Saikolojia: Fahamu tabia ya hasira, madhara yake na namna za kuishinda

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
393
1,000
"In the midst of great joy, do not promise anyone anything. In the midst of great anger, do not answer anyone's letter." —Chinese proverb


1. MWANZO
upload_2018-3-22_3-53-52.png


Kama binadamu kila mmoja wetu kwa namna tofauti tofauti tuna mapito mengi sana ya kujifunza kuhusu maisha kiuhalisi na mashuhuda wazuri wa namna gani tabia ya hasira ilivyotugharimu.

kwa namna tofauti tofauti katika maeneo ya ajira, kazi, mahusiano, familia na ushirikiano na watu mbalimbali kifupi sisi wenyewe ni mashuhuda kwa namna gani hasira ilivyofungua mlango wa uharibifu na wakati mwingine umeacha makovu ambayo yanahitaji neema ya Mungu kuweza kufutika kwa namna tulivyowapoteza tuwapendao au kuharibu mahusiano na heshima iliyokuwepo awali.

Zipo semi nyingi za kiswahili zinazosema “Hasira hasara” na “Hasira ya Mkizi furaha ya Mvuvi” ni kujaribu kutupa picha ijapokuwa kila mwanadamu ana hasira ndani yake lakini ni kitu ambacho kimegharimu maisha ya wanadamu toka vizazi kwa vizazi na semi hizi zilikuwepo kusudi kutupa mwongozo wa namna gani maauzi tunayotoa hayapaswi kutokana au kuambatana na hisia za Hasira au ghadhabu.

MIFANO HALISI KUHUSU GHARAMA YA TABIA HASIRA

MFANO WA I

Nilipokuwa nasoma kitabu kinachoitwa Historia ya ulimwengu wa kale kilichoandikwa mwaka 1988 na Umoja wa nchi za kisovieti kabla haujasambaratika. Sababu historia hasa zinazoegemea au kufuata mlengo wa Marxist huwa zina msingi wa kuandika kuhusu “class struggle” kati ya tabaka la juu Wanyonyaji Makabaila, na mabepari dhidi ya tabaka la chini wanyonywaji yaani wakulima, watumwa, wafanyakazi na wasanii.

KIPINDI CHA VITA YA WAGIRIKI NA WAAJEMI 480 B.C.

upload_2018-3-22_3-57-3.png


Katika hii vita kulikuwa na kabila dogo linaloitwa Sparta na kabila hili lilikuwa linajumuisha moja ya makabila ya waagiriki ambalo lilikuwa lina jeshi dogo na imara sana na maaskari wenye nidhamu ya hali ya juu sana wenye ushujaa. Kuna sinema moja ilijaribu kuwaelezea inaitwa “Prepare for glory 300”.

Hawa walipokuwa wakipigana vita au wakienda vitani ndio walioanzisha utaratibu wa kwenda na bendi yaani wapiga ala za muziki na tamaduni hii iliendelea mpaka miaka ya vita ya napoleon Bonaparte 1800 sikuwahi kuelewa maana yake ilikuwa ni nini? kwenda uwanja wa mapambano na ala za muziki.

Kumbe nyuma yake siri ilikuwa ni hivi kutengeneza hali yaku relax wanapopigana vita vyovyote wasipigane kwa hisia ya HASIRA hivyo kabla ya kwenda vitani walipambana kwanza na hisia zao yaani kwa mazingira yoyote yale HASIRA isichukue nafasi ndani yao hivyo vita vingi walivyopigana walisifika kwa kuwa na jeshi lenye nidhamu ya hali ya juu na kupiga kishujaa sana hivyo.

Kulikuwa na misemo kama” kuishi kisparta” na” Ngao uibebe au ikubebe”wakiwa na maana nidhamu ya kupigana hadi mwisho pasipo kupoteza ngao na upanga wako hata ukifa askari wenzako wakukute umekufa na siraha zako pembeni (Ndipo walitumia ngao kubebea maiti za askari wenzao).

Na kwahiyo walichangia kwa kiasi kikubwa sana kuiangusha Dola ya Umedi na Uajemi ambayo ndilo lilikuwa taifa babe kwa wakati huo na mtawala wake wa kwanza wa taifa hilo alikuwa anajulikana kama Mfalme Nebukadneza wa babeli.

Na baada ya vita hiyo ya kishujaa ijapokuwa wengi walikufa akiwemo mfalme wao alieitwa leonido1 ndio walioweka misingi ya kuinuka dola jipya la wagiriki chini ya Mfalme Alexander the great wa Macedonia katika karne zilizofuatia lenye jeshi linalopigana kwa namna hiyo ya kisparta.

Katika ulimwengu huu wa leo mambo mengi yamebadilika sana na mbinu ambazo sasa hivi zimekuwa zinatumiwa katika kuwasaidia kuwa na utulivu wa kihisia kwa wanajeshi hasa wanapoenda vitani ni tofauti na zile za kwenda na vyombo vya ala za muziki.

upload_2018-3-22_3-57-19.png


Katika wakati vijana wanapochukuliwa na kujiunga katika jeshi lolote duniani huwa katika siku za mwanzo au awali kuwa kuna mazoezi ambayo yanasimamiwa na wakufunzi( Drill Sergent ) ambao huwa ni wakali sana na wenye kutia hasira na maelekezo yao huyatoa kwa namna ambayo yanakusudia kukufanya upatwe na hasira kwa haraka lakini lengo lao si kukufanya upatwe na hasira ila ni kukutengeneza katika mazingira yoyote kuwa na emotion stability ili uweze fanya maamuzi sahihi pasipo kuwa na jazba na ghadhabu za kipumbavu na hiyo imekuwa ikiwagharimu sana wapiganaji wanapigana kwa hasira wakati wote wameonekana na matendo ya kishujaa kwa muda mfupi sana kabla ya kupoteza maisha katika uwanja wa vita .

MFANO WA II

PAMBANO LA MCHEZO WA NGUMI “Thriller in Manila” kati ya JOE FRAIZER na MUHAMMAD ALI

upload_2018-3-22_3-57-31.png


Joe Fraizer atakumbukwa kama bondia mmojawapo aliyewahi kumpiga Muhammad Ali katika pambano na kumfanya apoteze mkanda wake wakati huo Muhammad Ali akiwa bado ni kijana na yupo katika kilele cha ubora wake katika miaka ya 1970.

Na kwenye pambano hilo Muhammad Ali alilopoteza alisikika akimwambia kocha wake “Huyu mtu ataniua leo hapa” kocha wake akamtuliza kwa kumtia moyo na kumuambia “hautakufa”.

Fraizer baada ya kumpiga Muhammad Ali hakutaka tena kupanda uwanjani na Muhammad Ali na alikuwa akikwepa kabisa, lakini Muhammad Ali alitaka pambano la marudiano na aliuelewa udhaifu wa Joe Fraizer vizuri alikuwa mtu mwenye hasira za karibu kwahiyo namna ambayo kwa urahisi angemrudisha ukumbini Frazier ni kwa kumchokoza na kumtania kwenye vyombo vya habari na katika maeneo ya umma au mbele ya kadamnasi.

Mara kwa mara Ali alijitokeza kwenye kadamnasi sababu alikuwa na kipaji si cha ngumi tu na hadi cha kuchekesha watu alitumia nafasi hiyo vizuri alijitokeza na mdoli wa Sokwe Mtu. Na aliuita Joe Fraizer sababu Joe alikuwa ni mweusi kwa rangi tofauti na Ali na alimtania matani ya kudhalilisha na kuchekesha kuna wakati akiupigapiga ngumi mdoli wa sokwe mtu huo huku akiupa jina Joe. Hivyo baada ya muda Joe kwa kuwa alikuwa mtu mwepesi wa hasira alikubali kwa haraka kurudi ukumbini kupigana na Ali tena.

upload_2018-3-22_3-57-42.png


Na pambano likaandaliwa Philippine na ndipo likapewa jina “Thriller in Manila” (Manila Mji mkuu wa Philippine) Na ndio lilikuwa ni moja ya mapambano ya mwisho ya Joe Fraizer akiwa katika ubora wake na ujana wake, na Pambano lililochangia miaka 20 mbeleni Muhammad Ali kuugua ugonjwa wa kutetemeka “Parkinson disease” huku Joe Mishipa ya jicho moja kukatika ukumbini na baadae miaka iliyofuatia kupatwa na stroke na hakuwa sawa tena Fraizer.

Katika pambano hilo kwa kuwa Joe Fraizer alipigana kwa Hasira aliishia kupigwa na kama isingekuwa refa kukatiza pambano lile baada kugundua Joe Fraizer alikuwa tiyari haoni vizuri mishipa ya ufahamu inayounganisha jicho imekatika sijui ingekuwaje? Mle ukumbini wapo wataalamu wanaosema mabondia wote walitaka kufia ulingoni.

Na mwisho Muhammad Ali aliibuka mshindi na kurudisha mkanda wake aliopoteza na kilichomsaidia ni mkakati wa nje ya ukumbi baada ya kumuelewa mpinzani wake udhaifu wa hasira za karibu sana.

2. BAADHI YA SABABU NANE YA WATU KUWA NA TABIA YA HASIRA AU KUSHINDWA JIDHIBITI KITABIA WANAPOKUWA NA HASIRA

Kama nilivyosema hapa awali hasira ni hisia kila mwanadamu anazaliwa nayo ila tuna viwango tofauti kutokana na kila mmoja wetu kimaumbile anavyoweza kukabiliana na mazingira yenye vichocheo vya tabia hiyo ya hasira na kujidhibiti au kushindwa na kujiachia.

Mfano kwa mwanadamu wa kawaida kabisa vichocheo vinaweza kuwa kuhisi umedharauliwa, kutotendewa haki, kuvunjiwa heshima au kupuuzwa. Hivi ndiyo vichocheo vikubwa vya tabia hiyo lakini zipo sababu nyingine nyuma ya pazia wengi tusizo zijua.

Ambazo nyingine hukaa katika ufahamu wa ndani (Unconscious) na zimekuwa zikiendesha tabia zetu au zikichangia tabia hii na kutufanya haraka hasira kwenda kwenye ghadhabu ni jambo dogo sana.

i. Maumbile ya Ubongo na tabia za kurithi

Maumbile ya ubongo wa binadamu mfano kunapokuwa na shida au hitilafu hasa mishipa inayounganisha sehemu za ubongo. Yaani eneo la ubongo linaloitwa “Amygdale” linalohusika na hisia ikiwemo hasira. Na sehemu ya ubongo wa mbele yaani katika paji la uso (Front Brain). Eneo hili huwa linahusika sana na fikra za uamuzi na utambuzi, nini cha kufanya katika mazingira unakutana nayo kila leo.

Hivyo kunapotokea shida katika mishipa hiyo inayounganisha “Amygdala” na “frontal brain”Mtu mwenye tatizo hilo huwa hasira yake ni mpaka haitimize kile alichokusudia. Kwa kweli huwa wakati mwingine hana tofauti na Mnyama kitabia sababu ya kushindwa jidhibiti nafsi yake. ASIYETAWALA ROHO YAKE NI MFANO WA MJI ULIOBOMOLEWA, USIO NA KUTA

Vile vile sababu nyingine ni kurithi tabia kutoka katika familia, ukoo na hata kabila. Yapo makabila ambayo hasira ina nafasi yake, na mara utakuta mtu akijisifia au wapo wanaojionea ufahari tabia ya Hasira

Labda tunafahamu baadhi ya mikoa ambayo ina udhaifu wa tabia hiyo na mara nyingi kumekuwa na habari za matukio ya kufanyiana ukatili wa kutisha au wengine kujiua pale wanapoudhiwa na kuwa hasira.

ii. Magonjwa ya kisaikolojia

Yapo magonjwa ya kisaikolojia ambayo yanatokana na mabadiliko ya kupungua au kuzidi kwa kemikali za mwilini hasa kwenye ubongo hivyo inapelekea mabadiliko ya kihisia pasipo mpangilio mfano wa magonjwa hayo ni Bipolar Disorder ambapo humfanya mtu kuwa na hisia au mabadiliko yasiyo ya kawaida ya kihisia.Na usababishwa na shida za kemikali katika ubongo Serotonin, dopamine, na norepinephrine

iii. Nadharia ya Kujifunza tabia

Kwa tabia za kujifunza hupo msemo unaosema “mbuyu ulianza kama mchicha” na “samaki mkunje angali mbichi”. Hisia za hasira sababu huwa ndani ya binadamu huwa zinasubilia kichochezi na huwa zinafikia kukomaa na moja ya vichochezi hivyo ni aina ya miziki inayohamasisha vurugu, Michezo ya kompyuta na televisheni yaani nikimaanisha “Video Games” na vipindi vyenye kuchochea vurugu na mauaji au vita. Kama unataka kupona tabia hiyo anza kuepuka vichochezi kama hivi visivyo vya lazima sana kwani safari ya maili elfu moja ilianza na hatua moja”

iv. Marafiki tunaokuwa nao

Katika eneo la marafiki kuna sheria moja katika saikolojia inaitwa “Law of Proximity” yaani vitu vinaavyoambatana pamoja ni vimoja na katika Kiswahili pia kuna msemo huo “Ndege wanaofanana huruka pamoja” tabia ni kama ugonjwa huwa zinaambukizana hasa kwa marafiki na watu wa karibu ambao ni negative au hasi.

v. Mapito au matukio wakati wa miaka ya utotoni

Unapopitia maisha ya watu wengi ambao walifanya mambo ya kushtua ulimwengu kutokana na kuwa ya kutisha na kuoghofya au ya kikatili.

Rudi nyuma ukaangalie sehemu za maisha waliopitia si tu hao wapo wengine walibakwa au kunajisiwa. Au waliteswa na walezi wao au wazazi wao hivyo maisha hayo yamewaachia alama ndani ya mioyo yao. Na wengine imewazalishia tabia ya hasira iliyokomaa yaani ghadhabu. “Tofauti ya mtoto mvulana na Mwanaume ni aina ya mdoli wa gari wanaouchezea”

vi. Sababu ya Mazingira

Kushuhudia mzazi wako mmoja akipigwa au akinyanyaswa au kutelekezwa na ndugu jamaa na na masuala yanayohusu wazazi kutalikiana, na zipo sababu nyingine za kijamii mfano mapigano ya labda ya wakulima na wafugaji, au kushuhudia vita au namna ya ubaguzi.

vii. Mabadiliko yanayogusa homoni

Mabadiliko hasa wakati wa kubarehe yaani kutoka katika utoto kwenda katika ujana “Adolescence”. Wakati huu kuna vijana hujikuta kuwa na hasira za karibu ambazo huzitoa kwa namna ya kiburi

Pia mabadiliko hasa kihomoni mwanamke anapokuwa katika kipindi cha ujauzito pia yanachangia tabia ya hasira

viii. Matumizi ya vilevi

Yapo matumizi ya vilevi Kama vile Bangi, heroine na Cocaine ambayo husabaisha mabadiliko ya kemikali katika Ubongo wa binadamu hivyo yanapelekea mtu kutokuwa sawa kihisia.

3. MATIBABU YATAKAYOSAIDIA MAUMBILE YA MWILINI

Matumizi ya Dawa za Akili japokuwa nafahamu kuhusu dawa gani hasa kwa wale ambao tabia ya hasira imetokana na matumizi ya vilevi au shida katika Mwili hasa ubongo. Lakini kitaaluma nashauri kama umeangukia katika kundi hili ni kwenda Hospitali hasa zinazoshghulika na matatizo ya akili kwa ushauri zaidi ni dawa zipi zitakazokufaa na namna ya matumizi yake kutokana na mwili na afya yako.

4. MATIBABU YANAYOSAIDIA AKILI AU FIKRA ZA MTU.

Katika sehemu hii ya B magonjwa mengi ya kiakili mwanzo wake huwa katika Mawazo na yanapokomaa huambukiza hisia za mtu hapo ndipo Tabia hujitokeza na baadae kuathiri mifumo mwili yetu na mengine hufikia hata kusababisha Kansa mwilini. Hivyo yapo katika mfano wa duara
628227-c77da8ef3bede9c70938ad4b7af02810.jpg

Kwa mujibu wa wanasaikolojia wanaotumia nadharia ya kutibu tabia inayoitwa Cognitive Behavioral Therapy au CBT mfano mmoja wapo hutumiwa pia katika vituo vya tiba na ushauri hasa kwa wenye maambukizi ya VVU.

Mfano yupo mama mmoja mumewe alifariki, baada ya miaka kama 8 mbele akawa anajisikia vibaya akaenda hospitalini hivyo madaktari wakamshauri afanye vipimo vya HIV na akagundua ameathirika na kumbe mume wake alifariki na yeye kwa ugonjwa huo huo.

Yule mama baada ya kupima na kuambiwa ni muathirika hapo ndipo hali yake ikazidi kuharibika ugonjwa ukawa ndio umechachamaa baada ya kupima. Lakini shida haikuwa ugonjwa ilikuwa katika fikra zake. Na Wengi wamepoteza maisha mapema sana kwa SI KWA MAGONJWA ILA KATIKA MAWAZO NA FIKRA ZAO.

5. SASA KATIKA KUKUSAIDIA KIFIKRA ILI MTAZAMO WAKO HUPONE KATIKA TABIA YA HASIRA FANYA HIVI

i. Epuka kufanya urafiki na watu wenye hasira za karibu au jitahidi ukae nao mbali kwa kadili inavyowezekana sababu kuu hapa Hasira zipo ndani ya kila mwanadamu ila zinajitokeza pale mazingira ya nje yanapokuwa na kichocheo cha hasira.

ii. Weka akilini ni heshima kubwa sana kwa mtu na sio upumbavu kuepuka mifarakano na ugomvi MTU KUJITENGA NA UGOMVI NI HESHIMA KWAKE; BALI KILA MPUMBAVU ATAKA KUGOMBANA

iii. Kama hasira yako inajitokeza katika mazingira ya kuhisi unadharaulika au kuvunjiwa heshima kumbuka “kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; na KABLA YA HESHIMA HUTANGULIA UNYENYEKEVU” kwahiyo unaposhinda mazingira ya kudharauliwa au kuhisi unavunjiwa heshima kwa kujinyenyekeza au kupuuzilia vichocheo vinavyokuja kwa namna hiyo wewe siyo Mjinga. MTU WA HASIRA HUCHOCHEA UGOMVI; NA MTU MWENYE GHADHABU HUASI SANA. KIBURI CHA MTU KITAMSHUSHA; BALI MWENYE ROHO YA UNYENYEKEVU ATAHESHIMIWA. Njia nyingine ya kulinda heshima yako ni kwa unyenyekevu.

iv. Wakati wote mtu mwenye busara ni Yule anayeweza kujidhibiti nafsi yake yaani “self-control” sababu “BUSARA YA MTU HUIAHIRISHA HASIRA YAKE; NAYO NI FAHARI YAKE KUSAMEHE MAKOSA” mwenye kuweza samehe na kuchukuliana na watu katika makosa yao sio mjinga ni ana ushujaa ndio maana sio wote wanaweza tabia hii.

v. Kuepuka wakati mwingine kumbuka “JAWABU LA UPOLE HUGEUZA HASIRA; BALI NENO LIUMIZALO HUCHOCHEA GHADHABU” wakati wa hasira jitahidi sana kukumbuka huwezi maliza “moto kwa moto” majibu ya upole ya suluhisho sana na wala sio ujinga kwahiyo mtu anapokuja juu tu jaribu mjibu kwa upole tu na anapoonesha hali ya ukibuli we jitengee tu na eneo hilo kama suala hilo litawezekana.

vi. Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; BALI MWENYE ROHO YA HAMAKI HUTUKUZA UPUMBAVU. Wakati unapotokewa kuudhiwa fahamu tu hamaki au haraka ya kuamua hasira ikutawale utafanya maamuzi ya kipumbavu kwa kujua wakati huo au kutojua na ni wakati wote hakuna mtu aliyefanya maamuzi katika hasira asijutie baadae au kujikuta akiomba msamaha kwa yaliyotokea wakati ushaharibu tayari na vitu haviwezi kuwa kama vilivyo. YEYE AONAYE HASIRA UPESI ATATENDA KWA UJINGA

vii. Wapo wengi tu ambao mazingira ya hasira zao kuinuka ni pale wanapokuwa katika majibizano. na kawaida ambayo baada ya muda hugeuka mashindano na mwisho ugomvi na kutukanana. Sasa elewa jambo moja kuwa KIBURI HULETA MASHINDANO TU; BALI HEKIMA HUKAA NAO WANAOSHAURIANA. Kwahiyo ukiona mtu hataki ushauri wako achana nae sababu utajizoeza tabia ya kiburi ukiamua kushindana nae na mwishoni hasira zisizokuwa na maana yoyote.

viii. Hasira inapotokea wakati unapokosolewa fahamu hivi akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe BALI YEYE ASIKILIZAYE LAWAMA HUJIPATIA UFAHAMU (yeye asikilizaye makosolewo au kukosolewa hujipatia ufahamu). Si kila anayekukosoa ni adui sababu hakuna mwanadamu asiye na mapungufu yake jifunze kuchukuliana na kila mtu katika hali zote pale inapobidi. Na pale unapokosolewa chukua mazuri ufanyie kazi na mabaya weka pembeni.

6. MATIBABU YANAYOSAIDIA KIROHO

Zipo sababu nyingine ambazo zina asili ya kiroho hasa inapokuja suala la kurithi kutoka katika vizazi vilivyotutangulia kwa hiyo muhimu sana kama unasumbuliwa na tabia ya hasira zipo ambazo ni udhaifu tunaoupata kutokana na asili ya mahali tulipozaliwa katika familia zetu ukoo na hata kabila

Hivyo ni vizuri sana kuhitaji msaada wa Mungu na ndio una nguvu na wa muujiza unaoweza kukutoa katikka namna ambayo ukashindwa kuelewa ilikuwaje.

HITIMISHO

Education Mentor ana shahada ya Saikolojia, ni mwanasaikolojia anayeegemea kutambua uwepo na asili ya Mwanadamu inatokana na Mungu (Creation Theory).
 

Attachments

  • circle.png
    File size
    25.2 KB
    Views
    255

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
14,014
2,000
Aseee uzi umeshiba mkuu ni mrefu ila hauchoshi nimependa pia ulivyotumia mifano hai kma thriller jn manila na 300 maana huwa inasaidia sana kuelewa mapema

Mimi pia nina shida ya hasira za karibu yaani neno moja linaweza nifanya nibadilike kabisa na kuwa mtu tofauti kabisa sijui nawezaje kuondokana na shida hii je na mmi nahitaji ninywe vidonge ama nipitie hiyo CBT

Kwa mara nyingine big up kwa uzi huu umetendea haki elimu yako
 

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
393
1,000
Aseee uzi umeshiba mkuu ni mrefu ila hauchoshi nimependa pia ulivyotumia mifano hai kma thriller jn manila na 300 maana huwa inasaidia sana kuelewa mapema

Mimi pia nina shida ya hasira za karibu yaani neno moja linaweza nifanya nibadilike kabisa na kuwa mtu tofauti kabisa sijui nawezaje kuondokana na shida hii je na mmi nahitaji ninywe vidonge ama nipitie hiyo CBT

Kwa mara nyingine big up kwa uzi huu umetendea haki elimu yako

Jitahidi kufanya utafiti katika sababu au vyanzo nilivyovitaja hapo kuhusu tabia ya hasira katika sehemu ya 2 hizo sababu nane.. ......ukipata uhakika sababu yake ndio msingi wa kuanza kupona
 

narumuk

JF-Expert Member
Feb 10, 2018
1,943
2,000
Umenifurahisha na pambano la Alli maana hata ulingoni alikuwa akimkasirisha kwa kumtukana kama; hiyo ni ngumi gani unatupa? n.k. Nakumbuka wakati tunajifunza ngumi enzi hizo tulikuwa tunaletewa hilo pambano ili tujifunze kuwafanya opponents wetu wapandwe na hasira ili tupate ushindi maana katika ngumi ukihamaki, utapigwa tu.
 

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
393
1,000
Umenifurahisha na pambano la Alli maana hata ulingoni alikuwa akimkasirisha kwa kumtukana kama; hiyo ni ngumi gani unatupa? n.k. Nakumbuka wakati tunajifunza ngumi enzi hizo tulikuwa tunaletewa hilo pambano ili tujifunze kuwafanya opponents wetu wapandwe na hasira ili tupate ushindi maana katika ngumi ukihamaki, utapigwa tu.
Ni kweli Mchezo wa Ngumi strategic zake ni kumpandisha hasira opponent wapo.. .....ndio sababu kuuweka kama Case study
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom