesa na simu zao, sasa polisi walijipanga kwa lipi hapo??? ebu jiulizeni
 
Hizi ni hisia zako tu; maana bila kufanya utafiti huna haki ya kuzungumza! Je wewe umetumia vigezo gani kutufanya tuamini sensa imefeli?!
Ni kweli kumekuwa na mapungufu ya hapa na pale na wameweka margin of error kwa sababu kazi hii inafanywa na binadamu sio malaika! lakini sidhani kama mapungufu hayo na changamoto zake zinakidhi kutoa "hukumu ya kifo" kufeili jumla!

Unaongea hivyo kwa kuwa unashinda kwa kukodolea macho komputa, ungekua huku tulipo usingepoteza muda kwa kukanusha jambo hata wewe mwenyewe hujalifanyia utafiti.
 
Jamani mie kulingana na kazi yangu natoka asubuhi na kurudi jioni na naishi pekeyangu so alipokuja karani wa sensa akanikosa. Wakaacha maswali matatu tu kwa jirani;
1. Jina kamili
2. Tarehe ya kuzaliwa
3. Kiwango cha elimu
Hii imekaa vizuri kweli, kwani kulingana na mkurugenzi wa Takwimu alisema kuna aina mbili ya dodoso;
1. Fupi, yenye maswali 32 na
2. Dodoso ya pili ina maswali zaidi ya 60
.

mie pia nilishanga kuulizwa maswali hayo kidogo siku amini nikamuuliza jamaa hee imekuwaje mbona nilisikia na vitambulisho vya taifa akasema watarudi tena sasa sijui watakuja na camera au vipi

Limefeli? Ni Maoni yako binafsi ama umeamua kutumia Bundle na time yako vibaya...kweli niamini baadhi ya Watanzania ...mwalimu yeye,Dr. Yeye,Mchumi yeye,Engineer yeye,Mwanasiasa yeye.na Mpuuzi yeye

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Tuache ubishi.... LIMEFELI, LIMEFELI kuna vijiji na mitaa mpaka leo hatujahesabiwa i mean sio mtaa wa watu 100 ni watu wengi sana. leo nimejaribu kuwapigia watu wanaoishi jirani zaidi na office za mtaa nao hawaja hesabiwa.... JAMANI tuache kujidanganya zoezi LIMEFELI Hasa mkoa wa pwani
 
Kwa mimi ambaye bado sijahesabiwa, ninapata hisia za zoezi kufeli. Au ndio niendelee kusubiri kuwa siku bado hazijesha?
 
...Idadi ya Watanzania tutaambiwa iko 25 millioni wengi wamehama nchi na wengine wamekufa kwa magonjwa mbali mbali ikiwemo ukimwi, kifua kikuu, magonjwa ya moyo n.k...... watazipika namba tu kamwe hii Serikali DHAIFU haitakubali kwamba zoezi la kuhesabu Watanzania limeshindwa vibaya sana.
 
Back
Top Bottom