Sababu 6 kwanini mwanamke amekuchunia na kukupotezea ghafla pamoja na suluhisho la jambo hilo

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Kwenye ulimwengu wa mahusiano kuna mtindo saivi kwamba wa kwanza kumpotezea, kumchunia au kumuacha mwenzake ndo mshindi, sio mtindo mzuri ni utoto.

Kama kweli mnajaliana mtaongea na kusuluhisha tatizo lililopo ila ikitokea mwanamke amekupotezea ujue upendo wake umepungua, mwache aende zake, hivyo utambue sababu hizi mapema;

~ Mtindo wa mahusiano aliozoea

Anaweza akawa amezoea mahusiano ya wasiwasi, au kazoea uhuru kwenye mahusiano au amezoea kutoamini watu.

Mfano, kama mwanamke mara nyingi ana wasiwasi, atakua hajiamini na kuwaza utavunja naye mahusiano hivyo atataka awe wa kwanza kukupotezea ili maumivu yapungue sababu wewe unaonesha kuwa mbali, japo ki ukweli unaweza ukawa bize na kazi na huna ata wazo la kumsaliti.

Mwanamke wa hivyo akikufanyia hivyo mwache aende zake mana hajiamini, hautajenga naye maisha ya amani. Kama amezoea uhuru ukimbana sana atataka kujitoa na kukupotezea.

~ Heshima yake kwako ikishuka, sababu umeonesha udhaifu

Ukianza kumnyenyekea, au kumuona yeye ndo namba moja katika kila kitu chako. Au kulazimisha mawasiliano na kumpigia sana mwanamke au kumtext mara kwa mara alafu asipokujibu unamshutumu “mbona hujibu text zangu”/ “mbona hupokei simu zangu”.

kama mwanamke hajakujibu au kupokea simu mwache, usimlazimishe la sivyo atakushusha heshima. Hicho huwafanya wajisikie vibaya na kutaka kujitoa katika iyo hali ya kutukuzwa haraka iwezekanavyo.

~ Anataka kukuumiza

Sote tunajua kupotezeana juu juu tu bila sababu kunaumiza. Hivyo wanawake hutumia njia hii kukuumiza ili kulipiza kuumia kwake, labda ulimsaliti au umemuumiza hisia zake kwa vyovyote. Wengine hufanya ivo kulipiza alichofanyiwa na Ex wake, wa hivyo akikupotezea mwache aende zake hauna haja ya kuumia kwa ajili yake.

~ Amenyanyasika vya kutosha

Inawezekana amekua akipigwa, au kidogo tu anapelekwa kwa wazazi wake au anasemwa vibaya na mwanaume wake. Huogopa kuongea na mwanaume kwaiyo njia pekee anayoona ni kumpotezea mwanaume na kujitoa kwenye maisha yake bila taarifa. Kwa hapa inabidi ujirekebishe kabla ya kukutana na mwanamke mwingine.

~ Majanga yakimpata au kitu kingine chenye kumuhitaji zaidi

Labda mzazi wake amefariki, au mzazi wake/ yeye mwenyewe ni mgonjwa au anahama nyumba au anajitahisi kulinda nafasi yake kazini au chochote kinachompa mawazo na kumfanya hisia zake kuwa juu ya hicho kitu zaidi ya mahusiano yenu. Kwa mwanamke mwenye utu na anayejielewa lazima atakupa taarifa mapema juu ya kimpatacho na yakiisha atayarudisha mawazo yake kwenye mahusiano yenu.

~ Akipata mwanaume mwingine

Mnaweza mkawa mnaongea vizuri leo lakini kesho kimya cha ghafla kama vile haujawahi kuwepo, kwa kuwa amepata wa kumridhisha zaidi.

Kama alikukubalia kwa huruma atakuacha kirahisi, mara nyingi hutokea kwa wanaume dhaifu, mwanamke anaogopa akimueleza ukweli kwamba hawawezi kuwa pamoja tena atamuumiza sana, hivyo anachukua njia rahisi ya kumpotezea. Pia hutokea mwanamke akirudi kwa ex wake.

Cha kufanya

Kama ameamua kukuchunia tu ghafla na kukupotezea mwache aende kwa sababu upendo wake unakua umepungua kwa muda huo, haijalishi unajisikiaje kuhusu huyo mwanamke ila ndo ivo ameshakutenda.
Kupotezeana au kimya cha ghafla ni kuumizana bila sababu.

Kama mwanamke anapitia wakati mgumu na anajielewa atakutafuta na kukueleza kwamba hatokua na wewe kwa kipindi hiko kigumu. Pia kama anahitaji muda wa peke yake atakuambia.

Hivyo mtu akikupotezea tu ghafla mwache aende zake, usipoteze muda kutaka kumrudisha, sababu unataka mahusiano na mtu aliyekua kiakili na anayejielewa mnayeweza kuzungumza na kutatua matatizo.

Na wewe pia inabidi ujifunze na kuwa bora zaidi ili uweze kumvutia na kumtunza mwanamke anayejielewa, yote hayo ni safari hivyo katika kundi la infinite kiumeni tutakua pamoja na utajifunza na wanaume wengine wenye kutaka kufanikiwa katika mapenzi yao, jinsi ya kuvutia na kumtunza mwanawake unayetaka kujenga naye maisha.
 
Amplifaya akiunguruma
FB_IMG_16735423366274092.jpg
 
Nyie mliopo kwenye mahusiono ya kuchombeza style ya mahusiono na waliopo kwenye ndoa ni tofauti kwenye ndoa mnawaza maisha kwa ujumla mahusiano yenu,koo zenu na Mipango yenu ,mnawaza jinsi ya kulea watoto mnawaza vitega uchumi mnawaza future ya watoto wenu darasa lake ni pana zaidi ya kuchuniana hapokeu simu aninipenda hanipendi hayo Ni mkiwa kwenye mahusiano ya kuchombezana tena ukute hata kuchumbiana.hamjachumbiana nyie mna darasa lenu tofauti
 
Mwanamke anaweza kulipenda lijamaa fulani hivi kumbe hilo lijamaa limevutiwa tu na dodo saa 6,siku mwanamke akiwa na malapa aka ndala lijamaa linasepa mazimaa, linahamia kwa kigori mpyaa.

Ni kweli msipokuwa makini mnapotezwa sana.
unafikiri hawa wana umakini wowote?

Hawana kabisa
 
Dawa ya hii tabia ni kukaza fuvu mkaushie kama vile hakuna kinachoendelea kati yenu.
Ikiwezekana tengeneza na mazingira ya kutoonana hata barabaran yaan Kwa kifupi msionane kabisa.
Km kweli anakupenda Toka moyoni atateseka yeye na kuhaha vibaya mno kama alikua kajiegesha basi atakuwa na ujasir wa kukaushiana na wewe mazima.

Kanuni ni Moja TU mwanamke wako asijue udhaifu wako pia asijue wewe ni mtu wa aina gn ,yaan hutabiriki.
 
Back
Top Bottom