Sababu inayotufanya tuendelee kuwa wajinga

Sababu inayotufanya tuendelee kuwa wajinga

Deinstein 01

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2024
Posts
2,090
Reaction score
3,926
Habari wakuu!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, sababu yenyewe ni kutokubali kukosolewa. kukosolewa ni kuoneshwa makosa unayoyafanya yaani kuoneshwa mapungufu yako.

Watu wengi hawapendi kuoneshwa mapungufu yao ila ni rahisi sana wao kutambua mapungufu ya wengine lakini ya kwao hawayafahamu. Of course kukasirika baada ya kukosolewa ni jambo la kawaida sana na hutokea kwa kila mtu. Lakini watu wengi wanareact ndivyosivyo baada ya kukosolewa hata hapa JF nimeliona hili swala unakuta dini fulani imekosolewa waumini wa dini husika wanaanza kutukana badala ya kujadili. Na hii inatokea pale ambapo hisia zimeovercome akili.

Ni jambo la kawaida pia kujiamini na kuamini ya kuwa you are special and you can do it. Lakini hii kitu isikufanye ukajitenga na wanaokukosoa na ukajiambatanisha na machawa. Unapokosolewa unatakiwa uweke hisia especially ego pembeni na uruhusu akili ifanye kazi, kama umekasirika vuta pumzi ndefu halafu itoe hii itasaidia kupunguza hasira ila kama umeshindwa kujicontroll ondoka eneo la tukio halafu ukalifikirie vizuri kuhusu pungufu ulilooneshwa.

Pia na wewe unapomkosoa mwenzako hakikisha haumkosoi mbele za watu au huku ukimfokea, hii itaumiza hisia zake. Chamuhimu ni kutambua ya kuwa hakuna aliyekamilika hivyo kosoa kwa nia ya kufundisha na si kwa kukejeli.

Kwa kuhitimisha, siku zote ujinga ni adui wa maendeleo hivyo ukiendekeza machawa badala ya wakosoaji utaona kibunda chako kinaisha na maendeleo hakuna. Wote tunajua kiburi cha CCM kilipoifikisha nchi. Hata malegend kama CR7 na Lapulga bado wanahitaji macoach (wakosoaji) ili kuendeleza vipaji vyao. Wasingefika hapo bila macoach waliowakosoa.

Yangu ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom